Check out the new design

Traducción de los significados del Sagrado Corán - Traducción al suajili - El Centro de Rowad Al- Taryamah * - Índice de traducciones


Traducción de significados Capítulo: Yusef   Versículo:

Yusuf

الٓرۚ تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ
Alif Lam Raa. Hizi ni Aya za Kitabu kinachobainisha.
Las Exégesis Árabes:
إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ قُرۡءَٰنًا عَرَبِيّٗا لَّعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ
Hakika Sisi tumeiteremsha Qur-ani kwa Kiarabu ili mpate kuzingatia.
Las Exégesis Árabes:
نَحۡنُ نَقُصُّ عَلَيۡكَ أَحۡسَنَ ٱلۡقَصَصِ بِمَآ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانَ وَإِن كُنتَ مِن قَبۡلِهِۦ لَمِنَ ٱلۡغَٰفِلِينَ
Sisi tunasimulia simulizi nzuri zaidi kwa kukufunulia Qur-ani hii. Na ijapokuwa kabla ya haya ulikuwa miongoni mwa walioghafilika.
Las Exégesis Árabes:
إِذۡ قَالَ يُوسُفُ لِأَبِيهِ يَٰٓأَبَتِ إِنِّي رَأَيۡتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوۡكَبٗا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ رَأَيۡتُهُمۡ لِي سَٰجِدِينَ
Yusuf alipomwambia baba yake: Ewe baba yangu! Hakika mimi nimeota nyota kumi na moja, na jua, na mwezi. Nimeviota vikinisujudia.
Las Exégesis Árabes:
قَالَ يَٰبُنَيَّ لَا تَقۡصُصۡ رُءۡيَاكَ عَلَىٰٓ إِخۡوَتِكَ فَيَكِيدُواْ لَكَ كَيۡدًاۖ إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ لِلۡإِنسَٰنِ عَدُوّٞ مُّبِينٞ
(Baba) akasema: Ewe mwanangu! Usiwasimulie nduguzo ndoto yako, wakaja kukufanyia njama. Hakika Shetani ni adui aliye dhahiri kwa mwanadamu.
Las Exégesis Árabes:
وَكَذَٰلِكَ يَجۡتَبِيكَ رَبُّكَ وَيُعَلِّمُكَ مِن تَأۡوِيلِ ٱلۡأَحَادِيثِ وَيُتِمُّ نِعۡمَتَهُۥ عَلَيۡكَ وَعَلَىٰٓ ءَالِ يَعۡقُوبَ كَمَآ أَتَمَّهَا عَلَىٰٓ أَبَوَيۡكَ مِن قَبۡلُ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡحَٰقَۚ إِنَّ رَبَّكَ عَلِيمٌ حَكِيمٞ
Na hivyo ndivyo Mola wako Mlezi atakuteua na atakufundisha katika tafsiri ya mambo. Na atatimiza neema zake juu yako na juu ya ukoo wa Yaa'qub, kama alivyowatimizia hapo zamani baba zako Ibrahim na Is-haq. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.
Las Exégesis Árabes:
۞ لَّقَدۡ كَانَ فِي يُوسُفَ وَإِخۡوَتِهِۦٓ ءَايَٰتٞ لِّلسَّآئِلِينَ
Kwa yakini katika Yusuf na nduguze ziko ishara kwa wanaouliza.
Las Exégesis Árabes:
إِذۡ قَالُواْ لَيُوسُفُ وَأَخُوهُ أَحَبُّ إِلَىٰٓ أَبِينَا مِنَّا وَنَحۡنُ عُصۡبَةٌ إِنَّ أَبَانَا لَفِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٍ
Pale waliposema: Hakika Yusuf na nduguye wanapendwa zaidi na baba yetu kuliko sisi, ilhali sisi ni kikundi chenye nguvu. Hakika baba yetu yumo katika upotovu wa dhahiri.
Las Exégesis Árabes:
ٱقۡتُلُواْ يُوسُفَ أَوِ ٱطۡرَحُوهُ أَرۡضٗا يَخۡلُ لَكُمۡ وَجۡهُ أَبِيكُمۡ وَتَكُونُواْ مِنۢ بَعۡدِهِۦ قَوۡمٗا صَٰلِحِينَ
Muueni Yusuf, au mtupeni nchi ya mbali ili uso wa baba yenu uwaelekee nyinyi tu. Na baada ya haya mtakuwa kaumu njema.
Las Exégesis Árabes:
قَالَ قَآئِلٞ مِّنۡهُمۡ لَا تَقۡتُلُواْ يُوسُفَ وَأَلۡقُوهُ فِي غَيَٰبَتِ ٱلۡجُبِّ يَلۡتَقِطۡهُ بَعۡضُ ٱلسَّيَّارَةِ إِن كُنتُمۡ فَٰعِلِينَ
Akasema msemaji miongoni mwao: Msimuue Yusuf. Lakini mtumbukizeni ndani ya kisima. Baadhi ya wasafiri watakuja mwokota; ikiwa kweli mnataka kufanya.
Las Exégesis Árabes:
قَالُواْ يَٰٓأَبَانَا مَا لَكَ لَا تَأۡمَ۬نَّا عَلَىٰ يُوسُفَ وَإِنَّا لَهُۥ لَنَٰصِحُونَ
Wakasema: Ewe baba yetu! Una nini hata hutuamini kwa Yusuf? Na hakika sisi ni wenye kumtakia heri!
Las Exégesis Árabes:
أَرۡسِلۡهُ مَعَنَا غَدٗا يَرۡتَعۡ وَيَلۡعَبۡ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَٰفِظُونَ
Muachilie kesho pamoja nasi, ale kwa furaha na acheze, na bila ya shaka sisi tutamhifadhi.
Las Exégesis Árabes:
قَالَ إِنِّي لَيَحۡزُنُنِيٓ أَن تَذۡهَبُواْ بِهِۦ وَأَخَافُ أَن يَأۡكُلَهُ ٱلذِّئۡبُ وَأَنتُمۡ عَنۡهُ غَٰفِلُونَ
Akasema: Kwa hakika inanihuzunisha kwamba nyinyi mwende naye, na ninahofia aje mbwa mwitu akamla ilhali nyinyi mmeghafilika naye.
Las Exégesis Árabes:
قَالُواْ لَئِنۡ أَكَلَهُ ٱلذِّئۡبُ وَنَحۡنُ عُصۡبَةٌ إِنَّآ إِذٗا لَّخَٰسِرُونَ
Wakasema: Ikiwa mbwa mwitu atamla na ilhali sisi ni kundi lenye nguvu kabisa, basi bila ya shaka sisi tutakuwa tumehasirika.
Las Exégesis Árabes:
فَلَمَّا ذَهَبُواْ بِهِۦ وَأَجۡمَعُوٓاْ أَن يَجۡعَلُوهُ فِي غَيَٰبَتِ ٱلۡجُبِّۚ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡهِ لَتُنَبِّئَنَّهُم بِأَمۡرِهِمۡ هَٰذَا وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ
Basi walipokwenda naye, na wakakubaliana kwamba wamtumbukize ndani ya kisima, tulimfunulia Yusuf: Hakika utakuja waambia jambo lao hili, na wala wao hawatambui.
Las Exégesis Árabes:
وَجَآءُوٓ أَبَاهُمۡ عِشَآءٗ يَبۡكُونَ
Wakamjia baba yao usiku wakilia.
Las Exégesis Árabes:
قَالُواْ يَٰٓأَبَانَآ إِنَّا ذَهَبۡنَا نَسۡتَبِقُ وَتَرَكۡنَا يُوسُفَ عِندَ مَتَٰعِنَا فَأَكَلَهُ ٱلذِّئۡبُۖ وَمَآ أَنتَ بِمُؤۡمِنٖ لَّنَا وَلَوۡ كُنَّا صَٰدِقِينَ
Wakasema: Ewe baba yetu! Hakika tulikwenda kushindana na tukamwacha Yusuf penye vitu vyetu. Basi mbwa mwitu akamla. Lakini wewe hutuamini ijapokuwa sisi ni wakweli.
