क़ुरआन के अर्थों का अनुवाद - स्वाहीली अनुवाद - अब्दुल्लाह मुहम्मद तथा नासिर ख़मीस * - अनुवादों की सूची


अर्थों का अनुवाद सूरा: सूरा अन्-नह़्ल   आयत:

Surat An-Nahl

أَتَىٰٓ أَمۡرُ ٱللَّهِ فَلَا تَسۡتَعۡجِلُوهُۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ
Kumekaribia kusimama Kiyama na kutoka amri ya Mwenyezi Mungu ya kuwaadhibu nyinyi, enyi makafiri, basi msiifanyie haraka adhabu kwa njia ya kuicheza shere ahadi ya Mtume kwenu. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Ameepukana na ushirika na washirikina.
अरबी तफ़सीरें:
يُنَزِّلُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ بِٱلرُّوحِ مِنۡ أَمۡرِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦٓ أَنۡ أَنذِرُوٓاْ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱتَّقُونِ
Mwenyezi Mungu Anawateremsha Malaika kuleta wahyi kwa amri Yake kwa anayemtaka miongoni mwa waja Wake waliotumilizwa kwamba watisheni watu na ushirikina na waambieni kwamba hapana wa kuabudiwa kwa haki isipokuwa mimi. Hivyo basi, nicheni kwa kutekeleza faradhi zangu na kunipwekesha kwa kuniabudu na kunitakasa.
अरबी तफ़सीरें:
خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّۚ تَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ
Ameziumba mbingu na ardhi kwa haki, ili waja kwa hizo wachukue ushahidi juu ya utukufu wa Muumba wa hizo na kwamba, Yeye Peke Yake, Ndiye Anayestahiki kuabudiwa, Ameepukana, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, na Ametukuka na ushirikina wao.
अरबी तफ़सीरें:
خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِن نُّطۡفَةٖ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٞ مُّبِينٞ
Amemuumba binadamu kutokana na maji matwevu, akitahamaki ajiona ana nguvu na majivuno, na akawa mkali wa utesi na kumjadili Mola wake katika kukanusha kufufuliwa na mengineyo, kama vile kusema, «Ni nani atakayeihuisha mifupa iwapo imeoza.» Na akawa ni mwenye kumsahau Mwenyezi Mungu Aliyemuumba kutoka kwenye hali ya kutokuwako.
अरबी तफ़सीरें:
وَٱلۡأَنۡعَٰمَ خَلَقَهَاۖ لَكُمۡ فِيهَا دِفۡءٞ وَمَنَٰفِعُ وَمِنۡهَا تَأۡكُلُونَ
Na wanyama miongoni mwa ngamia, ng’ombe na mbuzi, Mwenyezi Mungu Amewaumbia, enyi watu, na akajaalia joto katika sufi na manyoa yake, na manufaa mengine katika maziwa yake na ngozi zake na kuwatumia kwa kuwapanda na, wengine miongoni mwao, kuwala.
अरबी तफ़सीरें:
وَلَكُمۡ فِيهَا جَمَالٌ حِينَ تُرِيحُونَ وَحِينَ تَسۡرَحُونَ
Na muna, kwa wanyama hao, pambo linaloingiza furaha kwenu, pindi mnapowarudisha kwenye mazizi yao jioni na pindi mnapowatoa kukicha kuwapeleka malishoni.
अरबी तफ़सीरें:
وَتَحۡمِلُ أَثۡقَالَكُمۡ إِلَىٰ بَلَدٖ لَّمۡ تَكُونُواْ بَٰلِغِيهِ إِلَّا بِشِقِّ ٱلۡأَنفُسِۚ إِنَّ رَبَّكُمۡ لَرَءُوفٞ رَّحِيمٞ
Na wanabeba wanyama hawa vyombo vyenu vizito kuvipeleka kwenye mji wa mbali ambao hamkuwa ni wenye kuufikia isipokuwa kwa usumbufu mwingi wa nafsi zenu na mashaka makubwa. Hakika Mola wenu ni Mpole, Mwenye huruma kwenu kwa kuwafanyia vitu mnavyovitaka kuwa vipesi. Hivyo basi kusifiwa ni Kwake na kushukuriwa.
अरबी तफ़सीरें:
وَٱلۡخَيۡلَ وَٱلۡبِغَالَ وَٱلۡحَمِيرَ لِتَرۡكَبُوهَا وَزِينَةٗۚ وَيَخۡلُقُ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Na Amewaumbia farasi, nyumbu na punda, mpate kuwapanda na wawe ni pambo kenu nyinyi na maangalizi mazuri. Na Anawaumbia nyinyi aina mbalimbali za vipando na vinginevyo ambavyo nyinyi hamna ujuzi navyo, ili mzidi kumuamini na kumshukuru.
अरबी तफ़सीरें:
وَعَلَى ٱللَّهِ قَصۡدُ ٱلسَّبِيلِ وَمِنۡهَا جَآئِرٞۚ وَلَوۡ شَآءَ لَهَدَىٰكُمۡ أَجۡمَعِينَ
Na ni juu ya Mwenyezi Mungu kuwaeleza njia iliolingana sawa ya kuwaongoa nyinyi, nayo ni Uislamu. Na miongoni mwa njia kuna iliyoenda kombo isiyofikisha kwenye uongofu, nayo ni kila njia iliyo kinyume na Uislamu miongoni mwa mila na itikadi. Na lau Angalitaka Mwenyezi Mungu kuwaongoza, basi Angaliwaongoza nyote kwenye Imani.
अरबी तफ़सीरें:
هُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗۖ لَّكُم مِّنۡهُ شَرَابٞ وَمِنۡهُ شَجَرٞ فِيهِ تُسِيمُونَ
Yeye Ndiye Aliyewateremshia mvua kutoka juu na Akawapatia nyinyi kwa hiyo mvua maji mnayokunywa na akawatolea kwa maji hayo miti ya nyinyi kuwalisha wanyama wenu, na yanarudi kwenu matumizi yake na manufaa yake.
अरबी तफ़सीरें:
يُنۢبِتُ لَكُم بِهِ ٱلزَّرۡعَ وَٱلزَّيۡتُونَ وَٱلنَّخِيلَ وَٱلۡأَعۡنَٰبَ وَمِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَتَفَكَّرُونَ
Anawatolea nyinyi kutoka kwenye ardhi, kwa maji haya mamoja, mazao mbalimbali: Anawatolea nyinyi kwayo mizaituni, mitende na mizabibu, na anawatolea nyinyi kwayo kila aina ya matunda, makubwa kwa madogo. Hakika katika hayo pana ushahidi waziwazi kwa watu wanaofikiri na wakazingatia.
अरबी तफ़सीरें:
وَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَ وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ وَٱلنُّجُومُ مُسَخَّرَٰتُۢ بِأَمۡرِهِۦٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ
Na Amewadhalilishia usiku kwa mapumziko yenu, na mchana kwa maisha yenu, na Amewadhalilishia jua likawa na mwangaza, na mwezi ukawa na nuru, na ili mpate kujua miaka na hesabu na manufaa mengine yasiyokuwa hayo. Na nyota huko mbinguni zimedhalilishwa kwa ajili yenu kwa amri ya Mwenyezi Mungu, ili mjue nyakati, kuiva kwa matunda na mazao na pia kuongoka kwa nyota hizo kwenye giza. Hakika, katika kudhalilisha huko, kuna alama waziwazi kwa watu wanaotia mambo akilini mwao kuhusu Mwenyezi Mungu, hoja Zake na alama Zake.
अरबी तफ़सीरें:
وَمَا ذَرَأَ لَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُخۡتَلِفًا أَلۡوَٰنُهُۥٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَذَّكَّرُونَ
Na Amewadhalilishia vile Alivyowaumbia katika ardhi miongoni mwa vinavyotambaa humo na matunda na madini na visivyokuwa hivyo ambavyo vina rangi na manufaa mbalimbali. Hakika katika uumbaji huo na kutafautiana rangi na manufaa pana mazingatio kwa watu wanaowaidhika na wanaojua kwamba katika kuvidhalilisha vitu hivyi pana alama nyingi juu ya umoja wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na juu ya kumpwekesha kwa ibada.
अरबी तफ़सीरें:
وَهُوَ ٱلَّذِي سَخَّرَ ٱلۡبَحۡرَ لِتَأۡكُلُواْ مِنۡهُ لَحۡمٗا طَرِيّٗا وَتَسۡتَخۡرِجُواْ مِنۡهُ حِلۡيَةٗ تَلۡبَسُونَهَاۖ وَتَرَى ٱلۡفُلۡكَ مَوَاخِرَ فِيهِ وَلِتَبۡتَغُواْ مِن فَضۡلِهِۦ وَلَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ
Na Yeye Ndiye Ambaye Amewadhalilishia bahari ili mpate kula nyama laini ya samaki mnaowavua, na mtoe humo pambo mnalolivaa kama lulu na marjani, na utaziona jahazi kubwa zinapasua uso wa maji zikienda na kurudi, na mnazipanda ili mtafute riziki ya Mwenyezi Mungu kwa kufanya biashara na kutafuta faida ndani yake. Kwani huenda nyinyi mkamshukuru Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa neema zake kubwa juu yenu na msimuabudu asiyekuwa Yeye.
अरबी तफ़सीरें:
وَأَلۡقَىٰ فِي ٱلۡأَرۡضِ رَوَٰسِيَ أَن تَمِيدَ بِكُمۡ وَأَنۡهَٰرٗا وَسُبُلٗا لَّعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ
Na Ameyakitisha kwenye ardhi majabali ya kuithibitisha ili isije ikawayumbisha nyinyi, na Ameiweka humo mito ili mpate kunywa maji yake, na Amefanya humo njia nyingi ili mpate kuongoka kwa njia hizo kuzifikia sehemu mnazozikusudia.
अरबी तफ़सीरें:
وَعَلَٰمَٰتٖۚ وَبِٱلنَّجۡمِ هُمۡ يَهۡتَدُونَ
Na kwenye hiyo ardhi Ameweka alama ambazo kwa alama hizo mnajielekeza njia kipindi cha mchana, kama alivyoziweka nyota ili kujiongoza kwa nyota hizo kipindi cha usiku.
अरबी तफ़सीरें:
أَفَمَن يَخۡلُقُ كَمَن لَّا يَخۡلُقُۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Basi mnamfanya Mwenyezi Mungu Ambaye Anaviumba vitu hivyi na vinginevyo, katika kustahiki Kwake kuabudiwa Peke Yake, ni kama waungu wanaodaiwa ambao hawaumbi chochote? Basi hamukumbuki utukufu wa Mwenyezi Mungu mkamuabudu Yeye Peke Yake?
अरबी तफ़सीरें:
وَإِن تَعُدُّواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ لَا تُحۡصُوهَآۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ
Na mkijaribu kuzidhibiti neema za Mwenyezi Mungu kwenu, ili mjue idadi yake, hamuwezi kuzidhibiti kwa wingi wake na utafauti wake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, ni Mwenye huruma kwenu, kwani Anasamehe kasoro zenu za kutotekeleza ushukuru wa neema, wala Hazikati kwenu, kwa kukiuka kwenu mipaka, wala Hawaharakishii mateso.
अरबी तफ़सीरें:
وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعۡلِنُونَ
Na Mwenyezi Mungu, Aliyetakata na kila aina ya upungufu, Anayajua matendo yenu yote, sawasawa yale mnayoyaficha ndani ya nafsi zenu kati ya hayo na yale mnayoyafanya waziwazi mbele ya wengine, na Atawalipa kwayo.
