क़ुरआन के अर्थों का अनुवाद - स्वाहीली अनुवाद - अब्दुल्लाह मुहम्मद तथा नासिर ख़मीस * - अनुवादों की सूची


अर्थों का अनुवाद आयत: (53) सूरा: सूरा अल्-आराफ़
هَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّا تَأۡوِيلَهُۥۚ يَوۡمَ يَأۡتِي تَأۡوِيلُهُۥ يَقُولُ ٱلَّذِينَ نَسُوهُ مِن قَبۡلُ قَدۡ جَآءَتۡ رُسُلُ رَبِّنَا بِٱلۡحَقِّ فَهَل لَّنَا مِن شُفَعَآءَ فَيَشۡفَعُواْ لَنَآ أَوۡ نُرَدُّ فَنَعۡمَلَ غَيۡرَ ٱلَّذِي كُنَّا نَعۡمَلُۚ قَدۡ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ وَضَلَّ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ
Kwani kuna wanachokingojea makafiri isipokuwa mateso, ambayo ndiyo kikomo cha mambo yao, waliyoahidiwa katika Qur’ani? Siku kitakapokuja kikomo cha mambo yao, cha kuhesabiwa, kulipwa na mateso Siku ya Kiyama, watasema makafiri walioiacha Qur’ani na wakaikanusha duniani, «Sasa imetubainikia kwamba Mitume wa Mola wetu wamekuja na haki na wametupa ushauri mzuri. Je, tunaweza kupata marafiki na waombezi wapate kutuombea kwa Mola wetu? Au tunaweza kupewa nafasi ya kurudi duniani mara nyingine tupate kufanya matendo ya kumfanya Mwenyezi Mungu Awe radhi na sisi? Hakika wamepata hasara nafsi zao kwa kuingia Motoni na kukaa milele humo, na vimewaondokea vile ambavyo walikuwa wakiviabudu badala ya Mwenyezi Mungu na yale ambayo walikuwa wakiyazua miongoni mwa yale ambayo Shetani alikuwa akiwaadi nayo.
अरबी तफ़सीरें:
 
अर्थों का अनुवाद आयत: (53) सूरा: सूरा अल्-आराफ़
सूरों की सूची पृष्ठ संख्या
 
क़ुरआन के अर्थों का अनुवाद - स्वाहीली अनुवाद - अब्दुल्लाह मुहम्मद तथा नासिर ख़मीस - अनुवादों की सूची

पवित्र क़ुरआन के अर्थों का सवाहिली अनुवाद, अनुवादक : डॉ. अब्दुल्लाह मुहम्मद अबू बक्र तथा शैख़ नासिर ख़मीस

बंद करें