Wala msiseme kuwa wale waliouwawa katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni maiti. Bali hao ni hai. Lakini nyinyi hamtambui.[1]
[1] Inajulikana kuwa kipenzi hakiachiwi na wenye akili timamu, isipokuwa kwa ajili ya kipenzi kilicho juu zaidi na kikubwa kukiliko. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kwamba mwenye kuuawa katika njia yake akipigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, ili neno la Mwenyezi Mungu liwe ndilo la juu zaidi; na dini yake iwe iliyo dhahiri zaidi. Basi yeye kwa hakika hajakosa uhai alioupenda, bali (alipouawa) alipata uhai mkubwa na kamili zaidi kuliko mnavyofikiria nyinyi. (Tafsir Assa'dii)
Wale ambao ukiwapata msiba, husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.[1]
[1] Wao husema hivyo kwa sababu wanajua kwamba wanamilikiwa na Mwenyezi Mungu, wanasimamiwa chini ya amri yake na uendeshaji wake. Kwa hivyo, hatuna chochote katika nafsi zetu wala mali zetu. Na akitujaribu kwa kitu katika hayo, basi Yeye Mwingi wa Rehema atakuwa amewaendesha wamilikiwa wake na mali zake. Kwa hivyo haifai kuwa na pingamizi lolote dhidi yake. (Tafsir Assa'dii)
Hakika, vilima vya Safaa na Marwa ni katika alama za Mwenyezi Mungu. Basi, anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akafanya Umra, si kosa kwake kuvizunguka. Na anayejitendea mwenyewe kheri. Basi bila ya shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye shukrani na Mwenye elimu.
Hakika, wale wanaoficha tuliyoyateremsha, nazo ni hoja zilizo wazi na uwongofu baada ya Sisi kuzibainisha kwa watu Kitabuni. Hao anawalaani Mwenyezi Mungu, na wanawalaani kila wenye kulaani.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
સંશોધનના પરિણામો:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".