Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis Abdurahman * - Translations’ Index


Translation of the meanings Surah: Hūd   Ayah:

Surat Hud

الٓرۚ كِتَٰبٌ أُحۡكِمَتۡ ءَايَٰتُهُۥ ثُمَّ فُصِّلَتۡ مِن لَّدُنۡ حَكِيمٍ خَبِيرٍ
Alif, Lām, Rā’. Maneno yashatangulia, kuhusu herufi zinazokatwa, katika mwanzo wa Sura ya Al-Baqarah. Hiki ni Kitabu ambacho Mwenyezi Mungu Amemteremshia Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, na ambacho aya zake zimepangwa vizuri zisizo na kasoro wala ubatilifu, kisha zimefafanuliwa kwa maamrisho na makatazo na maelezo ya halali na haramu yatokayo kwa Mwenyezi Mungu Aliye na hekima katika uendeshaji mambo Aliye Mtambuzi wa vile yanavyoishia.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَلَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّا ٱللَّهَۚ إِنَّنِي لَكُم مِّنۡهُ نَذِيرٞ وَبَشِيرٞ
Na kuteremsha Qur’ani na kuzifafanua hukumu zake na kuzipambanua na kuipanga vizuri, ili mpate kumuabudu Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Asiye na mshirika. Mimi kwenu nyinyi, enyi watu, ni muonyaji kutoka kwa Mwenyezi Mungu mwenye kuwaonya mateso Yake na ni mwenye kuwabashiria habari njema ya malipo Yake mema.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَأَنِ ٱسۡتَغۡفِرُواْ رَبَّكُمۡ ثُمَّ تُوبُوٓاْ إِلَيۡهِ يُمَتِّعۡكُم مَّتَٰعًا حَسَنًا إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمّٗى وَيُؤۡتِ كُلَّ ذِي فَضۡلٖ فَضۡلَهُۥۖ وَإِن تَوَلَّوۡاْ فَإِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٖ كَبِيرٍ
Na muombeni Awasamehe dhambi zenu kisha mrudi Kwake hali ya kujuta, Atawapumbaza katika ulimwengu wenu kwa kuwastarehesha vizuri kwa maisha mazuri humo mpaka ufikie kikomo muda wenu wa kuishi na Ampe kila mwenye wema wa elimu na matendo malipo makamilifu ya wema wake yasiyo na upungufu. Na mkiyapa mgongo yale ninayowaitia kwayo, basi nawachelea nyinyi kufikiwa na adhabu ya Siku ngumu, nayo ni Siku ya Kiyama. Hili ni onyo kali kwa aliyezipa mgongo amri za Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na akawakanusha Mitume Wake.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِلَى ٱللَّهِ مَرۡجِعُكُمۡۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ
Ni kwa Mwenyezi Mungu marejeo yenu baada ya kufa kwenu nyote, basi jitahadharini na mateso Yake. Na Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, ni Muweza wa kuwafufua nyinyi, kuwakusanya na kuwalipa.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَلَآ إِنَّهُمۡ يَثۡنُونَ صُدُورَهُمۡ لِيَسۡتَخۡفُواْ مِنۡهُۚ أَلَا حِينَ يَسۡتَغۡشُونَ ثِيَابَهُمۡ يَعۡلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعۡلِنُونَۚ إِنَّهُۥ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ
Hakika washirikina hawa wanaficha ukafiri katika nyoyo zao wakidhani kwamba yale ambayo nafsi zao zinayadhamiria yanafichika kwa Mwenyezi Mungu. Kwani hawajui wanapoifinika miili yao kwa nguo zao kwamba hayafichiki kwa Mwenyezi Mungu mambo yao ya siri na ya wazi? Hakika Yeye ni Mjuzi wa kila ambacho vifua vyao vinakifinika miongoni mwa nia, madhamirio na siri.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ وَمَا مِن دَآبَّةٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِ رِزۡقُهَا وَيَعۡلَمُ مُسۡتَقَرَّهَا وَمُسۡتَوۡدَعَهَاۚ كُلّٞ فِي كِتَٰبٖ مُّبِينٖ
Mwenyezi Mungu Amechukua dhamana kuviruzuku vyote vinavyotambaa kwenye uso wa ardhi, kwa hisani Yake, na Anajua mahala pa kutulia kwake katika uhai wake na baada ya kufa kwake, na Anajua mahala ambapo vitakufa. Yote hayo yameandikwa kwenye Kitabu kilichoko kwa Mwenyezi Mungu chenye kueleza yote hayo.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَهُوَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ وَكَانَ عَرۡشُهُۥ عَلَى ٱلۡمَآءِ لِيَبۡلُوَكُمۡ أَيُّكُمۡ أَحۡسَنُ عَمَلٗاۗ وَلَئِن قُلۡتَ إِنَّكُم مَّبۡعُوثُونَ مِنۢ بَعۡدِ ٱلۡمَوۡتِ لَيَقُولَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ مُّبِينٞ
Na Yeye Ndiye Ambaye Aliumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake kwa Siku Sita na Arshi Yake ilikuwa iko juu ya maji kabla ya hapo, Apate kuwajaribu nyinyi, ni nani kati yenu mzuri zaidi wa utiifu na utendaji. Utendaji wenye kumtakasia Mwenyezi Mungu, wenye kulingana na vile Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, alivyokuwa. Na lau unasema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina wa watu wako, «Nyinyi mtafufuliwa mkiwa hai baada ya kufa kwenu.» Watafanya haraka kukanusha na watasema, «Haikuwa hii Qur’ani unayotusomea isipokuwa ni uchawi ulio wazi.»
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَئِنۡ أَخَّرۡنَا عَنۡهُمُ ٱلۡعَذَابَ إِلَىٰٓ أُمَّةٖ مَّعۡدُودَةٖ لَّيَقُولُنَّ مَا يَحۡبِسُهُۥٓۗ أَلَا يَوۡمَ يَأۡتِيهِمۡ لَيۡسَ مَصۡرُوفًا عَنۡهُمۡ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ
Na lau tutawacheleweshea adhabu, hawa washirikina, mpaka muda maalumu, wakaona imekawia, watasema kwa njia ya shere na kukanusha, «Ni kitu gani kinachozuia adhabu hii isitukie ikiwa ni kweli?» Jueni mtanabahi, siku itakapowajia adhabu hiyo hakuna atakayeweza kuwaondolea, wala yoyote mwenye kuizuia, na iatawazunguka wao, kutoka kila upande, adhabu waliokuwa wakiifanyia shere kabla haijawajia..
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَئِنۡ أَذَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ مِنَّا رَحۡمَةٗ ثُمَّ نَزَعۡنَٰهَا مِنۡهُ إِنَّهُۥ لَيَـُٔوسٞ كَفُورٞ
Na lau tutampa mwanadamu neema ya afya na amani na zisokuwa hizo kisha tukamuondolea, hakika yeye atakuwa ni mwenye kukata tamaa sana na rehema ya Mwenyezi Mungu, ni mkanushaji sana wa neema ambazo Mwenyezi Mungu Amemneemesha nazo.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَئِنۡ أَذَقۡنَٰهُ نَعۡمَآءَ بَعۡدَ ضَرَّآءَ مَسَّتۡهُ لَيَقُولَنَّ ذَهَبَ ٱلسَّيِّـَٔاتُ عَنِّيٓۚ إِنَّهُۥ لَفَرِحٞ فَخُورٌ
Na lau tutamnyoshea mwanadamu dunia yake na tukamkunjulia riziki yake baada ya dhiki za maisha, atasema hapo, «Nimeondokewa na dhiki na shida.» Hakika yeye ni mwenye kujigamba kwa hizo neema, ni mwenye kuendelea sana katika kujifahiri na kujitukuza kwa watu.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِلَّا ٱلَّذِينَ صَبَرُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُم مَّغۡفِرَةٞ وَأَجۡرٞ كَبِيرٞ
Lakini wale waliosubiri juu ya yaliyowapata ya shida kwa kumuamini Mwenyezi Mungu na kutaka malipo kutoka Kwake, wakafanya mema kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema Zake, wao watakuwa na msamaha wa dhambi zao na malipo makubwa Akhera.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَلَعَلَّكَ تَارِكُۢ بَعۡضَ مَا يُوحَىٰٓ إِلَيۡكَ وَضَآئِقُۢ بِهِۦ صَدۡرُكَ أَن يَقُولُواْ لَوۡلَآ أُنزِلَ عَلَيۡهِ كَنزٌ أَوۡ جَآءَ مَعَهُۥ مَلَكٌۚ إِنَّمَآ أَنتَ نَذِيرٞۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ وَكِيلٌ
Huenda wewe, ewe Mtume, kwa ukafiri na ukanushaji mkubwa unaouona kwao, ukawa ni mwenye kuyaacha baaadhi ya yale unaoyoletewa wahyi kati ya yale ambayo Mwenyezi Mungu Alikuteremshia na Akakuamuru kuyafikisha, na kifua chako kikawa ni chenye kuhisi dhiki kwa hayo, kwa kuogopa wasije wakataka baadhi ya mambo kutoka kwako kwa njia ya kukusumbua, kama vile kusema, «Kwa nini asiteremshiwe mali mengi, au asijiwe na Malaika ambaye atamuamini katika ujumbe wake?» Basi wafikishie yale niliyokuletea wahyi kwayo, kwani lako wewe si lingine isipokuwa ni kuonya kwa yale uliyoletewa wahyi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtunzi wa kila kitu, Anaendesha mambo yote ya viumbe vyake.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَمۡ يَقُولُونَ ٱفۡتَرَىٰهُۖ قُلۡ فَأۡتُواْ بِعَشۡرِ سُوَرٖ مِّثۡلِهِۦ مُفۡتَرَيَٰتٖ وَٱدۡعُواْ مَنِ ٱسۡتَطَعۡتُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Au je, washirikina hawa, miongoni mwa watu wa Makkah, wanasema kwamba Muhammad ameizua hii Qur’ani? Waambie basi, «Iwapo mambo ni kama mnavyodai, leteni sura kumi mfano wake za kuzuliwa, na muwaite mnaowaweza miongoni mwa viumbe wote wa Mwenyezi Mungu, ili wawasaidie kuzileta hizi sura kumi, iwapo nyinyi ni wa kweli katika madai yenu.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَإِلَّمۡ يَسۡتَجِيبُواْ لَكُمۡ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّمَآ أُنزِلَ بِعِلۡمِ ٱللَّهِ وَأَن لَّآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ فَهَلۡ أَنتُم مُّسۡلِمُونَ
Iwapo washirikina hawa hawatawaitikia nyinyi, ewe Mtume na walio pamoja na wewe, kwa yale mnayowaitia , kwa kulemewa kufanya hivyo, basi jueni kwamba hii Qur’ani, kwa hakika Mwenyezi Mungu Amemteremshia Mtume Wake kwa ujuzi Wake, na si maneno ya binadamu. Na jueni kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu. Je nyinyi, baada ya kusimama hoja hii kwenu, ni wenye kujisalimisha, ni wenye kunyosha shingo kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake?
Arabic explanations of the Qur’an:
مَن كَانَ يُرِيدُ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيۡهِمۡ أَعۡمَٰلَهُمۡ فِيهَا وَهُمۡ فِيهَا لَا يُبۡخَسُونَ
Yoyote atakaye, kwa matendo yake, maisha ya kilimwengu na starehe zake, tutawapa wao walichogawiwa cha malipo mazuri ya matendo yao katika uhai wa kilimwengu, yakiwa kamili yasiyopunguzwa.