Las Exégesis Árabes:
وَجَآءُو عَلَىٰ قَمِيصِهِۦ بِدَمٖ كَذِبٖۚ قَالَ بَلۡ سَوَّلَتۡ لَكُمۡ أَنفُسُكُمۡ أَمۡرٗاۖ فَصَبۡرٞ جَمِيلٞۖ وَٱللَّهُ ٱلۡمُسۡتَعَانُ عَلَىٰ مَا تَصِفُونَ
Na walikuja na shati lake likiwa lina damu ya uongo. Akasema: Bali nafsi zenu zimewashawishi kutenda kitendo. Lakini subira ni njema; na Mwenyezi Mungu ndiye wa kuombwa msaada kwa haya mnayoyaeleza.
Las Exégesis Árabes:
وَجَآءَتۡ سَيَّارَةٞ فَأَرۡسَلُواْ وَارِدَهُمۡ فَأَدۡلَىٰ دَلۡوَهُۥۖ قَالَ يَٰبُشۡرَىٰ هَٰذَا غُلَٰمٞۚ وَأَسَرُّوهُ بِضَٰعَةٗۚ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِمَا يَعۡمَلُونَ
Na ukaja msafara, kisha wakamtuma mchota maji wao, naye akatumbukiza ndoo yake. Alisema: Hii ni bishara njema! Huyu hapa mvulana! Wakamficha ili kumfanya ni bidhaa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema hayo wanayoyatenda.
Las Exégesis Árabes:
وَشَرَوۡهُ بِثَمَنِۭ بَخۡسٖ دَرَٰهِمَ مَعۡدُودَةٖ وَكَانُواْ فِيهِ مِنَ ٱلزَّٰهِدِينَ
Na wakamuuza kwa thamani duni, dirhamu za kuhesabika tu. Wala hawakuwa na haja naye.
Las Exégesis Árabes:
وَقَالَ ٱلَّذِي ٱشۡتَرَىٰهُ مِن مِّصۡرَ لِٱمۡرَأَتِهِۦٓ أَكۡرِمِي مَثۡوَىٰهُ عَسَىٰٓ أَن يَنفَعَنَآ أَوۡ نَتَّخِذَهُۥ وَلَدٗاۚ وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلِنُعَلِّمَهُۥ مِن تَأۡوِيلِ ٱلۡأَحَادِيثِۚ وَٱللَّهُ غَالِبٌ عَلَىٰٓ أَمۡرِهِۦ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ
Na yule aliyemnunua huko Misri alimwambia mkewe: Mtengenezee makazi ya heshima huyu; huenda akatufaa au tukamfanya mwanetu. Basi hivyo ndivyo tulivyomuweka Yusuf imara katika ardhi ili tumfundishe kufasiri mambo. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini wengi wa watu hawajui.
Las Exégesis Árabes:
وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُۥٓ ءَاتَيۡنَٰهُ حُكۡمٗا وَعِلۡمٗاۚ وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Na alipofikia utu uzima wake, tukampa hukumu na elimu. Na hivyo ndivyo tunavyowalipa watendao mazuri.
Las Exégesis Árabes:
وَرَٰوَدَتۡهُ ٱلَّتِي هُوَ فِي بَيۡتِهَا عَن نَّفۡسِهِۦ وَغَلَّقَتِ ٱلۡأَبۡوَٰبَ وَقَالَتۡ هَيۡتَ لَكَۚ قَالَ مَعَاذَ ٱللَّهِۖ إِنَّهُۥ رَبِّيٓ أَحۡسَنَ مَثۡوَايَۖ إِنَّهُۥ لَا يُفۡلِحُ ٱلظَّٰلِمُونَ
Na yule bibi wa nyumba aliyokuwamo Yusuf akamtamani kinyume cha nafsi yake, na akafungafunga milango. Akamwambia: Njoo! Yusuf akasema: Audhubillahi (Najikinga na Mwenyezi Mungu!). Hakika Yeye ni Bwana wangu, aliniweka maskani nzuri, na hakika madhalimu hawafaulu.
Las Exégesis Árabes:
وَلَقَدۡ هَمَّتۡ بِهِۦۖ وَهَمَّ بِهَا لَوۡلَآ أَن رَّءَا بُرۡهَٰنَ رَبِّهِۦۚ كَذَٰلِكَ لِنَصۡرِفَ عَنۡهُ ٱلسُّوٓءَ وَٱلۡفَحۡشَآءَۚ إِنَّهُۥ مِنۡ عِبَادِنَا ٱلۡمُخۡلَصِينَ
Na hakika yule mwanamke alimtamani, na Yusuf angelimtamani lau kuwa hakuona ishara ya Mola wake Mlezi. Ilikuwa hivyo, ili tumuepushie mabaya na uchafu. Hakika yeye alikuwa katika waja wetu walioteuliwa.
Las Exégesis Árabes:
وَٱسۡتَبَقَا ٱلۡبَابَ وَقَدَّتۡ قَمِيصَهُۥ مِن دُبُرٖ وَأَلۡفَيَا سَيِّدَهَا لَدَا ٱلۡبَابِۚ قَالَتۡ مَا جَزَآءُ مَنۡ أَرَادَ بِأَهۡلِكَ سُوٓءًا إِلَّآ أَن يُسۡجَنَ أَوۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ
Na wote wawili wakakimbilia mlangoni, na mwanamke akalirarua shati lake Yusuf kwa nyuma. Na wakamkuta bwana wake mlangoni. Mwanamke akasema: Hakuna malipo ya mwenye kutaka kumfanyia mabaya mkeo isipokuwa afungwe au kupewa adhabu chungu.
Las Exégesis Árabes:
قَالَ هِيَ رَٰوَدَتۡنِي عَن نَّفۡسِيۚ وَشَهِدَ شَاهِدٞ مِّنۡ أَهۡلِهَآ إِن كَانَ قَمِيصُهُۥ قُدَّ مِن قُبُلٖ فَصَدَقَتۡ وَهُوَ مِنَ ٱلۡكَٰذِبِينَ
Yusuf akasema: Yeye ndiye aliyenitaka bila ya mimi kumtaka. Na shahidi aliyekuwa katika jamaa za mwanamke akasema: Ikiwa shati lake limechanwa kwa mbele, basi mwanamke amesema kweli, naye Yusuf ni katika waongo.
Las Exégesis Árabes:
وَإِن كَانَ قَمِيصُهُۥ قُدَّ مِن دُبُرٖ فَكَذَبَتۡ وَهُوَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ
Na ikiwa shati lake limechanwa kwa nyuma, basi mwanamke amesema uongo, naye Yusuf ni katika wakweli.
Las Exégesis Árabes:
فَلَمَّا رَءَا قَمِيصَهُۥ قُدَّ مِن دُبُرٖ قَالَ إِنَّهُۥ مِن كَيۡدِكُنَّۖ إِنَّ كَيۡدَكُنَّ عَظِيمٞ
Basi yule bwana alipoona shati lake limechanwa kwa nyuma, akasema: Hakika haya ni katika vitimbi vyenu wanawake. Hakika vitimbi vyenu ni vikuu.
Las Exégesis Árabes:
يُوسُفُ أَعۡرِضۡ عَنۡ هَٰذَاۚ وَٱسۡتَغۡفِرِي لِذَنۢبِكِۖ إِنَّكِ كُنتِ مِنَ ٱلۡخَاطِـِٔينَ
Yusuf! Achilia mbali haya. Na wewe, mwanamke, omba msamaha kwa dhambi zako. Hakika wewe ni katika waliofanya makosa.
Las Exégesis Árabes:
۞ وَقَالَ نِسۡوَةٞ فِي ٱلۡمَدِينَةِ ٱمۡرَأَتُ ٱلۡعَزِيزِ تُرَٰوِدُ فَتَىٰهَا عَن نَّفۡسِهِۦۖ قَدۡ شَغَفَهَا حُبًّاۖ إِنَّا لَنَرَىٰهَا فِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ
Na wanawake wa mjini wakawa wanasema: Mke wa Mheshimiwa anamtamani mtumishi wake bila ya yeye kumtaka! Hakika mapenzi yamemuingia sana moyoni. Sisi hakika tunamwona yumo katika upotovu ulio dhahiri.
