Check out the new design

क़ुरआन के अर्थों का अनुवाद - सवाहिली अनुवाद - अनुवाद अग्रदूत केंद्र * - अनुवादों की सूची


अर्थों का अनुवाद सूरा: अश्-शु-अ़-रा   आयत:
إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا خُلُقُ ٱلۡأَوَّلِينَ
Haya si chochote isipokuwa ni mtindo wa watu wa tokea zamani.
अरबी तफ़सीरें:
وَمَا نَحۡنُ بِمُعَذَّبِينَ
Wala sisi hatutaadhibiwa.
अरबी तफ़सीरें:
فَكَذَّبُوهُ فَأَهۡلَكۡنَٰهُمۡۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ
Wakamkadhibisha; nasi tukawaangamiza. Hakika bila ya shaka katika haya ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
अरबी तफ़सीरें:
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.
अरबी तफ़सीरें:
كَذَّبَتۡ ثَمُودُ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Kina Thamud waliwakadhibisha Mitume.
अरबी तफ़सीरें:
إِذۡ قَالَ لَهُمۡ أَخُوهُمۡ صَٰلِحٌ أَلَا تَتَّقُونَ
Alipowaambia ndugu yao Saleh: Je, hamumchi Mungu?
अरबी तफ़सीरें:
إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ
Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
अरबी तफ़सीरें:
فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nitiini.
अरबी तफ़सीरें:
وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Wala siwaulizi ujira wowote juu yake. Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
अरबी तफ़सीरें:
أَتُتۡرَكُونَ فِي مَا هَٰهُنَآ ءَامِنِينَ
Je, mtaachwa salama usalimina katika haya yaliyopo hapa?
अरबी तफ़सीरें:
فِي جَنَّٰتٖ وَعُيُونٖ
Katika mabustani, na chemchemi?
अरबी तफ़सीरें:
وَزُرُوعٖ وَنَخۡلٖ طَلۡعُهَا هَضِيمٞ
Na konde na mitende yenye makole yaliyowiva.
अरबी तफ़सीरें:
وَتَنۡحِتُونَ مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتٗا فَٰرِهِينَ
Na mnachonga milimani majumba kwa ustadi.
अरबी तफ़सीरें:
فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nitiini mimi.
अरबी तफ़सीरें:
وَلَا تُطِيعُوٓاْ أَمۡرَ ٱلۡمُسۡرِفِينَ
Wala msitii amri za waliopitiliza mipaka
अरबी तफ़सीरें:
ٱلَّذِينَ يُفۡسِدُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا يُصۡلِحُونَ
Ambao wanafanya uharibifu katika nchi, wala hawatengenezi.
अरबी तफ़सीरें:
قَالُوٓاْ إِنَّمَآ أَنتَ مِنَ ٱلۡمُسَحَّرِينَ
Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa waliorogwa.
अरबी तफ़सीरें:
مَآ أَنتَ إِلَّا بَشَرٞ مِّثۡلُنَا فَأۡتِ بِـَٔايَةٍ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ
Wewe si chochote isipokuwa ni mtu kama sisi. Basi leta Ishara ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli.
अरबी तफ़सीरें:
قَالَ هَٰذِهِۦ نَاقَةٞ لَّهَا شِرۡبٞ وَلَكُمۡ شِرۡبُ يَوۡمٖ مَّعۡلُومٖ
Akasema: Huyu ngamia jike; awe na zamu yake ya kunywa, na nyinyi muwe na zamu yenu ya kunywa katika siku maalumu.
अरबी तफ़सीरें:
وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوٓءٖ فَيَأۡخُذَكُمۡ عَذَابُ يَوۡمٍ عَظِيمٖ
Wala msimguse kwa wovu, ikawashika adhabu ya Siku Kubwa.
अरबी तफ़सीरें:
فَعَقَرُوهَا فَأَصۡبَحُواْ نَٰدِمِينَ
Lakini wakamuua, na wakawa wenye kujuta.
अरबी तफ़सीरें:
فَأَخَذَهُمُ ٱلۡعَذَابُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ
Basi ikawapata adhabu. Hakika katika hayo ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
अरबी तफ़सीरें:
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.
अरबी तफ़सीरें:
 
अर्थों का अनुवाद सूरा: अश्-शु-अ़-रा
सूरों की सूची पृष्ठ संख्या
 
क़ुरआन के अर्थों का अनुवाद - सवाहिली अनुवाद - अनुवाद अग्रदूत केंद्र - अनुवादों की सूची

इसका अनुवाद, अनुवाद अग्रदूत केंद्र द्वारा नियुक्त एक समूह ने अल-रब्वाह आह्वान संस्था और भाषाओं में इस्लामिक सामग्री की सेवा करने वाली संस्था के सहयोग से किया है।

बंद करें