Arabic explanations of the Qur’an:
أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ لَيۡسَ لَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ إِلَّا ٱلنَّارُۖ وَحَبِطَ مَا صَنَعُواْ فِيهَا وَبَٰطِلٞ مَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Hao hawana huko Akhera isipokuwa Moto wa Jahanamu wakiadhibika kwa joto lake, na yatawaondokea wao manufaa na yale mema waliyoyatenda, na matendo yao yatatanguka kwa kuwa hayakuwa yanakusudiwa Mwenyezi Mungu.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَفَمَن كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّهِۦ وَيَتۡلُوهُ شَاهِدٞ مِّنۡهُ وَمِن قَبۡلِهِۦ كِتَٰبُ مُوسَىٰٓ إِمَامٗا وَرَحۡمَةًۚ أُوْلَٰٓئِكَ يُؤۡمِنُونَ بِهِۦۚ وَمَن يَكۡفُرۡ بِهِۦ مِنَ ٱلۡأَحۡزَابِ فَٱلنَّارُ مَوۡعِدُهُۥۚ فَلَا تَكُ فِي مِرۡيَةٖ مِّنۡهُۚ إِنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يُؤۡمِنُونَ
Je, yule aliyekuwa kwenye hoja na uangalifu kutoka kwa Mola wake katika kile anachokiamini na anachokilingania kwa wahyi ambao ndani yake Mwenyezi Mungu Ameuteremsha ushahidi huu, na ukafuatiwa na hoja nyingine kutoka Kwake yenye kuutolea ushahidi, nayo ni Jibrili au ni Muhammad, rehema na amani ziwashukie, na ukatiliwa nguvu na dalili ya tatu kabla ya Qur’ani, nayo ni Taurati - Kitabu alichotemshiwa Mūsā chenye uongozi na rehema kwa waliokiamini- (je yeye) ni kama yule ambaye hamu yake ilikuwa ni maisha yenye kutoweka na pambo lake? Hao wanaiamini hii Qur’ani wanazifuata hukumu zake kivitendo. Na mwenye kuikanusha hii Qur’ani, miongoni mwa wale waliojikusanya kumpinga Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, basi malipo yake ni Moto, hapana budi atauingia. Basi usiwe na shaka juu ya jambo la Qur’ani na kuwa inatoka kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka baada ya dalili na hoja kulitolea ushahidi hilo. Na ujue kwamba Dini hii ndio ukweli unaotoka kwa Mola wako, lakini wengi wa watu hawaamini wala hawayatendi yale wanayoamrishwa. Huu ni muongozo unaowaenea ummah wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًاۚ أُوْلَٰٓئِكَ يُعۡرَضُونَ عَلَىٰ رَبِّهِمۡ وَيَقُولُ ٱلۡأَشۡهَٰدُ هَٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ كَذَبُواْ عَلَىٰ رَبِّهِمۡۚ أَلَا لَعۡنَةُ ٱللَّهِ عَلَى ٱلظَّٰلِمِينَ
Na hakuna yoyote aliye dhalimu zaidi kuliko yule aliyemzulia Mwenyezi Mungu urongo. Hao wataorodheshwa kwa Mola wao Siku ya Kiyama, ili Awahesabu kwa matendo yao. Na watasema waliohudhuria miongoni mwa Malaika na Manabii na wengineo, «Hawa ndio wale waliosema urongo kumsingizia Mola wao ulimwenguni. Mwenyezi Mungu Amewakasirikia wao na Amewalaani laana isiyokatika, kwa kuwa udhalimu walioufanya umekuwa ni sifa inayoambatana na wao.
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱلَّذِينَ يَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَيَبۡغُونَهَا عِوَجٗا وَهُم بِٱلۡأٓخِرَةِ هُمۡ كَٰفِرُونَ
Hawa madhalimu ni wale ambao wanawazuia watu na njia ya Mwenyezi Mungu yenye kupelekea kumuubudu na wanataka njia hizi ziwe kombo ziambatane na matamanio yao na wao wanaikanusha Akhera, hawaamini kufufuliwa wa kulipwa.
Arabic explanations of the Qur’an:
أُوْلَٰٓئِكَ لَمۡ يَكُونُواْ مُعۡجِزِينَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا كَانَ لَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِنۡ أَوۡلِيَآءَۘ يُضَٰعَفُ لَهُمُ ٱلۡعَذَابُۚ مَا كَانُواْ يَسۡتَطِيعُونَ ٱلسَّمۡعَ وَمَا كَانُواْ يُبۡصِرُونَ
Makafiri hao hawakuwa ni wenye kumhepa Mwenyezi Mungu kwa kumkimbia, na hawakuwa na wasaidizi wa kuwazuia wao wasipata mateso ya Mwenyezi Mungu. Wataongezewa adhabu katika Jahanamu, kwa kuwa wao walikuwa hawawezi kuisikia Qur’ani kwa namna ya kuwafanya wanufaike au wazione alama za Mwenyezi Mungu katika ulimwengu kwa namana ya kuwafanya waongoke, kwani wao walikuwa wameshughulika na ukafiri ambao walikuwa wamedumu nao.
Arabic explanations of the Qur’an:
أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ وَضَلَّ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ
Hao ndio wale waliopata hasara ya nafsi zao kwa kumzulia kwao Mwenyezi Mungu urongo na waliwaondokea wao wauungu waliokuwa wakiwazua na kudai kwamba wao watawaombea.
Arabic explanations of the Qur’an:
لَا جَرَمَ أَنَّهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ هُمُ ٱلۡأَخۡسَرُونَ
Ukweli ni kwamba wao kesho Akhera ni wenye kapata hasara zaidi kibiashara, kwa kuwa wao waliacha daraja za Pepo na kuchukuwa mashimo ya Moto, kwa hivyo wakawa kwenye Moto wa Jahanamu. Huko ndiko kupata hasara waziwazi.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَأَخۡبَتُوٓاْ إِلَىٰ رَبِّهِمۡ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَنَّةِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ
Hakika wale ambao walimuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakafanya matendo mema, wakanyenyekea kwa Mwenyezi Mungu katika kila walichoamrishwa na kukatazwa. Hao ndio watu wa Peponi, hawatakufa humo wala hawatatoka kabisa.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ مَثَلُ ٱلۡفَرِيقَيۡنِ كَٱلۡأَعۡمَىٰ وَٱلۡأَصَمِّ وَٱلۡبَصِيرِ وَٱلسَّمِيعِۚ هَلۡ يَسۡتَوِيَانِ مَثَلًاۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Mfano wa makundi mawili, ya ukafiri na Imani, ni mfano wa kipofu asiyeona na kiziwi asiyesikia na yule anayeona na kusikia: kundi la ukafiri haliioni haki likapata kuifuata wala halimsikii mlinganizi wa Mwenyezi Mungu likapata kuongoka kwa sababu yake. Ama kundi la Imani limishaziona hoja za Mwenyezi Mungu na limemsikia mlinganizi wa Mwenyezi Mungu na limemuitikia. Je, yanafanana makundi mawili haya? Kwani hamzingatii na mkafikiri?
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوۡمِهِۦٓ إِنِّي لَكُمۡ نَذِيرٞ مُّبِينٌ
Hakika tulimtuma Nūḥ, kwa watu wake akasema kuwaambia, «Mimi ni muonyaji kwenu adhabu ya Mwenyezi Mungu, ni mwenye kuwabainishia yale niliyotumwa kwenu ya maamrisho ya Mwenyezi Mungu na makatazo yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَن لَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّا ٱللَّهَۖ إِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٍ أَلِيمٖ
«Nawaamrisha kwamba msiabudu isipokuwa Mwenyezi Mungu. Mimi nawachelea nyinyi, mkitompwekesha Mwenyezi Mungu, Peke Yake, kwa Ibada, adhabu ya Siku yenye kuumiza.»
Arabic explanations of the Qur’an:
فَقَالَ ٱلۡمَلَأُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦ مَا نَرَىٰكَ إِلَّا بَشَرٗا مِّثۡلَنَا وَمَا نَرَىٰكَ ٱتَّبَعَكَ إِلَّا ٱلَّذِينَ هُمۡ أَرَاذِلُنَا بَادِيَ ٱلرَّأۡيِ وَمَا نَرَىٰ لَكُمۡ عَلَيۡنَا مِن فَضۡلِۭ بَلۡ نَظُنُّكُمۡ كَٰذِبِينَ
Wakasema wakubwa wa ukafiri miongoni mwa watu wake, «Wewe si Malaika bali wewe ni binadamu, inakuwaje wewe uletewe wahyi bila sisi? Na hatukuoni umefuatwa isipokuwa na watwevu wetu, na wao wamekufuata bila kufikiria wala kupima. Na sisi hatuwaoni nyinyi kuwa muna ubora wowote juu yetu, wa riziki wala mali, tangu mlipoingia kwenye dini yenu hii. Bali sisi tunaamini kwamba nyinyi ni warongo katika madai yenu.
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَءَيۡتُمۡ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّي وَءَاتَىٰنِي رَحۡمَةٗ مِّنۡ عِندِهِۦ فَعُمِّيَتۡ عَلَيۡكُمۡ أَنُلۡزِمُكُمُوهَا وَأَنتُمۡ لَهَا كَٰرِهُونَ
Nūḥ akasema, «Enyi watu wangu, iwapo mimi niko kwenye hoja iliyo wazi kutoka kwa Mola wangu katika yale niliyokuja nayo kutoka Kwake, itawafunukia nyinyi kwamba mimi niko kwenye haki inayotoka Kwake na kwamba Ameniletea rehema kutoka Kwake, nayo ni unabii na utume na kwamba Mwenyezi Mungu Amewafichia hayo kwa sababu ya ujinga wenu na kuhadaika kwenu. Basi je kwani inafaa niwalazimishe nayo kwa nguvu hali nyinyi mnaikanusha? Hatutafanya hivyo, lakini tunayategemeza mambo yenu kwa Mwenyezi Mungu ili Atoe uamuzi Anaoutaka kuhusu mambo yenu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَيَٰقَوۡمِ لَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مَالًاۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِۚ وَمَآ أَنَا۠ بِطَارِدِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْۚ إِنَّهُم مُّلَٰقُواْ رَبِّهِمۡ وَلَٰكِنِّيٓ أَرَىٰكُمۡ قَوۡمٗا تَجۡهَلُونَ
Nūḥ, amani imshukiye, akaendelea kuwaambia watu wake, «Enyi watu wangu, siwaombi kwa kuwaita nyinyi kumpwekesha Mwenyezi Mungu, munipatie mali baada ya kuamini kwenu, kwani malipo ya ushauri wangu kwenu yako kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake. Na si shughuli yangu mimi kuwafukuza Waumini, kwani wao ni wenye kukutana na Mola wao Siku ya Kiyama. Lakini mimi nawaona nyinyi kuwa ni watu msiojua, kwa kuwa mnaniamrisha niwafukuze vipenzi vya Mwenyezi Mungu na niwaepushe na mimi.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَيَٰقَوۡمِ مَن يَنصُرُنِي مِنَ ٱللَّهِ إِن طَرَدتُّهُمۡۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
«Na enyi watu wangu, ni nani mwenye kunizuia mimi na Mwenyezi Mungu Akinitesa kwa kuwafukuza kwangu Waumini? Kwani hamyazingatii mambo mkayajua yenye nafuu zaidi kwenu na yenye kufaa zaidi?
