NA LAU kuwa tungeli wateremshia Malaika, na maiti wakazungumza nao, na tukawakusanyia kila kitu mbele yao, bado wasingeli amini, ila Mwenyezi Mungu atake. Lakini wengi wao wamo ujingani.
Hakika hao walio apa kuwa ikiwajia Ishara wataiamini, ni waongo. Mwenyezi Mungu anaijua vilivyo imani yao. Lau kuwa sisi tungeli teremsha Malaika wakawaona kwa macho, na maiti wakawasemeza baada ya kufufuliwa makaburini mwao, na kuwakusanyia kila kitu mbele yao kikiwakabili na kuwabainishia haki, bado wasingeli amini ila akipenda Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa waamini. Na wengi hawaitambui Haki wala hawaifuati, kwa sababu nyoyo zao zimesibiwa na upofu wa kijahiliya.
Na kadhaalika tumemfanyia kila Nabii maadui mashet'ani wa kiwatu, na kijini, wakifundishana wao kwa wao maneno ya kupamba-pamba, kwa udanganyifu. Na angeli penda Mola wako Mlezi wasingeli fanya hayo. Basi waache na wanayo yazua.
Kama ilivyo kuwa hao wamekufanyia uadui na inadi, na hali wewe unataka kuwaongoa, basi kadhaalika tumemfanyia kila Nabii anaye peleka ujumbe wetu, maadui katika wanaadamu majeuri na majini majeuri, ambao wanajificha kwako na huwaoni, wakitiliana wasiwasi kwa maneno ya kupamba-pamba na udanganyifu, yasiyo na ukweli. Basi kwa hayo huingiza ghururi kwa uwongo! Na hayo yote ni kwa kudra ya Mwenyezi Mungu na kutaka kwake. Na lau angeli taka wasingeli fanya hayo. Lakini hayo ni kwa ajili ya kuzisafisha nyoyo za Waumini. Basi waachilie mbali hao walio potea na kufuru zao za maneno yao wanayo yazua.
Na ili nyoyo za wasio amini Akhera zielekee hayo, nao wayaridhie na wayachume wanayo yachuma.
Wao huyapindua maneno ya upotovu wazidanganye nafsi zao na ziridhie, na zielekee huko huko vile vile nyoyo za walio kama wao majeuri wasio iogopa Akhera, wanao itakidi kuwa uhai ni dunia tu, na waingie katika madhambi na maasi kwa sababu ya kuto iamini kwao Siku ya Akhera.
Je, nimtafute hakimu ghairi ya Mwenyezi Mungu, naye ndiye aliye kuteremshieni Kitabu kilicho elezwa waziwazi? Na hao tulio wapa Kitabu wanajua ya kwamba kimeteremshwa na Mola wako Mlezi kwa Haki. Basi usiwe katika wanao tia shaka.
Ewe Nabii! Waambie: Hii ni hukumu ya Mwenyezi Mungu kwa Haki, iliyo bainishwa na Aya zilio zagaa. Basi haijuzu nitafute hukumu isiyo kuwa yake Yeye ya kutupambanua baina yangu na nyinyi. Mwenyewe Subhana kesha hukumu, na ameteremsha Kitabu kitukufu kiwe ni hoja juu yenu. Nanyi mmeshindwa kuleta mfano wake. Nacho kinabainisha Haki na uadilifu. Na wale walio pewa Kitabu wanajua kuwa hii Qur'ani imetoka kwa Mwenyezi Mungu, na imekusanya Haki, kama vilivyo bashiri vitabu vyao, ijapo kuwa wanajaribu kuyaficha hayo. Basi wewe Nabii, pamoja na walio kufuata, msiwe katika wenye kutilia shaka Haki baada ya kubainishwa kwake.
Na yametimia maneno ya Mola Mlezi wako kwa kweli na uadilifu. Hapana awezaye kuyabadilisha maneno yake. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua.
Na hakika hukumu ya Mwenyezi Mungu imekwisha toka. Basi maneno ya Mola wako Mlezi ya kweli na ya uadilifu yametimia kwa kuteremshwa Kitabu hichi Kitukufu, chenye kukusanya ukweli. Na ndani imo mizani ya kweli ya kupimia Haki na upotovu. Wala hapana wa kuyageuza maneno ya Mwenyezi Mungu na Kitabu chake. Naye Subhana ni Mwenye kusikia kila lisemwalo, Mwenye kukijua kila kinacho toka kwao.
Na ukiwat'ii wengi katika hawa waliomo duniani watakupoteza na Njia ya Mwenyezi Mungu. Hawa hawafuati ila dhana tu, na hawakuwa ila ni wenye kusema uwongo tu.
Na ikiwa Subhanahu ndiye mwenye hukumu ya uadilifu inayo rejewa kwenye Vitabu vyake katika kutafuta Haki na kuijua, basi ewe Nabii, usiwe wewe na walio pamoja nawe, mkamfuata yeyote anaye achana na kauli ya Haki, hata ikiwa hao ni wengi wa idadi. Kwani ukiwafuata aghlabu ya watu ambao hawategemei Sharia iliyo teremshwa na Mwenyezi Mungu, watakuweka mbali na Njia ya Haki iliyo nyooka. Na hiyo ndiyo Njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na watu hao hawendi ila nyuma ya dhana na mawazo tu, na wala hawasemi ila kwa kukisia tu; hawategemei hoja na ushahidi.
Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mjuzi kushinda wote kuwajua walio potea Njia yake, na ndiye Mjuzi kushinda wote kuwajua walio hidika.
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye kujua kwa ujuzi ambao hapana mfano wake, kuwajua hao ambao wamekuwa mbali na Njia ya Haki, na hao ambao wameongoka na uwongofu ukawa ndio sifa yao.
Basi kuleni katika walio somewa jina la Mwenyezi Mungu, ikiwa mnaziamini Aya zake.
Ilivyo kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye anaye wajua walio hidika na walio potea, basi msielekee kwenye upotovu wa washirikina wa kuharimisha baadhi ya nyama hoa (nyama wa kufuga). Basi kuleni katika hao, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu amekuruzukuni hao, na amewafanya ni halali na wazuri, na hapana madhara kuwala. Na mnapo wachinja litajeni jina la Mwenyezi Mungu juu yao, maadamu nyinyi mnamuamini Yeye na mnamnyenyekea.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
Résultats de la recherche:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".