अरबी तफ़सीरें:
وَٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ لَا يَخۡلُقُونَ شَيۡـٔٗا وَهُمۡ يُخۡلَقُونَ
Na wale waungu ambao washirikina wanawaabudu hawaumbi chochote hata kama ni kidogo vipi. Hao ni viumbe ambazo washirikina wamevitengeneza kwa mikono yao. Vipi basi wataviabudu?
अरबी तफ़सीरें:
أَمۡوَٰتٌ غَيۡرُ أَحۡيَآءٖۖ وَمَا يَشۡعُرُونَ أَيَّانَ يُبۡعَثُونَ
Wote hao ni visiki, havina uhai, wala hawajui wakati ambao Mwenyezi Mungu Atawafufua wale wanaowaabudu. Na waungu hao pamoja na wanaowaabudu wote watatupwa Motoni Siku ya Kiyama.
अरबी तफ़सीरें:
إِلَٰهُكُمۡ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۚ فَٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ قُلُوبُهُم مُّنكِرَةٞ وَهُم مُّسۡتَكۡبِرُونَ
Mola wenu Ndiye Mstahiki wa kuabudiwa Peke Yake. Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu Mmoja Peke Yake, hivyo basi wale wasioamini kufufuliwa, nyoyo zao ni zenye kuukanusha upweke Wake, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, kwa kutoogopa mateso Yake. Kwa hivyo, wao wana ujeuri wa kutoikubali haki na kukataa kumuabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake.
अरबी तफ़सीरें:
لَا جَرَمَ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعۡلِنُونَۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُسۡتَكۡبِرِينَ
Ni kweli kwamba Mwenyezi Mungu Anayajua wanayoyaficha ya itikadi, maneno na vitendo, na wanayoyaonyesha waziwazi katika hayo, na Atawalipa kwa hayo. Kwa kweli Yeye, Aliyeshinda na kutukuka, Hawapendi wanaofanya ujeuri wa kukataa kumuabudu na kumtii, na Atawalipa kwa hilo.
अरबी तफ़सीरें:
وَإِذَا قِيلَ لَهُم مَّاذَآ أَنزَلَ رَبُّكُمۡ قَالُوٓاْ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ
Na pindi wanapoulizwa, hawa washirikina, kuhusu yale yaliyoteremshiwa Nabii Muhammad, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, wanasema kwa urongo na uzushi, «Hakuleta isipokuwa visa vya waliotangulia na porojo zao.»
अरबी तफ़सीरें:
لِيَحۡمِلُوٓاْ أَوۡزَارَهُمۡ كَامِلَةٗ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَمِنۡ أَوۡزَارِ ٱلَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيۡرِ عِلۡمٍۗ أَلَا سَآءَ مَا يَزِرُونَ
Mwisho wao utakuwa ni kuzibeba dhambi zao kamili Siku ya Kiyama, hawatasamehewa chochote, na watazibeba dhambi za wale waliowadanganya ili kuwaepusha na Uislamu, bila ya kupunguziwa dhambi zao. Jueni mtanabahi, ni ubaya ulioje wa dhambi watakazozibeba!
अरबी तफ़सीरें:
قَدۡ مَكَرَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ فَأَتَى ٱللَّهُ بُنۡيَٰنَهُم مِّنَ ٱلۡقَوَاعِدِ فَخَرَّ عَلَيۡهِمُ ٱلسَّقۡفُ مِن فَوۡقِهِمۡ وَأَتَىٰهُمُ ٱلۡعَذَابُ مِنۡ حَيۡثُ لَا يَشۡعُرُونَ
Kabla ya washirikina hawa, makafiri waliwafanyia vitimbi Mitume wao, na kuifanyia vitimbi haki waliokuja nayo. Hapo amri ya Mwenyezi Mungu ililijia jengo lao kutoka kwenye asili yake na msingi wake, na sakafu ikawaangukia, na maangamivu yakawajia kwenye sehemu ambazo walijimakini kuwa ni za amani, kutoka mahali wasipodhania kuwa maangamivu yatawajia kutoka hapo.
अरबी तफ़सीरें:
ثُمَّ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يُخۡزِيهِمۡ وَيَقُولُ أَيۡنَ شُرَكَآءِيَ ٱلَّذِينَ كُنتُمۡ تُشَٰٓقُّونَ فِيهِمۡۚ قَالَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ إِنَّ ٱلۡخِزۡيَ ٱلۡيَوۡمَ وَٱلسُّوٓءَ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ
Kisha Siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu Atawafedhehi na Atawafanya wanyonge kwa adhabu na Atasema, «Wako wapi washirika wangu miongoni mwa waungu mliowaabudu badala yangu ili wawatetee msipate adhabu, na hali mlikuwa mkiwapiga vita Manabii na Waumini na mkiwafanyia uadui kwa sababu ya waungu hao?» Wanavyuoni wachamungu watasema, «Hakika utwevu na adhabu ndani ya Siku hii zitawashukia wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu na Mitume Wake
अरबी तफ़सीरें:
ٱلَّذِينَ تَتَوَفَّىٰهُمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ ظَالِمِيٓ أَنفُسِهِمۡۖ فَأَلۡقَوُاْ ٱلسَّلَمَ مَا كُنَّا نَعۡمَلُ مِن سُوٓءِۭۚ بَلَىٰٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمُۢ بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
ambao Malaika watazichukua roho zao, na wao wako katika hali ya kuzidhulumu nafsi zao kwa kukanusha.» Hapo watajisalimisha kwenye amri ya Mwenyezi Mungu pindi wanapoyaona mauti, na watavikanusha vile walivyokuwa wakiviabudu badala ya Mwenyezi Mungu na watasema, «Hatukuwa tukifanya maasia yoyote.» Na wataambiwa, «Mnasema urongo! Kwa hakika, mlikuwa mkiyafanya. Mwenyezi Mungu Anayajua matendo yenu yote na Atawalipa kwayo.»
अरबी तफ़सीरें:
فَٱدۡخُلُوٓاْ أَبۡوَٰبَ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَاۖ فَلَبِئۡسَ مَثۡوَى ٱلۡمُتَكَبِّرِينَ
Ingieni milango ya Jahanamu. Hamtotoka humo milele. Na mahali hapo ni paovu pa kukaa wenye kiburi waliokataa kumuamini Mwenyezi Mungu, kumuabudu Yeye Peke Yake na kumtii.
अरबी तफ़सीरें:
۞ وَقِيلَ لِلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ مَاذَآ أَنزَلَ رَبُّكُمۡۚ قَالُواْ خَيۡرٗاۗ لِّلَّذِينَ أَحۡسَنُواْ فِي هَٰذِهِ ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٞۚ وَلَدَارُ ٱلۡأٓخِرَةِ خَيۡرٞۚ وَلَنِعۡمَ دَارُ ٱلۡمُتَّقِينَ
Na wanapoambiwa Waumini wenye kumuogopa Mwenyezi Mungu, «Ni kitu gani Alichokiteremsha Mwenyezi Mungu kwa Nabii Muhammad, rehema na amani zimshukie?» wanasema, «Mwenyezi Mungu Amemteremshia wema na uongofu.» Wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake hapa duniani na wakawalingania waja wa Mwenyezi Mungu kwenye Imani na matendo mema, watapata heshima kubwa ya kupewa ushindi duniani na riziki kunjufu. Na nyumba ya Akhere ni bora kwao na ni kubwa kuliko vile walivyopewa duniani. Na nyumba yenye neema zaidi ya wale wachamungu wenye kumuogopa Mwenyezi Mungu ni Akhera.
अरबी तफ़सीरें:
جَنَّٰتُ عَدۡنٖ يَدۡخُلُونَهَا تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ لَهُمۡ فِيهَا مَا يَشَآءُونَۚ كَذَٰلِكَ يَجۡزِي ٱللَّهُ ٱلۡمُتَّقِينَ
Makazi yao ni mabustani ya Pepo ya Milele, watatulia humo, hawatatoka humo kabisa, mito itakuwa ikipita chini ya miti yake na majumba yake ya fahari. Watakuwa na kila kinachotamaniwa na nafsi zao. Kwa mfano wa malipo haya mazuri, Mwenyezi Mungu Atawalipa wachamungu wenye kumuogopa
अरबी तफ़सीरें:
ٱلَّذِينَ تَتَوَفَّىٰهُمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ طَيِّبِينَ يَقُولُونَ سَلَٰمٌ عَلَيۡكُمُ ٱدۡخُلُواْ ٱلۡجَنَّةَ بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
ambao Malaika watazichukua roho zao, na hali nyoyo zimetakasika na ukafiri. Malaika watawaambia, «Amani iwe juu yenu, Maamkizi yenu peke yenu , na muokoke na kila ovu, ingieni Peponi kwa yale mliyokuwa mkiyafanya ya kumuamini Mwenyezi Mungu na kufuata amri Yake.»
अरबी तफ़सीरें:
هَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن تَأۡتِيَهُمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ أَوۡ يَأۡتِيَ أَمۡرُ رَبِّكَۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ وَمَا ظَلَمَهُمُ ٱللَّهُ وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ
Washirikina hawangojei isipokuwa wajiwe na Malaika wazichukue roho zao wakiwa katika hali ya ukafiri, au ije ya amri ya Mwenyewzi Mungu na adhabu ya haraka ya kuwaangamiza. Na kama walivyokanusha hawa, walikanusha makafiri kabla yao, Mwenyezi Mungu Akawaangamiza. Wala Mwenyezi Mungu Hakuwadhulumu kwa kuwaangamiza na kuwaadhibu, lakini wao ndio waliokuwa wakizidhulumu nafsi zao kwa mambo yaliyowafanya wastahili kuadhibiwa.
अरबी तफ़सीरें:
فَأَصَابَهُمۡ سَيِّـَٔاتُ مَا عَمِلُواْ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ
Basi yaliwateremkia mateso ya madhambi yao ambayo waliyatenda na ikawazingira wao adhabu ambayo walikuwa wakiifanyia shere.
अरबी तफ़सीरें:
وَقَالَ ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْ لَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا عَبَدۡنَا مِن دُونِهِۦ مِن شَيۡءٖ نَّحۡنُ وَلَآ ءَابَآؤُنَا وَلَا حَرَّمۡنَا مِن دُونِهِۦ مِن شَيۡءٖۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ فَهَلۡ عَلَى ٱلرُّسُلِ إِلَّا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ
Na washirikina walisema, «Lau kama Mwenyezi Mungu Alitaka tumuabudu Yeye Peke Yake, hatungalimuabudu yoyote asiyekuwa Yeye, sisi wala baba zetu kabla yetu, wala hatungaliharamisha chochote Asichokiharamisha». Ni hoja kama hizi za kipotofu walizozitumia makafifiri waliopita. Na wao ni warongo, kwani Mwenyezi Mungu Aliwaamrisha na Akawakataza na Akawawezesha kuyasimamia Aliyowakalifisha nayo, na Akawapa nguvu na matakwa yanayotokamana na vitendo vyao. Kwa hivyo, kujenga hoja kwao wakitegemea mapitisho ya Mwenyezi Mungu na makadirio Yake ni ubatilifu mkubwa baada ya kuonywa kwao na Mitume. Na Mitume wenye kuwaonya hawana la zaidi isipokuwa kuufikisha ujumbe ulio wazi waliokalifishwa nao.