Las Exégesis Árabes:
فَلَمَّا سَمِعَتۡ بِمَكۡرِهِنَّ أَرۡسَلَتۡ إِلَيۡهِنَّ وَأَعۡتَدَتۡ لَهُنَّ مُتَّكَـٔٗا وَءَاتَتۡ كُلَّ وَٰحِدَةٖ مِّنۡهُنَّ سِكِّينٗا وَقَالَتِ ٱخۡرُجۡ عَلَيۡهِنَّۖ فَلَمَّا رَأَيۡنَهُۥٓ أَكۡبَرۡنَهُۥ وَقَطَّعۡنَ أَيۡدِيَهُنَّ وَقُلۡنَ حَٰشَ لِلَّهِ مَا هَٰذَا بَشَرًا إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا مَلَكٞ كَرِيمٞ
Basi aliposikia yule bibi masengenyo yao, aliwaita, na akawawekea matakia ya kuegemea, na akampa kila mmoja wao kisu. Akamwambia Yusuf: Tokeza mbele yao. Basi walipomwona, waliona ni kitu kikubwa kabisa, na wakajikatakata mikono yao. Wakasema: Hasha Lillahi! Huyu si mwanadamu. Huyu si isipokuwa Malaika mtukufu.
Las Exégesis Árabes:
قَالَتۡ فَذَٰلِكُنَّ ٱلَّذِي لُمۡتُنَّنِي فِيهِۖ وَلَقَدۡ رَٰوَدتُّهُۥ عَن نَّفۡسِهِۦ فَٱسۡتَعۡصَمَۖ وَلَئِن لَّمۡ يَفۡعَلۡ مَآ ءَامُرُهُۥ لَيُسۡجَنَنَّ وَلَيَكُونٗا مِّنَ ٱلصَّٰغِرِينَ
Yule bibi akasema: Huyu basi ndiye huyo mliyenilaumia! Na kweli mimi nilimtaka naye akakataa. Na asipofanya ninayomwamrisha, basi hapana shaka atafungwa gerezani, na atakuwa miongoni mwa walio duni kabisa.
Las Exégesis Árabes:
قَالَ رَبِّ ٱلسِّجۡنُ أَحَبُّ إِلَيَّ مِمَّا يَدۡعُونَنِيٓ إِلَيۡهِۖ وَإِلَّا تَصۡرِفۡ عَنِّي كَيۡدَهُنَّ أَصۡبُ إِلَيۡهِنَّ وَأَكُن مِّنَ ٱلۡجَٰهِلِينَ
Yusuf akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Ninapendelea kifungo kuliko haya anayoniitia. Na usiponiondoshea vitimbi vya wanawake, mimi nitaelekea kwao, na nitakuwa katika wajinga.
Las Exégesis Árabes:
فَٱسۡتَجَابَ لَهُۥ رَبُّهُۥ فَصَرَفَ عَنۡهُ كَيۡدَهُنَّۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ
Basi Mola wake Mlezi akamwitikia, na akamwondoshea vitimbi vyao. Hakika Yeye ni Msikizi, Mwenye kujua vyema.
Las Exégesis Árabes:
ثُمَّ بَدَا لَهُم مِّنۢ بَعۡدِ مَا رَأَوُاْ ٱلۡأٓيَٰتِ لَيَسۡجُنُنَّهُۥ حَتَّىٰ حِينٖ
Kisha ikawadhihirikia baada ya kuona Ishara kuwa lazima wamfunge kwa muda.
Las Exégesis Árabes:
وَدَخَلَ مَعَهُ ٱلسِّجۡنَ فَتَيَانِۖ قَالَ أَحَدُهُمَآ إِنِّيٓ أَرَىٰنِيٓ أَعۡصِرُ خَمۡرٗاۖ وَقَالَ ٱلۡأٓخَرُ إِنِّيٓ أَرَىٰنِيٓ أَحۡمِلُ فَوۡقَ رَأۡسِي خُبۡزٗا تَأۡكُلُ ٱلطَّيۡرُ مِنۡهُۖ نَبِّئۡنَا بِتَأۡوِيلِهِۦٓۖ إِنَّا نَرَىٰكَ مِنَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Na wakaingia gerezani pamoja naye vijana wawili. Mmoja wao akasema: Hakika mimi nimeota kuwa ninakamua mvinyo. Na mwingine akasema: Hakika mimi nimeota kuwa nimebeba mikate juu ya kichwa changu, na ndege wanakula kwayo. Hebu tuambie tafsiri yake, kwani sisi tunakuona wewe ni katika watu wazuri.
Las Exégesis Árabes:
قَالَ لَا يَأۡتِيكُمَا طَعَامٞ تُرۡزَقَانِهِۦٓ إِلَّا نَبَّأۡتُكُمَا بِتَأۡوِيلِهِۦ قَبۡلَ أَن يَأۡتِيَكُمَاۚ ذَٰلِكُمَا مِمَّا عَلَّمَنِي رَبِّيٓۚ إِنِّي تَرَكۡتُ مِلَّةَ قَوۡمٖ لَّا يُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَهُم بِٱلۡأٓخِرَةِ هُمۡ كَٰفِرُونَ
Akasema: hakitawajia chakula mtakachoruzukiwa isipokuwa nitawaambia hakika yake kabla ya kuwajia. Hayo ni katika yale aliyonifundisha Mola wangu Mlezi. Hakika mimi nimeacha mila ya kaumu wasiomuamini Mwenyezi Mungu, na wakawa wameikufuru Akhera.
Las Exégesis Árabes:
وَٱتَّبَعۡتُ مِلَّةَ ءَابَآءِيٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَۚ مَا كَانَ لَنَآ أَن نُّشۡرِكَ بِٱللَّهِ مِن شَيۡءٖۚ ذَٰلِكَ مِن فَضۡلِ ٱللَّهِ عَلَيۡنَا وَعَلَى ٱلنَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَشۡكُرُونَ
Na nimefuata mila ya baba zangu, Ibrahim, na Is-haq, na Yaa'qub. Haikutufailia sisi kumshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote. Hiyo ni katika fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yetu na juu ya watu, lakini wengi wa watu hawashukuru.
Las Exégesis Árabes:
يَٰصَٰحِبَيِ ٱلسِّجۡنِ ءَأَرۡبَابٞ مُّتَفَرِّقُونَ خَيۡرٌ أَمِ ٱللَّهُ ٱلۡوَٰحِدُ ٱلۡقَهَّارُ
Enyi wafungwa wenzangu wawili! Je, mabwana wengi tofautitofauti ni bora au Mwenyezi Mungu Mmoja Mwenye nguvu?
Las Exégesis Árabes:
مَا تَعۡبُدُونَ مِن دُونِهِۦٓ إِلَّآ أَسۡمَآءٗ سَمَّيۡتُمُوهَآ أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلۡطَٰنٍۚ إِنِ ٱلۡحُكۡمُ إِلَّا لِلَّهِ أَمَرَ أَلَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّآ إِيَّاهُۚ ذَٰلِكَ ٱلدِّينُ ٱلۡقَيِّمُ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ
Hamuabudu badala yake isipokuwa majina tu mliyowaita nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuyateremshia hayo uthibitisho wowote. Hakuna hukumu isipokuwa ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipokuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo Dini iliyonyooka. Lakini wengi wa watu hawajui.
Las Exégesis Árabes:
يَٰصَٰحِبَيِ ٱلسِّجۡنِ أَمَّآ أَحَدُكُمَا فَيَسۡقِي رَبَّهُۥ خَمۡرٗاۖ وَأَمَّا ٱلۡأٓخَرُ فَيُصۡلَبُ فَتَأۡكُلُ ٱلطَّيۡرُ مِن رَّأۡسِهِۦۚ قُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ ٱلَّذِي فِيهِ تَسۡتَفۡتِيَانِ
Enyi wafungwa wenzangu wawili! Ama mmoja wenu, yeye atamnywesha bwana wake mvinyo. Na ama mwengine, yeye atasulubiwa, na ndege watakula katika kichwa chake. Imekwisha katwa hukumu ya hilo jambo mlilokuwa mkiuliza.
