Check out the new design

Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis * - Translations’ Index


Translation of the meanings Surah: Al-Jāthiyah   Ayah:
قُل لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ يَغۡفِرُواْ لِلَّذِينَ لَا يَرۡجُونَ أَيَّامَ ٱللَّهِ لِيَجۡزِيَ قَوۡمَۢا بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ
Sema, ewe Mtume, uwaambie wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na wakamfuata Mtume Wake, wawasamehe na kuwaachilia wale ambao hawana matarajio ya malipo mema ya Mwenyezi Mungu na hawaogopi adhabu Yake wanapowakusudia Waumini kuwaudhi na kuwakera, ili Mwenyezi Mungu Awalipe washirikina hawa kwa yale waliyoyachuma duniani ya madhambi na kuwaudhi Waumini.
Arabic explanations of the Qur’an:
مَنۡ عَمِلَ صَٰلِحٗا فَلِنَفۡسِهِۦۖ وَمَنۡ أَسَآءَ فَعَلَيۡهَاۖ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمۡ تُرۡجَعُونَ
Yoyote yule, miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu, Anayefanya matendo ya utiifu Kwake, basi malipo mema ya utiifu wake atayapata mwenyewe, na mwenye kufanya matendo mabaya duniani kwa kumuasi Mwenyezi Mungu, basi atakuwa amejikosea mwenyewe. Kisha nyinyi, enyi watu, mtaishia kwa Mola wenu baada ya kufa kwenu, Amlipe mwema kwa wema wake na mbaya kwa ubaya wake.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحُكۡمَ وَٱلنُّبُوَّةَ وَرَزَقۡنَٰهُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَٰتِ وَفَضَّلۡنَٰهُمۡ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ
Hakika tuliwapatia Wana wa Isrāīl Taurati na Injili na tukawaamuru kuhukumu kulingana na yaliyomo kwenye vitabu viwili hivyo, na tukawafanya wengi wa Manabii watokanao na kizazi cha Ibrāhīm, amani imshukie, ni katika wao, na tukawaruzuku vitu vizuri miongoni mwa vitu vya kukimu maisha, matunda na vyakula, na tukawafadhilisha juu ya walimwengu wa zama zao.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَءَاتَيۡنَٰهُم بَيِّنَٰتٖ مِّنَ ٱلۡأَمۡرِۖ فَمَا ٱخۡتَلَفُوٓاْ إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَهُمُ ٱلۡعِلۡمُ بَغۡيَۢا بَيۡنَهُمۡۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقۡضِي بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فِيمَا كَانُواْ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ
Na tukawapatia Wana wa Isrāīl Sheria zilizo wazi juu ya halali na haramu, na dalili zenye kutenganisha haki na batili. Hawakutafautiana isipokuwa baada ya kujiwa na elimu na hoja ikasimama juu yao. Na lililowapelekea wafanye hivyo ni lile jambo la kudhulumiana wao kwa wao kwa kutaka ukubwa na uongozi. Hakika Mola wako Atahukumu baina ya wanaotafautiana miongoni mwa Wana wa Isrāīl Siku ya Kiyama katika yale waliokuwa wakitafautiana juu yake duniani. Kwenye maelezo haya pana onyo kwa ummah huu wasifuate mwenendo wao.
Arabic explanations of the Qur’an:
ثُمَّ جَعَلۡنَٰكَ عَلَىٰ شَرِيعَةٖ مِّنَ ٱلۡأَمۡرِ فَٱتَّبِعۡهَا وَلَا تَتَّبِعۡ أَهۡوَآءَ ٱلَّذِينَ لَا يَعۡلَمُونَ
Kisha tukakufanya, ewe Mtume, uwe kwenye njia iliyofunuka wazi kuhusu jambo la Dini. Basi fuata Sheria ambayo Mwenyezi Mungu Amekupatia, na usifuate matamanio ya wajinga wa Sheria ya Mwenyezi Mungu, wasiojua haki. Katika hii aya kuna ushahidi mkubwa juu ya ukamilifu wa Dini hii na utukufu wake na ulazima wa kufuata hukumu zake na kutopotoka kuelemea kwenye matamanio ya makafiri na wapotofu.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّهُمۡ لَن يُغۡنُواْ عَنكَ مِنَ ٱللَّهِ شَيۡـٔٗاۚ وَإِنَّ ٱلظَّٰلِمِينَ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلِيَآءُ بَعۡضٖۖ وَٱللَّهُ وَلِيُّ ٱلۡمُتَّقِينَ
Hawa waliomshirikisha Mola wao wanaokuita ufuate matamanio yao, hawatakufalia kitu, ewe Mtume, kwa kukuepushia adhabu ya Mwenyezi Mungu iwapo umefuata matamanio yao. Na hakika madhalimu wenye kukiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu miongoni mwa wanafiki, Mayahudi na wasiokuwa hao wanasaidiana wao kwa wao dhidi ya wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na walio watiifu Kwake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwapa ushindi wenye kumcha Mola wao kwa kutekeleza faradhi Zake na kujiepusha na makatazo Yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
هَٰذَا بَصَٰٓئِرُ لِلنَّاسِ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٞ لِّقَوۡمٖ يُوقِنُونَ
Hii Qur’ani tuliyokuteremshia, ewe Mtume, ni miangaza ya watu kuiona haki na kuipambanua na batili, na kuijua kwayo njia ya usawa, na ni uongofu na rehema kwa watu wenye kuwa na Imani ya yakini juu ya uhakika wa usahihi wake, na kwamba hiyo ni teremsho kutoka kwa Mshindi Mwenye hekima.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَمۡ حَسِبَ ٱلَّذِينَ ٱجۡتَرَحُواْ ٱلسَّيِّـَٔاتِ أَن نَّجۡعَلَهُمۡ كَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ سَوَآءٗ مَّحۡيَاهُمۡ وَمَمَاتُهُمۡۚ سَآءَ مَا يَحۡكُمُونَ
Bali je, wanadhani wale wanaotenda maovu na wanaowakanusha Mitume wa Mwenyezi Mungu na kuenda kinyume na amri ya Mola wao na wakamuabudu asiyekuwa Yeye, kuwa tutawafanya wao ni kama wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na wakawasadiki Mitume Wake na wakafanya matendo mema na wakamtakasia Yeye ibada na sio wengine, na tuwasawazishe na wao ulimwenguni na Akhera? Ni uamuzi mbaya huo wao wa kuwsawazisha baina ya waovu na wema kesho Akhera.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَخَلَقَ ٱللَّهُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّ وَلِتُجۡزَىٰ كُلُّ نَفۡسِۭ بِمَا كَسَبَتۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ
Na Mwenyezi Mungu Ameumba mbingu na ardhi kwa haki, uadilifu na hekima , na ili kila nafsi ilipwe huko Akhera kwa ilichokitenda cha kheri au cha shari, na wao hawatadhulumiwa malipo ya matendo yao.
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Surah: Al-Jāthiyah
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis - Translations’ Index

Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Sh. Naser Khamis

close