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَآ أَقُولُ لَكُمۡ عِندِي خَزَآئِنُ ٱللَّهِ وَلَآ أَعۡلَمُ ٱلۡغَيۡبَ وَلَآ أَقُولُ إِنِّي مَلَكٞ وَلَآ أَقُولُ لِلَّذِينَ تَزۡدَرِيٓ أَعۡيُنُكُمۡ لَن يُؤۡتِيَهُمُ ٱللَّهُ خَيۡرًاۖ ٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا فِيٓ أَنفُسِهِمۡ إِنِّيٓ إِذٗا لَّمِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ
«Na wala siwaambii nyinyi kuwa mimi nina mahazina ya Mwenyezi Mungu, wala mimi siyajui yasiyoonekana, na mimi si mmoja kati ya Malaika, wala siwaambii hawa mnaowadharau miongoni mwa madhaifu wa Waumini kwamba Mwenyezi Mungu hatawapa malipo mema ya matendo yao. Mwenyezi Mungu, Peke Yake, ni Mjuzi kabisa kwa yaliyomo ndani ya vifua vyao na nyoyo zao. Na nikifanya hivyo, basi mimi wakati huo nitakuwa ni miongoni mwa wale wenye kujidhulumu wao wenyewe na kuwadhulumu wengineo»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالُواْ يَٰنُوحُ قَدۡ جَٰدَلۡتَنَا فَأَكۡثَرۡتَ جِدَٰلَنَا فَأۡتِنَا بِمَا تَعِدُنَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ
Wakasema, «Ewe Nūḥ„ umelumbana na sisi na umezidisha katika malumbano yako kwetu, basi tuletee hiyo adhabu unayotuahidi, iwapo wewe ni miongoni mwa wakweli katika madai yako.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ إِنَّمَا يَأۡتِيكُم بِهِ ٱللَّهُ إِن شَآءَ وَمَآ أَنتُم بِمُعۡجِزِينَ
Nūḥ, akasema kuwaambia watu wake, «Mwenyezi Mungu , Peke Yake, Ndiye Atakayewaletea nyinyi adhabu atakapo, na nyinyi si wenye kuiponyoka Akitaka kuwaadhibu, kwani Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, hakuna chochote chenye kumlemea katika ardhi wala katika mbingu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَا يَنفَعُكُمۡ نُصۡحِيٓ إِنۡ أَرَدتُّ أَنۡ أَنصَحَ لَكُمۡ إِن كَانَ ٱللَّهُ يُرِيدُ أَن يُغۡوِيَكُمۡۚ هُوَ رَبُّكُمۡ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ
«Na hautawanufaisha nyinyi ushauri wangu na bidii yangu katika kuwalingania kwenye Imani, iwapo Mwenyezi Mungu Anataka kuwpoteza na kuwaangamiza. Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye mwenye kuwamiliki, na Kwake Yeye mtarejeshwa kesho Akhera kwa kuhesabiwa na kulipwa.»
Arabic explanations of the Qur’an:
أَمۡ يَقُولُونَ ٱفۡتَرَىٰهُۖ قُلۡ إِنِ ٱفۡتَرَيۡتُهُۥ فَعَلَيَّ إِجۡرَامِي وَأَنَا۠ بَرِيٓءٞ مِّمَّا تُجۡرِمُونَ
Au je, wanasema hawa washirikina miongoni mwa watu wa Nūḥ, kwamba Nūḥ, amezua neno hili? Waambie, «Nikiwa nimemzulia urongo Mwenyezi Mungu hilo, basi ni juu yangu mimi, peke yangu, dhambi ya hilo; na nikiwa ni mkweli, basi nyinyi ndio wahalifu wenye dhambi, na mimi niko mbali na ukfiri wenu, ukanushaji wenu uhalifu wenu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَأُوحِيَ إِلَىٰ نُوحٍ أَنَّهُۥ لَن يُؤۡمِنَ مِن قَوۡمِكَ إِلَّا مَن قَدۡ ءَامَنَ فَلَا تَبۡتَئِسۡ بِمَا كَانُواْ يَفۡعَلُونَ
Na Mwenyezi Mungu, Aliyetakata na sifa za upungufu na kutukuka, Alimletea wahyi Nūḥ„ amani imshukiye, ilipolazimika adhabu juu ya watu wake kwamba hawatamuamini Mwenyezi Mungu isipokuwa walioamini kabla ya hapo, «basi usisikitike, ewe Nūḥ„ juu ya yale waliokuwa wakiyafanaya.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱصۡنَعِ ٱلۡفُلۡكَ بِأَعۡيُنِنَا وَوَحۡيِنَا وَلَا تُخَٰطِبۡنِي فِي ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓاْ إِنَّهُم مُّغۡرَقُونَ
«Na utengeneze jahazi kwa maangalizi yetu na kwa amri yetu na msaada wetu, hali ya kuwa wewe uko kwenye utunzi wetu na hifadhi yetu, na usitake kwangu kuwapa muhula hawa waliojidhulumu nafsi zao, miongoni mwa watu wako, kwa ukafiri wao, kwani wao ni wenye kuzamishwa kwa mafuriko.» Katika hii aya pana kuthibitisha sifa ya 'ayn (jicho ) kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa namna inavyonasibiana na Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَيَصۡنَعُ ٱلۡفُلۡكَ وَكُلَّمَا مَرَّ عَلَيۡهِ مَلَأٞ مِّن قَوۡمِهِۦ سَخِرُواْ مِنۡهُۚ قَالَ إِن تَسۡخَرُواْ مِنَّا فَإِنَّا نَسۡخَرُ مِنكُمۡ كَمَا تَسۡخَرُونَ
Na Nūḥ, akawa anatengeneza jahazi, na kila kundi la wakubwa wa watu wake likimpitia, humcheza shere. Nūḥ, aliwaambia, «Iwapo nyinyi mnatucheza shere leo, kwa ujinga wenu wa kutojua ukweli wa ahadi ya Mwenyezi Mungu, basi sisi tutawacheza shere nyinyi kesho wakati wa kuzama kama mnavyotucheza shere.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَسَوۡفَ تَعۡلَمُونَ مَن يَأۡتِيهِ عَذَابٞ يُخۡزِيهِ وَيَحِلُّ عَلَيۡهِ عَذَابٞ مُّقِيمٌ
Mtajua hapo, itakapokuja amri ya Mwenyezi mungu kwa hilo, ni yupi yule ambaye itamjia , hapa ulimwenguni, adhabu ya Mwenyezi Mungu yenye kumtweza na itamshukia, huko Akhera, adhabu ya daima isiyokatika.»
Arabic explanations of the Qur’an:
حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَ أَمۡرُنَا وَفَارَ ٱلتَّنُّورُ قُلۡنَا ٱحۡمِلۡ فِيهَا مِن كُلّٖ زَوۡجَيۡنِ ٱثۡنَيۡنِ وَأَهۡلَكَ إِلَّا مَن سَبَقَ عَلَيۡهِ ٱلۡقَوۡلُ وَمَنۡ ءَامَنَۚ وَمَآ ءَامَنَ مَعَهُۥٓ إِلَّا قَلِيلٞ
Mpaka ilipokuja amri yetu ya kuwaangamiza wao kama tulivyomuahidi Nūḥ, kwa hilo, na maji yakachimbuka kwa nguvu kutoka kwenye tanuri, mahala pa kuchomea mikate, ikiwa ni alama ya kuja adhabu, tulimuambia Nūḥ, «Beba ndani ya jahazi kila aina, miongoni mwa aina za wanyama wa kiume na wa kike, na uwabebe ndani yake watu wa nyumbani kwako, isipokuwa yule aliyetanguliwa na Neno kuwa wataadhibiwa katika wale wasiomuamini Mwenyezi Mungu kama mtoto wake na mke wake, na ubebe ndani yake aliyeamini pamoja na wewe katika watu wako.» Na hakuna aliyeamini pamoja na yeye isipokuwa wachache ingawa yeye alikaa na wao kwa muda mrefu.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ وَقَالَ ٱرۡكَبُواْ فِيهَا بِسۡمِ ٱللَّهِ مَجۡر۪ىٰهَا وَمُرۡسَىٰهَآۚ إِنَّ رَبِّي لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ
Nūḥ alisema kuwaambia walioamini pamoja na yeye, «Pandeni kwenye jahazi kwa jina la Mwenyezi Mungu. Kwa jina la Mwenyezi Mungu itatembea majini, na kwa jina la Mwenyezi Mungu itafika mwisho wa kwenda kwake na kutia nanga kwake. Hakika Mola wangu ni Mwingi wa kusamehe dhambi za mwenye kutubia na kurudi Kwake miongoni mwa waja Wake, ni Mwingi wa huruma kwao kwa kutowaadhibu baada ya kutubia.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَهِيَ تَجۡرِي بِهِمۡ فِي مَوۡجٖ كَٱلۡجِبَالِ وَنَادَىٰ نُوحٌ ٱبۡنَهُۥ وَكَانَ فِي مَعۡزِلٖ يَٰبُنَيَّ ٱرۡكَب مَّعَنَا وَلَا تَكُن مَّعَ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Nayo ikawa inatembea na wao kwenye mawimbi yanayopaa na kwenda juu mpaka yakawa kama majabali kwa urefu wake wa kwenda juu. Hapo Nūḥ alimwita mtoto wakewa kiume, na ambaye alikuwa yupo mahali kando na amejiepusha na Waumini, akamwambia, «Ewe mwanangu, panda na sisi kwenye jahazi na usiwe pamoja na wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu, utakujazama.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ سَـَٔاوِيٓ إِلَىٰ جَبَلٖ يَعۡصِمُنِي مِنَ ٱلۡمَآءِۚ قَالَ لَا عَاصِمَ ٱلۡيَوۡمَ مِنۡ أَمۡرِ ٱللَّهِ إِلَّا مَن رَّحِمَۚ وَحَالَ بَيۡنَهُمَا ٱلۡمَوۡجُ فَكَانَ مِنَ ٱلۡمُغۡرَقِينَ
Mtoto wa Nūḥ akasema, «Nitakimbilia kwenye jabali nijihifadhi na maji na hilo litanizuia na kuzama. Nūḥ akamjibu, «Leo hakuna kitu chenye kuzuia amri ya Mwenyezi Mungu na hukumu Yake iliyoteremka kwa viumbe, ya gharika na maangamivu, isipokuwa yule aliyehurumiwa na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, basi amini na upande jahazini pamoja na sisi.» Hapo mawimbi makubwa yalitenganisha baina ya Nūḥ na mwanawe na akawa ni miongoni mwa waliogharikishwa wenye kuangamia.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَقِيلَ يَٰٓأَرۡضُ ٱبۡلَعِي مَآءَكِ وَيَٰسَمَآءُ أَقۡلِعِي وَغِيضَ ٱلۡمَآءُ وَقُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ وَٱسۡتَوَتۡ عَلَى ٱلۡجُودِيِّۖ وَقِيلَ بُعۡدٗا لِّلۡقَوۡمِ ٱلظَّٰلِمِينَ
Akasema Mwenyezi Mungu kuiambia ardhi, baada ya watu wa Nūḥ kuangamia, «Ewe ardhi! Kunywa maji yako. Na ewe mbingu! Simamisha kunyesha mvua.» Na maji yakapungua na yakanywea, na amri ya Mwenyezi Mungu ikapitishwa ya kuangamia watu wa Nūḥ, na jahazi ikaegesha juu jabali la Jūdīy. Na hapo kukasemwa, «Kuwa mbali (na rehema ya Mwenyezi Mungu) ni kwa wale madhalimu waliokiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu na wasiamini.»