अरबी तफ़सीरें:
وَلَقَدۡ بَعَثۡنَا فِي كُلِّ أُمَّةٖ رَّسُولًا أَنِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ وَٱجۡتَنِبُواْ ٱلطَّٰغُوتَۖ فَمِنۡهُم مَّنۡ هَدَى ٱللَّهُ وَمِنۡهُم مَّنۡ حَقَّتۡ عَلَيۡهِ ٱلضَّلَٰلَةُۚ فَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَٱنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُكَذِّبِينَ
Kwa hakika tulipeleka kwa kila ummah uliopita mjumbe wa kuwaamrisha wao kumuabudu Mwenyezi Mungu na kumtii Peke Yake, na kuacha kumuabudu asiyekuwa Yeye miongoni mwa Mashetani, mizimu, wafu na vinginevyo kati ya vile vinavyotegemewa badala ya Mwenyezi Mungu. Basi wakawa miongoni mwao wale ambao Mwenyezi Mungu aliwaongoa wakafuata njia ya Mitume, na kati yao wakapatikana wakaidi waliofuata njia za upotofu, hapo ikapasa kwao upotevu na Mwenyezi Mungu Asiwaafikie. Basi tembeeni katika ardhi na mjionee kwa macho yenu vipi yalivyokuwa marejeo ya hawa wakanushaji na maangamivu yaliyowashukia, mpate kuzingatia?
अरबी तफ़सीरें:
إِن تَحۡرِصۡ عَلَىٰ هُدَىٰهُمۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي مَن يُضِلُّۖ وَمَا لَهُم مِّن نَّٰصِرِينَ
Utakapofanya bidii yako ya mwisho, ewe Mtume, kuwaongoa hawa washirikina, basi jua kwamba Mwenyezi Mungu Hamuongozi Anayepotosha, na hawana wao yoyote asiyekuwa Mwenyezi Mungu atakayewaokoa na kuwazuilia adhabu Yake.
अरबी तफ़सीरें:
وَأَقۡسَمُواْ بِٱللَّهِ جَهۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡ لَا يَبۡعَثُ ٱللَّهُ مَن يَمُوتُۚ بَلَىٰ وَعۡدًا عَلَيۡهِ حَقّٗا وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ
Na hawa washirikina waliapa kwa Mwenyezi Mungu viapo vizito kwamba Mwenyezi Mungu Hatamfufua aliyekufa baada na kumalizika na kutawanyika. Kwani, Atawafufufa Mwenyezi Mungu kwa lazima, hiyo ni ahadi ya kweli Aliyojilazimisha nayo, lakini wengi wa watu hawaujui uweza wa Mwenyezi Mungu wa kufufua, ndio maana wanaukanusha.
अरबी तफ़सीरें:
لِيُبَيِّنَ لَهُمُ ٱلَّذِي يَخۡتَلِفُونَ فِيهِ وَلِيَعۡلَمَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَنَّهُمۡ كَانُواْ كَٰذِبِينَ
Mwenyezi Mungu Atwafufua waja wote, ili awafunulie ukweli wa Ufufuzi ambao wametafautiana juu yake, na ili makafiri wenye kuukanusha wapate kujua kwamba wao wako kwenye ubatilifu na kwamba wao ni warongo pindi walipoapa kwamba hakuna kufufuliwa.
अरबी तफ़सीरें:
إِنَّمَا قَوۡلُنَا لِشَيۡءٍ إِذَآ أَرَدۡنَٰهُ أَن نَّقُولَ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ
Hakika jambo la kufufua ni pesi kwetu. Kwani sisi tutakapo kitu, tunakiambia «Kuwa» ukitahamaki kimeshakuwa na kimeshapatikana.
अरबी तफ़सीरें:
وَٱلَّذِينَ هَاجَرُواْ فِي ٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ مَا ظُلِمُواْ لَنُبَوِّئَنَّهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗۖ وَلَأَجۡرُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَكۡبَرُۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ
Na wale walioacha makao yao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na wakahama baada ya matukio ya kudhulumiwa, tutawakalisha duniani makao mema. Na malipo ya Akhera ni makubwa zaidi, kwani malipo yao huko ni Pepo. Lau wale waliosalia nyuma wakaacha kugura wanayajuwa, ujuzi wa uhakika, yale yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ya malipo na thawabu kwa wale wanaogura katika njia Yake, hangalisalia nyuma yoyote katika wao.
अरबी तफ़सीरें:
ٱلَّذِينَ صَبَرُواْ وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ
Hawa wenye kugura katika njia ya Mwenyezi Mungu ndio waliovumilia juu ya amri ya Mwenyezi Mungu na makatazo Yake na juu ya makadirio Yake yenye uchungu, na kwa Mola wao Peke Yake wanategemea, ndipo wakastahiki cheo hiki kikubwa.
अरबी तफ़सीरें:
وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ إِلَّا رِجَالٗا نُّوحِيٓ إِلَيۡهِمۡۖ فَسۡـَٔلُوٓاْ أَهۡلَ ٱلذِّكۡرِ إِن كُنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ
Na hatukuwatuma kwa waliotangulia kabla yako, ewe Mtume, isipokuwa Mitume miongoni mwa wanaume, sio Malaika, tunaowaletea wahyi. Na iwapo nyinyi, enyi washirikina wa Kikureshi, hamliamini hilo, basi waulizeni waliopewa vitabu vilivyopita, watawapa habari kwamba Manabii walikuwa ni binadamu, mkiwa hamjui kwamba wao ni binadamu. Aya hii inakusanya kila suala kati ya masuala ya Dini, iwapo mtu hana ujuzi nalo amuulize anayelijua miongoni mwa wanavyuoni waliovama katika elimu.
अरबी तफ़सीरें:
بِٱلۡبَيِّنَٰتِ وَٱلزُّبُرِۗ وَأَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ ٱلذِّكۡرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيۡهِمۡ وَلَعَلَّهُمۡ يَتَفَكَّرُونَ
Na tuliwatuma Mitume waliotangulia wakiwa na dalili waziwazi na vitabu vya mbinguni. Na tumekuteremshia wewe, ewe Mtume, Qur’ani upate kuwafunulia watu maana yake na hukumu zake zilizofichika, na ili wapate kuizingatia na waongoke kwayo.
अरबी तफ़सीरें:
أَفَأَمِنَ ٱلَّذِينَ مَكَرُواْ ٱلسَّيِّـَٔاتِ أَن يَخۡسِفَ ٱللَّهُ بِهِمُ ٱلۡأَرۡضَ أَوۡ يَأۡتِيَهُمُ ٱلۡعَذَابُ مِنۡ حَيۡثُ لَا يَشۡعُرُونَ
Je, wanajiaminisha wale makafiri wanaopanga vitimbi kwamba Mwenyezi Mungu Hatawadidimiza ndani ya ardhi kama Alivyomfanya Qarun au kwamba adhabu haitawafikia kutoka mahali wasipopadhania na wasipopatarajia
अरबी तफ़सीरें:
أَوۡ يَأۡخُذَهُمۡ فِي تَقَلُّبِهِمۡ فَمَا هُم بِمُعۡجِزِينَ
au adhabu haitawapata hali wakiwa wanazunguka kwenye safari zao na shughuli zao? Wao si wenye kumtangulia Mwenyezi Mungu wala kumponyoka wala kuokoka na adhabu Yake, kwani Yeye Ndiye Mwenye nguvu Ambaye hakuna chenye kumuelemea.
अरबी तफ़सीरें:
أَوۡ يَأۡخُذَهُمۡ عَلَىٰ تَخَوُّفٖ فَإِنَّ رَبَّكُمۡ لَرَءُوفٞ رَّحِيمٌ
Au Mwenyezi Mungu Awapatilize kwa upungufu wa mali na watu na matunda au katika hali ya kuogopa kwao Asiwatie mkononi. Kwani Mola wenu ni Mpole kwa waja Wake, ni Mwenye huruma kwao.
अरबी तफ़सीरें:
أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ إِلَىٰ مَا خَلَقَ ٱللَّهُ مِن شَيۡءٖ يَتَفَيَّؤُاْ ظِلَٰلُهُۥ عَنِ ٱلۡيَمِينِ وَٱلشَّمَآئِلِ سُجَّدٗا لِّلَّهِ وَهُمۡ دَٰخِرُونَ
Je, kwani makafiri hawa wamekuwa vipofu wakawa hawaangalii vitu venye vivuli Alivyoviumba Mwenyezi Mungu, kama vile majabali na miti ambayo vivuli vyake vinapinduka, mara nyingine upande wa kulia na mara nyingine upande wa kushoto, kufuatia mwendo wa jua kipindi cha mchana na mwendo wa mwezi kipindi cha usiku.Vyote hivyo ni vyenye kuunyenyekea ukuu wa Mwenyezi Mungu na utukufu Wake. Navyo viko chini ya uendeshaji Wake, mipango Yake na utendeshaji nguvu Wake.
अरबी तफ़सीरें:
وَلِلَّهِۤ يَسۡجُدُۤ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ مِن دَآبَّةٖ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَهُمۡ لَا يَسۡتَكۡبِرُونَ
Na vinamsujudia Mwenyezi Mungu Peke Yake vyote vilivyo mbinguni na vilivyo ardhini, miongoni mwa vinavyotambaa. Na Malaika wanamsujudia Mwenyezi Mungu, na wao hawafanyi ujeuri kwa kukataa kumuabudu Yeye. Na Amewahusu Malaika kwa kuwataja baada ya kuwakusanya pamoja na viumbe wengine, kutokana na utukufu wao, ubora wao na wingi wa kuabudu kwao.
अरबी तफ़सीरें:
يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوۡقِهِمۡ وَيَفۡعَلُونَ مَا يُؤۡمَرُونَ۩
Hao Malaika wanamuogopa Mola wao Ambaye Yuko juu yao kwa dhati Yake, utendeshaji nguvu Wake na ukamilifu wa sifa Zake, na wanafanya wanayoamrishwa ya kumtii Mwenyezi Mungu. Katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya kuwa Mwenyezi Mungu Yuko juu ya viumbe vyake vyote, kama inavyonasibiana na utukufu Wake na ukamilifu Wake.
अरबी तफ़सीरें:
۞ وَقَالَ ٱللَّهُ لَا تَتَّخِذُوٓاْ إِلَٰهَيۡنِ ٱثۡنَيۡنِۖ إِنَّمَا هُوَ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞ فَإِيَّٰيَ فَٱرۡهَبُونِ
Na Alisema Mwenyezi Mungu kuwaambia waja Wake, «Msiabudu waungu wawili, kwani muabudiwa wenu ni Mola Mmoja. Basi niogopeni mimi na sio mwingine asiyekuwa mimi.»
अरबी तफ़सीरें:
وَلَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلَهُ ٱلدِّينُ وَاصِبًاۚ أَفَغَيۡرَ ٱللَّهِ تَتَّقُونَ
Na ni vya Mwenyezi Mungu, Peke Yake, vyote vilivyoko mbinguni na ardhini, kwa kuviumba, kuvimiliki na kuviendesha. Na ibada inaelekezwa Kwake PekeYake, na pia kutiiwa na kutakaswa daima. Basi je, inafaa kwenu nyinyi mumuogope asiyekuwa Yeye na mumuabudu?
अरबी तफ़सीरें:
وَمَا بِكُم مِّن نِّعۡمَةٖ فَمِنَ ٱللَّهِۖ ثُمَّ إِذَا مَسَّكُمُ ٱلضُّرُّ فَإِلَيۡهِ تَجۡـَٔرُونَ
Na neema yoyote mliyonayo ya uongofu au afya ya mwili, ukunjufu wa riziki na watoto na yasiyokuwa hayo, inatoka kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake, Yeye Ndiye Mwenye kuwaneemesha nayo. Kisha yanapowapata magonjwa, matatizo na ukame, basi ni kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake mnalia kwa maombi.