Las Exégesis Árabes:
وَقَالَ لِلَّذِي ظَنَّ أَنَّهُۥ نَاجٖ مِّنۡهُمَا ٱذۡكُرۡنِي عِندَ رَبِّكَ فَأَنسَىٰهُ ٱلشَّيۡطَٰنُ ذِكۡرَ رَبِّهِۦ فَلَبِثَ فِي ٱلسِّجۡنِ بِضۡعَ سِنِينَ
Na akamwambia yule aliyejua kuwa ataokoka katika wawili hao: Nikumbuke kwa bwana wako. Lakini Shetani alimsahaulisha kumtaja kwa bwana wake. Basi Yusuf akakaa gerezani miaka kadhaa.
Las Exégesis Árabes:
وَقَالَ ٱلۡمَلِكُ إِنِّيٓ أَرَىٰ سَبۡعَ بَقَرَٰتٖ سِمَانٖ يَأۡكُلُهُنَّ سَبۡعٌ عِجَافٞ وَسَبۡعَ سُنۢبُلَٰتٍ خُضۡرٖ وَأُخَرَ يَابِسَٰتٖۖ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡمَلَأُ أَفۡتُونِي فِي رُءۡيَٰيَ إِن كُنتُمۡ لِلرُّءۡيَا تَعۡبُرُونَ
Na siku moja mfalme alisema: Hakika mimi nimeota ng'ombe saba wanene wanaliwa na ng'ombe saba waliokonda. Na mashuke saba mabichi na mengine makavu. Enyi waheshimiwa! Niambieni maana ya ndoto zangu, ikiwa nyinyi mnaweza kuagua ndoto.
Las Exégesis Árabes:
قَالُوٓاْ أَضۡغَٰثُ أَحۡلَٰمٖۖ وَمَا نَحۡنُ بِتَأۡوِيلِ ٱلۡأَحۡلَٰمِ بِعَٰلِمِينَ
Wakasema: Hizi ni ndoto zilizoparaganyika, wala sisi sio wenye kujua tafsiri ya ndoto hizi.
Las Exégesis Árabes:
وَقَالَ ٱلَّذِي نَجَا مِنۡهُمَا وَٱدَّكَرَ بَعۡدَ أُمَّةٍ أَنَا۠ أُنَبِّئُكُم بِتَأۡوِيلِهِۦ فَأَرۡسِلُونِ
Hapo akasema yule aliyeokoka katika wale wawili na akakumbuka baada ya muda. Mimi nitawaambia tafsiri yake. Basi nitumeni.
Las Exégesis Árabes:
يُوسُفُ أَيُّهَا ٱلصِّدِّيقُ أَفۡتِنَا فِي سَبۡعِ بَقَرَٰتٖ سِمَانٖ يَأۡكُلُهُنَّ سَبۡعٌ عِجَافٞ وَسَبۡعِ سُنۢبُلَٰتٍ خُضۡرٖ وَأُخَرَ يَابِسَٰتٖ لَّعَلِّيٓ أَرۡجِعُ إِلَى ٱلنَّاسِ لَعَلَّهُمۡ يَعۡلَمُونَ
Yusuf! Ewe mkweli! Tueleze ni nini maana ya ng'ombe saba wanene kuliwa na ng'ombe saba waliokonda. Na mashuke saba mabichi na mengine makavu, ili nirejee kwa watu ili wapate kujua.
Las Exégesis Árabes:
قَالَ تَزۡرَعُونَ سَبۡعَ سِنِينَ دَأَبٗا فَمَا حَصَدتُّمۡ فَذَرُوهُ فِي سُنۢبُلِهِۦٓ إِلَّا قَلِيلٗا مِّمَّا تَأۡكُلُونَ
Akasema: Mtalima miaka saba kwa juhudi. Kwa hivyo mtakachovuna, kiwacheni katika mashuke yake, isipokuwa kidogo mtachokula kwacho.
Las Exégesis Árabes:
ثُمَّ يَأۡتِي مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ سَبۡعٞ شِدَادٞ يَأۡكُلۡنَ مَا قَدَّمۡتُمۡ لَهُنَّ إِلَّا قَلِيلٗا مِّمَّا تُحۡصِنُونَ
Kisha itakuja baadaye miaka saba ya shida itakayokula kile mlichoiwekea isipokuwa kidogo katika kile mtakachokihifadhi.
Las Exégesis Árabes:
ثُمَّ يَأۡتِي مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ عَامٞ فِيهِ يُغَاثُ ٱلنَّاسُ وَفِيهِ يَعۡصِرُونَ
Kisha baada ya haya utakuja mwaka ambao katika mwaka huo watu watasaidiwa, na watakamua.
Las Exégesis Árabes:
وَقَالَ ٱلۡمَلِكُ ٱئۡتُونِي بِهِۦۖ فَلَمَّا جَآءَهُ ٱلرَّسُولُ قَالَ ٱرۡجِعۡ إِلَىٰ رَبِّكَ فَسۡـَٔلۡهُ مَا بَالُ ٱلنِّسۡوَةِ ٱلَّٰتِي قَطَّعۡنَ أَيۡدِيَهُنَّۚ إِنَّ رَبِّي بِكَيۡدِهِنَّ عَلِيمٞ
Na mfalme akasema: Nijieni naye! Basi mjumbe huyo alipomjia, Yusuf akasema: Rudi kwa bwana wako na umuulize wana nini wale wanawake waliojikatakata mikono yao. Hakika Mola wangu Mlezi anazijua vyema njama zao.
Las Exégesis Árabes:
قَالَ مَا خَطۡبُكُنَّ إِذۡ رَٰوَدتُّنَّ يُوسُفَ عَن نَّفۡسِهِۦۚ قُلۡنَ حَٰشَ لِلَّهِ مَا عَلِمۡنَا عَلَيۡهِ مِن سُوٓءٖۚ قَالَتِ ٱمۡرَأَتُ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡـَٰٔنَ حَصۡحَصَ ٱلۡحَقُّ أَنَا۠ رَٰوَدتُّهُۥ عَن نَّفۡسِهِۦ وَإِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ
Mfalme alisema: Mlikuwa mna nini mlipomtaka Yusuf kinyume na nafsi yake? Wakasema: Hasha Lillahi (Mwenyezi Mungu apishe mbali!) Sisi hatukujua ubaya wowote kwake. Mke wa Mheshimiwa yule akasema: Sasa haki imedhihiri. Mimi ndiye niliyemtaka kinyume na nafsi yake, na hakika yeye ni katika wakweli.
Las Exégesis Árabes:
ذَٰلِكَ لِيَعۡلَمَ أَنِّي لَمۡ أَخُنۡهُ بِٱلۡغَيۡبِ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي كَيۡدَ ٱلۡخَآئِنِينَ
Hayo ni ili ajue ya kwamba sikumfanyia hiyana alipokuwa hayupo, na ya kwamba Mwenyezi Mungu haziongoi njama za wahaini.
Las Exégesis Árabes:
۞ وَمَآ أُبَرِّئُ نَفۡسِيٓۚ إِنَّ ٱلنَّفۡسَ لَأَمَّارَةُۢ بِٱلسُّوٓءِ إِلَّا مَا رَحِمَ رَبِّيٓۚ إِنَّ رَبِّي غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Nami sijitoi lawamani. Kwa hakika nafsi ni yenye kuamrisha mno mabaya, isipokuwa kile alichorehemu Mola wangu Mlezi. Hakika Mola wangu Mlezi ni Msamehevu mno, Mwenye kurehemu sana.