Arabic explanations of the Qur’an:
وَنَادَىٰ نُوحٞ رَّبَّهُۥ فَقَالَ رَبِّ إِنَّ ٱبۡنِي مِنۡ أَهۡلِي وَإِنَّ وَعۡدَكَ ٱلۡحَقُّ وَأَنتَ أَحۡكَمُ ٱلۡحَٰكِمِينَ
Na Nūḥ alimlingania Mola Wake kwa kumuomba na akasema, «Mola wangu, wewe umeniahidi kwamba utaniokoa, mimi na jamaa zangu, tusizame na tusiangamie, na hakika mototo wangu ni miongoni mwa watu wa nyumbani kwangu, na ahadi yako ndio kweli ambayo haibadiliki, na wewe ndiye hodari zaidi wa wenye kuhukumu na muadilifu wao zaidi.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ يَٰنُوحُ إِنَّهُۥ لَيۡسَ مِنۡ أَهۡلِكَۖ إِنَّهُۥ عَمَلٌ غَيۡرُ صَٰلِحٖۖ فَلَا تَسۡـَٔلۡنِ مَا لَيۡسَ لَكَ بِهِۦ عِلۡمٌۖ إِنِّيٓ أَعِظُكَ أَن تَكُونَ مِنَ ٱلۡجَٰهِلِينَ
Mwenyezi Mungu Akasema, «Ewe Nūḥ, hakika yule mototo wako aliyeangamia si katika jamaa ambao nilikuahidi kuwa nitawaokoa. Hii ni kwa sababu ya ukafiri wake na kufanya kwake matendo yasiyokuwa mema. Na mimi nakukataza usiniombe jambo usiokuwa na ujuzi nalo. Mimi nakusihi usiwe ni miongoni mwa wajinga kwa kuniomba hilo.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ رَبِّ إِنِّيٓ أَعُوذُ بِكَ أَنۡ أَسۡـَٔلَكَ مَا لَيۡسَ لِي بِهِۦ عِلۡمٞۖ وَإِلَّا تَغۡفِرۡ لِي وَتَرۡحَمۡنِيٓ أَكُن مِّنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ
Akasema Nūḥ, «Ewe Mola wangu, Mimi najihami kwako na nataka hifadhi kukuomba kitu nisokuwa na ujuzi nacho, na usiponisamehe dhambi zangu na ukanihurumia kwa rehema zako,nitakuwa ni miongoni mwa wale waliojinyima hadhi zao na wakaangamia.
Arabic explanations of the Qur’an:
قِيلَ يَٰنُوحُ ٱهۡبِطۡ بِسَلَٰمٖ مِّنَّا وَبَرَكَٰتٍ عَلَيۡكَ وَعَلَىٰٓ أُمَمٖ مِّمَّن مَّعَكَۚ وَأُمَمٞ سَنُمَتِّعُهُمۡ ثُمَّ يَمَسُّهُم مِّنَّا عَذَابٌ أَلِيمٞ
Mwenyezi Mungu Akasema, «Ewe Nūḥ, Shuka kwenye ardhi kavu kutoka kwenye jahazi, kwa amani na salama zitokazo kwetu, na baraka ikishuka juu yako na juu ya ummah katika wale walioko na wewe. Na kuna umma na makundi miongoni mwa watu wa uovu ambao tutawastarehesha katika uhai wa kilimwengu mpaka ufike muda wao wa kuishi kisha iwapate wao kutoka kwetu adhabu iumizayo Siku ya Kiyama.»
Arabic explanations of the Qur’an:
تِلۡكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلۡغَيۡبِ نُوحِيهَآ إِلَيۡكَۖ مَا كُنتَ تَعۡلَمُهَآ أَنتَ وَلَا قَوۡمُكَ مِن قَبۡلِ هَٰذَاۖ فَٱصۡبِرۡۖ إِنَّ ٱلۡعَٰقِبَةَ لِلۡمُتَّقِينَ
Habari hiyo tuliyokuhadithia kuhusu Nūḥ na watu wake ni miongoni mwa habari za ghaibu zilizopita, ambazo tunakuletea wahyi juu yake, hukuwa ukizijua, wewe wala watu wako, kabla ya maelezo haya. Basi subiri juu ya ukanushaji wa watu wako na makero yao wanayokufanyia kama walivyosubiri Manabii huko nyuma. Na mwisho mwema wa duniani na Akhera ni wa waogopao wanaomcha Mwenyezi Mungu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمۡ هُودٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥٓۖ إِنۡ أَنتُمۡ إِلَّا مُفۡتَرُونَ
Na tuliwamtumia watu wa kabila la 'Ād ndugu yao Hūd. Alisema kuwaambia, «Enyi watu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake. Nyinyi hamuna mungu anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye. Basi mtakasieni Yeye ibada. Kwani nyinyi hamkuwa, katika kumshirikisha kwenu Mwenyezi Mungu, isipokuwa ni warongo.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَٰقَوۡمِ لَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ أَجۡرًاۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَى ٱلَّذِي فَطَرَنِيٓۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ
«Enyi watu wangu, mimi siwaombi malipo yoyote, kwa haya niwalinganiyao ya kumtakasia Mwenyezi Mungu ibada na kuacha kuabudu masanamu,. Malipo yangu mimi ya kuwalingania nyinyi hayako juu ya yoyote isipokuwa Mwenyezi Mungu aliyeniumba. Basi hamtii akili mkatenganisha baina ya ukweli na upotofu?
Arabic explanations of the Qur’an:
وَيَٰقَوۡمِ ٱسۡتَغۡفِرُواْ رَبَّكُمۡ ثُمَّ تُوبُوٓاْ إِلَيۡهِ يُرۡسِلِ ٱلسَّمَآءَ عَلَيۡكُم مِّدۡرَارٗا وَيَزِدۡكُمۡ قُوَّةً إِلَىٰ قُوَّتِكُمۡ وَلَا تَتَوَلَّوۡاْ مُجۡرِمِينَ
«Enyi watu wangu, takeni msamaha wa Mwenyezi Mungu kwa kumuamini Yeye, kisha mtubie Kwake kutokana na dhambi zenu. Kwani nyinyi mkifanya hivyo, Atawateremshia mvua yenye kufuatana iliyo nyinygi, hivyo basi mazuri yenu yatakuwa mengi na Atawaongezea nguvu juu ya nguvu mlizonazo kwa wingi wa watoto wenu na mfuatano wa neema juu yenu. Na msiyape mgongo yale ninayowalingania nyinyi kwayo mkawa ni wenye kuendelea juu ya makosa yenu.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالُواْ يَٰهُودُ مَا جِئۡتَنَا بِبَيِّنَةٖ وَمَا نَحۡنُ بِتَارِكِيٓ ءَالِهَتِنَا عَن قَوۡلِكَ وَمَا نَحۡنُ لَكَ بِمُؤۡمِنِينَ
Wakasema, «Ewe Hūd, hukutujia na hoja zilizo wazi juu ya usahihi wa yale unayotuitia. Na sisi si wenye kuwaacha waungu wetu tunaowaabudu kwa sababu ya maneno yako. Na sisi si wenye kukuamini wewe katika hilo unalolidai.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِن نَّقُولُ إِلَّا ٱعۡتَرَىٰكَ بَعۡضُ ءَالِهَتِنَا بِسُوٓءٖۗ قَالَ إِنِّيٓ أُشۡهِدُ ٱللَّهَ وَٱشۡهَدُوٓاْ أَنِّي بَرِيٓءٞ مِّمَّا تُشۡرِكُونَ
«Sisi hatusemi isipokuwa kwamba baadhi ya waungu wetu wamekutia wazimu kwa sababu ya kukataza kwako wasiabudiwe.» Akawaambia, «Mimi namshuhudisha Mwenyezi Mungu haya ninayoyasema na nawashuhudiza nyinyi kwamba mimi niko mbali na vile mnavyovishirikisha
Arabic explanations of the Qur’an:
مِن دُونِهِۦۖ فَكِيدُونِي جَمِيعٗا ثُمَّ لَا تُنظِرُونِ
badala ya Mwenyezi Mungu, miongoni mwa wale wafananishwao na Yeye na masanamu. Basi angalieni na mfanye bidii, nyinyi na hao mnaodai kati ya waungu wenu, kunipatia madhara, kisha msilicheleweshe hilo hata kitambo kidogo kiasi cha kupepesa jicho. Hivyo ni kwamba Hūd ana imani thabiti kwamba hayatampata yeye kutoka kwao wala kutoka kwa waungu wao madhara yoyote.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنِّي تَوَكَّلۡتُ عَلَى ٱللَّهِ رَبِّي وَرَبِّكُمۚ مَّا مِن دَآبَّةٍ إِلَّا هُوَ ءَاخِذُۢ بِنَاصِيَتِهَآۚ إِنَّ رَبِّي عَلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ
«Mimi nimetegemea kwa Mwenyezi Mungu, Mola wangu na Mola wenu, Mmiliki wa kila kitu na Mwenye kukiendesha. Hakuna kitu chenye kunipata isipokuwa kwa amri Yake. Na Yeye Ndiye Muweza wa kila kitu, Hakuna kitu chochote kinachotambaa kwnye ardhi hii isipokuwa Mwenyezi Mungu Amekimiliki na kiko chini ya mamlaka Yake na uendeshaji Wake. Hakika Mola wangu Yuko kwenye njia iliyolingana sawa, kwa maana kwamba ni muadilifu katika hukumu Zake, sheria Zake na amri Zake, Anamlipa mwema kwa wema Wake na muovu kwa uovu wake.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَقَدۡ أَبۡلَغۡتُكُم مَّآ أُرۡسِلۡتُ بِهِۦٓ إِلَيۡكُمۡۚ وَيَسۡتَخۡلِفُ رَبِّي قَوۡمًا غَيۡرَكُمۡ وَلَا تَضُرُّونَهُۥ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ رَبِّي عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٍ حَفِيظٞ
«Mkiyapa mgongo yale ninayowalingania kwayo ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtakasia ibada, basi nimeshaufikisha ujumbe wa Mola wangu kwneu na hoja ishasimama kwenu nyinyi, na Mwenyezi Mungu atawaangamiza kwa kuwa hamkumuamini, na Atawaleta watu wengine ambao watashika nafasi zenu katika majumba yenu na mali yenu, na ambao watamtakasia Mwenyezi Mungu ibada. Na nyinyi hamtamdhuru Yeye kitu chochote. Hakika Mola wangu amekidhibiti kila kitu na kukihifadhi; Yeye Ndiye Mwenye kunitunza msinifanyie ubaya.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا نَجَّيۡنَا هُودٗا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ بِرَحۡمَةٖ مِّنَّا وَنَجَّيۡنَٰهُم مِّنۡ عَذَابٍ غَلِيظٖ
Na ilipokuja amri yetu kuwaadhibu watu wa Hūd, tulimuokoa Hūd na Waumini miongoni mwao kwa wema wetu juu yao na huruma, na tukawaokoa wao na adhabu kali Aliyoishukisha Mwenyezi Mungu kwa hao 'Ād, wakapambaukiwa na huku hakuna kionekanacho isipokuwa makazi yao.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَتِلۡكَ عَادٞۖ جَحَدُواْ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِمۡ وَعَصَوۡاْ رُسُلَهُۥ وَٱتَّبَعُوٓاْ أَمۡرَ كُلِّ جَبَّارٍ عَنِيدٖ
Hao ndio'Ād, walikanusha aya za Mwenyezi Mungu, wakaasi Mitume Wake na wakatii amri ya kila anayemfanyia kiburi Mwenyezi mungu asiyekubali haki wala kuinyoshea shingo.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَأُتۡبِعُواْ فِي هَٰذِهِ ٱلدُّنۡيَا لَعۡنَةٗ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ أَلَآ إِنَّ عَادٗا كَفَرُواْ رَبَّهُمۡۗ أَلَا بُعۡدٗا لِّعَادٖ قَوۡمِ هُودٖ
