Check out the new design

Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center * - Translations’ Index


Translation of the meanings Surah: Al-Anbiyā’   Ayah:
وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِيٓ إِلَيۡهِ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱعۡبُدُونِ
Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa tulimfunulia ya kwamba hakuna mungu isipokuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَقَالُواْ ٱتَّخَذَ ٱلرَّحۡمَٰنُ وَلَدٗاۗ سُبۡحَٰنَهُۥۚ بَلۡ عِبَادٞ مُّكۡرَمُونَ
Na walisema: Arrahman (Mwingi wa rehema) alijifanyia mwana! Subhanahu (Ametakasika mbali na hayo!) Bali hao (wanaowaita wana) ni waja waliotukuzwa.
Arabic explanations of the Qur’an:
لَا يَسۡبِقُونَهُۥ بِٱلۡقَوۡلِ وَهُم بِأَمۡرِهِۦ يَعۡمَلُونَ
Hawamtangulii kwa neno, nao wanafanya amri zake.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَعۡلَمُ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَمَا خَلۡفَهُمۡ وَلَا يَشۡفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ٱرۡتَضَىٰ وَهُم مِّنۡ خَشۡيَتِهِۦ مُشۡفِقُونَ
Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawamfanyii yeyote uombezi isipokuwa yule anayemridhia Yeye, nao kwa sababu ya kumhofu wanaogopa.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ وَمَن يَقُلۡ مِنۡهُمۡ إِنِّيٓ إِلَٰهٞ مِّن دُونِهِۦ فَذَٰلِكَ نَجۡزِيهِ جَهَنَّمَۚ كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلظَّٰلِمِينَ
Na yeyote kati yao atakayesema: Mimi ni mungu, badala yake, basi huyo tutamlipa Jahannamu. Hivyo ndivyo tuwalipavyo madhalimu.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَوَلَمۡ يَرَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَنَّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ كَانَتَا رَتۡقٗا فَفَتَقۡنَٰهُمَاۖ وَجَعَلۡنَا مِنَ ٱلۡمَآءِ كُلَّ شَيۡءٍ حَيٍّۚ أَفَلَا يُؤۡمِنُونَ
Je, hao waliokufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana, kisha Sisi tukazibandua? Na tukafanya kwa maji kila kilicho hai? Basi je, hawaamini?
Arabic explanations of the Qur’an:
وَجَعَلۡنَا فِي ٱلۡأَرۡضِ رَوَٰسِيَ أَن تَمِيدَ بِهِمۡ وَجَعَلۡنَا فِيهَا فِجَاجٗا سُبُلٗا لَّعَلَّهُمۡ يَهۡتَدُونَ
Na tukaweka katika ardhi milima iliyo thabiti ili isiwayumbishe, na tukaweka humo njia pana ili wapate kuongoka.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَجَعَلۡنَا ٱلسَّمَآءَ سَقۡفٗا مَّحۡفُوظٗاۖ وَهُمۡ عَنۡ ءَايَٰتِهَا مُعۡرِضُونَ
Na tukaifanya mbingu kuwa dari iliyohifadhiwa, lakini wanazipuuza Ishara zake.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَهُوَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَ وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ كُلّٞ فِي فَلَكٖ يَسۡبَحُونَ
Na Yeye ndiye aliyeumba usiku na mchana na jua na mwezi, vyote katika anga vinaogelea.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَا جَعَلۡنَا لِبَشَرٖ مِّن قَبۡلِكَ ٱلۡخُلۡدَۖ أَفَإِيْن مِّتَّ فَهُمُ ٱلۡخَٰلِدُونَ
Nasi hatukumfanya mwanadamu yeyote kabla yako kuwa na uhai wa milele. Basi je, ukifa wewe, wao wataishi milele?
Arabic explanations of the Qur’an:
كُلُّ نَفۡسٖ ذَآئِقَةُ ٱلۡمَوۡتِۗ وَنَبۡلُوكُم بِٱلشَّرِّ وَٱلۡخَيۡرِ فِتۡنَةٗۖ وَإِلَيۡنَا تُرۡجَعُونَ
Kila nafsi itaonja mauti; na tunawajaribu kwa mtihani wa maovu na heri. Na kwetu Sisi mtarejeshwa.
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Surah: Al-Anbiyā’
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center - Translations’ Index

translated by Rowwad Translation Center, in cooperation with the Islamic Propagation Office in Rabwah and the Association for Serving Islamic Content in Languages.

close