Las Exégesis Árabes:
وَقَالَ ٱلۡمَلِكُ ٱئۡتُونِي بِهِۦٓ أَسۡتَخۡلِصۡهُ لِنَفۡسِيۖ فَلَمَّا كَلَّمَهُۥ قَالَ إِنَّكَ ٱلۡيَوۡمَ لَدَيۡنَا مَكِينٌ أَمِينٞ
Basi mfalme akasema, "Nijieni naye, awe wangu mwenyewe hasa." Basi alipomsemesha, akasema, "Hakika wewe leo umekwisha kuwa imara kwetu na umeaminika."
Las Exégesis Árabes:
قَالَ ٱجۡعَلۡنِي عَلَىٰ خَزَآئِنِ ٱلۡأَرۡضِۖ إِنِّي حَفِيظٌ عَلِيمٞ
Yusuf akasema: Nifanye msimamizi wa hazina za nchi. Kwani hakika mimi ni mlinzi mzuri, mwenye elimu sana.
Las Exégesis Árabes:
وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي ٱلۡأَرۡضِ يَتَبَوَّأُ مِنۡهَا حَيۡثُ يَشَآءُۚ نُصِيبُ بِرَحۡمَتِنَا مَن نَّشَآءُۖ وَلَا نُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Basi hivyo ndivyo tulivyomuimarisha Yusuf katika ardhi, akawa anakaa humo popote anapotaka. Tunamfikishia rehema zetu tumtakaye, wala hatupotezi malipo ya wafanyao mazuri.
Las Exégesis Árabes:
وَلَأَجۡرُ ٱلۡأٓخِرَةِ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَكَانُواْ يَتَّقُونَ
Na hakika malipo ya Akhera ni bora zaidi, kwa wale walioamini na wakawa wanamcha Mungu.
Las Exégesis Árabes:
وَجَآءَ إِخۡوَةُ يُوسُفَ فَدَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَعَرَفَهُمۡ وَهُمۡ لَهُۥ مُنكِرُونَ
Wakaja ndugu zake Yusuf, na wakaingia alimokuwa. Yeye akawajua, na wao hawakumjua.
Las Exégesis Árabes:
وَلَمَّا جَهَّزَهُم بِجَهَازِهِمۡ قَالَ ٱئۡتُونِي بِأَخٖ لَّكُم مِّنۡ أَبِيكُمۡۚ أَلَا تَرَوۡنَ أَنِّيٓ أُوفِي ٱلۡكَيۡلَ وَأَنَا۠ خَيۡرُ ٱلۡمُنزِلِينَ
Na alipowatengenezea tayari haja yao, alisema: Nileteeni ndugu yenu wa kwa baba yenu. Je, hamuoni ya kwamba mimi hakika ninatimiza kipimo, nami ni mbora wa wanaokirimu?
Las Exégesis Árabes:
فَإِن لَّمۡ تَأۡتُونِي بِهِۦ فَلَا كَيۡلَ لَكُمۡ عِندِي وَلَا تَقۡرَبُونِ
Na msiponijia naye, basi hamtapata kipimo chochote kwangu, wala msinikaribie.
Las Exégesis Árabes:
قَالُواْ سَنُرَٰوِدُ عَنۡهُ أَبَاهُ وَإِنَّا لَفَٰعِلُونَ
Wakasema: Sisi tutamrai baba yake juu yake, na bila ya shaka tutafanya hilo.
Las Exégesis Árabes:
وَقَالَ لِفِتۡيَٰنِهِ ٱجۡعَلُواْ بِضَٰعَتَهُمۡ فِي رِحَالِهِمۡ لَعَلَّهُمۡ يَعۡرِفُونَهَآ إِذَا ٱنقَلَبُوٓاْ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِمۡ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ
Na Yusuf akawaambia watumishi wake: Tieni bidhaa zao katika mizigo yao, ili wazione watakaporudi kwa watu wao ili wapate kurejea tena.
Las Exégesis Árabes:
فَلَمَّا رَجَعُوٓاْ إِلَىٰٓ أَبِيهِمۡ قَالُواْ يَٰٓأَبَانَا مُنِعَ مِنَّا ٱلۡكَيۡلُ فَأَرۡسِلۡ مَعَنَآ أَخَانَا نَكۡتَلۡ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَٰفِظُونَ
Basi waliporejea kwa baba yao, walisema: Ewe baba yetu! Tumenyimwa chakula zaidi. Basi muachilie ndugu yetu pamoja nasi ili tupate kupimiwa. Nasi hakika tutamlinda.
Las Exégesis Árabes:
قَالَ هَلۡ ءَامَنُكُمۡ عَلَيۡهِ إِلَّا كَمَآ أَمِنتُكُمۡ عَلَىٰٓ أَخِيهِ مِن قَبۡلُ فَٱللَّهُ خَيۡرٌ حَٰفِظٗاۖ وَهُوَ أَرۡحَمُ ٱلرَّٰحِمِينَ
Je, niwaamini juu yake isipokuwa kama nilivyowaamini kwa nduguye zamani? Lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mbora zaidi wa kulinda, naye ndiye Mbora zaidi wa wanaorehemu.
Las Exégesis Árabes:
وَلَمَّا فَتَحُواْ مَتَٰعَهُمۡ وَجَدُواْ بِضَٰعَتَهُمۡ رُدَّتۡ إِلَيۡهِمۡۖ قَالُواْ يَٰٓأَبَانَا مَا نَبۡغِيۖ هَٰذِهِۦ بِضَٰعَتُنَا رُدَّتۡ إِلَيۡنَاۖ وَنَمِيرُ أَهۡلَنَا وَنَحۡفَظُ أَخَانَا وَنَزۡدَادُ كَيۡلَ بَعِيرٖۖ ذَٰلِكَ كَيۡلٞ يَسِيرٞ
Na walipofungua mizigo yao, wakakuta bidhaa zao wamerudishiwa. Wakasema: Ewe baba yetu! Tutake nini zaidi? Hizi bidhaa zetu tumerudishiwa. Wacha tuwaletee watu wetu chakula, na tutamlinda ndugu yetu, na tutaongeza shehena ya ngamia. Na hicho ni kipimo kidogo.
Las Exégesis Árabes:
قَالَ لَنۡ أُرۡسِلَهُۥ مَعَكُمۡ حَتَّىٰ تُؤۡتُونِ مَوۡثِقٗا مِّنَ ٱللَّهِ لَتَأۡتُنَّنِي بِهِۦٓ إِلَّآ أَن يُحَاطَ بِكُمۡۖ فَلَمَّآ ءَاتَوۡهُ مَوۡثِقَهُمۡ قَالَ ٱللَّهُ عَلَىٰ مَا نَقُولُ وَكِيلٞ
Akasema: Sitamuachilia pamoja nanyi mpaka mnipe agano kwa Mwenyezi Mungu kwamba lazima mtanijia naye isipokuwa ikiwa mtazungukwa. Basi walipompa agano yao, alisema: Mwenyezi Mungu ndiye Mtegemewa kwa tuyasemayo.
Las Exégesis Árabes:
وَقَالَ يَٰبَنِيَّ لَا تَدۡخُلُواْ مِنۢ بَابٖ وَٰحِدٖ وَٱدۡخُلُواْ مِنۡ أَبۡوَٰبٖ مُّتَفَرِّقَةٖۖ وَمَآ أُغۡنِي عَنكُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٍۖ إِنِ ٱلۡحُكۡمُ إِلَّا لِلَّهِۖ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُۖ وَعَلَيۡهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُتَوَكِّلُونَ
Na akasema: Enyi wanangu! Msiingie kupitia mlango mmoja, bali ingieni kwa kupitia milango tofautitofauti. Wala mimi siwafai kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Hukumu haiko isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu tu. Juu yake Yeye mimi nimetegemea, na juu yake Yeye na wategemee wanaotegemea.