Wakafuatiwa, katika ulimwengu huu, na laana ya Mwenyezi Mungu, na wakafuatwa na hasira Zake Siku ya Kiyama. Jueni mtanabahi kwamba 'Ād walimkanusha Mola wao na wakawakanusha Mitume Wake. Jueni mtanabahi kwamba umbali na rehema ya Mwenyezi Mungu na maangamivu yatawashukia 'Ād, watu wa Hūd, kwa sababu ya ushirikina wao na kukanusha kwao neema ya Mola wao.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمۡ صَٰلِحٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥۖ هُوَ أَنشَأَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ وَٱسۡتَعۡمَرَكُمۡ فِيهَا فَٱسۡتَغۡفِرُوهُ ثُمَّ تُوبُوٓاْ إِلَيۡهِۚ إِنَّ رَبِّي قَرِيبٞ مُّجِيبٞ
Na tulimtuma kwenda kwa Thamūd ndugu yao Ṣāliḥ akasema kuwaambia, «Enyi watu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake. Nyinyi hamuna mungu yoyote anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu. Basi mtakasieni ibada. Yeye Ndiye Aliyeanza kuwaumba kutokamana na ardhi, kwa kumuumba baba yenu Ādam kutokamana na hiyo, na akawafanya nyinyi ni wenye kuiimarisha. Hivyo basi, muombeni Awasamehe madhambi yenu, na rudini Kwake kwa kutubia kidhati. Hakika Mola wangu yuko karibu na yule anayemtakasia ibada na akawa na hamu ya kuja Kwake kwa kutubia, ni Mwenye kumuitikia anapomuomba.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالُواْ يَٰصَٰلِحُ قَدۡ كُنتَ فِينَا مَرۡجُوّٗا قَبۡلَ هَٰذَآۖ أَتَنۡهَىٰنَآ أَن نَّعۡبُدَ مَا يَعۡبُدُ ءَابَآؤُنَا وَإِنَّنَا لَفِي شَكّٖ مِّمَّا تَدۡعُونَآ إِلَيۡهِ مُرِيبٖ
Tahamūd wakasema kumwambia Ṣāliḥ, «Kwa hakika, kabla ya neno hili ulilotwambia, tulikuwa tuna matumaini kwamba utakuwa ni kiongozi mwenye kusikizwa,. Je, unatukataza kuwaabudu waungu ambao baba zetu walikuwa wakiwaabudu? Hakika sisi tuko kwenye shaka yenye kutia wasiwasi juu ya mwito wako wa kutuita sisi tumuabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَءَيۡتُمۡ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّي وَءَاتَىٰنِي مِنۡهُ رَحۡمَةٗ فَمَن يَنصُرُنِي مِنَ ٱللَّهِ إِنۡ عَصَيۡتُهُۥۖ فَمَا تَزِيدُونَنِي غَيۡرَ تَخۡسِيرٖ
Ṣāliḥ akasema kuwaambia watu wake, «Enyi watu wangu, iwapo niko kwenye hoja ya Mwenyezi Mungu na ukanijia mimi utume na hekima kutoka Kwake, niambieni mimi: ni nani atakayeniondolea adhabu ya Mwenyezi Mungu nikimuasi, nisiufikishe ujumbe na nisitoe ushauri mzuri kwenu? Hapo hamtaniogezea isipokuwa upotevu na kuwa mbali na wema.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَيَٰقَوۡمِ هَٰذِهِۦ نَاقَةُ ٱللَّهِ لَكُمۡ ءَايَةٗۖ فَذَرُوهَا تَأۡكُلۡ فِيٓ أَرۡضِ ٱللَّهِۖ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوٓءٖ فَيَأۡخُذَكُمۡ عَذَابٞ قَرِيبٞ
«Na enyi watu wangu, huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, Amemjaalia ni hoja na alama ya kuonesha ukweli wangu katika yale ninayowaitia. Basi muacheni ale katika ardhi ya Mawenyezi Mungu, kwani chakula chake hakiko juu yenu. Na wala msimguse kumchinja, kwani nyinyi mkifanya hivyo itawapata adhabu kutoka Kwake kwa muda mfupi baada kumchinja.»
Arabic explanations of the Qur’an:
فَعَقَرُوهَا فَقَالَ تَمَتَّعُواْ فِي دَارِكُمۡ ثَلَٰثَةَ أَيَّامٖۖ ذَٰلِكَ وَعۡدٌ غَيۡرُ مَكۡذُوبٖ
Wakamkanusha na wakamchinja ngamia, hapo Ṣāliḥ akawaambia, «Stareheni na maisha yenu katika mji wenu kwa muda wa siku tatu, kwani adhabu ni yenye kuwashukia baada yake, na hiyo ni ahadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu isiyokanushika, haina budi kutukia.»
Arabic explanations of the Qur’an:
فَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا نَجَّيۡنَا صَٰلِحٗا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ بِرَحۡمَةٖ مِّنَّا وَمِنۡ خِزۡيِ يَوۡمِئِذٍۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ ٱلۡقَوِيُّ ٱلۡعَزِيزُ
Basi amri yetu ilipokuja ya kuwaangamiza Thamūd, tulimuokoa Ṣāliḥ na walioamini pamoja na yeye na maangamivu kwa rehema kutoka kwetu. Na tuliwaokoa wao na unyonge wa Siku hiyo na udhalilifu wake. Hakika Mola wako, ewe Mtume, Ndiye Mwenye nguvu, Mwenye ushindi. Na miongoni mwa nguvu Zake na ushindi Wake ni kuwa Aliwaangamiza watu wenye kupita kiasi kwenye uasi na akawaokoa Mitume na wafuasi wao.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَأَخَذَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ ٱلصَّيۡحَةُ فَأَصۡبَحُواْ فِي دِيَٰرِهِمۡ جَٰثِمِينَ
Na ukelele wa nguvu uliwapata Thamūd walio madhalimu, hapohapo wakawa kwenye majumba yao ni wafu waliokauka na kuanguka kwa nyuso zao, hakuna anayetikisika.
Arabic explanations of the Qur’an:
كَأَن لَّمۡ يَغۡنَوۡاْ فِيهَآۗ أَلَآ إِنَّ ثَمُودَاْ كَفَرُواْ رَبَّهُمۡۗ أَلَا بُعۡدٗا لِّثَمُودَ
Kama kwamba wao, kwa haraka ya kuondoka kwao na kutoeka kwao, hawakuishi humo. Jueni mtanabahi kwamba Thamūd walikanusha aya za Mola wao na hoja Zake. Jueni mtanabahi kwamba kuwa mbali na kufukuzwa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu ni kwa hao Thamūd; ni upotevu ulioje na unyonge ulioje huo wao.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَقَدۡ جَآءَتۡ رُسُلُنَآ إِبۡرَٰهِيمَ بِٱلۡبُشۡرَىٰ قَالُواْ سَلَٰمٗاۖ قَالَ سَلَٰمٞۖ فَمَا لَبِثَ أَن جَآءَ بِعِجۡلٍ حَنِيذٖ
Hakika Malaika walimjia Ibrāhīm, amani imshukiye, wakimpa yeye na mke wake bishara ya Isḥḥḥaq na Ya'qūb baada yake, wakasema, «Salām (amani)» Akasema kuwarudishia maamkuzi yao, «Salām (amani)» Hapo akaondoka haraka na akrudi na mwanang>ombe wa kuchoma aliyenona ili wao wale.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَلَمَّا رَءَآ أَيۡدِيَهُمۡ لَا تَصِلُ إِلَيۡهِ نَكِرَهُمۡ وَأَوۡجَسَ مِنۡهُمۡ خِيفَةٗۚ قَالُواْ لَا تَخَفۡ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمِ لُوطٖ
Alipoona Ibrāhīm kuwa mikono yao haifikikishwi kwenye yule mwanang>ombe aliyewaletea na kuwa wao hawamli, alikataa hilo kutoka kwao na akaingiwa na hisia ya uoga ndani ya moyo wake. Malaika wakasema, walipoona uoga uliomuingia Ibrāhīm, «Usiogope! Sisi ni Malaika wa Mola wako tumetumwa kwenda kwa watu wa Lūṭ kuwaangamiza.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱمۡرَأَتُهُۥ قَآئِمَةٞ فَضَحِكَتۡ فَبَشَّرۡنَٰهَا بِإِسۡحَٰقَ وَمِن وَرَآءِ إِسۡحَٰقَ يَعۡقُوبَ
Na Sārah, mke wa Ibrāhīm, alikuwa amesimema nyuma ya pazia yuwasikia hayo maneno. Alicheka kwa kuyaonea ajabu aliyoyasikia. Hapo tukampa habari njema, kupitia kwa ndimi za Malaika, kwamba atazaa, kwa mume wake Ibrāhīm, mtoto atakayeitwa Isḥāq; na mtoto wake ataishi, na baada ya Isḥāq atakuwa na mjukuu kutoka kwake, naye ni Ya’qūb.
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَتۡ يَٰوَيۡلَتَىٰٓ ءَأَلِدُ وَأَنَا۠ عَجُوزٞ وَهَٰذَا بَعۡلِي شَيۡخًاۖ إِنَّ هَٰذَا لَشَيۡءٌ عَجِيبٞ
Alipopewa bishara ya Isḥāq, Sārah alisema kwa kustaajabu, «Ee mimi ee! Vipi nitakuwa na mtoto na mimi ni mkongwe na huyu mume wangu yuko katika hali ya uzee na utu uzima? Kuzaa kwa mtu mfano wangu mimi na mfano wa mume wangu pamoja na ukuu wa myaka ni jambo la ajabu.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالُوٓاْ أَتَعۡجَبِينَ مِنۡ أَمۡرِ ٱللَّهِۖ رَحۡمَتُ ٱللَّهِ وَبَرَكَٰتُهُۥ عَلَيۡكُمۡ أَهۡلَ ٱلۡبَيۡتِۚ إِنَّهُۥ حَمِيدٞ مَّجِيدٞ
Wajumbe walisema kumwambia , «Hivi wewe unaionea ajabu amri ya Mwenyezi Mungu na hukumu Yake? Rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka Zake ziwashukie nyinyi, enyi watu wa nyumba ya unabii. Hakika Yeye, kutakata na kutukuka ni Kwake, ni mhimidiwa wa sifa na vitendo, ni Mwenye utukufu na ukubwa katika hizo.»
Arabic explanations of the Qur’an:
فَلَمَّا ذَهَبَ عَنۡ إِبۡرَٰهِيمَ ٱلرَّوۡعُ وَجَآءَتۡهُ ٱلۡبُشۡرَىٰ يُجَٰدِلُنَا فِي قَوۡمِ لُوطٍ
Ulipomuondokea Ibrāhīm uoga uliompata kwa wale wageni kutokula chakula, na ikamjia bishara njema ya Isḥāq na Ya’qūb, aliendelea kuwajadili Wajumbe wetu juu ya kile tulichowatuma cha kuwaadhibu watu wa Lūṭ na kuwaangamiza.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ إِبۡرَٰهِيمَ لَحَلِيمٌ أَوَّٰهٞ مُّنِيبٞ
Hakika Ibrāhīm ni mwingi wa uhalimu, hapendi uharakishaji wa adhabu, ni mwingi wa kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu na kumuomba, ni mwenye kutubia, anarejea kwa Mwenyezi Mungu katika mambo yake yote.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَٰٓإِبۡرَٰهِيمُ أَعۡرِضۡ عَنۡ هَٰذَآۖ إِنَّهُۥ قَدۡ جَآءَ أَمۡرُ رَبِّكَۖ وَإِنَّهُمۡ ءَاتِيهِمۡ عَذَابٌ غَيۡرُ مَرۡدُودٖ
Wajumbe wa Mwenyezi Mungu wakasema, «Ewe Ibrāhīm, uacha mjadala huu kuhusu mambo ya watu wa Lūṭ na kuwaombea huruma, kwani hakika ya mambo ni kwamba imithibiti juu yao adhabu na amri ya Mola wako aliyowapangia. Na wao, adhabu inayotoka Mwenyezi Mungu ni yenye kuwashukia, si yenye kuepushwa na wao wala kuzuiliwa..»
