Alif Laam Raa.[1] Hizi ni Aya za Kitabu kinachobainisha.
[1] Herufi hizi "Alif Laam Raa" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Na hivyo ndivyo Mola wako Mlezi atakuteua na atakufundisha katika tafsiri ya mambo. Na atatimiza neema zake juu yako na juu ya ukoo wa Yaa'qub, kama alivyowatimizia hapo zamani baba zako Ibrahim na Is-haq. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.
Pale waliposema: Hakika Yusuf na nduguye wanapendwa zaidi na baba yetu kuliko sisi, ilhali sisi ni kikundi chenye nguvu. Hakika baba yetu yuko katika upotovu wa dhahiri.
Basi walipokwenda naye, na wakakubaliana kwamba wamtumbukize ndani ya kisima, tulimfunulia Yusuf: Hakika utakujawaambia jambo lao hili, na wala wao hawatambui.
Wakasema: Ewe baba yetu! Hakika tulikwenda kushindana na tukamwacha Yusuf penye vitu vyetu. Basi mbwa mwitu akamla. Lakini wewe hutuamini ijapokuwa sisi ni wakweli.
Na walikuja na shati lake likiwa lina damu ya uongo. Akasema: Bali nafsi zenu zimewashawishi kutenda kitendo. Lakini subira ni njema; na Mwenyezi Mungu ndiye wa kuombwa msaada kwa haya mnayoyaeleza.
Na ukaja msafara, kisha wakamtuma mchota maji wao, naye akatumbukiza ndoo yake. Alisema: Hii ni bishara njema! Huyu hapa mvulana! Wakamficha ili kumfanya ni bidhaa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema hayo wanayoyatenda.
Na yule aliyemnunua huko Misri alimwambia mkewe: "Mtengenezee makazi ya heshima huyu; huenda akatufaa au tukamfanya mwanetu." Basi hivyo ndivyo tulivyomuweka Yusuf imara katika ardhi ili tumfundishe kufasiri mambo. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini wengi wa watu hawajui.
Na yule bibi wa nyumba aliyokuwamo Yusuf akamtamani kinyume cha nafsi yake, na akafungafunga milango. Akamwambia: "Njoo!" Yusuf akasema: Audhubillahi (najikinga na Mwenyezi Mungu)! Hakika Yeye ni bwana wangu, aliniweka maskani nzuri, na hakika madhalimu hawafaulu.
Na hakika yule mwanamke alimuazimia, na Yusuf akamuazimia lau kuwa hakuona ishara ya Mola wake Mlezi. Ilikuwa hivyo, ili tumuepushie mabaya na uchafu. Hakika yeye alikuwa katika waja wetu walioteuliwa.
Na wote wawili wakakimbilia mlangoni, na mwanamke akalirarua shati lake Yusuf kwa nyuma. Na wakamkuta bwana wake mlangoni. Mwanamke akasema: Hakuna malipo ya mwenye kutaka kumfanyia mabaya mkeo isipokuwa afungwe au kupewa adhabu chungu.
Yusuf akasema: Yeye ndiye aliyenitaka bila ya mimi kumtaka. Na shahidi aliyekuwa katika jamaa za mwanamke akasema: Ikiwa shati lake limechanwa kwa mbele, basi mwanamke amesema kweli, naye Yusuf ni katika waongo.
Na wanawake wa mjini wakawa wanasema: Mke wa Mheshimiwa anamtamani mtumishi wake bila ya yeye kumtaka! Hakika mapenzi yamemuingia sana moyoni. Sisi hakika tunamwona yuko katika upotovu ulio dhahiri.
Basi aliposikia yule bibi masengenyo yao, aliwaita, na akawawekea matakia ya kuegemea, na akampa kila mmoja wao kisu. Akamwambia Yusuf: "Jitokeze mbele yao." Basi walipomwona, waliona ni kitu kikubwa kabisa, na wakajikatakata mikono yao. Wakasema: Hasha Lillahi (Ametakasika Mwenyezi Mungu)! Huyu si mwanadamu. Huyu si isipokuwa Malaika mtukufu.
Yule bibi akasema: Huyu basi ndiye huyo mliyenilaumia! Na kweli mimi nilimtaka naye akakataa. Na asipofanya ninayomwamrisha, basi hakuna shaka atafungwa gerezani, na atakuwa miongoni mwa walio duni kabisa.
Yusuf akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Ninapendelea kifungo kuliko haya anayoniitia. Na usiponiondoshea vitimbi vya wanawake, mimi nitaelekea kwao, na nitakuwa katika wajinga.
Na wakaingia gerezani pamoja naye vijana wawili. Mmoja wao akasema: Hakika mimi nimeota kuwa ninakamua mvinyo. Na mwingine akasema: Hakika mimi nimeota kuwa nimebeba mikate juu ya kichwa changu, na ndege wanakula kwayo. Hebu tuambie tafsiri yake, kwani sisi tunakuona wewe ni katika watu wazuri.