Las Exégesis Árabes:
وَلَمَّا دَخَلُواْ مِنۡ حَيۡثُ أَمَرَهُمۡ أَبُوهُم مَّا كَانَ يُغۡنِي عَنۡهُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٍ إِلَّا حَاجَةٗ فِي نَفۡسِ يَعۡقُوبَ قَضَىٰهَاۚ وَإِنَّهُۥ لَذُو عِلۡمٖ لِّمَا عَلَّمۡنَٰهُ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ
Na walipoingilia pale alipowaamrisha baba yao, hakuwa wa kuwafaa kitu kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa ni haja tu iliyokuwa katika nafsi ya Yaa'qub aliyoitimiza. Na hakika yeye alikuwa na elimu kwa sababu tulimfundisha, lakini wengi wa watu hawajui.
Las Exégesis Árabes:
وَلَمَّا دَخَلُواْ عَلَىٰ يُوسُفَ ءَاوَىٰٓ إِلَيۡهِ أَخَاهُۖ قَالَ إِنِّيٓ أَنَا۠ أَخُوكَ فَلَا تَبۡتَئِسۡ بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Na walipoingia alimokuwa Yusuf, alimkumbatia nduguye na akasema: Mimi hakika ndiye yule nduguyo. Basi usihuzunike kwa yale waliyokuwa wakiyafanya.
Las Exégesis Árabes:
فَلَمَّا جَهَّزَهُم بِجَهَازِهِمۡ جَعَلَ ٱلسِّقَايَةَ فِي رَحۡلِ أَخِيهِ ثُمَّ أَذَّنَ مُؤَذِّنٌ أَيَّتُهَا ٱلۡعِيرُ إِنَّكُمۡ لَسَٰرِقُونَ
Na alipokwisha watayarishia mahitaji yao, akakitia kikopo cha kunywea maji katika mzigo wa nduguye huyo, kisha mwenye kunadi akanadi: Enyi msafara! Hakika nyinyi ni wezi!
Las Exégesis Árabes:
قَالُواْ وَأَقۡبَلُواْ عَلَيۡهِم مَّاذَا تَفۡقِدُونَ
Wakasema huku wamegeuka kuwaelekea, “Kwani mmepoteza nini?”
Las Exégesis Árabes:
قَالُواْ نَفۡقِدُ صُوَاعَ ٱلۡمَلِكِ وَلِمَن جَآءَ بِهِۦ حِمۡلُ بَعِيرٖ وَأَنَا۠ بِهِۦ زَعِيمٞ
Wakasema: Tumepoteza kopo la mfalme. Na atakayenijia nalo, atapewa shehena nzima abebayo ngamia. Nami ni mdhamini juu ya hilo.
Las Exégesis Árabes:
قَالُواْ تَٱللَّهِ لَقَدۡ عَلِمۡتُم مَّا جِئۡنَا لِنُفۡسِدَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا كُنَّا سَٰرِقِينَ
Wakasema: Tallahi! Hakika mlikwisha jua vyema kwamba sisi hatukuja kufanya uharibifu katika nchi hii, wala sisi si wezi.
Las Exégesis Árabes:
قَالُواْ فَمَا جَزَٰٓؤُهُۥٓ إِن كُنتُمۡ كَٰذِبِينَ
Wakasema: Basi malipo yake ni nini ikiwa nyinyi ni waongo?
Las Exégesis Árabes:
قَالُواْ جَزَٰٓؤُهُۥ مَن وُجِدَ فِي رَحۡلِهِۦ فَهُوَ جَزَٰٓؤُهُۥۚ كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلظَّٰلِمِينَ
Wakasema: Malipo yake ni kwamba yule ambaye litapatikana katika shehena naye, basi huyo ndiye malipo yake. Hivyo ndivyo tunavyowalipa madhalimu.
Las Exégesis Árabes:
فَبَدَأَ بِأَوۡعِيَتِهِمۡ قَبۡلَ وِعَآءِ أَخِيهِ ثُمَّ ٱسۡتَخۡرَجَهَا مِن وِعَآءِ أَخِيهِۚ كَذَٰلِكَ كِدۡنَا لِيُوسُفَۖ مَا كَانَ لِيَأۡخُذَ أَخَاهُ فِي دِينِ ٱلۡمَلِكِ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُۚ نَرۡفَعُ دَرَجَٰتٖ مَّن نَّشَآءُۗ وَفَوۡقَ كُلِّ ذِي عِلۡمٍ عَلِيمٞ
Basi akaanza na mizigo yao kabla ya mzigo wa nduguye. Kisha akalitoa katika mzigo wa nduguye. Hivyo ndivyo tulivyompangia njama Yusuf. Hakuwa ni wa kumzuia nduguye kwa sheria ya mfalme huyo isipokuwa Mwenyezi Mungu akitaka. Tunamuinua daraja tumtakaye. Na juu ya kila ajuaye yupo ajuaye zaidi.
Las Exégesis Árabes:
۞ قَالُوٓاْ إِن يَسۡرِقۡ فَقَدۡ سَرَقَ أَخٞ لَّهُۥ مِن قَبۡلُۚ فَأَسَرَّهَا يُوسُفُ فِي نَفۡسِهِۦ وَلَمۡ يُبۡدِهَا لَهُمۡۚ قَالَ أَنتُمۡ شَرّٞ مَّكَانٗاۖ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا تَصِفُونَ
Wakasema: Akiwa ameiba huyu, basi hakika nduguye vile vile aliiba hapo zamani. Lakini Yusuf akaliweka hilo kisiri katika moyo wake wala hakulionyesha kwao. Akasema: Nyinyi ndio mko katika pahali paovu zaidi, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi hayo mnayosingizia.
Las Exégesis Árabes:
قَالُواْ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡعَزِيزُ إِنَّ لَهُۥٓ أَبٗا شَيۡخٗا كَبِيرٗا فَخُذۡ أَحَدَنَا مَكَانَهُۥٓۖ إِنَّا نَرَىٰكَ مِنَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Wakasema: Ewe Mheshimiwa! Hakika huyu anaye baba mzee sana. Kwa hivyo mchukue mmoja wetu badala yake. Hakika sisi tunakuona wewe ni katika watu wazuri.
Las Exégesis Árabes:
قَالَ مَعَاذَ ٱللَّهِ أَن نَّأۡخُذَ إِلَّا مَن وَجَدۡنَا مَتَٰعَنَا عِندَهُۥٓ إِنَّآ إِذٗا لَّظَٰلِمُونَ
Akasema: Mwenyezi Mungu apishe mbali kumshika yeyote yule isipokuwa yule tuliyemkuta naye kitu chetu. Hakika, basi tutakuwa ni wenye kudhulumu.
Las Exégesis Árabes:
فَلَمَّا ٱسۡتَيۡـَٔسُواْ مِنۡهُ خَلَصُواْ نَجِيّٗاۖ قَالَ كَبِيرُهُمۡ أَلَمۡ تَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ أَبَاكُمۡ قَدۡ أَخَذَ عَلَيۡكُم مَّوۡثِقٗا مِّنَ ٱللَّهِ وَمِن قَبۡلُ مَا فَرَّطتُمۡ فِي يُوسُفَۖ فَلَنۡ أَبۡرَحَ ٱلۡأَرۡضَ حَتَّىٰ يَأۡذَنَ لِيٓ أَبِيٓ أَوۡ يَحۡكُمَ ٱللَّهُ لِيۖ وَهُوَ خَيۡرُ ٱلۡحَٰكِمِينَ
Basi walipokata tamaa naye, wakenda kando kunong'ona. Mkubwa wao akasema: Je! Hamjui ya kwamba baba yenu amechukua ahadi kutoka kwenu kwa Mwenyezi Mungu, na kabla ya hapo namna mlivyokosa katika agano lenu juu ya Yusuf? Basi mimi sitatoka nchi hii mpaka baba yangu anipe ruhusa au Mwenyezi Mungu anihukumie. Na Yeye ndiye Mbora wa mahakimu.
Las Exégesis Árabes:
ٱرۡجِعُوٓاْ إِلَىٰٓ أَبِيكُمۡ فَقُولُواْ يَٰٓأَبَانَآ إِنَّ ٱبۡنَكَ سَرَقَ وَمَا شَهِدۡنَآ إِلَّا بِمَا عَلِمۡنَا وَمَا كُنَّا لِلۡغَيۡبِ حَٰفِظِينَ
Rudini kwa baba yenu, na mwambieni: Ee baba yetu! Hakika mwanao ameiba. Na sisi hatutoi ushahidi isipokuwa kwa tunayoyajua. Wala sisi hatukuwa wenye kuhifadhi mambo ya ghaibu.