अरबी तफ़सीरें:
ثُمَّ إِذَا كَشَفَ ٱلضُّرَّ عَنكُمۡ إِذَا فَرِيقٞ مِّنكُم بِرَبِّهِمۡ يُشۡرِكُونَ
Kisha Anapowaondolea matatizo na magonjwa, kitahamaki linatoka kundi la watu miongoni mwenu wakawa wanawafanya asiyekuwa Yeye kuwa ni washirika pamoja na Yeye na wategemewa.
अरबी तफ़सीरें:
لِيَكۡفُرُواْ بِمَآ ءَاتَيۡنَٰهُمۡۚ فَتَمَتَّعُواْ فَسَوۡفَ تَعۡلَمُونَ
Ili wapate kuzikanusha neema zetu kwao, na miongoni mwazo ni kuondolewa matatizo. Basi jistarehesheni na ulimwengu wenu, nao mwisho wake ni kutoweka, hapo mtajua mwisho wa ukanushaji wenu na uasi wenu.
अरबी तफ़सीरें:
وَيَجۡعَلُونَ لِمَا لَا يَعۡلَمُونَ نَصِيبٗا مِّمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡۗ تَٱللَّهِ لَتُسۡـَٔلُنَّ عَمَّا كُنتُمۡ تَفۡتَرُونَ
Na miongoni mwa uovu wa matendo yao ni kwamba wao wanawatengea masanamu waliowafanya ni waungu, wasiojua chochote na wasionufaisha wala kudhuru, sehemu ya mali zao walizoruzukiwa na Mwenyezi Mungu ili kujisongeza kwao. Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu! Mtaulizwa tena mtaulizwa Siku ya Kiyama kuhusu yale ya urongo ambayo mlikuwa mkimzulia Mwenyezi mungu.
अरबी तफ़सीरें:
وَيَجۡعَلُونَ لِلَّهِ ٱلۡبَنَٰتِ سُبۡحَٰنَهُۥ وَلَهُم مَّا يَشۡتَهُونَ
Na makafiri wanamsingizia Mwenyezi Mungu kuwa ana watoto wa kike na huwa wakisema, «Malaika ni watoto wa kike wa Mwenyezi Mungu». Ameepukana Mwenyezi Mungu na neno lao. Na wanajichukulia wao wenyewe watoto wa kiume wanaowapenda.
अरबी तफ़सीरें:
وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِٱلۡأُنثَىٰ ظَلَّ وَجۡهُهُۥ مُسۡوَدّٗا وَهُوَ كَظِيمٞ
Na pindi anapokuja mwenye kumpasha habari mmoja wao ya kuzaliwa mtoto wa kike, uso wake hapohapo unageuka mweusi, kwa kuyachukia aliyoyasikia, na akajawa na hasira na huzuni.
अरबी तफ़सीरें:
يَتَوَٰرَىٰ مِنَ ٱلۡقَوۡمِ مِن سُوٓءِ مَا بُشِّرَ بِهِۦٓۚ أَيُمۡسِكُهُۥ عَلَىٰ هُونٍ أَمۡ يَدُسُّهُۥ فِي ٱلتُّرَابِۗ أَلَا سَآءَ مَا يَحۡكُمُونَ
Anajificha kwa kuchukia asionekane na watu wake, akiona aibu na kuingiwa na huzuni kwa habari iliyomchukiza ya kuzaliwa mtoto wa kike, huku akiwa ametunduwaa juu ya tukio la mtoto huyo aliyezaliwa: je, amuache kuishi kwenye hali ya unyonge na utwevu au amzike mchangani akiwa hai? Jueni mtanabahi kwamba ni uamuzi mbaya mno wanaouamua ya kuwafanya watoto wa kike ni wa Mwenyezi Mungu na watoto wakiume ni wao.
अरबी तफ़सीरें:
لِلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ مَثَلُ ٱلسَّوۡءِۖ وَلِلَّهِ ٱلۡمَثَلُ ٱلۡأَعۡلَىٰۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ
Wale wasioiamini Akhera na wasiofanya matendo ya kuwafaa huko wana sifa mbaya za ulemevu, uhitaji, ujinga na ukafiri, na Mwenyezi Mungu Ana sifa tukufu za ukamilifu, kujitosheleza na viumbe Vyake. Na Yeye Ndiye Mshindi katika mamlaka Yake, ni Mwenye hekima katika uendeshaji Wake.
अरबी तफ़सीरें:
وَلَوۡ يُؤَاخِذُ ٱللَّهُ ٱلنَّاسَ بِظُلۡمِهِم مَّا تَرَكَ عَلَيۡهَا مِن دَآبَّةٖ وَلَٰكِن يُؤَخِّرُهُمۡ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمّٗىۖ فَإِذَا جَآءَ أَجَلُهُمۡ لَا يَسۡتَـٔۡخِرُونَ سَاعَةٗ وَلَا يَسۡتَقۡدِمُونَ
Lau kwamba Mwenyezi Mungu Anawapatiliza watu kwa ukafiri wao na uzushi wao, Hangalimuacha juu ya ardhi mtu yoyote mwenye kutembea, lakini Anawabakisha mpaka wakati uliopanagwa, nao ni mwisho wa muda wao wa kuishi, basi utakapofika wakati wao wa kuondoka duniani, hawatacheleweshwa nao hata muda mchache wala hawatatangulia.
अरबी तफ़सीरें:
وَيَجۡعَلُونَ لِلَّهِ مَا يَكۡرَهُونَۚ وَتَصِفُ أَلۡسِنَتُهُمُ ٱلۡكَذِبَ أَنَّ لَهُمُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ لَا جَرَمَ أَنَّ لَهُمُ ٱلنَّارَ وَأَنَّهُم مُّفۡرَطُونَ
Na miongoni mwa maovu yao, ni kwamba wao wanawafanya ni wa Mwenyezi Mungu watoto wa kike ambao wao wenyewe wanawachukia. Na ndimi zao zinasema urongo kwamba wao watakuwa na mwisho mwema. Kwa kweli, wao watakuwa na Moto na wao ni wenye kuachwa humo na kusahauliwa.
अरबी तफ़सीरें:
تَٱللَّهِ لَقَدۡ أَرۡسَلۡنَآ إِلَىٰٓ أُمَمٖ مِّن قَبۡلِكَ فَزَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَعۡمَٰلَهُمۡ فَهُوَ وَلِيُّهُمُ ٱلۡيَوۡمَ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ
Naapa kwa Mwenyezi Mungu, hakika tumewapeleka Mitume kwa makundi ya watu kabla yako, ewe Mtume, Shetani akawapambia matendo waliyoyafanya ya ukafiri, ukanushaji na kuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Yeye anasimamia kazi ya kuwapoteza wao ulimwenguuni, na hao wenye kupotezwa, watakuwa na adhabu kali yenye kuumiza kesho akhera.
अरबी तफ़सीरें:
وَمَآ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ إِلَّا لِتُبَيِّنَ لَهُمُ ٱلَّذِي ٱخۡتَلَفُواْ فِيهِ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ
Na hatukukuteremshia Qur’ani, ewe Mtume, isipokuwa ni uwafunulie watu wazi yale ambayo walikuwa wakitafautiana juu yake, ya dini na hukumu, ili hoja zisimame kwao kwa maelezo yako ambayo hayauachii upotofu njia ya kuingia nyoyoni. Na kwa kuwa Qur’ani ni uongofu, haitoi nafasi ya kutunduwaa, nayo ni rehema kwa Waumini katika kufuata kwao uongofu na kujiepusha kwao na upotevu.
अरबी तफ़सीरें:
وَٱللَّهُ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَحۡيَا بِهِ ٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ مَوۡتِهَآۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَسۡمَعُونَ
Na Mwenyezi Mungu Ameteremsha mvua kutoka mawinguni, na Akatoa kwa mvua hiyo mimea kutoka ardhini baada ya kuwa kame na kavu. Hakika katika kuteremsha mvua na kuotesha mimea pana ushahidi juu ya uweza wa Mwenyezi Mungu wa kufufua, na pia pana ushahidi juu ya upweke Wake kwa watu wanaosikia, wanaozingatia, wanaomtii Mwenyezi Mungu na wanaomuogopa.
अरबी तफ़सीरें:
وَإِنَّ لَكُمۡ فِي ٱلۡأَنۡعَٰمِ لَعِبۡرَةٗۖ نُّسۡقِيكُم مِّمَّا فِي بُطُونِهِۦ مِنۢ بَيۡنِ فَرۡثٖ وَدَمٖ لَّبَنًا خَالِصٗا سَآئِغٗا لِّلشَّٰرِبِينَ
Kwa kweli muna nyinyi, enyi watu, mazingatio katika wanyama howa, nao ni ng’ombe, ngamia na mbuzi na kondoo. Kwani mumeshuhudia kwamba sisi tunawanywesha kutoka kwenye nyato zao maziwa yanayotoka kati ya choo, kilicho ndani ya tumbo, na damu yakiwa yamesafishika na kila uchafu, yenye ladha, hayamkeri mwenye kuyanywa.
अरबी तफ़सीरें:
وَمِن ثَمَرَٰتِ ٱلنَّخِيلِ وَٱلۡأَعۡنَٰبِ تَتَّخِذُونَ مِنۡهُ سَكَرٗا وَرِزۡقًا حَسَنًاۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ
Na miongoni mwa neema zetu kwenu ni yale matunda ya mitende na mizabibu mnayoyachukuwa mkayatengeneza pombe yenye kulewesha - na hii na kabla haijaharamishwa- na chakula kizuri. Hakika katika hayo yaliyotajwa pana ushahidi juu ya uweza wa Mwenyezi Mungu kwa watu wenye kuzitia akilini hoja hizo wakazizingatia.
अरबी तफ़सीरें:
وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ إِلَى ٱلنَّحۡلِ أَنِ ٱتَّخِذِي مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتٗا وَمِنَ ٱلشَّجَرِ وَمِمَّا يَعۡرِشُونَ
Na Mola wako, ewe Mtume, Aliwapa nyuki ufunzi kwamba jifanyieni nyumba kwenye majabali, kwenye miti na kwenye nyumba na sakafu zinazojengwa na watu.
अरबी तफ़सीरें:
ثُمَّ كُلِي مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ فَٱسۡلُكِي سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلٗاۚ يَخۡرُجُ مِنۢ بُطُونِهَا شَرَابٞ مُّخۡتَلِفٌ أَلۡوَٰنُهُۥ فِيهِ شِفَآءٞ لِّلنَّاسِۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَتَفَكَّرُونَ
Kisha kuleni katika kila tunda mnalolipenda na mzifuate njia za Mola wenu mlizotayarishiwa ili kutafuta riziki majabalini na kati ya miti. Na Mwenyezi Mungu Amewasahilishia njia hizo, hamupotei katika kurudi hata kama ni mbali. Inatoka kwenye matumbo ya nyuke asali yenye rangi tafauti: nyeupe, manjano, nyekundu na nyiginezo. Na kwenye hiyo asali pana tiba ya magonjwa ya watu. Hakika katika hayo wanayoyafanya nyuki pana ushahidi wenye nguvu juu ya uweza wa Muumba wao kwa watu wanaofikiria na wakazingatia.
