Check out the new design

Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center * - Translations’ Index


Translation of the meanings Surah: Al-Anbiyā’   Ayah:
وَإِذَا رَءَاكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِن يَتَّخِذُونَكَ إِلَّا هُزُوًا أَهَٰذَا ٱلَّذِي يَذۡكُرُ ءَالِهَتَكُمۡ وَهُم بِذِكۡرِ ٱلرَّحۡمَٰنِ هُمۡ كَٰفِرُونَ
Na wanapokuona wale waliokufuru, hawakufanyi wewe isipokuwa ni kitu cha masihara tu, (wakisema): Je, huyu ndiye anayeitaja miungu yenu? Na hali wao wanakufuru kumkumbuka Arrahman (Mwingi wa Rehema)!
Arabic explanations of the Qur’an:
خُلِقَ ٱلۡإِنسَٰنُ مِنۡ عَجَلٖۚ سَأُوْرِيكُمۡ ءَايَٰتِي فَلَا تَسۡتَعۡجِلُونِ
Mwanadamu ameumbwa na haraka. Nitawaonyesha Ishara zangu. Basi msinihimize.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا ٱلۡوَعۡدُ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi mnasema kweli?
Arabic explanations of the Qur’an:
لَوۡ يَعۡلَمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ حِينَ لَا يَكُفُّونَ عَن وُجُوهِهِمُ ٱلنَّارَ وَلَا عَن ظُهُورِهِمۡ وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ
Lau wangelijua wale waliokufuru wakati ambao hawatauzuia Moto kwenye nyuso zao wala migongo yao, na wala hawatanusuriwa!
Arabic explanations of the Qur’an:
بَلۡ تَأۡتِيهِم بَغۡتَةٗ فَتَبۡهَتُهُمۡ فَلَا يَسۡتَطِيعُونَ رَدَّهَا وَلَا هُمۡ يُنظَرُونَ
Bali utawafikia kwa ghafla, na utawashitua na wala hawataweza kuurudisha, wala hawatapewa muhula!
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَقَدِ ٱسۡتُهۡزِئَ بِرُسُلٖ مِّن قَبۡلِكَ فَحَاقَ بِٱلَّذِينَ سَخِرُواْ مِنۡهُم مَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ
Na Mitume walio kabla yako walikwisha dhihakiwa. Kwa hivyo wale waliowafanyia masikhara yaliwafika yale waliyokuwa wakiyafanyia dhihaka.
Arabic explanations of the Qur’an:
قُلۡ مَن يَكۡلَؤُكُم بِٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِ مِنَ ٱلرَّحۡمَٰنِۚ بَلۡ هُمۡ عَن ذِكۡرِ رَبِّهِم مُّعۡرِضُونَ
Sema: Ni nani anayewalinda usiku na mchana kutokana na Arrahmani (Mwingi wa Rehema)? Bali wao wanapuuza kumkumbuka Mola wao Mlezi.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَمۡ لَهُمۡ ءَالِهَةٞ تَمۡنَعُهُم مِّن دُونِنَاۚ لَا يَسۡتَطِيعُونَ نَصۡرَ أَنفُسِهِمۡ وَلَا هُم مِّنَّا يُصۡحَبُونَ
Au wao wanao miungu watakaoweza kuwakinga kutokana nasi? Hao hawawezi kujinusuru wao wenyewe, wala hawatalindwa kutokana nasi!
Arabic explanations of the Qur’an:
بَلۡ مَتَّعۡنَا هَٰٓؤُلَآءِ وَءَابَآءَهُمۡ حَتَّىٰ طَالَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡعُمُرُۗ أَفَلَا يَرَوۡنَ أَنَّا نَأۡتِي ٱلۡأَرۡضَ نَنقُصُهَا مِنۡ أَطۡرَافِهَآۚ أَفَهُمُ ٱلۡغَٰلِبُونَ
Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka umri ukawa mrefu kwao. Je, hawaoni ya kwamba Sisi tunaijia ardhi tukiipunguza kutokea kwenye ncha zake? Basi je, hao ndio watashinda?
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Surah: Al-Anbiyā’
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center - Translations’ Index

translated by Rowwad Translation Center, in cooperation with the Islamic Propagation Office in Rabwah and the Association for Serving Islamic Content in Languages.

close