Firo maanaaji al-quraan tedduɗo oo - Firo sawahiliiwo. - Abdullaay Muhammad e Naadir Kamiis. * - Tippudi firooji ɗii


Firo maanaaji Aaya: (43) Simoore: Simoore al-araaf
وَنَزَعۡنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنۡ غِلّٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهِمُ ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ وَقَالُواْ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِي هَدَىٰنَا لِهَٰذَا وَمَا كُنَّا لِنَهۡتَدِيَ لَوۡلَآ أَنۡ هَدَىٰنَا ٱللَّهُۖ لَقَدۡ جَآءَتۡ رُسُلُ رَبِّنَا بِٱلۡحَقِّۖ وَنُودُوٓاْ أَن تِلۡكُمُ ٱلۡجَنَّةُ أُورِثۡتُمُوهَا بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ataziondoa chuki na mafundo ndani ya vifua vya watu wa Peponi. Na miongoni mwa kukamilika neema zao ni kwamba mito ya maji itakuwa ikipita chini yao. Na watasema watu wa Peponi pindi watakapoingia humo, «Shukrani ni za Mwenyezi Mungu Aliyetuafikia kufanya vitendo vyema ambavyo vimetupatia starehe hizi ambazo tuko nazo. Na hatukuwa tuna uwezo wa kuifuata njia iliyolingana sawa kama si Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kutuongoza kufuata njia hii na kutuwezesha kukita juu yake. Mitume wa Mola wetu wametuletea habari za ukweli za ahadi njema kwa wenye kumtii na za kuwaonya wenye kumuasi. Na wataitwa kwa kupongezwa na kukirimiwa waambiwe, «Hiyo ndiyo pepo Mwenyezi Mungu Aliyowapa ni urathi kwa rehema Zake na kwa mliyoyatanguliza ya Imani na matendo mema.»
Faccirooji aarabeeji:
 
Firo maanaaji Aaya: (43) Simoore: Simoore al-araaf
Tippudi cimooje Tonngoode hello ngoo
 
Firo maanaaji al-quraan tedduɗo oo - Firo sawahiliiwo. - Abdullaay Muhammad e Naadir Kamiis. - Tippudi firooji ɗii

Firo maanaaji al-quraan tedduɗo oo fayde e ɗemngal sawaahili, firi ɗum ko Doktoor Abdullaay Muhammad Abuubakri. E mawɗo Naasir Kamiis.

Uddude