Alif Laam Raa.[1] Hiki ni Kitabu tulichokuteremshia ili uwatoe watu kwenye giza mbalimbali uwapeleke kwenye mwangaza, kwa idhini ya Mola wao Mlezi, uwafikishe kwenye Njia ya Mwenye nguvu, Msifika.
[1] Herufi hizi "Alif Laam Raa" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Wale wanaofadhilisha uhai wa dunia kuliko Akhera, na wanawazuilia watu Njia ya Mwenyezi Mungu, na wanataka kuipotosha. Hao wako katika upotofu wa mbali.
Na hatukumtuma Mtume yeyote isipokuwa kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia. Basi Mwenyezi Mungu anampoteza amtakaye, na anamwongoa amtakaye. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Na hakika tulimtuma Musa na miujiza yetu, tukamwambia: Watoe kaumu yako kwenye giza mbalimbali uwapeleke kwenye nuru. Na uwakumbushe siku za Mwenyezi Mungu. Hakika katika hayo zipo ishara kwa kila mwenye kusubiri sawasawa, mwenye kushukuru sana.
Na Musa alipowaambia kaumu yake, "Kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu pale alipowaokoa kutokana na watu wa Firauni waliokuwa wakiwatia adhabu mbaya kabisa, wakiwachinja wana wenu wanaume, na wakiwaacha hai wanawake wenu. Na katika hayo ulikuwa mtihani mkubwa unaotoka kwa Mola wenu Mlezi."
Je, hazikuwafikia habari za wale waliokuwa kabla yenu? Kaumu ya Nuhu, na 'Aadi, na Thamud, na wale waliokuwa baada yao, ambao hakuna awajuaye isipokuwa Mwenyezi Mungu? Mitume wao waliwajia na hoja zilizo wazi, na wao wakarudisha mikono yao kwenye vinywa vyao, wakasema: Hakika sisi tumeyakufuru hayo mliyotumwa nayo, na hakika sisi tuko katika shaka kubwa na hayo mnayotuitia.
Mitume wao wakasema: Ati kuna shaka kuhusiana na Mwenyezi Mungu, Muumba mbingu na ardhi? Yeye anawaita ili awafutie madhambi yenu, na awape muhula mpaka muda uliowekwa. Wakasema: Nyinyi si chochote isipokuwa ni wanadamu tu kama sisi. Mnataka kutuzuilia mbali na yale waliyokuwa wakiabudu baba zetu. Basi tujieni na hoja iliyo wazi.
Mitume wao wakawaambia: Sisi kweli si chochote isipokuwa ni wanadamu kama nyinyi. Lakini Mwenyezi Mungu humneemesha amtakaye katika waja wake. Wala sisi hatuwezi kuwaletea uthibitisho isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na juu ya Mwenyezi Mungu basi na wategemee Waumini.
Na tuna nini hata tusimtegemee Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ametuongoa kwenye njia zetu. Na hakuna hakika tutayavumilia hayo maudhi mnayotuudhi nayo. Na juu ya Mwenyezi Mungu na wategemee wanaotegemea.
Na wale waliokufuru wakawaambia Mitume wao: Hakika, tutawatoa katika nchi yetu, au lazima mtarudi katika mila yetu. Basi Mola wao Mlezi akawafunulia ufunuo (wahyi): Hakika tutawaangamiza madhalimu!
Mfano wa wale waliomkufuru Mola wao Mlezi, vitendo vyao ni kama jivu linalopeperushwa kwa nguvu za upepo katika siku ya upepo mkali. Hawawezi kupata chochote katika yale waliyoyachuma. Huko ndiko kupotea kwa mbali!
