Check out the new design

Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis * - Translations’ Index


Translation of the meanings Surah: Al-Jāthiyah   Ayah:
أَفَرَءَيۡتَ مَنِ ٱتَّخَذَ إِلَٰهَهُۥ هَوَىٰهُ وَأَضَلَّهُ ٱللَّهُ عَلَىٰ عِلۡمٖ وَخَتَمَ عَلَىٰ سَمۡعِهِۦ وَقَلۡبِهِۦ وَجَعَلَ عَلَىٰ بَصَرِهِۦ غِشَٰوَةٗ فَمَن يَهۡدِيهِ مِنۢ بَعۡدِ ٱللَّهِۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Unamuona vipi, ewe Mtume, yule aliyoyachukuwa matamanio yake akayafanya ndiye Mola wake, akawa hatamani kitu isipokuwa anakifanya, na Mwenyezi Mungu Akampoteza baada ya ujuzi kumfikia na kusimamiwa na hoja, akawa hasikii mawaidha ya Mwenyezi Mungu wala hazingatii kwa mawaidha hayo, na Mwenyezi Mungu akapiga muhuri juu ya moyo wake akawa hafahamu kitu, na Akaweka finiko kwenye macho yake akawa hazioni hoja za Mwenyezi Mungu? Basi ni nani atakayemuongoza kuifikia haki na uongofu baada ya Mwenyezi Mungu kumpoteza? Kwani hamkumbuki, enyi watu mkajua kwamba mwenye kufanywa hivyo na Mwenyezi Mungu hataongoka kabisa na hatapata wa kumsaidia na kumuongoza? Aya hii ndio msingi wa kuonya kwamba matamanio hayafai kuwa ndio msukumo wa Waumini katika matendo yao.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَقَالُواْ مَا هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا ٱلدُّنۡيَا نَمُوتُ وَنَحۡيَا وَمَا يُهۡلِكُنَآ إِلَّا ٱلدَّهۡرُۚ وَمَا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنۡ عِلۡمٍۖ إِنۡ هُمۡ إِلَّا يَظُنُّونَ
Na wanasema hawa washirikina, “Hakuna maisha isipokuwa haya maisha yetu ya duniani tuliyonayo; hakuna maisha mengineyo,” kwa njia ya kukanusha kufufuliwa baada ya kufa. “Na hakuna kinachotuangamiza isipokuwa kupitiwa na masiku na michana na umri mrefu,“ wakikanusha kuwa wana Mola Anaowatowesha na kuwaangamiza.” Na hawa washirikina hawana ujuzi wowote juu ya hilo, hawana lolote isipokuwa ni kusema kwa kudhania, kufikiria na kuwaza.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتُنَا بَيِّنَٰتٖ مَّا كَانَ حُجَّتَهُمۡ إِلَّآ أَن قَالُواْ ٱئۡتُواْ بِـَٔابَآئِنَآ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Na wanaposomewa, hawa washirikina wakanushaji, aya zetu zilizo waziwazi, huwa hawana hoja isipokuwa ni kutoa maneno yao kumwambia Mtume Muhammad, “Wahuishe, wewe na Waumini, baba zetu waliokufa iwapo nyinyi ni wakweli kwa mnayoyasema.”
Arabic explanations of the Qur’an:
قُلِ ٱللَّهُ يُحۡيِيكُمۡ ثُمَّ يُمِيتُكُمۡ ثُمَّ يَجۡمَعُكُمۡ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ لَا رَيۡبَ فِيهِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ
Sema, ewe Mtume, uwaambie hawa washirikina wenye kukanusha kufufuliwa, “Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, Atawahuisha duniani kipindi Anachotaka muishi, kisha Atawafisha humo, kisha Atawakusanya mkiwa hai kwenye Siku ya Kiyama isiyokuwa na shaka.» Lakini wengi wa watu hawajui kwamba Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwafisha, kisha kuwafufua Siku ya Kiyama.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلِلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَيَوۡمَ تَقُومُ ٱلسَّاعَةُ يَوۡمَئِذٖ يَخۡسَرُ ٱلۡمُبۡطِلُونَ