अरबी तफ़सीरें:
وَٱللَّهُ خَلَقَكُمۡ ثُمَّ يَتَوَفَّىٰكُمۡۚ وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰٓ أَرۡذَلِ ٱلۡعُمُرِ لِكَيۡ لَا يَعۡلَمَ بَعۡدَ عِلۡمٖ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٞ قَدِيرٞ
Na mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Amewaumba, kisha Atawafisha katika mwisho wa umri wenu. Na kati yenu kuna wale ambao watafikia umri muovu, nao ni ukongwe, kama alivyokuwa uchangani mwake, hajui chochote ambacho alikuwa akikijua. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, ni muweza, ujuzi Wake na uweza wake vimezunguka kila kitu. Mwenyezi Mungu Aliyemrudisha mwanadamu kwenye hali hii ni muweza wa kumfisha kisha kumfufua.
अरबी तफ़सीरें:
وَٱللَّهُ فَضَّلَ بَعۡضَكُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ فِي ٱلرِّزۡقِۚ فَمَا ٱلَّذِينَ فُضِّلُواْ بِرَآدِّي رِزۡقِهِمۡ عَلَىٰ مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُهُمۡ فَهُمۡ فِيهِ سَوَآءٌۚ أَفَبِنِعۡمَةِ ٱللَّهِ يَجۡحَدُونَ
Mwenyezi Mungu Amewafanya bora baadhi yenu kuliko wengine katika riziki Aliyowapa ulimwenguni: katika nyinyi kuna tajiri na katika nyinyi kuna masikini, katika nyinyi kuna anayemiliki na katika nyinyi kuna anayemilikiwa, wenye kumiliki hawawapi wenye kuwamilikiwa kile Alichowapa Mwenyezi Mungu cha kuwafanya wawe na kiwango cha mali sawa na wao. Basi iwapo hawaliridhii hilo kwenye nafsi zao, ni kwa nini wanaridhika kumfanya Mwenyezi Mungu kuwa Ana washirika miongoni mwa watumwa Wake? Kwa kweli huu ni udhalimu mkubwa kabisa na ukanushaji mkubwa kabisa wa neema za Mwenyezi mungu.
अरबी तफ़सीरें:
وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ أَزۡوَٰجٗا وَجَعَلَ لَكُم مِّنۡ أَزۡوَٰجِكُم بَنِينَ وَحَفَدَةٗ وَرَزَقَكُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَٰتِۚ أَفَبِٱلۡبَٰطِلِ يُؤۡمِنُونَ وَبِنِعۡمَتِ ٱللَّهِ هُمۡ يَكۡفُرُونَ
Na Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Amewaumba wake kutokana na na nyinyi ili nafsi zenu ziliwazike na wao, na amewapa kutokana nao watoto, na kutokana na kizazi chao wajukuu, na Amewaruzuku vyakula vizuri miongoni mwa matunda, nafaka, nyama na visivyokuwa hivyo. Je, kwani wanauamini upotofu wa uungu wa washirika wao na wanazikanusha neema za Mwenyezi Mungu zisizohesabika na hawamshukuru kwa kumpwekesha Yeye Peke Yake, Aliyetukuka na kuwa juu, kwa ibada?
अरबी तफ़सीरें:
وَيَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَمۡلِكُ لَهُمۡ رِزۡقٗا مِّنَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ شَيۡـٔٗا وَلَا يَسۡتَطِيعُونَ
Na washirikina wanaabudu masanamu ambayo hayana mamlaka ya kuwapa riziki itokayo mbinguni kama mvua wala itokayo ardhini kama mazao. Wao hawamiliki kitu chochote wala hapana uezekano wowote kwa wao kukimiliki, kwani wao hawawezi.
अरबी तफ़सीरें:
فَلَا تَضۡرِبُواْ لِلَّهِ ٱلۡأَمۡثَالَۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ وَأَنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ
Na mjuapo kwamba masanamu na mizimu havinufaishi, basi msimfanye Mwenyezi Mungu Ana ambao ni kama Yeye wenye kufanana na Yeye miongoni mwa viumbe Wake mkawa mnawashirikisha wao pamoja na Yeye katika ibada. Hakika Mwenyezi Mungu Anayajua mnayoyafanya, na nyinyi mumeghafilika hamjui makosa yenu na ubaya wa mwisho wenu.
अरबी तफ़सीरें:
۞ ضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا عَبۡدٗا مَّمۡلُوكٗا لَّا يَقۡدِرُ عَلَىٰ شَيۡءٖ وَمَن رَّزَقۡنَٰهُ مِنَّا رِزۡقًا حَسَنٗا فَهُوَ يُنفِقُ مِنۡهُ سِرّٗا وَجَهۡرًاۖ هَلۡ يَسۡتَوُۥنَۚ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ
Na Mwenyezi Mungu Amepiga mfano, Akafafanua kwa mfano huo ubatilifu wa itikadi ya washirikina. Mfano wenyewe ni wa mtu aliyemilikiwa asiyeweza kujipitishia jambo asiyemiliki chochote, na mtu mwingine aliye huru, mwenye mali ya halali ambayo Mwenyezi Mungu Amemruzuku, anayemiliki kupitisha atakalo katika mali hayo, akawa anapeana kwa siri na kwa dhahiri. Je, kuna yoyote mwenye akili atakayesema kwamba watu wawili hawa wako sawa? Hivyo ndivyo Alivyo Mwenyezi Mungu Anayemiliki na Anayepitisha. Yeye Hafanani na viumbe Vyake na watumwa wake. Basi vipi mtasawazisha baina yao? Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Peke Yake. Yeye Ndiye Anayestahiki kushukuriwa na kusifiwa. Lakini wengi wa washirikina hawajui kwamba sifa njema na neema ni za Mwenyezi mungu na kwamba Yeye, Peke Yake, Ndiye Anayestahiki kuabudiwa.
अरबी तफ़सीरें:
وَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلٗا رَّجُلَيۡنِ أَحَدُهُمَآ أَبۡكَمُ لَا يَقۡدِرُ عَلَىٰ شَيۡءٖ وَهُوَ كَلٌّ عَلَىٰ مَوۡلَىٰهُ أَيۡنَمَا يُوَجِّههُّ لَا يَأۡتِ بِخَيۡرٍ هَلۡ يَسۡتَوِي هُوَ وَمَن يَأۡمُرُ بِٱلۡعَدۡلِ وَهُوَ عَلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ
Na Mwenyezi Mungu Amepiga mfano mwingine wa ubatilifu wa ushirikina. Mfano wenyewe ni wa watu wawili, mmoja wao ni bubu kiziwi, haelewi wala haelezi, hawezi kujinufaisha yeye mwenyewe wala wengine, naye ni mzigo mzito kwa anyesimamia mambo yake na kumwangalia kwa mahitaji yake, akimtuma kwa jambo lolote alitekeleze hafaulu wala hamletei jambo lolote zuri. Na mtu mwengine ana hisia zilizo sawa, anajinufaisha yeye na wengine, anaamuru utunzaji wa haki, na yeye yuko kwenye njia iliyo wazi isiyopotoka. Je, watu wawili hawa wanalingana katika maoni ya wenye akili? Basi vipi mtasawazisha baina ya sanamu kiziwi na Mwenyezi Mungu Muweza Mwenye kuneemesha kila zuri ?
अरबी तफ़सीरें:
وَلِلَّهِ غَيۡبُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَمَآ أَمۡرُ ٱلسَّاعَةِ إِلَّا كَلَمۡحِ ٱلۡبَصَرِ أَوۡ هُوَ أَقۡرَبُۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ
Ni wa Mwenyezi Mungu, Aliyetakata na kutukuka, ujuzi wa mambo yasiyoonekana ya mbinguni na ardhini. Na jambo la Kiyama halikuwa, kwa uharaka wa kuja kwake, isipokuwa ni kama mtazamo wa haraka wa jicho au ni haraka zaidi kuliko huo. Hakika Mwenyezi Mungu kwa kila jambo ni Muweza.
अरबी तफ़सीरें:
وَٱللَّهُ أَخۡرَجَكُم مِّنۢ بُطُونِ أُمَّهَٰتِكُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ شَيۡـٔٗا وَجَعَلَ لَكُمُ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡأَبۡصَٰرَ وَٱلۡأَفۡـِٔدَةَ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ
Na Mwenyezi Mungu , Aliyetakata na kutukuka, Amewatoa nyinyi kutoka kwenye matumbo ya mama zenu baada ya kipindi cha mimba, hali hamtambui chochote kilichoko pambizoni mwenu, na akawapatia sababu za kutambua miongoni mwa mashikio ya kusikia na macho ya kuonea na nyoyo, huenda nyiyi mkamshukuru Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa neema hizo na mukampwekesha, Aliyeshinda na kutukuka, kwa ibada.
अरबी तफ़सीरें:
أَلَمۡ يَرَوۡاْ إِلَى ٱلطَّيۡرِ مُسَخَّرَٰتٖ فِي جَوِّ ٱلسَّمَآءِ مَا يُمۡسِكُهُنَّ إِلَّا ٱللَّهُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ
Je, hawakutazama washirikina kuwaangalia ndege walivyoendeshwa na kuwezeshwa kuruka angani, baina ya mbingu na ardhi, kwa amri ya Mwenyezi Mungu? Hakuna anaowazuia wasianguke isipokuwa Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, kwa kuwa amewaumbia mbawa na mikia na Akawawezesha kuruka. Hakika katika huko kuendeshwa na kuzuiliwa kuna alama za ushahidi kwa wale wanaoziamini dalili za uweza wa Mwenyezi Mungu
अरबी तफ़सीरें:
وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّنۢ بُيُوتِكُمۡ سَكَنٗا وَجَعَلَ لَكُم مِّن جُلُودِ ٱلۡأَنۡعَٰمِ بُيُوتٗا تَسۡتَخِفُّونَهَا يَوۡمَ ظَعۡنِكُمۡ وَيَوۡمَ إِقَامَتِكُمۡ وَمِنۡ أَصۡوَافِهَا وَأَوۡبَارِهَا وَأَشۡعَارِهَآ أَثَٰثٗا وَمَتَٰعًا إِلَىٰ حِينٖ
Mwenyezi Mungu, Aliyetakata na sifa za upungufu, Amewapatia nyinyi mapumziko na utulivu kwenye nyumba zenu pamoja na watu wenu mkiwa mijini, na Amewapatia nyinyi mahema na mindule ya ngozi za wanyama- howa, ambayo ni sahali kwenu mkiwa safarini, na ambayo ni sahali kwenu kuisimamisha pale mkaapo baada ya safari, na Amewapatia nyinyi kutokana na manyoya ya kondoo, manywele ya ngamia na nwyele za mbuzi vyombo vya matumizi yenu ya kuvaa, kujifinika, kutandika na pambo la nyinyi kujifurahisha kwalo mpaka kipindi kilichotajwa na wakati ujulikanao.
अरबी तफ़सीरें:
وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّمَّا خَلَقَ ظِلَٰلٗا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ ٱلۡجِبَالِ أَكۡنَٰنٗا وَجَعَلَ لَكُمۡ سَرَٰبِيلَ تَقِيكُمُ ٱلۡحَرَّ وَسَرَٰبِيلَ تَقِيكُم بَأۡسَكُمۡۚ كَذَٰلِكَ يُتِمُّ نِعۡمَتَهُۥ عَلَيۡكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تُسۡلِمُونَ
Na Mwenyezi Mungu Amewaptia miti na vinginevyo vya kuwaletea vivuli, na amewafanyia kwenye majabali na pango sehemu za kuhamia mnapohitajia, na Amewafanyia nguo kutokana na pamba na sufi na vinginevyo za kuwahifadhi na joto na baridi, na Amewaumbia chuma cha nyinyi kujikinga na silaha za kudunga za maadui wenu na madhara yao katika vita vyenu na wao. Kama vile Alivyowaneemesha kwa neema hizi, atawakamilishia neema Zake kwenu kwa kuwafafanulia wazi Dini ya haki, ili mjisalimishe kwa amri ya Mwenyezi Mungu, Peke Yake, na msimshirikishe na kitu chochote katika ibada Yake.
