Check out the new design

क़ुरआन के अर्थों का अनुवाद - सवाहिली अनुवाद - अनुवाद अग्रदूत केंद्र * - अनुवादों की सूची


अर्थों का अनुवाद सूरा: हूद   आयत:
فَلَا تَكُ فِي مِرۡيَةٖ مِّمَّا يَعۡبُدُ هَٰٓؤُلَآءِۚ مَا يَعۡبُدُونَ إِلَّا كَمَا يَعۡبُدُ ءَابَآؤُهُم مِّن قَبۡلُۚ وَإِنَّا لَمُوَفُّوهُمۡ نَصِيبَهُمۡ غَيۡرَ مَنقُوصٖ
Basi usiwe katika shaka juu ya yale wanayoyaabudu hawa. Hawaabudu isipokuwa kama walivyoabudu baba zao zamani. Na hakika Sisi tutawatimilizia fungu lao bila ya kupunguzwa.
अरबी तफ़सीरें:
وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ فَٱخۡتُلِفَ فِيهِۚ وَلَوۡلَا كَلِمَةٞ سَبَقَتۡ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيۡنَهُمۡۚ وَإِنَّهُمۡ لَفِي شَكّٖ مِّنۡهُ مُرِيبٖ
Na hakika tulimpa Musa Kitabu, lakini kukazuka kuhitilafiana ndani yake. Na lau kuwa si neno lililokwisha tangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi, bila ya shaka ingelihukumiwa baina yao. Na hakika wao wamo katika shaka juu yake inayowahangaisha.
अरबी तफ़सीरें:
وَإِنَّ كُلّٗا لَّمَّا لَيُوَفِّيَنَّهُمۡ رَبُّكَ أَعۡمَٰلَهُمۡۚ إِنَّهُۥ بِمَا يَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ
Na hakika Mola wako Mlezi atawatimilizia malipo ya matendo yao wote. Hakika Yeye anayo habari ya wayatendayo.
अरबी तफ़सीरें:
فَٱسۡتَقِمۡ كَمَآ أُمِرۡتَ وَمَن تَابَ مَعَكَ وَلَا تَطۡغَوۡاْۚ إِنَّهُۥ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ
Basi, nyooka kama ulivyoamrishwa, wewe na wale wanaotubia kwa Mwenyezi Mungu pamoja nawe, wala msivuke mipaka. Hakika Yeye anayaona yote myatendayo.
अरबी तफ़सीरें:
وَلَا تَرۡكَنُوٓاْ إِلَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ فَتَمَسَّكُمُ ٱلنَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِنۡ أَوۡلِيَآءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ
Wala msiwategemee wale waliodhulumu, mkaja kuguswa na Moto. Wala nyinyi hamna walinzi wowote kando na Mwenyezi Mungu, wala tena hamtanusuriwa.
अरबी तफ़सीरें:
وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ طَرَفَيِ ٱلنَّهَارِ وَزُلَفٗا مِّنَ ٱلَّيۡلِۚ إِنَّ ٱلۡحَسَنَٰتِ يُذۡهِبۡنَ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ ذَٰلِكَ ذِكۡرَىٰ لِلذَّٰكِرِينَ
Na simamisha Swala katika ncha mbili za mchana na nyakati za usiku zilizo karibu na mchana. Hakika mazuri huondoa mabaya. Huu ni ukumbusho kwa wanaokumbuka.
अरबी तफ़सीरें:
وَٱصۡبِرۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Na subiri, kwani hakika Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wafanyao mazuri.
अरबी तफ़सीरें:
فَلَوۡلَا كَانَ مِنَ ٱلۡقُرُونِ مِن قَبۡلِكُمۡ أُوْلُواْ بَقِيَّةٖ يَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡفَسَادِ فِي ٱلۡأَرۡضِ إِلَّا قَلِيلٗا مِّمَّنۡ أَنجَيۡنَا مِنۡهُمۡۗ وَٱتَّبَعَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مَآ أُتۡرِفُواْ فِيهِ وَكَانُواْ مُجۡرِمِينَ
Basi mbona hawakuwamo katika vizazi vya kabla yenu wenye vyeo na wasaa wanaokataza uharibifu katika nchi, isipokuwa wachache tu, miongoni mwa wale tuliowaokoa miongoni mwao? Na wale waliodhulumu walifuata yale waliyostareheshwa kwayo, na walikuwa wahalifu.
अरबी तफ़सीरें:
وَمَا كَانَ رَبُّكَ لِيُهۡلِكَ ٱلۡقُرَىٰ بِظُلۡمٖ وَأَهۡلُهَا مُصۡلِحُونَ
Wala hakuwa Mola wako Mlezi wa kuiangamiza miji kwa dhuluma tu ilhali watu wake ni watenda mema.
अरबी तफ़सीरें:
 
अर्थों का अनुवाद सूरा: हूद
सूरों की सूची पृष्ठ संख्या
 
क़ुरआन के अर्थों का अनुवाद - सवाहिली अनुवाद - अनुवाद अग्रदूत केंद्र - अनुवादों की सूची

अनुवाद अनुवाद अग्रदूत केंद्र द्वारा नियुक्त एक समूह ने अल-रब्वाह आह्वान संस्था और भाषाओं में इस्लामिक सामग्री की सेवा करने वाली संस्था के सहयोग से किया है।

बंद करें