Check out the new design

Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahilie - 'Alî Muhsin Al Barwânî * - Lexique des traductions

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Traduction des sens Sourate: Al Anbiyâ'   Verset:
فَجَعَلَهُمۡ جُذَٰذًا إِلَّا كَبِيرٗا لَّهُمۡ لَعَلَّهُمۡ إِلَيۡهِ يَرۡجِعُونَ
Basi akayavunja vipande vipande, ila kubwa lao, ili wao walirudie. [58]
[58] Baada ya kwisha ondoka wale watu, Ibrahim aliwaendea masanamu akayavunja vipande vipande, isipokuwa sanamu kumbwa, hilo aliliacha ili wapate kuliregea waliulize yalio wasibu miungu yao nalo halikujibu kitu, kwa hivyo upotovu wa ibada yao ikabainika.
Les exégèses en arabe:
قَالُواْ مَن فَعَلَ هَٰذَا بِـَٔالِهَتِنَآ إِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ
Wakasema: Nani aliye ifanyia haya miungu yetu? Hakika huyu ni katika walio dhulumu. [59]
[59] Baada ya kwisha ona yaliyo wapata miungu yao wakasema: Nani aliye itendea haya miungu yetu? Hakika mtu huyu hapana shaka ni katika walio jidhulumu wenyewe kwa adhabu itayo mpata..
Les exégèses en arabe:
قَالُواْ سَمِعۡنَا فَتٗى يَذۡكُرُهُمۡ يُقَالُ لَهُۥٓ إِبۡرَٰهِيمُ
Wakasema: Tumemsikia kijana mmoja akiwataja. Anaitwa Ibrahim. [60]
[60] Wakasema baadhi yao: Tumemsikia kijana mmoja akiitaja kwa kuisubu (kuitukana) ; naye anaitwa Ibrahim.
Les exégèses en arabe:
قَالُواْ فَأۡتُواْ بِهِۦ عَلَىٰٓ أَعۡيُنِ ٱلنَّاسِ لَعَلَّهُمۡ يَشۡهَدُونَ
Wakasema: Mleteni mbele ya macho ya watu, wapate kumshuhudia [61]
[61] Wakasema wakubwa wao: Nendeni mkamlete, ahukumiwe mbele ya macho ya watu, na washuhudie aliyo yatenda!
Les exégèses en arabe:
قَالُوٓاْ ءَأَنتَ فَعَلۡتَ هَٰذَا بِـَٔالِهَتِنَا يَٰٓإِبۡرَٰهِيمُ
Wakasema: Je! Wewe umeifanyia haya miungu yetu, ewe Ibrahim? [62]
[62] Baada ya kwisha mhudhurisha, wakasema: Ni wewe ulio itenda haya miungu yetu, ewe Ibrahim?
Les exégèses en arabe:
قَالَ بَلۡ فَعَلَهُۥ كَبِيرُهُمۡ هَٰذَا فَسۡـَٔلُوهُمۡ إِن كَانُواْ يَنطِقُونَ
Akasema: Bali amefanya hayo huyu mkubwa wao. Basi waulizeni ikiwa wanaweza kutamka. [63]
[63] Kuwanabihisha upotovu wao, alisema kwa kuwakejeli: Hili kubwa lao ndilo lililo tenda hayo! Iulizeni hiyo miungu aliyo yatenda huyu, kama kweli inaweza kujibu suala yenu!
Les exégèses en arabe:
فَرَجَعُوٓاْ إِلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ فَقَالُوٓاْ إِنَّكُمۡ أَنتُمُ ٱلظَّٰلِمُونَ
Basi wakajirudi nafsi zao, wakasema: Hakika nyinyi mlikuwa madhaalimu! [64]
[64] Wakazirejea nafsi zao wakiifikiria ile ibada yao kuabudu vitu visivyo mnufaisha yeyote wala haviwezi kujitetea wenyewe. Wakayaona makosa yao. Baadhi yao wakasema: Ibrahim si katika walio dhulumu, bali nyinyi ndio madhaalimu kwa kuabudu vitu visio stahiki kuabudiwa.
Les exégèses en arabe:
ثُمَّ نُكِسُواْ عَلَىٰ رُءُوسِهِمۡ لَقَدۡ عَلِمۡتَ مَا هَٰٓؤُلَآءِ يَنطِقُونَ
Kisha wakarejea kwenye ule ule upotovu wao wakasema: Wewe unajua kwamba hawa hawesemi. [65]