Las Exégesis Árabes:
وَسۡـَٔلِ ٱلۡقَرۡيَةَ ٱلَّتِي كُنَّا فِيهَا وَٱلۡعِيرَ ٱلَّتِيٓ أَقۡبَلۡنَا فِيهَاۖ وَإِنَّا لَصَٰدِقُونَ
Na uliza mji tuliokuwamo, na msafara tuliokuja nao. Na hakika sisi ni wakweli.
Las Exégesis Árabes:
قَالَ بَلۡ سَوَّلَتۡ لَكُمۡ أَنفُسُكُمۡ أَمۡرٗاۖ فَصَبۡرٞ جَمِيلٌۖ عَسَى ٱللَّهُ أَن يَأۡتِيَنِي بِهِمۡ جَمِيعًاۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡحَكِيمُ
Akasema: Bali nafsi zenu zimewashawishi kwenye jambo fulani. Basi subira ni nzuri! Huenda Mwenyezi Mungu akaniletea wote pamoja. Hakika Yeye ndiye Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.
Las Exégesis Árabes:
وَتَوَلَّىٰ عَنۡهُمۡ وَقَالَ يَٰٓأَسَفَىٰ عَلَىٰ يُوسُفَ وَٱبۡيَضَّتۡ عَيۡنَاهُ مِنَ ٱلۡحُزۡنِ فَهُوَ كَظِيمٞ
Naye akajitenga nao, na akasema: Ah! Huzuni wangu kubwa juu ya Yusuf! Na macho yake yakawa meupe kutokana na huzuni, na aliizuia bila ya kuidhirisha.
Las Exégesis Árabes:
قَالُواْ تَٱللَّهِ تَفۡتَؤُاْ تَذۡكُرُ يُوسُفَ حَتَّىٰ تَكُونَ حَرَضًا أَوۡ تَكُونَ مِنَ ٱلۡهَٰلِكِينَ
Wakasema: Tallahi! Huachi kumkumbuka Yusuf mpaka uwe mgonjwa sana au uwe katika walioangamia.
Las Exégesis Árabes:
قَالَ إِنَّمَآ أَشۡكُواْ بَثِّي وَحُزۡنِيٓ إِلَى ٱللَّهِ وَأَعۡلَمُ مِنَ ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Akasema: Hakika mimi namshitakia Mwenyezi Mungu tu sikitiko langu na huzuni wangu. Na ninajua kutoka kwa Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua nyinyi.
Las Exégesis Árabes:
يَٰبَنِيَّ ٱذۡهَبُواْ فَتَحَسَّسُواْ مِن يُوسُفَ وَأَخِيهِ وَلَا تَاْيۡـَٔسُواْ مِن رَّوۡحِ ٱللَّهِۖ إِنَّهُۥ لَا يَاْيۡـَٔسُ مِن رَّوۡحِ ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡقَوۡمُ ٱلۡكَٰفِرُونَ
Enyi wanangu! Nendeni mumtafute Yusuf na nduguye, wala msikate tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu. Hakika hawakati tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kaumu makafiri.
Las Exégesis Árabes:
فَلَمَّا دَخَلُواْ عَلَيۡهِ قَالُواْ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡعَزِيزُ مَسَّنَا وَأَهۡلَنَا ٱلضُّرُّ وَجِئۡنَا بِبِضَٰعَةٖ مُّزۡجَىٰةٖ فَأَوۡفِ لَنَا ٱلۡكَيۡلَ وَتَصَدَّقۡ عَلَيۡنَآۖ إِنَّ ٱللَّهَ يَجۡزِي ٱلۡمُتَصَدِّقِينَ
Basi walipoingia alimokuwa Yusuf, wakasema: Ewe Mheshimiwa! Imetupata shida kubwa, sisi na ahali zetu. Na tumekujia na mali kidogo. Basi tutimizie tu kipimo na tupe sadaka. Hakika Mwenyezi Mungu huwalipa watoao sadaka.
Las Exégesis Árabes:
قَالَ هَلۡ عَلِمۡتُم مَّا فَعَلۡتُم بِيُوسُفَ وَأَخِيهِ إِذۡ أَنتُمۡ جَٰهِلُونَ
Akasema: Je, mnajua yale mliyomfanyia Yusuf na nduguye mlipokuwa wajinga?
Las Exégesis Árabes:
قَالُوٓاْ أَءِنَّكَ لَأَنتَ يُوسُفُۖ قَالَ أَنَا۠ يُوسُفُ وَهَٰذَآ أَخِيۖ قَدۡ مَنَّ ٱللَّهُ عَلَيۡنَآۖ إِنَّهُۥ مَن يَتَّقِ وَيَصۡبِرۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Wakasema: Kumbe hakika wewe ndiye Yusuf? Akasema: Mimi ndiye Yusuf, na huyu ni ndugu yangu. Mwenyezi Mungu ametufanyia hisani. Hakika anayemcha Mungu na akasubiri, basi Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wafanyao mazuri.
Las Exégesis Árabes:
قَالُواْ تَٱللَّهِ لَقَدۡ ءَاثَرَكَ ٱللَّهُ عَلَيۡنَا وَإِن كُنَّا لَخَٰطِـِٔينَ
Wakasema: Tallahi! Mwenyezi Mungu amekufadhilisha wewe kuliko sisi, na hakika sisi tulikuwa wenye kukosa.
Las Exégesis Árabes:
قَالَ لَا تَثۡرِيبَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡيَوۡمَۖ يَغۡفِرُ ٱللَّهُ لَكُمۡۖ وَهُوَ أَرۡحَمُ ٱلرَّٰحِمِينَ
Akasema: Leo hakuna lawama yoyote juu yenu. Mwenyezi Mungu atawasamehe, naye ni Mwingi wa kurehemu kuliko wote wanaorehemu.
Las Exégesis Árabes:
ٱذۡهَبُواْ بِقَمِيصِي هَٰذَا فَأَلۡقُوهُ عَلَىٰ وَجۡهِ أَبِي يَأۡتِ بَصِيرٗا وَأۡتُونِي بِأَهۡلِكُمۡ أَجۡمَعِينَ
Nendeni na shati langu hili na mlitupe usoni mwa baba yangu, atakuwa mwenye kuona. Na mnijie na ahali zenu wote.
Las Exégesis Árabes:
وَلَمَّا فَصَلَتِ ٱلۡعِيرُ قَالَ أَبُوهُمۡ إِنِّي لَأَجِدُ رِيحَ يُوسُفَۖ لَوۡلَآ أَن تُفَنِّدُونِ
Na ulipoondoka tu msafara, baba yao akasema: Hakika mimi ninaipata harufu ya Yusuf, lau kuwa hamtanituhumu.
Las Exégesis Árabes:
قَالُواْ تَٱللَّهِ إِنَّكَ لَفِي ضَلَٰلِكَ ٱلۡقَدِيمِ
Wakasema: Tallahi! Hakika wewe bado ungali katika upotovu wako wa zamani.
Las Exégesis Árabes:
فَلَمَّآ أَن جَآءَ ٱلۡبَشِيرُ أَلۡقَىٰهُ عَلَىٰ وَجۡهِهِۦ فَٱرۡتَدَّ بَصِيرٗاۖ قَالَ أَلَمۡ أَقُل لَّكُمۡ إِنِّيٓ أَعۡلَمُ مِنَ ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Basi alipofika tu mbashiri huyo, akalitupa shati hilo usoni pake, basi akarejea kuona. Akasema: Je, sikuwaambia kuwa mimi ninajua kutoka kwa Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua nyinyi?
Las Exégesis Árabes:
قَالُواْ يَٰٓأَبَانَا ٱسۡتَغۡفِرۡ لَنَا ذُنُوبَنَآ إِنَّا كُنَّا خَٰطِـِٔينَ
Wakasema: Ewe baba yetu! Tuombee msamaha kwa dhambi zetu. Hakika sisi tulikuwa katika waliokosa.