अरबी तफ़सीरें:
فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَإِنَّمَا عَلَيۡكَ ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ
Wakikupa mgongo, ewe Mtume, baada ya kuziona hizi aya, basi usisikitike. Kwani jukumu lako ni kuufikisha ujumbe uliotumwa nao waziwazi, ama kuongoa ni kwetu sisi.
अरबी तफ़सीरें:
يَعۡرِفُونَ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ ثُمَّ يُنكِرُونَهَا وَأَكۡثَرُهُمُ ٱلۡكَٰفِرُونَ
Washirikina hawa wazijua neema za Mwenyezi Mungu juu yao za kutumilizwa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwao, kisha wanaukanusha utume wake. Na wengi wa watu wake ni wale wanaoukanusha utume wake na sio wanaoukubali.
अरबी तफ़सीरें:
وَيَوۡمَ نَبۡعَثُ مِن كُلِّ أُمَّةٖ شَهِيدٗا ثُمَّ لَا يُؤۡذَنُ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ وَلَا هُمۡ يُسۡتَعۡتَبُونَ
Na wakumbushe, ewe Mtume, yale yatakayokuwa Siku ya Kiyama, tutakapowaletea kila kundi la watu Mtume wao akitolea ushahidi Imani ya walioamini miongoni mwao na ukanushaji wa wenye kukanusha. Kisha hao waliokanusha hawatapewa nafasi ya kuomba msamaha kwa waliyoyafanya, na hawatatakiwa kumridhisha Mola wao kwa kutubia na kufanya matendo mema, kwani wakati wa hilo ushapita.
अरबी तफ़सीरें:
وَإِذَا رَءَا ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ ٱلۡعَذَابَ فَلَا يُخَفَّفُ عَنۡهُمۡ وَلَا هُمۡ يُنظَرُونَ
Na wale waliokanusha watakapoishuhudia adhabu ya Mwenyezi huko Akhera, basi hawatapunguziwa chochote katika hiyo adhabu, hawatapewa muhula wala hawatacheleweshwa.
अरबी तफ़सीरें:
وَإِذَا رَءَا ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْ شُرَكَآءَهُمۡ قَالُواْ رَبَّنَا هَٰٓؤُلَآءِ شُرَكَآؤُنَا ٱلَّذِينَ كُنَّا نَدۡعُواْ مِن دُونِكَۖ فَأَلۡقَوۡاْ إِلَيۡهِمُ ٱلۡقَوۡلَ إِنَّكُمۡ لَكَٰذِبُونَ
Na wale waliokanusha watakapowaona Siku ya Kiyama waungu wao waliokuwa wakiwaabudu pamoja na MwenyeziMungu watasema, «Mola wetu! Hawa ndio washirika wetu tuliokuwa tukiwaabudu badala yako.» Hapo waungu hao watatamka kuwakanusha wale waliowaabudu na watasema, «Hakika nyinyi, enyi washirikina, ni warongo, mlipotufanya sisi ni washirika wa Mwenyezi Mungu na mkatuabudu pamoja na Yeye. Sisi hatukuwaamuru hilo, wala hatukudai kwamba sisi tunastahiki uungu, lawama ni juu yenu.»
अरबी तफ़सीरें:
وَأَلۡقَوۡاْ إِلَى ٱللَّهِ يَوۡمَئِذٍ ٱلسَّلَمَۖ وَضَلَّ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ
Na hiyo Siku ya Kiyama, washirikina wataonyesha kusalimu amri na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, na yatawapotea yale ya urongo waliokuwa wakiyazua na kwamba waungu wao watawaombea.
अरबी तफ़सीरें:
ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ زِدۡنَٰهُمۡ عَذَابٗا فَوۡقَ ٱلۡعَذَابِ بِمَا كَانُواْ يُفۡسِدُونَ
Wale ambao waliukanusha upweke wa Mwenyezi Mungu na unabii wako, ewe mtume, na wakakukanusha wewe, wakawakataza wengine wasimuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, tutawazidishia adhabu juu ya ukanushaji wao na adhabu juu ya kuwazuia watu kuifuata haki. Na hili ni kwa sababu ya kukusudia kwao kufanya uharibifu na kuwapoteza waja kwa ukafiri na uasi.
अरबी तफ़सीरें:
وَيَوۡمَ نَبۡعَثُ فِي كُلِّ أُمَّةٖ شَهِيدًا عَلَيۡهِم مِّنۡ أَنفُسِهِمۡۖ وَجِئۡنَا بِكَ شَهِيدًا عَلَىٰ هَٰٓؤُلَآءِۚ وَنَزَّلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ تِبۡيَٰنٗا لِّكُلِّ شَيۡءٖ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُسۡلِمِينَ
Na kumbuka, ewe Mtume, pindi tutakapomleta, Siku ya Kiyama, katika kila ummah miongoni mwa ummah zote, shahidi juu yao: naye ni Mtume ambaye Mwenyezi Mungu Alimpeleka kwao anayetokana na wao wenyewe na kwa lugha yao, na tukakuleta wewe, ewe Mtume, ukiwa ni shahidi juu ya ummah wako. Na kwa kweli, tumekuteremshia Qur’ani ikiwa na ufafanuzi wa kila jambo linalohitajia maelezo, kama hukumu za halali na haramu, malipo mema na mateso na yasiyokuwa hayo, na ili iwe ni uongofu wenye kutoa kwenye upotevu, na ni rehema kwa atakayeiamini na kuifuata kivitendo, na iwe ni bishara njema kwa Waumini kwamba watakuwa na mwisho mwema.
अरबी तफ़सीरें:
۞ إِنَّ ٱللَّهَ يَأۡمُرُ بِٱلۡعَدۡلِ وَٱلۡإِحۡسَٰنِ وَإِيتَآيِٕ ذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَيَنۡهَىٰ عَنِ ٱلۡفَحۡشَآءِ وَٱلۡمُنكَرِ وَٱلۡبَغۡيِۚ يَعِظُكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ
Hakika Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Anawaamrisha waja Wake ndani ya Qur’ani hii wawe waadilifu, wafanye usawa katika kutunza haki Yake, kwa kumpwekesha Yeye na kutomshirikisha, na haki ya waja Wake, kwa kumpa haki yake kila mwenye haki. Na Anaamrisha kufanya wema katika kutekeleza haki Yake, kwa kumuabudu na kutekeleza faradhi Zake kwa namna ilivyopasishwa na Sheria, na kuwafanyia wema viumbe Wake katika maneno na vitendo. Na Anaamrisha kuwapa walio na ukaribu wa ujamaa kitu cha kuwaunga na kuwatendea wema. Na Anakataza kila ambalo ni ovu, likiwa ni neno au ni tendo, na ambalo Sheria inalipinga na haikubaliani nalo la ukafiri na maasia, na kuwadhulumu watu na kuwafanyia maonevu. Na Mwenyezi Mungu, kwa maamrisho haya na makatazo haya, Anawaidhia na kuwakumbusha mwisho mbaya, ili mzikumbuke amri za Mweneyzi Mungu na mnufaike nazo.
अरबी तफ़सीरें:
وَأَوۡفُواْ بِعَهۡدِ ٱللَّهِ إِذَا عَٰهَدتُّمۡ وَلَا تَنقُضُواْ ٱلۡأَيۡمَٰنَ بَعۡدَ تَوۡكِيدِهَا وَقَدۡ جَعَلۡتُمُ ٱللَّهَ عَلَيۡكُمۡ كَفِيلًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا تَفۡعَلُونَ
Na jilazimisheni kutekeleza kila ahadi mliyojilazimisha nayo juu ya nafsi zenu, baina yenu nyinyi na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, au baina yenu na watu katika yale yasiyoenda kinyume na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Nabii Wake. Wala msirudi nyuma kwenye viapo mlivyovitilia mkazo, na hali mlimfanya Mwenyezi Mungu Ndiye mdhamini na msimamizi mlipomuahidi. Hakika Mwenyezi Mungu Anayajua mnayoyafanya na Atawalipa kwayo.
अरबी तफ़सीरें:
وَلَا تَكُونُواْ كَٱلَّتِي نَقَضَتۡ غَزۡلَهَا مِنۢ بَعۡدِ قُوَّةٍ أَنكَٰثٗا تَتَّخِذُونَ أَيۡمَٰنَكُمۡ دَخَلَۢا بَيۡنَكُمۡ أَن تَكُونَ أُمَّةٌ هِيَ أَرۡبَىٰ مِنۡ أُمَّةٍۚ إِنَّمَا يَبۡلُوكُمُ ٱللَّهُ بِهِۦۚ وَلَيُبَيِّنَنَّ لَكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ مَا كُنتُمۡ فِيهِ تَخۡتَلِفُونَ
Wala msirudi nyuma kwenye ahadi zenu, ukawa mfano wenu ni kama wa mwanamke aliyefuma mfumo akautengeneza vizuri kisha akaufumua, Mnavifanya viapo vyenu mlivyoviapa wakati wa makubaliano kuwa ni udanganyifu kwa mliyopatana naye, mkawa mnazivunja ahadi zenu mnapopata kundi la watu wenye mali kuliko wale mlioahidiana nao. Kwa hakika, Mwenyezi Mungu Anawapa mtihani kwa kuwaamrisha nyinyi mtekeleze ahadi na kuwakataza nyinyi msizivunje. Na ili Apate kuwaeleza, Siku ya Kiyama, yale ambayo mlikuwa mkitafautiana kwayo kuhusu kumuamini Mwenyezi Mungu na kuuamini unabii wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie.
अरबी तफ़सीरें:
وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَعَلَكُمۡ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ وَلَٰكِن يُضِلُّ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُۚ وَلَتُسۡـَٔلُنَّ عَمَّا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Na lau Mwenyezi Mungu angalitaka angaliwaafikia nyote Akawafanya muwe kwenye muelekeo mmoja, nao ni Uislamu na Imani, na Angaliwalazimisha nao. Lakini Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Anampoteza Anayemtaka, kati ya wale ambao Yeye Alijua kuwa walichagua upotevu, Asimuongoze kwa uadilifu Wake. Na Anamuongoza Anayemtaka, kati ya wale ambao Yeye Alijua kuwa wao walichagua haki, Akampa muelekeo kwa wema Wake. Na Mwenyezi Mungu Atawauliza nyinyi nyote, Siku ya Kiyama, yale ambayo mlikuwa mkiyafanya ulimwenguni kati ya yale Aliyowaamrisha nayo na Aliyowakataza, na Atawalipa nyinyi kwa hayo.
अरबी तफ़सीरें:
وَلَا تَتَّخِذُوٓاْ أَيۡمَٰنَكُمۡ دَخَلَۢا بَيۡنَكُمۡ فَتَزِلَّ قَدَمُۢ بَعۡدَ ثُبُوتِهَا وَتَذُوقُواْ ٱلسُّوٓءَ بِمَا صَدَدتُّمۡ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَكُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٞ
Wala msifanye , kati ya viapo mnavyoviapa, udanganyifu kwa wale mliowaapia, mkaja kuangamia baada ya kuwa kwenye amani. Ni kama yule ambaye nyayo zake ziliteleza baada ya kuwa zimekita. Na mtaonja adhabu ya kuwaudhi ulimwenguni kwa vile mlisababisha kuwakataza wengine na Dini hii kwa ukiukaji ahadi waliouona kutoka kwenu, na huko Akhera mtapata adhabu kubwa.