[65] Kisha wakarejea tena, wakaacha uwongofu, wakarudia upotovu. Wakamwambia Ibrahim: Hakika wewe umekwisha jua kuwa haya masanamu tunayo yaabudu hayasemi kitu. Basi vipi unatutaka tuyaulize?
Les exégèses en arabe:
قَالَ أَفَتَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُكُمۡ شَيۡـٔٗا وَلَا يَضُرُّكُمۡ
Akasema: Basi nyinyi mnawaabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu wasio kufaini kitu wala kukudhuruni? [66]
[66] Ibrahim akasema: Ikiwa hali yao haya masanamu ni hii, hayawezi kitu, na nyinyi ndio makhusiano yenu nao ni hivi, basi nyinyi mmekuwa mnaacha kumuabudu Mwenyezi Mungu, na badala yake mnaabudu vitu visivyo kupeni faida hata chembe mkiviabudu, wala havikudhuruni kwa lolote mkiviachilia mbali?
Les exégèses en arabe:
أُفّٖ لَّكُمۡ وَلِمَا تَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ
Aibu yenu nyinyi na hivyo mnavyo viabudu badala ya Mwenyezi Mungu! Basi nyinyi hamtii akilini? [67]
[67] Aibu yenu! Nyinyi na miungu yenu mmelaanika! Mnaacha fikra zenu zipotee, na mnapuuza kuzingatia? Bila ya shaka haya masanamu hayafai kuabudiwa!
Les exégèses en arabe:
قَالُواْ حَرِّقُوهُ وَٱنصُرُوٓاْ ءَالِهَتَكُمۡ إِن كُنتُمۡ فَٰعِلِينَ
Wakasema: Mchomeni moto, na muinusuru miungu yenu, ikiwa nyinyi ni watendao jambo! [68]
[68] Wakaambiana wenyewe kwa wenyewe: Mchomeni moto mpate kuinusuru miungu yenu kwa mateso haya, ikiwa nyinyi mnataka kufanya kitu cha kuiunusuru miungu yenu.
Les exégèses en arabe:
قُلۡنَا يَٰنَارُ كُونِي بَرۡدٗا وَسَلَٰمًا عَلَىٰٓ إِبۡرَٰهِيمَ
Sisi tukasema: Ewe moto! Kuwa baridi na salama kwa Ibrahim! [69]
[69] Sisi tukaufanya moto ule uwe baridi na salama, hauna madhara yoyote, kwa Ibrahim.
Les exégèses en arabe:
وَأَرَادُواْ بِهِۦ كَيۡدٗا فَجَعَلۡنَٰهُمُ ٱلۡأَخۡسَرِينَ
Wao walimkusudia maovu, lakini Sisi tukawafanya wao ndio walio khasiri. [70]
[70] Wao walitaka kumuangamiza, lakini Sisi tukamwokoa, na tukawafanya wao ndio watu walio khasiri mno.
Les exégèses en arabe:
وَنَجَّيۡنَٰهُ وَلُوطًا إِلَى ٱلۡأَرۡضِ ٱلَّتِي بَٰرَكۡنَا فِيهَا لِلۡعَٰلَمِينَ
Na tukamwokoa yeye na Luut'i tukawapeleka kwenye nchi tulio ibariki kwa ajili ya walimwengu wote. [71]
[71] Na tukamwokoa yeye na Luut'i na njama zilizo pangwa, wakaelekea kwenye nchi tuliyo ijaalia kheri nyingi kwa watu wote, na tukawapeleka huko Manabii wengi.
Les exégèses en arabe:
وَوَهَبۡنَا لَهُۥٓ إِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ نَافِلَةٗۖ وَكُلّٗا جَعَلۡنَا صَٰلِحِينَ
Naye tukampa Is-haq, na Yaaqub kuwa ni ziada. Na wote tukawajaalia wawe watu wema. [72]
[72] Na tukampa Ibrahim mtoto Is-haq, na kutokana na Is-haq tukampa Yaaqubu, zaidi kuliko aliyo taka. Na wote wawili, Is-haq na Yaaqubu tuliwajaalia kuwa ni watu wema.
Les exégèses en arabe:
 
Traduction des sens Sourate: Al Anbiyâ'
Lexique des sourates Numéro de la page
 
Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahilie - 'Alî Muhsin Al Barwânî - Lexique des traductions

Traduit par 'Alî Muhsin Al Barwânî.

Fermeture