Ni ya Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, mamlaka ya mbingu saba na ardhi kwa kuziumba, kuzimiliki na kuwa ziko chini ya amri Yake. Na siku Kiyama kitakapokuja ambapo wafu watafufuliwa kutoka kwenye makaburi yao na watahesabiwa, hapo watapata hasara wale waliomkanusha Mwenyezi Mungu na kukataa kile Alichomteremshia Mtume Wake miongoni mwa aya zilizbainika na dalili zilizofunuka wazi.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَتَرَىٰ كُلَّ أُمَّةٖ جَاثِيَةٗۚ كُلُّ أُمَّةٖ تُدۡعَىٰٓ إِلَىٰ كِتَٰبِهَا ٱلۡيَوۡمَ تُجۡزَوۡنَ مَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Utaona, ewe Mtume, Siku ya Kiyama, watu wa kila mila na dini wamepiga magoti, kila ummah wanaitwa kushuhudia kitabu matendo yao, na wataambiwa, «Leo mtalipwa kwa yale mliokuwa mkiyafanya ya kheri au ya shari.
Arabic explanations of the Qur’an:
هَٰذَا كِتَٰبُنَا يَنطِقُ عَلَيۡكُم بِٱلۡحَقِّۚ إِنَّا كُنَّا نَسۡتَنسِخُ مَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
«Hiki ni Kitabu chetu kinatamka kuhusu matendo yenu yote, bila kuongeza wala kupunguza. Sisi tulikuwa tukiwaamrisha Watunzi wenye kudhibiti wayaandike matendo yenu.»
Arabic explanations of the Qur’an:
فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ فَيُدۡخِلُهُمۡ رَبُّهُمۡ فِي رَحۡمَتِهِۦۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡمُبِينُ
Ama wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake duniani, wakafuata amri Zake na wakajiepusha makatazo Yake, hao Atawatia Mola wao kwenye Pepo Yake kwa rehema Zake. Kuingia huko ndiko kufaulu kuliko wazi ambako hakuna kufaulu kupita huko.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَأَمَّا ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَفَلَمۡ تَكُنۡ ءَايَٰتِي تُتۡلَىٰ عَلَيۡكُمۡ فَٱسۡتَكۡبَرۡتُمۡ وَكُنتُمۡ قَوۡمٗا مُّجۡرِمِينَ
Na ama wale waliokataa kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa haki, wakawakanusha Mitume Wake, na wasifuate Sheria Yake kivitendo, basi wataambiwa kwa kukaripiwa na kulaumiwa, «Kwani aya zangu hazikuwa zikisomwa kwenu huko duniani, mkazifanyia kiburi kwa kutozisikiliza na kutoziamini, na mkawa ni watu wenye kushirikisha, mnachuma maasia na hamuamini thawabu wala mateso?»
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِذَا قِيلَ إِنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٞ وَٱلسَّاعَةُ لَا رَيۡبَ فِيهَا قُلۡتُم مَّا نَدۡرِي مَا ٱلسَّاعَةُ إِن نَّظُنُّ إِلَّا ظَنّٗا وَمَا نَحۡنُ بِمُسۡتَيۡقِنِينَ
Na mnapoambiwa, «Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kuwafufua watu kutoka kwenye makaburi yao ni kweli, na kwamba kipindi cha kusimama Kiyama ni jambo lisilo na shaka, mnasema, ‘Hatujui ni nini Kiyama? Na hatudhani kuwa kitatokea isipokuwa ni kudhania tu, na sisi si wenye uhakika kuwa kipindi hicho cha Kiyama ni chenye kuja.’»
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Surah: Al-Jāthiyah
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis - Translations’ Index

Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Sh. Naser Khamis

close