Akasema: Hakitawajia chakula mtakachoruzukiwa isipokuwa nitawaambia hakika yake kabla ya kuwajia. Hayo ni katika yale aliyonifundisha Mola wangu Mlezi. Hakika mimi nimeacha mila ya kaumu wasiomuamini Mwenyezi Mungu, na wakawa wameikufuru Akhera.
Na nimefuata mila ya baba zangu, Ibrahim, na Is-haq, na Yaa'qub. Haikutufailia sisi kumshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote. Hiyo ni katika fadhila za Mwenyezi Mungu juu yetu na juu ya watu, lakini wengi wa watu hawashukuru.
Hamuabudu badala yake isipokuwa majina tu mliyowaita nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuyateremshia hayo uthibitisho wowote. Hakuna hukumu isipokuwa ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipokuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo Dini iliyonyooka. Lakini wengi wa watu hawajui.
Enyi wafungwa wenzangu wawili! Ama mmoja wenu, yeye atamnywesha bwana wake mvinyo. Na ama mwengine, yeye atasulubiwa, na ndege watakula katika kichwa chake. Imekwishakatwa hukumu ya hilo jambo mlilokuwa mkiuliza.
Na akamwambia yule aliyejua kuwa ataokoka katika wawili hao: "Nikumbuke kwa bwana wako." Lakini Shetani alimsahaulisha kumtaja kwa bwana wake. Basi Yusuf akakaa gerezani miaka kadhaa.
Na siku moja mfalme alisema: Hakika mimi nimeota ng'ombe saba wanene wanaliwa na ng'ombe saba waliokonda. Na mashuke saba mabichi na mengine makavu. Enyi waheshimiwa! Niambieni maana ya ndoto zangu, ikiwa nyinyi mnaweza kuagua ndoto.
Yusuf! Ewe mkweli! Tueleze ni nini maana ya ng'ombe saba wanene kuliwa na ng'ombe saba waliokonda. Na mashuke saba mabichi na mengine makavu, ili nirejee kwa watu ili wapate kujua.
Na mfalme akasema: "Nijieni naye!" Basi mjumbe huyo alipomjia, Yusuf akasema: Rudi kwa bwana wako na umuulize wana nini wale wanawake waliojikatakata mikono yao. Hakika Mola wangu Mlezi anazijua vyema njama zao.
Mfalme alisema: Mlikuwa mna nini mlipomtaka Yusuf kinyume na nafsi yake? Wakasema: Hasha Lillahi (Mwenyezi Mungu apishe mbali)! Sisi hatukujua ubaya wowote kwake. Mke wa Mheshimiwa yule akasema: Sasa haki imedhihiri. Mimi ndiye niliyemtaka kinyume na nafsi yake, na hakika yeye ni katika wakweli.
Basi hivyo ndivyo tulivyomuimarisha Yusuf katika ardhi, akawa anakaa humo popote anapotaka. Tunamfikishia rehema zetu tumtakaye, wala hatupotezi malipo ya wafanyao mazuri.
Na alipowatengenezea tayari haja yao, alisema: Nileteeni ndugu yenu wa kwa baba yenu. Je, hamuoni ya kwamba mimi hakika ninatimiza kipimo, nami ni mbora wa wanaokaribisha?
Basi waliporejea kwa baba yao, walisema: Ewe baba yetu! Tumenyimwa chakula zaidi. Basi muachilie ndugu yetu pamoja nasi ili tupate kupimiwa. Nasi hakika tutamlinda.
Akasema: Je, niwaamini juu yake isipokuwa kama nilivyowaamini kwa nduguye zamani? Lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mbora zaidi wa kulinda, naye ndiye Mbora zaidi wa wanaorehemu.
Na walipofungua mizigo yao, wakakuta bidhaa zao wamerudishiwa. Wakasema: Ewe baba yetu! Tutake nini zaidi? Hizi hapa bidhaa zetu tumerudishiwa. Wacha tuwaletee watu wetu chakula, na tutamlinda ndugu yetu, na tutaongeza shehena ya ngamia. Na hicho ni kipimo kidogo.
Akasema: Sitamuachilia pamoja nanyi mpaka mnipe agano kwa Mwenyezi Mungu kwamba lazima mtanijia naye isipokuwa ikiwa mtazungukwa. Basi walipompa agano lao, alisema: Mwenyezi Mungu ndiye Mtegemewa kwa tuyasemayo.
Na akasema: Enyi wanangu! Msiingie kupitia mlango mmoja, bali ingieni kwa kupitia milango tofautitofauti. Wala mimi siwafai kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Hukumu haiko isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu tu. Juu yake mimi nimetegemea, na juu yake na wategemee wanaotegemea.
Na walipoingilia pale alipowaamrisha baba yao, hakuwa wa kuwafaa kitu kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa ni haja tu iliyokuwa katika nafsi ya Yaa'qub aliyoitimiza. Na hakika yeye alikuwa na elimu kwa sababu tulimfundisha, lakini wengi wa watu hawajui.
