Check out the new design

Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassarar Sawahil - Cibiyar fassara ta Ruwwad * - Teburin Bayani kan wasu Fassarori


Fassarar Ma'anoni Sura: Al'waki'ah   Aya:

Al-Waqi'ah

إِذَا وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ
Litakapotokea hilo Tukio.
Tafsiran larabci:
لَيۡسَ لِوَقۡعَتِهَا كَاذِبَةٌ
Hapana cha kukanusha kutokea kwake.
Tafsiran larabci:
خَافِضَةٞ رَّافِعَةٌ
Literemshalo linyanyualo.
Tafsiran larabci:
إِذَا رُجَّتِ ٱلۡأَرۡضُ رَجّٗا
Itakapotikiswa ardhi kwa mtikiso.
Tafsiran larabci:
وَبُسَّتِ ٱلۡجِبَالُ بَسّٗا
Na milima itakaposagwasagwa.
Tafsiran larabci:
فَكَانَتۡ هَبَآءٗ مُّنۢبَثّٗا
Basi iwe mavumbi yanayopeperushwa.
Tafsiran larabci:
وَكُنتُمۡ أَزۡوَٰجٗا ثَلَٰثَةٗ
Na nyinyi mtakuwa namna tatu.
Tafsiran larabci:
فَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ
Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani?
Tafsiran larabci:
وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ
Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni?
Tafsiran larabci:
وَٱلسَّٰبِقُونَ ٱلسَّٰبِقُونَ
Na wa mbele watakuwa mbele.
Tafsiran larabci:
أُوْلَٰٓئِكَ ٱلۡمُقَرَّبُونَ
Hao ndio watakaowekwa karibu (na Mwenyezi Mungu).
Tafsiran larabci:
فِي جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ
Katika Bustani zenye neema.
Tafsiran larabci:
ثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ
Fungu kubwa katika wa mwanzo.
Tafsiran larabci:
وَقَلِيلٞ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ
Na wachache katika wa mwisho.
Tafsiran larabci:
عَلَىٰ سُرُرٖ مَّوۡضُونَةٖ
Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyotonewa.
Tafsiran larabci:
مُّتَّكِـِٔينَ عَلَيۡهَا مُتَقَٰبِلِينَ
Wakiviegemea wakielekeana.
Tafsiran larabci:
يَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ وِلۡدَٰنٞ مُّخَلَّدُونَ
Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele.
Tafsiran larabci:
بِأَكۡوَابٖ وَأَبَارِيقَ وَكَأۡسٖ مِّن مَّعِينٖ
Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemichemi safi.
Tafsiran larabci:
لَّا يُصَدَّعُونَ عَنۡهَا وَلَا يُنزِفُونَ
Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa.
Tafsiran larabci:
وَفَٰكِهَةٖ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ
Na matunda wayapendayo.
Tafsiran larabci:
وَلَحۡمِ طَيۡرٖ مِّمَّا يَشۡتَهُونَ
Na nyama za ndege kama wanavyotamani.
Tafsiran larabci:
وَحُورٌ عِينٞ
Na Mahurulaini.
Tafsiran larabci:
كَأَمۡثَٰلِ ٱللُّؤۡلُوِٕ ٱلۡمَكۡنُونِ
Walio kama mfano wa lulu zilizohifadhiwa.
Tafsiran larabci:
جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Ni malipo kwa waliyokuwa wakiyatenda.
Tafsiran larabci:
لَا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوٗا وَلَا تَأۡثِيمًا
Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi.
Tafsiran larabci:
إِلَّا قِيلٗا سَلَٰمٗا سَلَٰمٗا
Isipokuwa maneno ya Salama, Salama.
Tafsiran larabci:
وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ
Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani?
Tafsiran larabci:
فِي سِدۡرٖ مَّخۡضُودٖ
Katika mikunazi isiyo na miba.
Tafsiran larabci:
وَطَلۡحٖ مَّنضُودٖ
Na migomba iliyopangiliwa.
Tafsiran larabci:
وَظِلّٖ مَّمۡدُودٖ
Na kivuli kilichotanda.
Tafsiran larabci:
وَمَآءٖ مَّسۡكُوبٖ
Na maji yanayomiminika.
Tafsiran larabci:
وَفَٰكِهَةٖ كَثِيرَةٖ
Na matunda mengi.
Tafsiran larabci:
لَّا مَقۡطُوعَةٖ وَلَا مَمۡنُوعَةٖ
Hayatindikii wala hayakatazwi.
Tafsiran larabci:
وَفُرُشٖ مَّرۡفُوعَةٍ
Na matandiko yaliyonyanyuliwa.
Tafsiran larabci:
إِنَّآ أَنشَأۡنَٰهُنَّ إِنشَآءٗ
Hakika Sisi tutawaumba (Mahurulaini) upya.
Tafsiran larabci:
فَجَعَلۡنَٰهُنَّ أَبۡكَارًا
Na tutawafanya vijana.
Tafsiran larabci:
عُرُبًا أَتۡرَابٗا
Wanapendana na waume zao, hirimu moja.
Tafsiran larabci:
لِّأَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ
Kwa ajili ya watu wa kuliani.
Tafsiran larabci:
ثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ
Fungu kubwa katika wa mwanzo.
Tafsiran larabci:
وَثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ
Na fungu kubwa katika wa mwisho.
Tafsiran larabci:
وَأَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ
Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni?
Tafsiran larabci:
فِي سَمُومٖ وَحَمِيمٖ
Katika upepo wa moto, na maji yanayochemka.
Tafsiran larabci:
وَظِلّٖ مِّن يَحۡمُومٖ
Na kivuli cha moshi mweusi.
Tafsiran larabci:
لَّا بَارِدٖ وَلَا كَرِيمٍ
Si baridi wala cha kustarehesha.
Tafsiran larabci:
إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُتۡرَفِينَ
Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa.
Tafsiran larabci:
وَكَانُواْ يُصِرُّونَ عَلَى ٱلۡحِنثِ ٱلۡعَظِيمِ
Na walikuwa wakiendelea tu kufanya madhambi makubwa.
Tafsiran larabci:
وَكَانُواْ يَقُولُونَ أَئِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ
Na walikuwa wakisema: 'Tutakapokufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndiyo tutafufuliwa?
Tafsiran larabci:
أَوَءَابَآؤُنَا ٱلۡأَوَّلُونَ
Au baba zetu wa zamani?'
Tafsiran larabci:
قُلۡ إِنَّ ٱلۡأَوَّلِينَ وَٱلۡأٓخِرِينَ
Sema: 'Hakika wa zamani na wa mwisho.'
Tafsiran larabci:
لَمَجۡمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَٰتِ يَوۡمٖ مَّعۡلُومٖ
Bila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa siku maalumu.
Tafsiran larabci:
ثُمَّ إِنَّكُمۡ أَيُّهَا ٱلضَّآلُّونَ ٱلۡمُكَذِّبُونَ
Kisha nyinyi, mliopotea, mnaokanusha.
Tafsiran larabci:
لَأٓكِلُونَ مِن شَجَرٖ مِّن زَقُّومٖ
Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu.
Tafsiran larabci:
فَمَالِـُٔونَ مِنۡهَا ٱلۡبُطُونَ
Na kwa mti huo mtajaza matumbo.
Tafsiran larabci:
فَشَٰرِبُونَ عَلَيۡهِ مِنَ ٱلۡحَمِيمِ
Na juu yake mtakunywa maji yanayochemka.
Tafsiran larabci:
فَشَٰرِبُونَ شُرۡبَ ٱلۡهِيمِ
Tena mtakunywa kama wanavyokunywa ngamia wenye kiu.
Tafsiran larabci:
هَٰذَا نُزُلُهُمۡ يَوۡمَ ٱلدِّينِ
Hiyo ndiyo karamu yao ya kuwakaribisha Siku ya Malipo.
Tafsiran larabci:
نَحۡنُ خَلَقۡنَٰكُمۡ فَلَوۡلَا تُصَدِّقُونَ
Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki?
Tafsiran larabci:
أَفَرَءَيۡتُم مَّا تُمۡنُونَ
Je, mnaiona mbegu ya uzazi mnayoidondokesha?
Tafsiran larabci:
ءَأَنتُمۡ تَخۡلُقُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡخَٰلِقُونَ
Je, mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji?
Tafsiran larabci:
نَحۡنُ قَدَّرۡنَا بَيۡنَكُمُ ٱلۡمَوۡتَ وَمَا نَحۡنُ بِمَسۡبُوقِينَ
Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi.
Tafsiran larabci:
عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ أَمۡثَٰلَكُمۡ وَنُنشِئَكُمۡ فِي مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilolijua.
Tafsiran larabci:
وَلَقَدۡ عَلِمۡتُمُ ٱلنَّشۡأَةَ ٱلۡأُولَىٰ فَلَوۡلَا تَذَكَّرُونَ
Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki?
Tafsiran larabci:
أَفَرَءَيۡتُم مَّا تَحۡرُثُونَ
Je, mnaona hivyo mnavyovipanda?
Tafsiran larabci:
ءَأَنتُمۡ تَزۡرَعُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلزَّٰرِعُونَ
Je, ni nyinyi mnayoyaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha?
Tafsiran larabci:
لَوۡ نَشَآءُ لَجَعَلۡنَٰهُ حُطَٰمٗا فَظَلۡتُمۡ تَفَكَّهُونَ
Tungelitaka, tungeliyafanya yakawa mapepe, mkabaki mnastaajabu.
Tafsiran larabci:
إِنَّا لَمُغۡرَمُونَ
Mkisema: 'Hakika sisi tumegharimika.'
Tafsiran larabci:
بَلۡ نَحۡنُ مَحۡرُومُونَ
Bali sisi tumenyimwa.
Tafsiran larabci:
أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلۡمَآءَ ٱلَّذِي تَشۡرَبُونَ
Je, mnayaona maji mnayoyanywa?
Tafsiran larabci:
ءَأَنتُمۡ أَنزَلۡتُمُوهُ مِنَ ٱلۡمُزۡنِ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنزِلُونَ
Je, ni nyinyi mnaoyateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha?
Tafsiran larabci:
لَوۡ نَشَآءُ جَعَلۡنَٰهُ أُجَاجٗا فَلَوۡلَا تَشۡكُرُونَ
Tungelipenda, tungeliyafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru?
Tafsiran larabci:
أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلنَّارَ ٱلَّتِي تُورُونَ
Je, mnauona moto mnaouwasha?
Tafsiran larabci:
ءَأَنتُمۡ أَنشَأۡتُمۡ شَجَرَتَهَآ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنشِـُٔونَ
Ni nyinyi mliouumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji?
Tafsiran larabci:
نَحۡنُ جَعَلۡنَٰهَا تَذۡكِرَةٗ وَمَتَٰعٗا لِّلۡمُقۡوِينَ
Sisi tumeufanya uwe ni ukumbusho na manufaa kwa walioko nyikani.
Tafsiran larabci:
فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ
Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu.
Tafsiran larabci:
۞ فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَوَٰقِعِ ٱلنُّجُومِ
Basi ninaapa kwa maanguko ya nyota.
Tafsiran larabci:
وَإِنَّهُۥ لَقَسَمٞ لَّوۡ تَعۡلَمُونَ عَظِيمٌ
Na hakika bila ya shaka hiki ni kiapo kikubwa, laiti mngelijua!
Tafsiran larabci:
إِنَّهُۥ لَقُرۡءَانٞ كَرِيمٞ
Hakika hii bila ya shaka ni Qur-ani Tukufu.
Tafsiran larabci:
فِي كِتَٰبٖ مَّكۡنُونٖ
Katika Kitabu kilichohifadhiwa.
Tafsiran larabci:
لَّا يَمَسُّهُۥٓ إِلَّا ٱلۡمُطَهَّرُونَ
Hapana akigusaye ila waliotakaswa.
Tafsiran larabci:
تَنزِيلٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Ni uteremsho unaotoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Tafsiran larabci:
أَفَبِهَٰذَا ٱلۡحَدِيثِ أَنتُم مُّدۡهِنُونَ
Ni maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza?
Tafsiran larabci:
وَتَجۡعَلُونَ رِزۡقَكُمۡ أَنَّكُمۡ تُكَذِّبُونَ
Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha?
Tafsiran larabci:
فَلَوۡلَآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلۡحُلۡقُومَ
Yawaje basi itakapofika roho kwenye koo.
Tafsiran larabci:
وَأَنتُمۡ حِينَئِذٖ تَنظُرُونَ
Na nyinyi wakati huo mnatazama!
Tafsiran larabci:
وَنَحۡنُ أَقۡرَبُ إِلَيۡهِ مِنكُمۡ وَلَٰكِن لَّا تُبۡصِرُونَ
Na Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi, lakini hamuoni.
Tafsiran larabci:
فَلَوۡلَآ إِن كُنتُمۡ غَيۡرَ مَدِينِينَ
Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu.
Tafsiran larabci:
تَرۡجِعُونَهَآ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Kwa nini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli?
Tafsiran larabci:
فَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ
Kwa hivyo, akiwa miongoni mwa wale walio karibu na Mwenyezi Mungu.
Tafsiran larabci:
فَرَوۡحٞ وَرَيۡحَانٞ وَجَنَّتُ نَعِيمٖ
Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema.
Tafsiran larabci:
وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ
Na akiwa katika wale wa upande wa kulia.
Tafsiran larabci:
فَسَلَٰمٞ لَّكَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ
Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa wale wa upande wa kulia.
Tafsiran larabci:
وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُكَذِّبِينَ ٱلضَّآلِّينَ
Na ama akiwa katika wale waliokadhibisha, wapotovu.
Tafsiran larabci:
فَنُزُلٞ مِّنۡ حَمِيمٖ
Basi karamu ya makaribisho yake ni maji yanayochemka.
Tafsiran larabci:
وَتَصۡلِيَةُ جَحِيمٍ
Na kutiwa Motoni.
Tafsiran larabci:
إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ حَقُّ ٱلۡيَقِينِ
Hakika hii ndiyo haki yenye yakini.
Tafsiran larabci:
فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ
Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu.
Tafsiran larabci:
 
Fassarar Ma'anoni Sura: Al'waki'ah
Teburin Jerin Sunayen Surori Lambar shafi
 
Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassarar Sawahil - Cibiyar fassara ta Ruwwad - Teburin Bayani kan wasu Fassarori

Wani gungu na cibiyar fassara ta Ruwad ne suka fassarasu tare da haɗin gwiwar Ƙungiyar Da'awa ta Rabwah da Kungiyar hidimtawa abinda Musulunci ya kunsa da yaruka

Rufewa