Check out the new design

કુરઆન મજીદના શબ્દોનું ભાષાંતર - સવાહિલી ભાષાતર - મરકઝ રુવાદ અત્-તરજુમા * - ભાષાંતરોની અનુક્રમણિકા


શબ્દોનું ભાષાંતર સૂરહ: અલ્ બકરહ   આયત:

Al-Baqarah

الٓمٓ
Alif Lam Mim.[1]
[1] Ama herufi za mkato mwanzoni mwa sura mbalimbali. Lililo salama zaidi kuhusiana nazo ni kukaa kimya na kutoziingilia maana zake bila ya dalili ya Kisheria, pamoja na kuwa na yakini kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuziteremsha bure, bali kwa hekima tusiyoijua. (Tafsir As-Sa'dii)
અરબી તફસીરો:
ذَٰلِكَ ٱلۡكِتَٰبُ لَا رَيۡبَۛ فِيهِۛ هُدٗى لِّلۡمُتَّقِينَ
Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu.[1]
[1] Na kwa sababu shaka ni kusitasita kati ya mambo, basi kitu chenye shaka hakiwezi kumuongoa mtu. Na kwa sababu sifa ya Qur-aani ni kwamba haina shaka yoyote, basi ikalazimu kwamba ni yenye kuongoa. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akasema: "Ni uwongofu kwa wachamungu" peke yao. Kwa sababu, wasiokuwa wachamungu na wakaidi hawakosi kuwa na shaka katika jambo hata kama halina shaka yoyote. (Tafsir Al-Baqa'ii)
અરબી તફસીરો:
ٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡغَيۡبِ وَيُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَمِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ يُنفِقُونَ
Ambao huyaamini ya ghaibu na hushika Sala, na hutoa katika[1] tuliyowapa (tuliyowaruzuku).
[1] Na alitumia neno “min (katika)” linalomaanisha baadhi (ya kitu), ili awatanabahishe kuwa yeye kwa hakika hakuta kutoka kwao isipokuwa sehemu ndogo kutoka kwa mali zao, ambayo haina madhara kwao wala uzito wowote, bali wao wanafaidika kwa kuitoa, na pia ndugu zao wanafaidika kwayo.
અરબી તફસીરો:
وَٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبۡلِكَ وَبِٱلۡأٓخِرَةِ هُمۡ يُوقِنُونَ
Na ambao wanayaamini yaliyoteremshwa kwako, na yaliyoteremshwa kabla yako; na Akhera wana yakini nayo.
અરબી તફસીરો:
أُوْلَٰٓئِكَ عَلَىٰ هُدٗى مِّن رَّبِّهِمۡۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ
Hao wapo juu ya uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio waliofaulu.[1]
[1] Kwa sababu Qur-ani ndio uwongofu wao, limetumika neno "juu" ili kuifananisha hali ya kuimarika kwa Waumini katika uwongofu na uthabiti wao juu yake; na kujaribu kwao kuuongeza na kutembea katika njia za heri. Na mwonekano wa (mtu) aliyepanda kipando (kama farasi) katika kuwa kwake juu ya kipando hicho, na uwezo wake wa kukiendesha na kukifanya kuwa kitiifu. (Tafsir At-Tahrir Wat-tanwiir cha Ibn 'Aashuur)
અરબી તફસીરો:
 
શબ્દોનું ભાષાંતર સૂરહ: અલ્ બકરહ
સૂરહ માટે અનુક્રમણિકા પેજ નંબર
 
કુરઆન મજીદના શબ્દોનું ભાષાંતર - સવાહિલી ભાષાતર - મરકઝ રુવાદ અત્-તરજુમા - ભાષાંતરોની અનુક્રમણિકા

રુવાદ ભાષાંતર કેન્દ્રની ટીમ દ્વારા અને રબ્વાહ ઇસ્લામિક પ્રચાર કાર્યાલય અને વિવિધ ભાષાઓમાં ઇસ્લામની સામગ્રી પ્રસ્તુત કરતું સંગઠનના સહયોગથી

બંધ કરો