Na alipokwishawatayarishia mahitaji yao, akakitia kikopo cha kunywea maji katika mzigo wa nduguye huyo, kisha mwenye kunadi akanadi: Enyi msafara! Hakika nyinyi ni wezi!
Basi akaanza na mizigo yao kabla ya mzigo wa nduguye. Kisha akalitoa katika mzigo wa nduguye. Hivyo ndivyo tulivyompangia njama Yusuf. Hakuwa ni wa kumzuia nduguye kwa sheria ya mfalme huyo isipokuwa Mwenyezi Mungu akitaka. Tunamuinua daraja tumtakaye. Na juu ya kila ajuaye yupo ajuaye zaidi.
Wakasema: Akiwa ameiba huyu, basi hakika nduguye vile vile aliiba hapo zamani. Lakini Yusuf akaliweka hilo kisiri katika moyo wake wala hakulionyesha kwao. Akasema: Nyinyi ndio mko katika pahali paovu zaidi, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi hayo mnayosingizia.
Wakasema: Ewe Mheshimiwa! Hakika huyu anaye baba mzee sana. Kwa hivyo mchukue mmoja wetu badala yake. Hakika sisi tunakuona wewe ni katika watu wazuri.
Basi walipokata tamaa naye, wakaenda kando kunong'ona. Mkubwa wao akasema: Je! Hamjui ya kwamba baba yenu amechukua ahadi kutoka kwenu kwa Mwenyezi Mungu, na kabla ya hapo namna mlivyokosa katika agano lenu juu ya Yusuf? Basi mimi sitatoka nchi hii mpaka baba yangu anipe ruhusa au Mwenyezi Mungu anihukumie. Na Yeye ndiye Mbora wa wanaohukumu.
Rudini kwa baba yenu, na mwambieni: Ee baba yetu! Hakika mwanao ameiba. Na sisi hatutoi ushahidi isipokuwa kwa tunayoyajua. Wala sisi hatukuwa wenye kuhifadhi mambo ya ghaibu.
Akasema: Bali nafsi zenu zimewashawishi kwenye jambo fulani. Basi subira ni nzuri! Huenda Mwenyezi Mungu akaniletea wote pamoja. Hakika Yeye ndiye Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.
Enyi wanangu! Nendeni mumtafute Yusuf na nduguye, wala msikate tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu. Hakika hawakati tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kaumu makafiri.
Basi walipoingia alimokuwa Yusuf, wakasema: Ewe Mheshimiwa! Imetupata shida kubwa, sisi na ahali zetu. Na tumekujia na mali kidogo. Basi tutimizie tu kipimo na tupe sadaka. Hakika Mwenyezi Mungu huwalipa watoao sadaka.
Wakasema: Kumbe hakika wewe ndiye Yusuf? Akasema: Mimi ndiye Yusuf, na huyu ni kaka yangu. Mwenyezi Mungu ametufanyia hisani. Hakika anayemcha Mungu na akasubiri, basi Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wafanyao mazuri.
Basi alipofika tu mbashiri huyo, akalitupa shati hilo usoni pake, basi akarejea kuona. Akasema: Je, sikuwaambia kuwa mimi ninajua kutoka kwa Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua nyinyi?
Na akawapandisha wazazi wake kwenye kiti cha enzi, na wote wakaporomoka kumsujudia. Akasema: Ewe baba yangu! Hii ndiyo tafsiri ya ile ndoto yangu ya zamani. Mola wangu Mlezi ameifanya kuwa kweli. Na Mwenyezi Mungu amenifanyia uzuri kunitoa gerezani, na akawaleta kutoka jangwani baada ya Shetani kuchochea baina yangu na ndugu zangu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mpole kwa alitakalo. Hakika Yeye ndiye Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.
Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika umenipa katika ufalme, na umenifunza katika tafsiri ya mambo. Ewe Muumba wa mbingu na ardhi! Wewe ndiye Mlinzi wangu katika dunia na Akhera. Nifishe hali ya kuwa ni Muislamu na niunganishe na walio wema.
Sema: Hii ndiyo njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa ufahamu mzuri - mimi na wale wanaonifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu, na wala mimi si katika washirikina.
Na hatukuwatuma Mitume kabla yako isipokuwa wanaume tuliowafunulia ufunuo (wahyi) miongoni mwa watu wa mijini. Je, hawakutembea katika ardhi wakaona jinsi ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Na hakika nyumba ya Akhera ndiyo bora kwa wamchao Mungu. Basi hamtumii akili?
Mpaka Mitume walipokata tamaa (ya watu wao kuamini) na wakaona kuwa wamekadhibishwa, hapo ikawajia nusura yetu, kwa hivyo wakaokolewa sawasawa tuwatakao. Na adhabu yetu haiwezi kurudishwa dhidi ya kaumu wahalifu.
Kwa hakika katika hadithi zao limo zingatio kwa wenye akili. Hazikuwa hadithi tu zilizozuliwa, bali ni za kusadikisha yale yaliyo kabla yake, na ufafanuzi wa kina wa kila kitu, na ni uongofu na rehema kwa kaumu inayoamini.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
搜索结果:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".