Na litapulizwa barugumu, wazimie waliomo mbinguni na waliomo katika ardhi, isipo kuwa aliye mtaka Mwenyezi Mungu. Kisha litapulizwa mara nyengine. Hapo watainuka wawe wanangojea. [68]
[68] Na litapulizwa barugumu kwa yakini, na watakufa walioko mbinguni na katika ardhi ila anaye mtaka Mwenyezi Mungu kumuakhirisha mpaka wakati mwengine. Kisha litapulizwa mara nyengine, na hapo wote watainuka kutoka makaburini mwao, wakingojea watafanywa nini? Hilo barugumu (S'ur) kilugha, ni tarumbeta, mbiu, siwa, parapanda. Barugumu inalo tusimulia Qur'ani ni katika mambo ya ulimwengu usio onekana, hatujui lilivyo na hakika yake.
Na ardhi itang'ara kwa Nuru ya Mola wake Mlezi, na Kitabu kitawekwa, na wataletwa Manabii na mashahidi, na patahukumiwa baina yao kwa haki, wala hawatadhulumiwa. [69]
[69] Na ardhi itang'ara siku hiyo kwa nuru ya Muumba wake na Mmiliki wake. Na kitatayarishwa Kitabu kilicho sajiliwa ndani yake vitendo vyao, na watahudhurishwa Manabii na mashahidi wapate kuwashuhudia viumbe vyote, na wapambanuliwe baina ya viumbe kwa uadilifu, na wala hawatadhulumiwa kwa kupunguziwa thawabu wala kuzidishiwa adhabu.
Na walio kufuru wataongozwa kuendea Jahannamu kwa makundi. Mpaka watakapo ifikia itafunguliwa milango yake, na walinzi wake watawaambia: Kwani hawakukujilieni Mitume miongoni mwenu wakikusomeeni Aya za Mola wenu Mlezi na kukuonyeni mkutano wa siku yenu hii? Watasema: Kwani! Lakini limekwisha thibiti neno la adhabu juu ya makafiri. [71]
[71] Na makafiri watahimizwa kwenda kwa nguvu kuendea Jahannamu kwa makundi makundi. Na hata watapo fika milango yake itafunguliwa, na walinzi wake watawaambia kwa kuwakebehi: Kwani hawakuja kwenu Wajumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu wa jinsi yenu, wakikusomeeni Aya za Mola wenu Mlezi, na wakakuhadharisheni na mkutano wenu huu? Makafiri watasema kwa kukiri: Kwani! Walitujia Mitume. Lakini neno la adhabu limekwisha wajibikia juu ya makafiri, kwa kuwa wao wamekhiari ukafiri kuliko Imani.
Itasemwa: Ingieni milango ya Jahannamu mdumu humo. Basi nayo ni ubaya ulioje wa makaazi ya wanao takabari! [72]
[72] Wataambiwa: Iingieni milango ya Jahannamu mliyo jaaliwa mkae humo milele. Jahannamu ni pahala paovu mno pa kukaa wenye kutakabari na wakakataa kuikubali Haki.
Na walio mcha Mola wao Mlezi wataongozwa kuendea Peponi kwa makundi, mpaka watakapo fikilia, nayo milango yake imekwisha funguliwa. Walinzi wake watawaambia: Salaam Alaikum, Amani iwe juu yenu! Mmet'ahirika. Basi ingieni humu mkae milele. [73]
[73] Na wachamngu watahimizwa kwenda Peponi kwa hishima makundi makundi, mpaka wakifika kwenye milango yake, wataambiwa na walinzi wake: Amani kubwa juu yenu! Mmet'ahirika duniani na uchafu wa maasi, na mmet'ahirika Akhera katika nafsi zenu kwa neema mlizo zipata. Basi ingieni Peponi mliko jaaliwa kukaa milele. Kwani nyinyi mna neema zisio pita akilini.
Nao watasema: Alhamdulillah, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliye tutimizia ahadi yake, na akaturithisha ardhi, tunakaa katika Bustani popote tupendapo. Basi ni malipo mazuri yaliyoje ya watendao! [74]
[74] Na wachamngu watasema: Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu peke yake, ambaye ametutimizia aliyo tuahidi kwa ndimi za Mitume wake, na akatumilikisha ardhi ya Peponi tunashukia tutakapo humo. Ama hakika bora ya ujira wa wenye kutenda mema ni Pepo.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
Résultats de la recherche:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".