Na wote watajitokeza mbele ya Mwenyezi Mungu. Wanyonge watawaambia wale waliotakabari: Hakika sisi tulikuwa wafwasi wenu; basi hebu mtuondolee kidogo hivi katika adhabu ya Mwenyezi Mungu? Watasema: Lau Mwenyezi Mungu angelituongoa, basi hakuna shaka nasi tungeliwaongoa. Ni mamoja kwetu tukipapatika au tukisubiri; hatuna popote pa kukimbilia.
Na shetani atasema itakapokatwa hukumu: Hakika Mwenyezi Mungu aliwaahidi ahadi ya kweli. Nami niliwaahidi; lakini sikuwatimizia ahadi yangu. Na sikuwa na mamlaka yoyote juu yenu, isipokuwa niliwaita, nanyi mkaniitikia. Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe. Mimi siwezi kuwa mtetezi wenu, wala nyinyi hamuwezi kuwa watetezi wangu. Hakika mimi nilikufuru tangu zamani huko kunishirikisha kwenu na Mwenyezi Mungu. Hakika madhalimu wana adhabu chungu.
Na wale walioamini na wakatenda mema wataingizwa katika Mabustani yapitayo mito kwa chini yake, wadumu humo kwa idhini ya Mola wao Mlezi. Maamkizi yao humo yatakuwa: Salaam (Amani)!
Mwenyezi Mungu huwaimarisha wale walioamini kwa kauli ya imara katika uhai wa dunia na katika Akhera. Na Mwenyezi Mungu huwapoteza madhalimu. Na Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo.
Waambie waja wangu walioamini, wadumishe Swala, na watoe katika tulivyowaruzuku, kwa siri na dhahiri, kabla ya kufika kwa Siku isiyokuwa na biashara yoyote wala urafiki wa dhati.
Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi, na akateremsha maji kutoka mbinguni, na kwa hayo akatoa matunda kuwa ni riziki yenu. Na akawatiishia majahazi yanayokwenda baharini kwa amri yake, na akawatiishia mito.
Na akawapa katika kila mlichomuomba. Na mkihesabu neema za Mwenyezi Mungu, hamuwezi kuzidhibiti. Hakika mwanadamu ni dhalimu mkubwa, mwenye kuzikufuru neema.
Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika hayo yamewapoteza wengi wa watu. Basi aliyenifuata mimi, huyo hakika ni miongoni mwangu. Na aliyeniasi, hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.
Mola wetu Mlezi! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuria yangu katika bonde lisilokuwa na mimea, kwenye Nyumba yako Takatifu, ewe Mola wetu Mlezi, ili wadumishe Swala. Basi zifanye nyoyo za watu zielekee kwao, na waruzuku matunda, ili wapate kushukuru.
Ewe Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe unajua tunayoyaweka hadharani na tunayoyaficha. Na hakuna kitu kinachofichikana kwa Mwenyezi Mungu katika ardhi wala katika mbingu.
Alhamdulillahi (sifa njema ni za Mwenyezi Mungu) aliyenitunuku pamoja na uzee wangu Ismail na Is-haq. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusikia sana maombi.
Na waonye watu siku itakapowajia adhabu, na wale waliodhulumu waseme, "Ewe Mola wetu Mlezi! Tuahirishe muda kidogo tuitikie wito wako na tuwafuate Mitume." Kwani nyinyi hamkuapa zamani kwamba kamwe hamuwezi kuondoka?
Na hakika walifanya vitimbi vyao, na vitimbi vyao hivyo anavijua Mwenyezi Mungu. Na kwa yakini vitimbi vyao hivyo vilikuwa ni vya kuweza kuondosha milima.
क़ुरआन के अर्थों का अनुवाद - सवाहिली अनुवाद - अनुवाद अग्रदूत केंद्र - अनुवादों की सूची
इसका अनुवाद, अनुवाद अग्रदूत केंद्र द्वारा नियुक्त एक समूह ने अल-रब्वाह आह्वान संस्था और भाषाओं में इस्लामिक सामग्री की सेवा करने वाली संस्था के सहयोग से किया है।
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
खोज परिणाम:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".