Check out the new design

Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik - Prevodilački centar Ruvvad * - Sadržaj prijevodā


Prijevod značenja Sura: El-A'araf   Ajet:
حَقِيقٌ عَلَىٰٓ أَن لَّآ أَقُولَ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡحَقَّۚ قَدۡ جِئۡتُكُم بِبَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ فَأَرۡسِلۡ مَعِيَ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ
Inastahiki zaidi juu yangu kwamba nisiseme juu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa haki tu. Hakika nimewajia na Ishara za waziwazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi waachilie pamoja nami Wana wa Israili.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ إِن كُنتَ جِئۡتَ بِـَٔايَةٖ فَأۡتِ بِهَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ
Akasema (Firauni), "Ikiwa umekuja na ishara yoyote, basi ilete ikiwa wewe ni katika wakweli."
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعۡبَانٞ مُّبِينٞ
Basi akaitupa fimbo yake, na tazama, ikawa joka lililo dhahiri.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَنَزَعَ يَدَهُۥ فَإِذَا هِيَ بَيۡضَآءُ لِلنَّٰظِرِينَ
Na akautoa nje mkono wake, na tazama ulikuwa mweupe kwa watazamao.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِ فِرۡعَوۡنَ إِنَّ هَٰذَا لَسَٰحِرٌ عَلِيمٞ
Wakasema waheshimiwa kutoka katika kaumu ya Firauni, "Hakika huyo ni mchawi ajuaye vyema."
Tefsiri na arapskom jeziku:
يُرِيدُ أَن يُخۡرِجَكُم مِّنۡ أَرۡضِكُمۡۖ فَمَاذَا تَأۡمُرُونَ
Anataka kuwatoa katika nchi yenu. Basi mnaamrisha nini?
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالُوٓاْ أَرۡجِهۡ وَأَخَاهُ وَأَرۡسِلۡ فِي ٱلۡمَدَآئِنِ حَٰشِرِينَ
Wakasema: Mwache kidogo yeye na kaka yake, na watume mijini wakusanyaji.
Tefsiri na arapskom jeziku:
يَأۡتُوكَ بِكُلِّ سَٰحِرٍ عَلِيمٖ
Wakujie na kila mchawi ajuaye vyema.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَجَآءَ ٱلسَّحَرَةُ فِرۡعَوۡنَ قَالُوٓاْ إِنَّ لَنَا لَأَجۡرًا إِن كُنَّا نَحۡنُ ٱلۡغَٰلِبِينَ
Na wakamjia wachawi Firauni, wakasema: Hakika tutapata ujira ikiwa tutakuwa sisi ndio washindi.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ نَعَمۡ وَإِنَّكُمۡ لَمِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ
Akasema: Ndiyo! Nanyi bila ya shaka ni katika waliotiwa karibu nami.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالُواْ يَٰمُوسَىٰٓ إِمَّآ أَن تُلۡقِيَ وَإِمَّآ أَن نَّكُونَ نَحۡنُ ٱلۡمُلۡقِينَ
Wakasema: Ewe Musa! Ima utupe wewe, au tuwe sisi ndio watupao?
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ أَلۡقُواْۖ فَلَمَّآ أَلۡقَوۡاْ سَحَرُوٓاْ أَعۡيُنَ ٱلنَّاسِ وَٱسۡتَرۡهَبُوهُمۡ وَجَآءُو بِسِحۡرٍ عَظِيمٖ
Akasema: Tupeni! Basi walipotupa, waliyafanyia uchawi macho ya watu na wakawatia hofu, na wakaleta uchawi mkubwa.
Tefsiri na arapskom jeziku:
۞ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنۡ أَلۡقِ عَصَاكَۖ فَإِذَا هِيَ تَلۡقَفُ مَا يَأۡفِكُونَ
Nasi tukamfunulia Musa kumwambia: Itupe fimbo yako, na tazama, ikawa inavimeza vyote vile walivyovizulia uwongo.
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَوَقَعَ ٱلۡحَقُّ وَبَطَلَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Basi haki ikathibiti na yakabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَغُلِبُواْ هُنَالِكَ وَٱنقَلَبُواْ صَٰغِرِينَ
Kwa hivyo wakashindwa huko, na wakageuka kuwa wadogo.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأُلۡقِيَ ٱلسَّحَرَةُ سَٰجِدِينَ
Na wachawi wakatupwa chini wakisujudu
Tefsiri na arapskom jeziku:
 
Prijevod značenja Sura: El-A'araf
Indeks sura Broj stranice
 
Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik - Prevodilački centar Ruvvad - Sadržaj prijevodā

Prevod: Prevodilački centar Ruvvad u saradnji sa Udruženjem za poziv u Rabwi i Udruženjem za pružanje islamskog sadržaja na jezicima.

Zatvaranje