अरबी तफ़सीरें:
وَلَا تَشۡتَرُواْ بِعَهۡدِ ٱللَّهِ ثَمَنٗا قَلِيلًاۚ إِنَّمَا عِندَ ٱللَّهِ هُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ
Na wala msivunje ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa kuchukua badala yake kitu kidogo cha starehe ya duniani. Hakika malipo mema yaliyoko kwa Mweneyzi Mungu ya utekelezaji ahadi ni bora kwenu kuliko thamani hii ndogo. Basi iwapo nyinyi ni watu mnaojua, zingatieni tafauti iliyopo baina ya mazuri mawili haya: ya ulimwenguni na ya Akhera.
अरबी तफ़सीरें:
مَا عِندَكُمۡ يَنفَدُ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ بَاقٖۗ وَلَنَجۡزِيَنَّ ٱلَّذِينَ صَبَرُوٓاْ أَجۡرَهُم بِأَحۡسَنِ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Hayo mliyonayo, miongoni mwa taka za kilimwengu, yataondoka na yale yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu, ya riziki na thawabu, hayataondoka. Na wale waliohimili kubeba mazito ya Sheria waliyotakiwa wayabebe, miongoni mwayo ikiwa ni utekelezaji ahadi, tutawalipa malipo mazuri zaidi ya matendo yao mema: tutawapa zaidi kwa matendo yao madogo kama tutakavyowapa zaidi kwa matendo yao makubwa kwa ukarimu wetu.
अरबी तफ़सीरें:
مَنۡ عَمِلَ صَٰلِحٗا مِّن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَلَنُحۡيِيَنَّهُۥ حَيَوٰةٗ طَيِّبَةٗۖ وَلَنَجۡزِيَنَّهُمۡ أَجۡرَهُم بِأَحۡسَنِ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Mwenye kufanya tendo zuri, akiwa ni mwanamume au ni mwanake, na huku ni mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake , basi tutampa maisha mema yenye utulivu duniani hata kama ni mchache wa mali, na tutawalipa huko Akhera thawabu zao kwa uzuri zaidi ya walivyofanya duniani.
अरबी तफ़सीरें:
فَإِذَا قَرَأۡتَ ٱلۡقُرۡءَانَ فَٱسۡتَعِذۡ بِٱللَّهِ مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ ٱلرَّجِيمِ
Na pindi ukitaka, ewe Muumini, kusoma chochote katika Qur’ani, basi jilinde kwa Mwenyezi Mungu na Shari la Shetani aliyefukuzwa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu kwa kusema, «A'ūdhu bi- Llāhi min ash-Shayttān ar-Rajīm»(Najilinda kwa Mwenyezi Mungu na Shetani Aliyefukuzwa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu).
अरबी तफ़सीरें:
إِنَّهُۥ لَيۡسَ لَهُۥ سُلۡطَٰنٌ عَلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ
Kwa hakika, Shetani hana uwezo wa kuwasaliti wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wanaomtegemea Mola wao.
अरबी तफ़सीरें:
إِنَّمَا سُلۡطَٰنُهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ يَتَوَلَّوۡنَهُۥ وَٱلَّذِينَ هُم بِهِۦ مُشۡرِكُونَ
Uwaezo wake wa kusaliti ni juu ya wale waliomfanya yeye ni msaidizi wao na wakamtii na wale ambao wao, kwa sababu ya kumtii yeye, wanamshirikisha Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.
अरबी तफ़सीरें:
وَإِذَا بَدَّلۡنَآ ءَايَةٗ مَّكَانَ ءَايَةٖ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا يُنَزِّلُ قَالُوٓاْ إِنَّمَآ أَنتَ مُفۡتَرِۭۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ
Na tunapoibadilisha aya kwa aya nyingine, na Mwenyezi Mungu Mwenye kuumba ni Anayajua zaidi maslahi ya viumbe Wake kwa hukumu Anazoziteremsha katika nyakati mbalimabali, makafiri wanasema, «Hakika yako wewe, Ewe Muhammad, ni mrongo mwenye kumzulia Mwenyezi Mungu Asiyoyasema.» Na Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amni zimshukiye, si kama wanavyodai. Lakini wengi wao hawana ujuzi juu ya Mola wao wala kuhusu Sheria Yake na hukumu Zake.
अरबी तफ़सीरें:
قُلۡ نَزَّلَهُۥ رُوحُ ٱلۡقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِٱلۡحَقِّ لِيُثَبِّتَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَهُدٗى وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُسۡلِمِينَ
Waambie, ewe Mtume, Qurani haikuzuliwa na mimi, bali aliyeiteremsha ni Jibrili kutoka kwa Mola wako kwa ukweli na uadilifu ili kuwafanya Waumini wawe imara, kuwaongoza wao kutoka kwenye upotevu , na kuwapa bishara njema wale waliojisalimisha na kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu, Bwana wa viumbe wote.
अरबी तफ़सीरें:
وَلَقَدۡ نَعۡلَمُ أَنَّهُمۡ يَقُولُونَ إِنَّمَا يُعَلِّمُهُۥ بَشَرٞۗ لِّسَانُ ٱلَّذِي يُلۡحِدُونَ إِلَيۡهِ أَعۡجَمِيّٞ وَهَٰذَا لِسَانٌ عَرَبِيّٞ مُّبِينٌ
Na kwa hakika tunajua kuwa washirikina wanasema kwamba Nabii anapokea Qur’ani kutoka kwa kiumbe miongoni mwa wanadamu. Wamesema urongo! Kwani ulimi wa yule waliomsingizia kuwa amemfundisha Nabii, rehema na amani zimshukie, si wa Kiarabu usiyotasua, na hii Qur’ani ni kwa lugha ya Kiarabu, imefikia upeo wa ufafanuzi na ubainifu.
अरबी तफ़सीरें:
إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ لَا يَهۡدِيهِمُ ٱللَّهُ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Hakika hao makafiri wasioiamini Qur’ani, Mwenyezi Mungu Hatawaelekeza kuipata haki, na Siku ya Akhera watakuwa na adhabu kali iumizayo.
अरबी तफ़सीरें:
إِنَّمَا يَفۡتَرِي ٱلۡكَذِبَ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَٰذِبُونَ
Kwa hakika wanaozua urongo ni wale wasiomuamini Mwenyezi Mungu na aya Zake, na wao ndio warongo kwa neno lao hilo. Ama Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, anayemuamini Mola wake na kumnyenyekea, haiwezekani kwake yeye kumkanusha Mwenyezi Mungu na kumsingizia Asiyoyasema.
अरबी तफ़सीरें:
مَن كَفَرَ بِٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ إِيمَٰنِهِۦٓ إِلَّا مَنۡ أُكۡرِهَ وَقَلۡبُهُۥ مُطۡمَئِنُّۢ بِٱلۡإِيمَٰنِ وَلَٰكِن مَّن شَرَحَ بِٱلۡكُفۡرِ صَدۡرٗا فَعَلَيۡهِمۡ غَضَبٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَلَهُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٞ
Hakika wanaozua urongo ni wanaotamka neno la ukafiri na akaritadi baada ya kuamini. Hao itawashukia wao hasira kutoka kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa yule aliyelazimishwa kutamaka maneno ya ukafiri na akayatamka kwa kuchelea kuangamia, hali moyo wake umejikita kwenye Imani, basi huyo hana lawama. Lakini mwenye kutamka ukafiri na moyo wake ukatulia juu yake, hao watashukiwa na hasira kali kutoka kwa Mwenyezi Munngu na watapata adhabu kubwa.
अरबी तफ़सीरें:
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ ٱسۡتَحَبُّواْ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا عَلَى ٱلۡأٓخِرَةِ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Hiyo ni kwa sababu ya kuchagua kwao dunia na pambo lake na kuifanya kwao hiyo dunia kuwa ni bora kuliko Akhera na malipo yake na kwamba Mwenyezi Mungu Hawaongozi makafiri wala hawaelekezi kwenye haki na usawa.
अरबी तफ़सीरें:
أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ طَبَعَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ وَسَمۡعِهِمۡ وَأَبۡصَٰرِهِمۡۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡغَٰفِلُونَ
Hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu Amewapiga muhuri nyoyo zao kwa ukafiri na ufadhilishaji dunia juu ya Akhera, hazitafikiwa na nuru ya uongofu, na Amewafanya viziwi masikio yao kutozisikia aya za Mwenyezi Mungu , kusikia kwa kuzingatia, na Amewafanya vipofu macho yao wasizione hoja zinazojulisha uungu wa Mwenyezi Mungu , na hao ndio wenye kughafilika na ile adhabu Aliyowaandalia Mwenyezi Mungu.
अरबी तफ़सीरें:
لَا جَرَمَ أَنَّهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ
Ni kweli kabisa kwamba wao, huko Akhera, ndio wenye hasara wenye kuangamia, waliotumia maisha yao kwa mambo yaliyopelekea kuadhibiwa na kuangamizwa.
अरबी तफ़सीरें:
ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ هَاجَرُواْ مِنۢ بَعۡدِ مَا فُتِنُواْ ثُمَّ جَٰهَدُواْ وَصَبَرُوٓاْ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعۡدِهَا لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ
Kisha Mola wako, kwa wale waliofanywa wanyonge ndani ya Makkah na wakaadhibiwa na washirikina mpaka wakakubali matendo yao kijuujuu, wakawafitini kwa kutamka yanayowaridhi, na hali nyoyo zao zimetulia katika Imani, na ilipowezekana kwao kujiokoa waligura kwenda Madina kisha wakapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na wakavumilia mashaka ya majukumu, hakika Mola wako , baada ya kutubia kwao ni Mwenye kuwasamehe , ni Mwenye kuwarehemu.
अरबी तफ़सीरें:
۞ يَوۡمَ تَأۡتِي كُلُّ نَفۡسٖ تُجَٰدِلُ عَن نَّفۡسِهَا وَتُوَفَّىٰ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا عَمِلَتۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ
Na wakumbushe wao, ewe Mtume, Siku ya Kiyama pindi itakapokuja kila nafsi ikijitetea yenyewe na kutoa nyudhuru za kila aina, na hapo Mwenyezi Mungu Ailipe kila nafsi malipo ya ilichokifanya bila ya kuidhulumu. Hatawaongezea mateso wala hawatapunguzia malipo yao.
अरबी तफ़सीरें:
وَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلٗا قَرۡيَةٗ كَانَتۡ ءَامِنَةٗ مُّطۡمَئِنَّةٗ يَأۡتِيهَا رِزۡقُهَا رَغَدٗا مِّن كُلِّ مَكَانٖ فَكَفَرَتۡ بِأَنۡعُمِ ٱللَّهِ فَأَذَٰقَهَا ٱللَّهُ لِبَاسَ ٱلۡجُوعِ وَٱلۡخَوۡفِ بِمَا كَانُواْ يَصۡنَعُونَ
Na Mwenyezi Mungu Amepiga mfano wa mji wa Makkh. Ulikuwa uko kwenye salama ya kutofanyiwa uadui, utulivu kutokana na dhiki za maisha na unajiliwa na riziki zake kwa uzuri na usahali kutoka kila upande, wakazi wake wakazikanusha neema za Mwenyezi Mungu kwao, wakamshirikisha na wasimshukuru, hapo Mwenyezi Mungu Akawatesa kwa njaa na kicho kwa kuviogopa vikosi vya Mtume, reheme ya Mwenyezi Mungu na amni zimshukiye, na majeshi yake yaliyokuwa yakiwatisha, na hili ni kwa sababu ya ukafiri wao na vitendo vyao vya ubatilifu.