Las Exégesis Árabes:
قَالَ سَوۡفَ أَسۡتَغۡفِرُ لَكُمۡ رَبِّيٓۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ
Akasema: Nitakuja waombea msamaha kwa Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusamehe mno, Mwenye kurehemu sana.
Las Exégesis Árabes:
فَلَمَّا دَخَلُواْ عَلَىٰ يُوسُفَ ءَاوَىٰٓ إِلَيۡهِ أَبَوَيۡهِ وَقَالَ ٱدۡخُلُواْ مِصۡرَ إِن شَآءَ ٱللَّهُ ءَامِنِينَ
Na wakati walipoingia alimokuwa Yusuf, aliwakumbatia wazazi wake na akasema: Ingieni Misri, Inshallah kwa amani.
Las Exégesis Árabes:
وَرَفَعَ أَبَوَيۡهِ عَلَى ٱلۡعَرۡشِ وَخَرُّواْ لَهُۥ سُجَّدٗاۖ وَقَالَ يَٰٓأَبَتِ هَٰذَا تَأۡوِيلُ رُءۡيَٰيَ مِن قَبۡلُ قَدۡ جَعَلَهَا رَبِّي حَقّٗاۖ وَقَدۡ أَحۡسَنَ بِيٓ إِذۡ أَخۡرَجَنِي مِنَ ٱلسِّجۡنِ وَجَآءَ بِكُم مِّنَ ٱلۡبَدۡوِ مِنۢ بَعۡدِ أَن نَّزَغَ ٱلشَّيۡطَٰنُ بَيۡنِي وَبَيۡنَ إِخۡوَتِيٓۚ إِنَّ رَبِّي لَطِيفٞ لِّمَا يَشَآءُۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡحَكِيمُ
Na akawapandisha wazazi wake kwenye kiti cha enzi. Na wote wakaporomoka kumsujudia. Na akasema: Ewe baba yangu! Hii ndiyo tafsiri ya ile ndoto yangu ya zamani. Na Mola wangu Mlezi ameifanya kuwa kweli. Na Mwenyezi Mungu amenifanyia uzuri kunitoa gerezani, na akawaleta kutoka jangwani baada ya Shetani kuchochea baina yangu na ndugu zangu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mpole kwa alitakalo. Hakika Yeye ndiye Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.
Las Exégesis Árabes:
۞ رَبِّ قَدۡ ءَاتَيۡتَنِي مِنَ ٱلۡمُلۡكِ وَعَلَّمۡتَنِي مِن تَأۡوِيلِ ٱلۡأَحَادِيثِۚ فَاطِرَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ أَنتَ وَلِيِّۦ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۖ تَوَفَّنِي مُسۡلِمٗا وَأَلۡحِقۡنِي بِٱلصَّٰلِحِينَ
Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika umenipa katika ufalme, na umenifunza katika tafsiri ya mambo. Ewe Muumba wa mbingu na ardhi! Wewe ndiye Mlinzi wangu katika dunia na Akhera. Nifishe hali ya kuwa ni Muislamu na niunganishe na walio wema.
Las Exégesis Árabes:
ذَٰلِكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلۡغَيۡبِ نُوحِيهِ إِلَيۡكَۖ وَمَا كُنتَ لَدَيۡهِمۡ إِذۡ أَجۡمَعُوٓاْ أَمۡرَهُمۡ وَهُمۡ يَمۡكُرُونَ
Hizo ni katika habari za ghaibu tulizokufunulia. Na hukuwa pamoja nao walipoazimia jambo lao hilo walipokuwa wanafanya njama zao.
Las Exégesis Árabes:
وَمَآ أَكۡثَرُ ٱلنَّاسِ وَلَوۡ حَرَصۡتَ بِمُؤۡمِنِينَ
Na wengi wa watu si wenye kuamini hata ukijitahidi vipi.
Las Exégesis Árabes:
وَمَا تَسۡـَٔلُهُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۚ إِنۡ هُوَ إِلَّا ذِكۡرٞ لِّلۡعَٰلَمِينَ
Wala wewe huwaombi ujira kwa haya. Hayakuwa haya isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu wote.
Las Exégesis Árabes:
وَكَأَيِّن مِّنۡ ءَايَةٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ يَمُرُّونَ عَلَيۡهَا وَهُمۡ عَنۡهَا مُعۡرِضُونَ
Na ni ishara ngapi katika mbingu na ardhi wanazozipitia, lakini wao wanazipuuza.
Las Exégesis Árabes:
وَمَا يُؤۡمِنُ أَكۡثَرُهُم بِٱللَّهِ إِلَّا وَهُم مُّشۡرِكُونَ
Na wengi wao hawamuamini Mwenyezi Mungu pasina kuwa ni washirikina.
Las Exégesis Árabes:
أَفَأَمِنُوٓاْ أَن تَأۡتِيَهُمۡ غَٰشِيَةٞ مِّنۡ عَذَابِ ٱللَّهِ أَوۡ تَأۡتِيَهُمُ ٱلسَّاعَةُ بَغۡتَةٗ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ
Je, wana amani kuwa iwajie adhabu ya Mwenyezi Mungu ya kuwagubika, au iwajie Saa ya Qiyama kwa ghafla, na hali hawatambui?
Las Exégesis Árabes:
قُلۡ هَٰذِهِۦ سَبِيلِيٓ أَدۡعُوٓاْ إِلَى ٱللَّهِۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا۠ وَمَنِ ٱتَّبَعَنِيۖ وَسُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa ufahamu mzuri - mimi na wale wanaonifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina.
Las Exégesis Árabes:
وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ إِلَّا رِجَالٗا نُّوحِيٓ إِلَيۡهِم مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡقُرَىٰٓۗ أَفَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۗ وَلَدَارُ ٱلۡأٓخِرَةِ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ
Na hatukuwatuma Mitume kabla yako isipokuwa wanaume tuliowafunulia wahyi miongoni mwa watu wa mijini. Je, hawakutembea katika ardhi wakaona jinsi ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Na hakika nyumba ya Akhera ndiyo bora kwa wamchao Mungu. Basi hamtumii akili?
Las Exégesis Árabes:
حَتَّىٰٓ إِذَا ٱسۡتَيۡـَٔسَ ٱلرُّسُلُ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُمۡ قَدۡ كُذِبُواْ جَآءَهُمۡ نَصۡرُنَا فَنُجِّيَ مَن نَّشَآءُۖ وَلَا يُرَدُّ بَأۡسُنَا عَنِ ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ
Hata Mitume walipokata tamaa (ya watu wao kuamini) na wakaona kuwa wamekadhibishwa, hapo ikawajia nusura yetu, kwa hivyo wakaokolewa sawasawa tuwatakao. Na adhabu yetu haiwezi kurudishwa dhidi ya kaumu wahalifu.
Las Exégesis Árabes:
لَقَدۡ كَانَ فِي قَصَصِهِمۡ عِبۡرَةٞ لِّأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِۗ مَا كَانَ حَدِيثٗا يُفۡتَرَىٰ وَلَٰكِن تَصۡدِيقَ ٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَتَفۡصِيلَ كُلِّ شَيۡءٖ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ
Kwa hakika katika hadithi zao limo zingatio kwa wenye akili. Hazikuwa hadithi tu zilizozuliwa, bali ni za kusadikisha yale yaliyo kabla yake, na ufafanuzi wa kina wa kila kitu, na ni uwongofu na rehema kwa kaumu inayoamini.
Las Exégesis Árabes:
 
Traducción de significados Capítulo: Yusef
Índice de Capítulos Número de página
 
Traducción de los significados del Sagrado Corán - Traducción al suajili - El Centro de Rowad Al- Taryamah - Índice de traducciones

Traducida por el equipo del Centro Rowad Al-Taryamah en cooperación con la Asociación de Dawah en Rabwa y la Asociación para el Servicio del Contenido Islámico en Idiomas.

Cerrar