Check out the new design

Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassara da harshen Sawahili - Abdullah Muhammad da Nasir Khamis * - Teburin Bayani kan wasu Fassarori


Fassarar Ma'anoni Sura: Houd   Aya:
إِن نَّقُولُ إِلَّا ٱعۡتَرَىٰكَ بَعۡضُ ءَالِهَتِنَا بِسُوٓءٖۗ قَالَ إِنِّيٓ أُشۡهِدُ ٱللَّهَ وَٱشۡهَدُوٓاْ أَنِّي بَرِيٓءٞ مِّمَّا تُشۡرِكُونَ
«Sisi hatusemi isipokuwa kwamba baadhi ya waungu wetu wamekutia wazimu kwa sababu ya kukataza kwako wasiabudiwe.» Akawaambia, «Mimi namshuhudisha Mwenyezi Mungu haya ninayoyasema na nawashuhudiza nyinyi kwamba mimi niko mbali na vile mnavyovishirikisha
Tafsiran larabci:
مِن دُونِهِۦۖ فَكِيدُونِي جَمِيعٗا ثُمَّ لَا تُنظِرُونِ
badala ya Mwenyezi Mungu, miongoni mwa wale wafananishwao na Yeye na masanamu. Basi angalieni na mfanye bidii, nyinyi na hao mnaodai kati ya waungu wenu, kunipatia madhara, kisha msilicheleweshe hilo hata kitambo kidogo kiasi cha kupepesa jicho. Hivyo ni kwamba Hūd ana imani thabiti kwamba hayatampata yeye kutoka kwao wala kutoka kwa waungu wao madhara yoyote.
Tafsiran larabci:
إِنِّي تَوَكَّلۡتُ عَلَى ٱللَّهِ رَبِّي وَرَبِّكُمۚ مَّا مِن دَآبَّةٍ إِلَّا هُوَ ءَاخِذُۢ بِنَاصِيَتِهَآۚ إِنَّ رَبِّي عَلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ
«Mimi nimetegemea kwa Mwenyezi Mungu, Mola wangu na Mola wenu, Mmiliki wa kila kitu na Mwenye kukiendesha. Hakuna kitu chenye kunipata isipokuwa kwa amri Yake. Na Yeye Ndiye Muweza wa kila kitu, Hakuna kitu chochote kinachotambaa kwnye ardhi hii isipokuwa Mwenyezi Mungu Amekimiliki na kiko chini ya mamlaka Yake na uendeshaji Wake. Hakika Mola wangu Yuko kwenye njia iliyolingana sawa, kwa maana kwamba ni muadilifu katika hukumu Zake, sheria Zake na amri Zake, Anamlipa mwema kwa wema Wake na muovu kwa uovu wake.
Tafsiran larabci:
فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَقَدۡ أَبۡلَغۡتُكُم مَّآ أُرۡسِلۡتُ بِهِۦٓ إِلَيۡكُمۡۚ وَيَسۡتَخۡلِفُ رَبِّي قَوۡمًا غَيۡرَكُمۡ وَلَا تَضُرُّونَهُۥ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ رَبِّي عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٍ حَفِيظٞ
«Mkiyapa mgongo yale ninayowalingania kwayo ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtakasia ibada, basi nimeshaufikisha ujumbe wa Mola wangu kwneu na hoja ishasimama kwenu nyinyi, na Mwenyezi Mungu atawaangamiza kwa kuwa hamkumuamini, na Atawaleta watu wengine ambao watashika nafasi zenu katika majumba yenu na mali yenu, na ambao watamtakasia Mwenyezi Mungu ibada. Na nyinyi hamtamdhuru Yeye kitu chochote. Hakika Mola wangu amekidhibiti kila kitu na kukihifadhi; Yeye Ndiye Mwenye kunitunza msinifanyie ubaya.
Tafsiran larabci:
وَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا نَجَّيۡنَا هُودٗا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ بِرَحۡمَةٖ مِّنَّا وَنَجَّيۡنَٰهُم مِّنۡ عَذَابٍ غَلِيظٖ
