Check out the new design

Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahilie - 'Alî Muhsin Al Barwânî * - Lexique des traductions

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Traduction des sens Sourate: Al Mâ'idah   Verset:
سَمَّٰعُونَ لِلۡكَذِبِ أَكَّٰلُونَ لِلسُّحۡتِۚ فَإِن جَآءُوكَ فَٱحۡكُم بَيۡنَهُمۡ أَوۡ أَعۡرِضۡ عَنۡهُمۡۖ وَإِن تُعۡرِضۡ عَنۡهُمۡ فَلَن يَضُرُّوكَ شَيۡـٔٗاۖ وَإِنۡ حَكَمۡتَ فَٱحۡكُم بَيۡنَهُم بِٱلۡقِسۡطِۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُقۡسِطِينَ
Hao ni wasikilizaji kwa ajili ya kusema uwongo, na ni walaji mno vya haramu! Basi wakikujia, wahukumu baina yao au jipuuze nao. Na ukijipuuza nao, basi wao hawatakudhuru kitu. Na ukiwahukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda waadilifu.
Hao hukithiri kusikiliza ili wapate kuzua, na hukithiri kula mali ya haramu ambayo hayana baraka yoyote, kama vile rushwa na riba na mengineyo. Basi wakikujia kukutaka uwahukumu, wewe wahukumu pindi ukiona hayo yana maslaha, au jipuuze nao. Na ukijipuuza nao hawatokudhuru kwa lolote, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye wa kukulinda na watu. Na ukihukumu baina yao basi hukumu kwa uadilifu alio kuamrisha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda waadilifu, naye huwahifadhi na huwalipa thawabu.
Les exégèses en arabe:
وَكَيۡفَ يُحَكِّمُونَكَ وَعِندَهُمُ ٱلتَّوۡرَىٰةُ فِيهَا حُكۡمُ ٱللَّهِ ثُمَّ يَتَوَلَّوۡنَ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَۚ وَمَآ أُوْلَٰٓئِكَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Na huwaje wakufanye wewe hakimu nao wanayo Taurati yenye hukumu za Mwenyezi Mungu? Kisha baada ya hayo wanageuka. Na hao si wenye kuamini.
Ama ajabu ya watu hawa Mayahudi! Vipi wanataka hukumu yako na hali wao wanayo hukumu ya Mwenyezi Mungu imeandikwa katika Taurati? Na kinacho staajabisha ni kuwa wao huikataa hukumu yako inapo kuwa haikubaliani na mapendeleo yao, ijapo kuwa imewafikiana na ilivyo katika kitabu chao! Watu hawa sio miongoni mwa Waumini wanaoit'ii Haki.
Les exégèses en arabe:
إِنَّآ أَنزَلۡنَا ٱلتَّوۡرَىٰةَ فِيهَا هُدٗى وَنُورٞۚ يَحۡكُمُ بِهَا ٱلنَّبِيُّونَ ٱلَّذِينَ أَسۡلَمُواْ لِلَّذِينَ هَادُواْ وَٱلرَّبَّٰنِيُّونَ وَٱلۡأَحۡبَارُ بِمَا ٱسۡتُحۡفِظُواْ مِن كِتَٰبِ ٱللَّهِ وَكَانُواْ عَلَيۡهِ شُهَدَآءَۚ فَلَا تَخۡشَوُاْ ٱلنَّاسَ وَٱخۡشَوۡنِ وَلَا تَشۡتَرُواْ بِـَٔايَٰتِي ثَمَنٗا قَلِيلٗاۚ وَمَن لَّمۡ يَحۡكُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَٰفِرُونَ
Hakika Sisi tuliteremsha Taurati yenye uwongofu na nuru, ambayo kwayo Manabii walio nyenyekea kiislamu, na wachamngu, na wanazuoni, waliwahukumu Mayahudi; kwani walikabidhiwa kukihifadhi Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Nao wakawa ni mashahidi juu yake. Basi msiwaogope watu, bali niogopeni Mimi. Wala msibadilishe Aya zangu kwa thamani chache. Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.
Hakika Sisi tumemteremshia Musa Taurati. Ndani yake mna uwongofu unao endea Haki, na mna bayana yenye kutoa mwangaza unao nawirisha hukumu wanazo zihukumia Manabii, na wale walio safisha nafsi zao kwa ajili ya Mola wao Mlezi, na wanazuoni wenye kufwata njia ya Manabii, na wale walio chukua ahadi kukihifadhi Kitabu cha Mwenyezi Mungu kisibadilishwe, kwa kukilinda na kushuhudia kuwa hicho ndiyo Haki. Basi msiwakhofu watu mnapo hukumu, na nikhofuni Mimi tu, Mimi Mola wenu Mlezi, Mola Mlezi wa walimwengu wote. Wala msizibadilishe Aya zangu nilizo ziteremsha kwa thamani duni ya kutaka starehe ya dunia, kama vile mrungura au kutaka cheo! Na wote wasio hukumu kwa mujibu alivyo teremsha Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa makafiri.
Les exégèses en arabe:
وَكَتَبۡنَا عَلَيۡهِمۡ فِيهَآ أَنَّ ٱلنَّفۡسَ بِٱلنَّفۡسِ وَٱلۡعَيۡنَ بِٱلۡعَيۡنِ وَٱلۡأَنفَ بِٱلۡأَنفِ وَٱلۡأُذُنَ بِٱلۡأُذُنِ وَٱلسِّنَّ بِٱلسِّنِّ وَٱلۡجُرُوحَ قِصَاصٞۚ فَمَن تَصَدَّقَ بِهِۦ فَهُوَ كَفَّارَةٞ لَّهُۥۚ وَمَن لَّمۡ يَحۡكُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّٰلِمُونَ
Na humo tuliwaandikia ya kwamba roho kwa roho, na jicho kwa jicho, na pua kwa pua, na sikio kwa sikio, na jino kwa jino, na kwa majaraha kisasi. Lakini atakaye samehe basi itakuwa ni kafara kwake. Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhaalimu.
Tumewalizimisha Mayahudi katika Taurati wafuate sharia ya kisasi kwa ajili ya kuhifadhi maisha ya watu. Basi tukahukumu mwenye kuuwa auwawe. Mwenye kutofoa jicho la mtu atofolewe. Kadhaalika pua kwa pua, sikio kwa sikio, jino kwa jino, na jaraha hivyo hivyo lilipiziwe kisasi ikimkinika. (Hiyo ni hukumu ya Mayahudi kama ilivyo katika Kutoka 21.23-25; Mambo ya Walawi 24.18-21; Kumbukumbu la Torati 19.21. Katika Uislamu ipo fursa ya msamaha.) Mwenye kusamehe akatolea sadaka ile haki ya kulipiza kisasi kwa mkhalifu, basi hiyo sadaka huwa ni kafara kwake. Mwenyezi Mungu naye atamfutia sehemu ya madhambi yake. Na watu wasio hukumu kwa mujibu wa alivyo teremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio wenye kudhulumu.
Les exégèses en arabe:
 
Traduction des sens Sourate: Al Mâ'idah
Lexique des sourates Numéro de la page
 
Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahilie - 'Alî Muhsin Al Barwânî - Lexique des traductions

Traduit par 'Alî Muhsin Al Barwânî.

Fermeture