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَمَّا جَآءَتۡ رُسُلُنَا لُوطٗا سِيٓءَ بِهِمۡ وَضَاقَ بِهِمۡ ذَرۡعٗا وَقَالَ هَٰذَا يَوۡمٌ عَصِيبٞ
Na Malaika wetu walipomjia Lūṭ, aliudhika kwa kuja kwao na akaingiwa na hamu kwa hilo. Hivyo ni kwa kuwa yeye hakuwa anajua kwamba wao ni wajumbe wa Mwenyezi Mungu, akawachelea wasidhuriwe na watu wake na akasema, «Hii ni siku ya mtihani na shida.»
Arabic explanations of the Qur’an:
وَجَآءَهُۥ قَوۡمُهُۥ يُهۡرَعُونَ إِلَيۡهِ وَمِن قَبۡلُ كَانُواْ يَعۡمَلُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ هَٰٓؤُلَآءِ بَنَاتِي هُنَّ أَطۡهَرُ لَكُمۡۖ فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلَا تُخۡزُونِ فِي ضَيۡفِيٓۖ أَلَيۡسَ مِنكُمۡ رَجُلٞ رَّشِيدٞ
Watu wa Lūṭ wakamjia kwa haraka kutaka kufanya uchafu, na kabla ya kuja kwao walikuwa wanawendea wanaume kwa njia ya matamanio badala ya wanawake. Lūṭ akasema kuwaambia watu wake, «Hawa ni watoto wangu wa kike, waoeni. Wao niwasafi zaidi kwenu kuliko hayo mnayoyataka.» Aliwaita kuwa ni watoto wake wa kike sababu Nabii wa umma ana daraja ya baba kwao. «Basi muogopeni Mwenyezi Mungu na mjihadhari na mateso Yake, wala msinifedhehi kwa kuwakosea wageni wangu. Kwani hakuna mtu yoyote katika nyinyi aliye mzuri wa kupima mambo apate kuwakataza wanaotaka kufanya machafu akawzuia wao na hayo? Kumdhalilisha mgeni ni jambo la kutukanisha hakuna alifanyalo isipokuwa ni watu wa utwevu.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالُواْ لَقَدۡ عَلِمۡتَ مَا لَنَا فِي بَنَاتِكَ مِنۡ حَقّٖ وَإِنَّكَ لَتَعۡلَمُ مَا نُرِيدُ
Wakasema watu wa Lūṭ kumwambia yeye, «Umeshajua tangu mbeleni kwamba sisi hatuna haja ya wanawake wala matamanio. Na wewe unajua tulitakalo. Yaani, sisi hatutaki isipokuwa wanaume na hatuna hamu ya kuoa wanawake.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ لَوۡ أَنَّ لِي بِكُمۡ قُوَّةً أَوۡ ءَاوِيٓ إِلَىٰ رُكۡنٖ شَدِيدٖ
Walipokataa isipokuwa ni kufanaya machafu, aliwaambia, «Lau mimi nina nguvu kwenu na nina wasaidizi pamoja na mimi, au niutemegee ukoo utakaonihami na nyinyi, ningaliwazuia nyinyi na hayo mnayoyataka.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالُواْ يَٰلُوطُ إِنَّا رُسُلُ رَبِّكَ لَن يَصِلُوٓاْ إِلَيۡكَۖ فَأَسۡرِ بِأَهۡلِكَ بِقِطۡعٖ مِّنَ ٱلَّيۡلِ وَلَا يَلۡتَفِتۡ مِنكُمۡ أَحَدٌ إِلَّا ٱمۡرَأَتَكَۖ إِنَّهُۥ مُصِيبُهَا مَآ أَصَابَهُمۡۚ إِنَّ مَوۡعِدَهُمُ ٱلصُّبۡحُۚ أَلَيۡسَ ٱلصُّبۡحُ بِقَرِيبٖ
Malaika wakasema, Ewe Lūṭ, sisi ni wajumbe wa Mola wako, Ametutuma kuwaangamiza watu wako, na wao hawatakufikia. Basi toka kwenye kijiji hiki, wewe na watu wako (waliokuamini), katika kipindi kilichosalia cha usiku, na asizunguke nyuma yoyote katika nyinyi, ili asiione adhabu ikampata. Lakini mke wako aliyeenda kinyume chako kwa kukanusha na kufanya unafiki, kitampata yeye kile kitakachowapata watu wako cha maangamivu. Hakika maagano ya kuangamia kwao ni wakati wa asubuhi, nao ni wakati ambao ni karibu kufika.»
Arabic explanations of the Qur’an:
فَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا جَعَلۡنَا عَٰلِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهَا حِجَارَةٗ مِّن سِجِّيلٖ مَّنضُودٖ
Basi amri yetu ilipokuja, ya adhabu kuwashukia, tuliifanya sehamu ya juu ya kijiji chao ambayo walikuwa wakiishi juu yake kuwa chini kwa kukigeuza. Na tuliwateremshia majiwe ya udongo ulio mgumu wenye nguvu, yamepangwa baadhi yake juu ya mengine na yamefuatana,
Arabic explanations of the Qur’an:
مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَۖ وَمَا هِيَ مِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ بِبَعِيدٖ
yamewekwa alama huko kwa Mwenyezi Mungu kwa alama inayojulikana, hayafanani na majiwe yaliyo ardhini. Na hayakuwa majiwe haya ambayo Mwenyezi Mungu aliwateremshia watu wa Lūṭ, yako mbali na makafiri wa kikureshi kuwa watateremshiwa mfano wake. Katika haya kuna onyo kwa kila aliyeasi aliyeshindana na Mwenyezi Mungu.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ وَإِلَىٰ مَدۡيَنَ أَخَاهُمۡ شُعَيۡبٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥۖ وَلَا تَنقُصُواْ ٱلۡمِكۡيَالَ وَٱلۡمِيزَانَۖ إِنِّيٓ أَرَىٰكُم بِخَيۡرٖ وَإِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٖ مُّحِيطٖ
Na tulimtuma kwenda kwa watu wa Madyan ndugu yao Shu'ayb, akasema , «Enyi watu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake. Nyinyi hamuna mungu yoyote anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, basi mtakasieni ibada.. Wala msiwapunguzie watu haki zao katika vipimo vyao na mizani zao. Mimi nawaona nyinyi muko kwenye ukunjufu wa maisha, na mimi nawachelea, kwa sababu ya kupunguza vipimo na mizani, adhabu ya siku itakayowazunguka
Arabic explanations of the Qur’an:
وَيَٰقَوۡمِ أَوۡفُواْ ٱلۡمِكۡيَالَ وَٱلۡمِيزَانَ بِٱلۡقِسۡطِۖ وَلَا تَبۡخَسُواْ ٱلنَّاسَ أَشۡيَآءَهُمۡ وَلَا تَعۡثَوۡاْ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُفۡسِدِينَ
«Na enyi watu wangu, timizeni vipimo vya vibaba na mizani kwa usawa Wala msiwapunguzie watu haki zao katika jumala ya vitu vyao. Wala msiende katika ardhi mkifanya mambo ya kumuasi Mwenyezi Mungu na kueneza uharibifu.
Arabic explanations of the Qur’an:
بَقِيَّتُ ٱللَّهِ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَۚ وَمَآ أَنَا۠ عَلَيۡكُم بِحَفِيظٖ
«Kile kitakachosalia kwenu cha faida ya halali, baada ya kutimiza vipimo na mizani, kina baraka na ni chema kwenu kuliko kile mkichukuacho cha pato la haramu kwa njia ya kupunja na mfano wake. Iwapo nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu kikweli, basi fuateni amri Yake. Na mimi si mtunzi kwenu wa kuwahesabia matendo yenu.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالُواْ يَٰشُعَيۡبُ أَصَلَوٰتُكَ تَأۡمُرُكَ أَن نَّتۡرُكَ مَا يَعۡبُدُ ءَابَآؤُنَآ أَوۡ أَن نَّفۡعَلَ فِيٓ أَمۡوَٰلِنَا مَا نَشَٰٓؤُاْۖ إِنَّكَ لَأَنتَ ٱلۡحَلِيمُ ٱلرَّشِيدُ
Wakasema, «Ewe Shu'ayb, je swala hii ambayo unaendelea nayo ndiyo inayokuamuru wewe kwamba sisi tuache masanamu na mizimu ambayo baba zetu wanaabudu, au kwamba sisi tujizuie tusitumie njia tuziwezazo za hila na vitimbi katika kuchuma mali yetu?» Wakasema kwa njia ya kumcheza shere, «Wewe ndiye mwenye akili na hodari wa mipango ya usimamizi wa mali.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَءَيۡتُمۡ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّي وَرَزَقَنِي مِنۡهُ رِزۡقًا حَسَنٗاۚ وَمَآ أُرِيدُ أَنۡ أُخَالِفَكُمۡ إِلَىٰ مَآ أَنۡهَىٰكُمۡ عَنۡهُۚ إِنۡ أُرِيدُ إِلَّا ٱلۡإِصۡلَٰحَ مَا ٱسۡتَطَعۡتُۚ وَمَا تَوۡفِيقِيٓ إِلَّا بِٱللَّهِۚ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُ وَإِلَيۡهِ أُنِيبُ
Akasema Shu'ayb, «Enyi watu wangu, Mwaonaje iwapo mimi niko kwenye njia iliyo wazi itokayo kwa Mola wangu katika yale ninayowaitia ya kumtakasia Yeye ibada, na katika yale ninayowakataza ya kuharibu mali, na Akawa Ameniruzuku riziki ya ukunjufu ya halali iliyo nzuri? Na sitaki kuenda kinyume na nyinyi, nikafanya jambo nililowakataza; na sitaki, katika niwaamrishalo na niwakatazalo, isipokuwa ni kuwarakibisha kadiri ya uweza wangu na kujimudu kwangu. Na kuafikiwa kwangu, katika kuipata haki na kujaribu kuwarakibisha, kuko kwa Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye, Peke Yake, nimejitegemeza, na Kwake Yeye narejea kwa kutubia na kuelekea.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَيَٰقَوۡمِ لَا يَجۡرِمَنَّكُمۡ شِقَاقِيٓ أَن يُصِيبَكُم مِّثۡلُ مَآ أَصَابَ قَوۡمَ نُوحٍ أَوۡ قَوۡمَ هُودٍ أَوۡ قَوۡمَ صَٰلِحٖۚ وَمَا قَوۡمُ لُوطٖ مِّنكُم بِبَعِيدٖ
«Na enyi watu wangu, usiwapelekee uadui wenu kwangu na kunichukia na kuiacha Dini niliyonayo, kufanya ukakamavu na kuendelea na ukanushaji wa Mwenyezi Mungu mlionao. Kwani mkifanya hivyo, yatawapata nyinyi maangamivu kama yaliyowapata watu wa Nūḥ, au watu wa Hūd au watu wa Ṣāliḥ,. Na hawakuwa watu wa Lūṭ, na adhabu iliyowashukia ni mbali na nyinyi, si nchi waliyoishi wala zama walizokuwako.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱسۡتَغۡفِرُواْ رَبَّكُمۡ ثُمَّ تُوبُوٓاْ إِلَيۡهِۚ إِنَّ رَبِّي رَحِيمٞ وَدُودٞ
Na ombeni kutoka kwa Mola wenu msamaha wa dhambi zenu, kisha rudini kumtii na endeleeni juu yake. Hakika Mola wangu ni Mwingi wa rehema, ni Mwingi wa mapenzi na mahaba kwa aliyetubia na akarejea Kwake.» Katika hii aya, pana kuthibitisha sifa ya raḥmah (kurehemu) na mawaddah (kupenda) kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kama inavyonasibiana na Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake.