अरबी तफ़सीरें:
وَلَقَدۡ جَآءَهُمۡ رَسُولٞ مِّنۡهُمۡ فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمُ ٱلۡعَذَابُ وَهُمۡ ظَٰلِمُونَ
Hakika Mwenyezi Mungu Alipeleka kwa watu wa Makkah Mtume miongoni mwao, yeye ni Nabii Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wanaijua nasaba yake, ukweli wake na uaminifu wake, wasiyakubali yale aliyowajia nayo na wasimuamini. Hapo iliwapata adhabu ya shida, njaa, kicho na kuuawa wakuu wao huko Badr na hali wao ni madhalimu wa nafsi zao kwa kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kuwazuia watu njia Yake.
अरबी तफ़सीरें:
فَكُلُواْ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ حَلَٰلٗا طَيِّبٗا وَٱشۡكُرُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ إِيَّاهُ تَعۡبُدُونَ
Basi kuleni, enyi Waumini, miongoni mwa vile ambavyo Mwenyezi Mungu Amewaruzuku na Akavifanya ni halali nzuri kwenu. Na shukuruni neema za Mwenyezi Mungu kwenu, kwa kuzitambua na kuzitumia katika kumtii Mwenyezi Mungu, iwapo nyinyi, kikweli, ni wenye kuandama amri Yake, ni wenye kusikia na kumtii Yeye, mnamuabudu Yeye Peke Yake, Asiye na mshirika.
अरबी तफ़सीरें:
إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَيۡتَةَ وَٱلدَّمَ وَلَحۡمَ ٱلۡخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ لِغَيۡرِ ٱللَّهِ بِهِۦۖ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ غَيۡرَ بَاغٖ وَلَا عَادٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Hakika Amewaharamishia mfu wa mnyama, damu yenye kutiririka kutoka kwa mnyama aliechinjwa pale achinjwapo, nyama ya nguruwe na mnyama aliyechinjiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini yoyote Aliyelazimika kula chochote kati ya vitu hivi vilivyoharamishwa, kwa dharura ya kuogopa kufa, na hali yeye si dhalimu wala si mkiukaji mpaka ya dharura, basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kumsamehe na ni Mwenye huruma naye, Hatamtesa kwa kwa kitendo alichokifanya.
अरबी तफ़सीरें:
وَلَا تَقُولُواْ لِمَا تَصِفُ أَلۡسِنَتُكُمُ ٱلۡكَذِبَ هَٰذَا حَلَٰلٞ وَهَٰذَا حَرَامٞ لِّتَفۡتَرُواْ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ لَا يُفۡلِحُونَ
wala msiseme, enyi washirikina, urongo unaotolewa na ndimi zenu: «hii ni halali» juu ya kitu kilichoharamishwa «na hii ni haramu» juu ya kitu kilichohalalishwa, ili kumzulia Mwenyezi Mungu urongo kwa kumnasibishia uhalalishaji na uharamishaji. Hakika wale wanaomzulia Mwenyezi Mungu urongo hawatafaulu kupata wema wowote ulimwenguni wala Akhera.
अरबी तफ़सीरें:
مَتَٰعٞ قَلِيلٞ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ
Starehe walionayo duniani na starehe yenye kuondoka na ni chache. Na huko Akhera watapata adhabu iumizayo.
अरबी तफ़सीरें:
وَعَلَى ٱلَّذِينَ هَادُواْ حَرَّمۡنَا مَا قَصَصۡنَا عَلَيۡكَ مِن قَبۡلُۖ وَمَا ظَلَمۡنَٰهُمۡ وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ
Na Mayahudi tuliwaharamishia vile vitu tulivyokupa habari zake, ewe Mtume, kabla, navyo ni kila mnyama mwenye kucha na mafuta ya ng’ombe, mbuzi na kondoo, isipokuwa kile kilichobebwa na migongo yao au matumbo yao au kilichotangamana na mifupa. Na sisi hatukuwadhulumu wao , lakini wao walikuwa ni wenye kuzidhulumu nafsi zao kwa kukanusha na kufanya uadui, ndipo wakastahili kuharamishiwa kwa njia ya kutiwa adabu.
अरबी तफ़सीरें:
ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ عَمِلُواْ ٱلسُّوٓءَ بِجَهَٰلَةٖ ثُمَّ تَابُواْ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ وَأَصۡلَحُوٓاْ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعۡدِهَا لَغَفُورٞ رَّحِيمٌ
Kisha hakika Mola wako, kwa wale waliofanya maasia, kwa kutojua mwisho wake na kwamba yanapasisha hasira za Mwenyezi Mungu - kwani kila anayemuasi Mwenyezi Mungu, kwa kukosea au kwa kusudia, huwa ni mjinga kwa mtazamo huu, hata kama anajua kuwa ni haramu-, kisha wakarudi kwa Mwenyezi Mungu na kuyaepuka yale madhambi waliokuwa wakiyafanya na wakazitengeneza nafsi zao na matendo yao, hakika Mola wako, baada ya kutubia kwao na kutengenea kwao, ni Mwenye kuwasamehe, ni Mwenye huruma kwao.
अरबी तफ़सीरें:
إِنَّ إِبۡرَٰهِيمَ كَانَ أُمَّةٗ قَانِتٗا لِّلَّهِ حَنِيفٗا وَلَمۡ يَكُ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Hakika Ibrāhīm alikuwa kiongozi katika mema, na alikuwa mtiifu mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, haendi kombo na Uislamu, ni mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu, si mwenye kumshirikisha.
अरबी तफ़सीरें:
شَاكِرٗا لِّأَنۡعُمِهِۚ ٱجۡتَبَىٰهُ وَهَدَىٰهُ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ
Na alikuwa ni mwenye kuzishukuru neema za Mwenyezi Mungu kwake. Mwenyezi Mungu Alimchagua kwa ujumbe Wake na Akamuongoza kwenye njia iliyolingana sawa, nayo ni Uislamu.
अरबी तफ़सीरें:
وَءَاتَيۡنَٰهُ فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗۖ وَإِنَّهُۥ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ لَمِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ
Na tulimpa ulimwenguni neema nzuri ya kusifiwa na watu waliokuja nyuma yake, kufuatwa na kuwa na watoto wema. Na yeye, mbele ya Mwenyezi Mungu, huko Akhera, ni miongoni mwa watu wema wenye daraja za juu.
अरबी तफ़सीरें:
ثُمَّ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ أَنِ ٱتَّبِعۡ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۖ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Kisha tukakuletea wahyi, ewe Mtume, kwamba uifuate dini ya Uislamu kama alivyoifuata Ibrāhīm na kwamba ulingane juu yake na usiiyepuke, kwani Ibrāhīm hakuwa ni miongoni mwa wale wanaowashrikisha wengine pamoja na Mwenyezi Mungu.
अरबी तफ़सीरें:
إِنَّمَا جُعِلَ ٱلسَّبۡتُ عَلَى ٱلَّذِينَ ٱخۡتَلَفُواْ فِيهِۚ وَإِنَّ رَبَّكَ لَيَحۡكُمُ بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فِيمَا كَانُواْ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ
Mwenyezi Mungu Ameufanya utukuzaji wa siku ya Jumamosi, kwa kuitenga kwa kufanya ibada ndani yake, kwa Myahudi ambao walitafautiana na Nabii wao juu yake, na wakaiteua badala ya siku ya Ijumaa ambayo waliamrishwa waitukuze. Hakika Mola wako , ewe Mtume, ni Mwenye kuhukumu baina ya wale waliotafautiana na Nabii wao Siku ya Kiyama na kumlipa kila mmoja kwa yale anayofaa kuyapata.
अरबी तफ़सीरें:
ٱدۡعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِٱلۡحِكۡمَةِ وَٱلۡمَوۡعِظَةِ ٱلۡحَسَنَةِۖ وَجَٰدِلۡهُم بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ
Lingania, ewe Mtume, wewe na aliyekufuata, kwenye Dini ya Mola wako na njia Yake iliyolingana sawa kwa kutumia hekima ambayo Mwenyezi Mungu alikuletea wahyi nayo ndani ya ya Qur’ani na Sunnah. Na uwazungumzie watu kwa njia inayolingana na wao, uwape nasaha kwa njia nzuri yenye kuwavutia kwenye kheri na kuwakimbiza wajiepushe na shari, na ujadiliane na wao kwa njia nzuri za kujadiliana za utaratibu na upole, kwani si juu yako isipokuwa ni kufikisha ujumbe, na ushafikisha. Ama kuwafanya waongoke, hilo ni juu ya Mwenyezi Mungu Peke Yake. Yeye Ndiye Anayemjua zaidi yule aliyepotea na akaiyepuka njia Yake, na Yeye Anawajua zaidi walioongoka.
अरबी तफ़सीरें:
وَإِنۡ عَاقَبۡتُمۡ فَعَاقِبُواْ بِمِثۡلِ مَا عُوقِبۡتُم بِهِۦۖ وَلَئِن صَبَرۡتُمۡ لَهُوَ خَيۡرٞ لِّلصَّٰبِرِينَ
Na mkitaka kuwalipiza kisasi, enyi Waumini, wale waliowafanyia uadui, msiongeze zaidi ya vile walivyowafanya. Na mkisubiri, basi hilo ni bora kwenu nyinyi ulimwenguni, kwa kupewa ushindi, na kesho Akhera, kwa kupewa malipo makubwa.
अरबी तफ़सीरें:
وَٱصۡبِرۡ وَمَا صَبۡرُكَ إِلَّا بِٱللَّهِۚ وَلَا تَحۡزَنۡ عَلَيۡهِمۡ وَلَا تَكُ فِي ضَيۡقٖ مِّمَّا يَمۡكُرُونَ
Na vumilia, ewe Mtume, kwa maudhi yanayokupata katika njia ya Mwenyezi Mungu mpaka ikujie faraji, na hakukuwa huku kuvumilia kwako isipokuwa ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwani Yeye Ndiye mwenye kukusaidia na kukupa uthabiti, na usisikitike juu ya wale wanaoenda kinyume na wewe na wasiitikie ulinganizi wako, wala usiwe na usijitie dhiki za moyo kutokana na hila zao na vitimbi vyao, kwani hilo litawarudia wao wenyewe kwa shari na mateso.
अरबी तफ़सीरें:
إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَواْ وَّٱلَّذِينَ هُم مُّحۡسِنُونَ
Kwa hakika Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, kwa taufiki Yake, msaada Wake, upaji nguvu Wake na nusura Yake Yuko pamoja na waliomcha kwa kuyafuata Aliyoyaamrisha na kuyaepuka Aliyoyakataza; na yuko pamoja na wale wanatenda wema, kwa kutekeleza faradhi Zake na kusimama kutimiza haki Zaka na kujilazimisha kumtii, kwa kuwapa msaada Wake, uongozi Wake na nusura Yake.
अरबी तफ़सीरें:
 
अर्थों का अनुवाद सूरा: सूरा अन्-नह़्ल
सूरों की सूची पृष्ठ संख्या
 
क़ुरआन के अर्थों का अनुवाद - स्वाहीली अनुवाद - अब्दुल्लाह मुहम्मद तथा नासिर ख़मीस - अनुवादों की सूची

पवित्र क़ुरआन के अर्थों का सवाहिली अनुवाद, अनुवादक : डॉ. अब्दुल्लाह मुहम्मद अबू बक्र तथा शैख़ नासिर ख़मीस

बंद करें