Na ilipokuja amri yetu kuwaadhibu watu wa Hūd, tulimuokoa Hūd na Waumini miongoni mwao kwa wema wetu juu yao na huruma, na tukawaokoa wao na adhabu kali Aliyoishukisha Mwenyezi Mungu kwa hao 'Ād, wakapambaukiwa na huku hakuna kionekanacho isipokuwa makazi yao.
Tafsiran larabci:
وَتِلۡكَ عَادٞۖ جَحَدُواْ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِمۡ وَعَصَوۡاْ رُسُلَهُۥ وَٱتَّبَعُوٓاْ أَمۡرَ كُلِّ جَبَّارٍ عَنِيدٖ
Hao ndio'Ād, walikanusha aya za Mwenyezi Mungu, wakaasi Mitume Wake na wakatii amri ya kila anayemfanyia kiburi Mwenyezi mungu asiyekubali haki wala kuinyoshea shingo.
Tafsiran larabci:
وَأُتۡبِعُواْ فِي هَٰذِهِ ٱلدُّنۡيَا لَعۡنَةٗ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ أَلَآ إِنَّ عَادٗا كَفَرُواْ رَبَّهُمۡۗ أَلَا بُعۡدٗا لِّعَادٖ قَوۡمِ هُودٖ
Wakafuatiwa, katika ulimwengu huu, na laana ya Mwenyezi Mungu, na wakafuatwa na hasira Zake Siku ya Kiyama. Jueni mtanabahi kwamba 'Ād walimkanusha Mola wao na wakawakanusha Mitume Wake. Jueni mtanabahi kwamba umbali na rehema ya Mwenyezi Mungu na maangamivu yatawashukia 'Ād, watu wa Hūd, kwa sababu ya ushirikina wao na kukanusha kwao neema ya Mola wao.
Tafsiran larabci:
۞ وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمۡ صَٰلِحٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥۖ هُوَ أَنشَأَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ وَٱسۡتَعۡمَرَكُمۡ فِيهَا فَٱسۡتَغۡفِرُوهُ ثُمَّ تُوبُوٓاْ إِلَيۡهِۚ إِنَّ رَبِّي قَرِيبٞ مُّجِيبٞ
Na tulimtuma kwenda kwa Thamūd ndugu yao Ṣāliḥ akasema kuwaambia, «Enyi watu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake. Nyinyi hamuna mungu yoyote anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu. Basi mtakasieni ibada. Yeye Ndiye Aliyeanza kuwaumba kutokamana na ardhi, kwa kumuumba baba yenu Ādam kutokamana na hiyo, na akawafanya nyinyi ni wenye kuiimarisha. Hivyo basi, muombeni Awasamehe madhambi yenu, na rudini Kwake kwa kutubia kidhati. Hakika Mola wangu yuko karibu na yule anayemtakasia ibada na akawa na hamu ya kuja Kwake kwa kutubia, ni Mwenye kumuitikia anapomuomba.»
Tafsiran larabci:
قَالُواْ يَٰصَٰلِحُ قَدۡ كُنتَ فِينَا مَرۡجُوّٗا قَبۡلَ هَٰذَآۖ أَتَنۡهَىٰنَآ أَن نَّعۡبُدَ مَا يَعۡبُدُ ءَابَآؤُنَا وَإِنَّنَا لَفِي شَكّٖ مِّمَّا تَدۡعُونَآ إِلَيۡهِ مُرِيبٖ
Tahamūd wakasema kumwambia Ṣāliḥ, «Kwa hakika, kabla ya neno hili ulilotwambia, tulikuwa tuna matumaini kwamba utakuwa ni kiongozi mwenye kusikizwa,. Je, unatukataza kuwaabudu waungu ambao baba zetu walikuwa wakiwaabudu? Hakika sisi tuko kwenye shaka yenye kutia wasiwasi juu ya mwito wako wa kutuita sisi tumuabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake.
Tafsiran larabci:
 
Fassarar Ma'anoni Sura: Houd
Teburin Jerin Sunayen Surori Lambar shafi
 
Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassara da harshen Sawahili - Abdullah Muhammad da Nasir Khamis - Teburin Bayani kan wasu Fassarori

Dr. Abdullahi Muhammad Abubakar da Sheikh Nasir Khamis suka fassarata.

Rufewa