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالُواْ يَٰشُعَيۡبُ مَا نَفۡقَهُ كَثِيرٗا مِّمَّا تَقُولُ وَإِنَّا لَنَرَىٰكَ فِينَا ضَعِيفٗاۖ وَلَوۡلَا رَهۡطُكَ لَرَجَمۡنَٰكَۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيۡنَا بِعَزِيزٖ
Walisema, «Ewe Shu'ayb! Hatuyafahamu mengi unayotwambia, na sisi tunakuona wewe kuwa ni mnyonge kwetu, wewe si miongoni mwa watu wakubwa wala viongozi, na lau sisi si kuwastahi jamaa zako tungalikuua kwa kukupiga mawe.»- Na kundi la jamaa zake lilikuwa ni katika watu wanaofuata mila yao.- «Na wewe huna cheo wala heshima katika nafsi zetu.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَهۡطِيٓ أَعَزُّ عَلَيۡكُم مِّنَ ٱللَّهِ وَٱتَّخَذۡتُمُوهُ وَرَآءَكُمۡ ظِهۡرِيًّاۖ إِنَّ رَبِّي بِمَا تَعۡمَلُونَ مُحِيطٞ
Akasema, «Enyi watu wangu! Kwani jamaa zangu ni wenye nguvu zaidi na ni watukufu zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu? Na mumeitupa amri ya Mola wenu, mkaiweka nyuma ya migongo yenu, mkawa hamjilazimishi kufuata amri Zake na hamjiepushi na makatazo Yake. Hakika Mola wangu ni kwa mnayoyafanya Ameyazunguka, hakuna chochote katika matendo yenu kinafichika Kwake hata kama kina uzito wa chungu mdogo, na Atawalipa kwa hizo kwa haraka au baadaye.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَيَٰقَوۡمِ ٱعۡمَلُواْ عَلَىٰ مَكَانَتِكُمۡ إِنِّي عَٰمِلٞۖ سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ مَن يَأۡتِيهِ عَذَابٞ يُخۡزِيهِ وَمَنۡ هُوَ كَٰذِبٞۖ وَٱرۡتَقِبُوٓاْ إِنِّي مَعَكُمۡ رَقِيبٞ
«Na enyi watu wangu! Fanyeni mnaloliweza kwa njia yenu na namna yenu. Mimi ni mwenye kuendelea kufanya kwa njia yangu na nikitumia kile Mwenyezi Mungu Amenipa cha kuwalingania nyinyi kwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu. Mtajua ni nani miongoni mwetu, itamjia adhabu yenye kumfanya mnyonge, na ni nani, miongoni mwetu, ni mrongo katika maneno yake: ni mimi au ni nyinyi? Na mngojee kitakachowashukia; mimi ni miongoni mwa wenye kungojea pamoja na nyinyi.» Hili ni onyo kali kwao.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا نَجَّيۡنَا شُعَيۡبٗا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ بِرَحۡمَةٖ مِّنَّا وَأَخَذَتِ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ ٱلصَّيۡحَةُ فَأَصۡبَحُواْ فِي دِيَٰرِهِمۡ جَٰثِمِينَ
Na amri yetu ilipokuja ya kuwaangamiza watu wa Shu'ayb, tulimuokoa mjumbe wetu Shu'ayb na wale walioamini pamoja na yeye kwa rehema yetu. Na wale waliodhulumu walipatwa na ukulele kutoka mbinguni ukawaangamiza na wakawa wako majumbani mwao wamepiga magoti wakiwa ni wafu hawatikisiki.
Arabic explanations of the Qur’an:
كَأَن لَّمۡ يَغۡنَوۡاْ فِيهَآۗ أَلَا بُعۡدٗا لِّمَدۡيَنَ كَمَا بَعِدَتۡ ثَمُودُ
Kama kwamba wao hawakukaa kwenye nyumba zao wakati wowote. Jueni kwamba watu wa Madyan waliepushwa na rehema ya Mwenyezi Mungu, kwa kuwa Mwenyezi Mungu aliwaangamiza watu wake na akawalaani, kama vile kina Thamūd walivyoepushwa na rehema Yake. Makabila mawili haya yalishirikiana katika kuwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu na kuangamia.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا مُوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَا وَسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٍ
Hakika tulimtuma Mūsā na dalili zetu za upweke wetu na hoja inayomfahamisha mwenye kuiona na kuitia akilini, kwa moyo wenye siha, kwamba zinatoa dalili ya upweke wa Mwenyezi Mungu na urongo wa kila anayedai uola asiyekuwa Yeye, Aliyetakata na sifa za upungufu na kutukuka.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ فَٱتَّبَعُوٓاْ أَمۡرَ فِرۡعَوۡنَۖ وَمَآ أَمۡرُ فِرۡعَوۡنَ بِرَشِيدٖ
Tulimtuma Mūsā kwa Fir'awn na wakubwa wa wafuasi wake na watukufu wa watu wake, Fir'awn akakanusha na akawaamuru watu wake wamfuate yeye, wakamtii yeye na wakaenda kinyume cha amri ya Mūsā. Na hakuna uongofu wowote wala muongozo mwema katika amri ya Fir'awn, ni ujinga mtupu, upotevu, ukanushaji na ujeuri.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَقۡدُمُ قَوۡمَهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فَأَوۡرَدَهُمُ ٱلنَّارَۖ وَبِئۡسَ ٱلۡوِرۡدُ ٱلۡمَوۡرُودُ
Fir'awn atatangulia akiwaongoza watu wake Siku ya Kiyama mpaka awatie Motoni. Ni mahali pabaya ambapo wao wataiangia.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَأُتۡبِعُواْ فِي هَٰذِهِۦ لَعۡنَةٗ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ بِئۡسَ ٱلرِّفۡدُ ٱلۡمَرۡفُودُ
Na Mwenyezi Mungu Amewafuatishia laana katika ulimwengu huu, pamoja na adhabu Aliyowaharakishia ya kuzamishwa baharini. Na Siku ya Kiyama pia atawapa laana nyingine kwa kuwatia Motoni. Ni mabaya sana mambo yaliyokusanyika kwao na yakafuatana juu yao, ya adhabu ya Mwenyezi Mungu na laana ya duniani na Akhera.
Arabic explanations of the Qur’an:
ذَٰلِكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلۡقُرَىٰ نَقُصُّهُۥ عَلَيۡكَۖ مِنۡهَا قَآئِمٞ وَحَصِيدٞ
Haya tuliyokutajia wewe, ewe Mtume, ni miongoni mwa habari za watu wa miji ambayo tuliwaangamiza watu wake, twakupasha habari zake. Na miongoni mwa miji hiyo kuna iliyo na athari zilizosalia; na miongoni mwazo kuna ambazo athari zake zimefutika, hakuna chochote katika hizo kilichosalia.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَا ظَلَمۡنَٰهُمۡ وَلَٰكِن ظَلَمُوٓاْ أَنفُسَهُمۡۖ فَمَآ أَغۡنَتۡ عَنۡهُمۡ ءَالِهَتُهُمُ ٱلَّتِي يَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٖ لَّمَّا جَآءَ أَمۡرُ رَبِّكَۖ وَمَا زَادُوهُمۡ غَيۡرَ تَتۡبِيبٖ
Hakukuwa kuwaangamiza wao ni bila ya sababu na dhambi zinazowafanya wastahili hayo, lakini walijidhulumu wenyewe kwa ushirikina wao na kuleta kwao uharibifu katika ardhi. Hawakuwapa nafuu wao hao waungu wao ambao walikuwa wakidai kuwa ni waungu na wakiwataka wawaondolee shida, wakati amri ya Mwenyezi Mungu ilipokuja ya kuwaadhibu wao. Na hao waungu wao hawakuwazidishia isipokuwa uvunjaji, maangamivu na hasara.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَكَذَٰلِكَ أَخۡذُ رَبِّكَ إِذَآ أَخَذَ ٱلۡقُرَىٰ وَهِيَ ظَٰلِمَةٌۚ إِنَّ أَخۡذَهُۥٓ أَلِيمٞ شَدِيدٌ
Na kama nilivyowapatiliza kwa adhabu watu wa miji iliyodhulumu kwa kuenda kinyume na amri yangu na kuwakanusha Mitume wangu, nitawapatiliza wengineo miongoni mwa watu wa miji wakizidhulumu nafsi zao kwa kumkanusha Mwenyezi Mungu na kumuasi Yeye na kuwakanusha Mitume Wake. Hakika mapatilizo Yake ya mateso ni makali, yenye kuumiza, yaliyo magumu.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّمَنۡ خَافَ عَذَابَ ٱلۡأٓخِرَةِۚ ذَٰلِكَ يَوۡمٞ مَّجۡمُوعٞ لَّهُ ٱلنَّاسُ وَذَٰلِكَ يَوۡمٞ مَّشۡهُودٞ
Hakika katika kuwapatiliza watu wa miji iliyotangulia iliyodhulumu, ni mazingatio na mawaidha kwa anayeogopa mateso ya Mwenyezi Mungu na adhabu Yake huko Akhea. Siku hiyo ni ambayo watakusanywa watu wote ili wahesabiwe na walipwe, na wataishuhudia viumbe wote.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَا نُؤَخِّرُهُۥٓ إِلَّا لِأَجَلٖ مَّعۡدُودٖ
Na hatuicheleweshi Siku ya Kiyama isipokuwa ni ukome muda uliyohesabiwa uliyo kwenye elimu yetu, hauzidi wala haupungui na kipimo chetu tulichoupimia kwa hekima yetu.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَوۡمَ يَأۡتِ لَا تَكَلَّمُ نَفۡسٌ إِلَّا بِإِذۡنِهِۦۚ فَمِنۡهُمۡ شَقِيّٞ وَسَعِيدٞ
Siku kitakapokuja Kiyama, hakuna nafsi itakayosema isipokuwa kwa idhini ya Mola Wake. Kati yao kuna shaqiyy (muovu) anayestahili adhabu na kuna sa'īd (mwema) aliyefadhiliwa kwa kupewa starehe.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَأَمَّا ٱلَّذِينَ شَقُواْ فَفِي ٱلنَّارِ لَهُمۡ فِيهَا زَفِيرٞ وَشَهِيقٌ
Ama wale waliokuwa waovu ulimwenguni kwa kuharibika akida yao na uovu wa vitendo vyao, basi Moto utakuwa ndio mahali pao pa kutulia; humo watakuwa na kutoa pumzi kutoka kwenye vifua kwa nguvu na kurudisha kwa shida, na sauti mbili hizo ni mbaya zaidi zilizopita kiasi.
Arabic explanations of the Qur’an:
خَٰلِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ ٱلسَّمَٰوَٰتُ وَٱلۡأَرۡضُ إِلَّا مَا شَآءَ رَبُّكَۚ إِنَّ رَبَّكَ فَعَّالٞ لِّمَا يُرِيدُ
Watakuwa ni wenye kukaa humo milele muda wa kuweko mbingu na ardhi, hivyo basi adhabu yao haitakatika wala haitakoma, bali ni adhabu ya daima iliyotiliwa mkazo, isipokuwa iwapo Mola wako atataka, kwa kuwatoa waliompwekesha waliofanya maasia baada ya muda fulani wa kukaa kwao Motoni. Hakika Mola wako ni Mwenye kufanya Analolitaka.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ وَأَمَّا ٱلَّذِينَ سُعِدُواْ فَفِي ٱلۡجَنَّةِ خَٰلِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ ٱلسَّمَٰوَٰتُ وَٱلۡأَرۡضُ إِلَّا مَا شَآءَ رَبُّكَۖ عَطَآءً غَيۡرَ مَجۡذُوذٖ
Na ama wale ambao Mwenyezi Mungu Amewaruzuku wema, wataingia Peponi wakae milele humo muda wa kuwako mbingu na ardhi, isipokuwa lile kundi ambalo Mwenyezi Mungu Atataka kulichelewesha, nalo ni lile la waliompwekesha Mwenyezi Mungu waliofanya maasia. Wao watasalia Motoni kwa kipindi fulani, kisha watatoka humo kwenda Peponi kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu na rehema Yake. Na Mwenyezi Mungu Atawapa watu wema hawa vipaji visizopunguzwa.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَلَا تَكُ فِي مِرۡيَةٖ مِّمَّا يَعۡبُدُ هَٰٓؤُلَآءِۚ مَا يَعۡبُدُونَ إِلَّا كَمَا يَعۡبُدُ ءَابَآؤُهُم مِّن قَبۡلُۚ وَإِنَّا لَمُوَفُّوهُمۡ نَصِيبَهُمۡ غَيۡرَ مَنقُوصٖ
Basi usiwe, ewe Mtume, katika shaka kuhusu ubatilifu wa vitu wanavyoviabudu washirikina hawa miongoni mwa watu wako. Wao hawaabudu, miongoni mwa masanamu, isipokuwa kama vile baba zao walikuwa wakiabudu huko nyuma. Na sisi ni wenye kuwatekelezea kile tulichowaahidi kikiwa kikamilifu kisichopunguzwa. Huu ni muelekezo kwa ummah wote, ingawa tamko lake limeelekezwa kwa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani ziwashukie.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ فَٱخۡتُلِفَ فِيهِۚ وَلَوۡلَا كَلِمَةٞ سَبَقَتۡ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيۡنَهُمۡۚ وَإِنَّهُمۡ لَفِي شَكّٖ مِّنۡهُ مُرِيبٖ
Na hakika tulimpa Mūsā Kitabu , nacho ni Taurati, wakatafautiana watu wake juu yake: baadhi yao walikiamini na wengine walikikanusha, kama walivyofanya watu wako kuhusu Qur'ani. Na lao si neno lililotangulia kutoka kwa Mola wako la kutowaharakishia adhabu viumbe Wake, ingaliwashukia wao duniani kwao hukumu ya Mwenyezi Mungu ya kuwaangamiza wenye kukanusha na kuwaokoa Waumini. Na makafiri wa watu wako, miongoni mwa mayahudi na washirikina, ewe Mtume, wako kwenye shaka inayowatia wasiwasi juu hii Qur'ani.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِنَّ كُلّٗا لَّمَّا لَيُوَفِّيَنَّهُمۡ رَبُّكَ أَعۡمَٰلَهُمۡۚ إِنَّهُۥ بِمَا يَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ
Na hakika watu wote hao wanaotafautiana tuliokutajia habari zao , ewe Mtume, Mwenyezi Mungu Atawatekelezea malipo ya matendo yao Siku ya Kiyama, yakiwa mema watalipwa wema na yakiwa maovu watalipwa uovu. Hakika Mola wako , kwa wanayoyafanya hawa washirikina, ni Mtambuzi, hakuna kitendo chao chochote kinachofichamana Kwake. Katika hii pana kitisho na onyo kwao.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَٱسۡتَقِمۡ كَمَآ أُمِرۡتَ وَمَن تَابَ مَعَكَ وَلَا تَطۡغَوۡاْۚ إِنَّهُۥ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ
Basi kumana msimamo, ewe Nabii, kama Alivyokuamurisha Mola wako, wewe na waliotubia pamoja nawe, wala msikipite kile Alichowaekea mpaka Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wenu, kwa matendo yote mnayoyafanya, ni Muoni, hakuna kitu kinachofichika Kwake, na Atawalipa nyinyi kwa hayo.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَا تَرۡكَنُوٓاْ إِلَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ فَتَمَسَّكُمُ ٱلنَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِنۡ أَوۡلِيَآءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ
Wala msilemee upande wa hawa makafiri walio madhalimu, msije mkapatwa na Moto. Na hamna nyinyi msaidizi mwenye kuwanusuru na kusimamia mambo yenu isipokuwa Mwenyezi Mungu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ طَرَفَيِ ٱلنَّهَارِ وَزُلَفٗا مِّنَ ٱلَّيۡلِۚ إِنَّ ٱلۡحَسَنَٰتِ يُذۡهِبۡنَ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ ذَٰلِكَ ذِكۡرَىٰ لِلذَّٰكِرِينَ
Na tekeleza Swala, ewe Nabii, kwa njia ya ukamilifu katika ncha mbili za mchana: asubuhi na jioni, na katika nyakati za usiku. Kwani kufanya mema kunafuta dhambi zilizopita na kuondoa athari zake. Kuamrisha kusimamisha Swala na kueleza kwamba mema huondoa mabaya ni mawaidha kwa anayewaidhika nayo na akakumbuka.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱصۡبِرۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Na usubiri, ew Nabii, juu ya hiyo Swala na juu ya makero unayoyakuta kutoka kwa washirina wa watu wako, kwani Mwenyezi Mungu Hapotezi malipo ya walio wema katika matendo yao.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَلَوۡلَا كَانَ مِنَ ٱلۡقُرُونِ مِن قَبۡلِكُمۡ أُوْلُواْ بَقِيَّةٖ يَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡفَسَادِ فِي ٱلۡأَرۡضِ إِلَّا قَلِيلٗا مِّمَّنۡ أَنجَيۡنَا مِنۡهُمۡۗ وَٱتَّبَعَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مَآ أُتۡرِفُواْ فِيهِ وَكَانُواْ مُجۡرِمِينَ
Si ilikuwa wapatikane, miongoni mwa vizazi viliyopita kabla yenu, wasalia wa watu wazuri walio wema wanaowakataza makafiri waache ukafiri wao na kufanya uharibifu katika ardhi. Hawakupatikana katika hao isipokuwa wachache miongoni mwa walioamini na Mwenyezi Mungu akawaokoa na adhabu Yake Alipowapatiliza madhalimu. Na waliozidhulumu nafsi zao, miongoni mwa watu wa kila ummah uliopita, walifuata ladha za duniani na anasa zake walizostareheshwa, na wakawa wahalifu, wenye kudhulumu kwa kufuata kwao starehe walizokuwa nazo, ndipo adhabu ikathibiti juu yao. Katika hii aya pana mazingatio na mawaidha kwa wanaofanya maasia miongoni mwa Waislamu, kwa kuwa hawaepukani na udhalimu wa nafsi zao.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَا كَانَ رَبُّكَ لِيُهۡلِكَ ٱلۡقُرَىٰ بِظُلۡمٖ وَأَهۡلُهَا مُصۡلِحُونَ
Na hakuwa Mola wako, ewe Mtume, ni Mwenye kuuangamiza mji wowote miongoni mwa miji na hali watu wake ni wenye kufanya mambo mazuri katika ardhi, wenye kujiepusha na uharibifu na udhalimu; Yeye huwaangamiza wao kwa sababu ya udhalimu wao na uharibifu wao.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَوۡ شَآءَ رَبُّكَ لَجَعَلَ ٱلنَّاسَ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗۖ وَلَا يَزَالُونَ مُخۡتَلِفِينَ
Na lau Mola wako Alitaka, Angaliwafanya watu wote ni kundi moja, wako kwenye dini moja , nayo ni dini ya Uislamu. Lakini Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, hakutaka hivyo. Basi watu hawataacha kuendelea kutafautiana katika dini zao, na hayo ndiyo yanayoambatana na hekima Yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِلَّا مَن رَّحِمَ رَبُّكَۚ وَلِذَٰلِكَ خَلَقَهُمۡۗ وَتَمَّتۡ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمۡلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ أَجۡمَعِينَ
Isipokuwa wale waliorehemewa na Mola wako, wakamuamini Yeye na wakawafuata Mitume Wake, kwani wao hawatafautiani juu ya kumpwkwesha Mwenyezi Mungu na yale ambayo Mitume wamekuja nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Ni matakwa ya Hekima Yake, Aliyetakata na sifa za upungufu na Akatukuka, kwamba Yeye Amewaumba wao wakiwa wametafautiana: kuna kundi ovu na kundi lema; na kila kundi limesahilishiwa kwa lile lililoumbiwa, na kwa hii ndipo agizo la Mwenyezi Mungu litatimia la kuwa Yeye Ataujaza, Moto wa Jahanamu, majini na binadamu waliomfuata Iblisi na askari wake na wasiongoke kwenye njia ya Imani.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَكُلّٗا نَّقُصُّ عَلَيۡكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلرُّسُلِ مَا نُثَبِّتُ بِهِۦ فُؤَادَكَۚ وَجَآءَكَ فِي هَٰذِهِ ٱلۡحَقُّ وَمَوۡعِظَةٞ وَذِكۡرَىٰ لِلۡمُؤۡمِنِينَ
Na tunakupa habari, ewe Mtume, za Mitume waliokuwa kabla yako zenye kila unalohitajia la kuupa nguvu moyo wako ya kusimama imara ili kubeba majukumu ya Utume. Na umekujia wewe, katika sura hii na hahabri zilizomo, ufafanuzi wa haki ambayo wewe uko juu yake. Na yamekujia wewe, katika hii sura, mawaidha ya kuwafanya makafiri wakomeke na ukumbusho wa kuwafanya wenye kumuamini Mwenyezi mungu na Mitume Wake wakumbuke.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَقُل لِّلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ ٱعۡمَلُواْ عَلَىٰ مَكَانَتِكُمۡ إِنَّا عَٰمِلُونَ
Waambie, ewe Mtume, makafiri wasiokubali upweke wa Mwenyezi Mungu, «Fanyeni mnayoyafanya kwa namna yenu na mbinu zenu za kuupinga Ulinganizi na kumkera Mtume na wale waliomuitika, kwani sisi ni wenye kufanya kwa namna yetu mbinu zetu za kusimama imara juu ya Dini yetu na kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱنتَظِرُوٓاْ إِنَّا مُنتَظِرُونَ
Na ungojeni mwisho wa jambo letu, na sisi tunangojea mwisho wa jambo lenu.» Katika hii pana onyo na kitisho kwao.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلِلَّهِ غَيۡبُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَإِلَيۡهِ يُرۡجَعُ ٱلۡأَمۡرُ كُلُّهُۥ فَٱعۡبُدۡهُ وَتَوَكَّلۡ عَلَيۡهِۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ
Ni wa Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, ujuzi wa kila kisichoonekana mbinguni na ardhini. Na Kwake yanarejeshwa mambo yote Siku ya Kiyama. Basi muabudu Yeye, ewe Nabii, na umtegemezee mambo yako Kwake. Na Mola wako Hakuwa ni mwenye kughafilika na yale mnayoyafanya ya wema na uovu na Atamlipa kila mtu kwa matendo yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Surah: Hūd
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis Abdurahman - Translations’ Index

Translation of the Quran meanings into Swahili by Dr. Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis

close