Check out the new design

क़ुरआन के अर्थों का अनुवाद - सवाहिली अनुवाद - अनुवाद अग्रदूत केंद्र * - अनुवादों की सूची


अर्थों का अनुवाद सूरा: अन्-नाज़िआ़त   आयत:
ٱذۡهَبۡ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ
Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri.
अरबी तफ़सीरें:
فَقُلۡ هَل لَّكَ إِلَىٰٓ أَن تَزَكَّىٰ
Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa?
अरबी तफ़सीरें:
وَأَهۡدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخۡشَىٰ
Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha.
अरबी तफ़सीरें:
فَأَرَىٰهُ ٱلۡأٓيَةَ ٱلۡكُبۡرَىٰ
Basi alimwonyesha Ishara kubwa.
अरबी तफ़सीरें:
فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ
Lakini alikadhibisha na akaasi.
अरबी तफ़सीरें:
ثُمَّ أَدۡبَرَ يَسۡعَىٰ
Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi.
अरबी तफ़सीरें:
فَحَشَرَ فَنَادَىٰ
Akakusanya watu akanadi.
अरबी तफ़सीरें:
فَقَالَ أَنَا۠ رَبُّكُمُ ٱلۡأَعۡلَىٰ
Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa.
अरबी तफ़सीरें:
فَأَخَذَهُ ٱللَّهُ نَكَالَ ٱلۡأٓخِرَةِ وَٱلۡأُولَىٰٓ
Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo.
अरबी तफ़सीरें:
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبۡرَةٗ لِّمَن يَخۡشَىٰٓ
Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanaoogopa.
अरबी तफ़सीरें:
ءَأَنتُمۡ أَشَدُّ خَلۡقًا أَمِ ٱلسَّمَآءُۚ بَنَىٰهَا
Je, ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliyeijenga!
अरबी तफ़सीरें:
رَفَعَ سَمۡكَهَا فَسَوَّىٰهَا
Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri.
अरबी तफ़सीरें:
وَأَغۡطَشَ لَيۡلَهَا وَأَخۡرَجَ ضُحَىٰهَا
Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake.
अरबी तफ़सीरें:
وَٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ ذَٰلِكَ دَحَىٰهَآ
Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi.
अरबी तफ़सीरें:
أَخۡرَجَ مِنۡهَا مَآءَهَا وَمَرۡعَىٰهَا
Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake.
अरबी तफ़सीरें:
وَٱلۡجِبَالَ أَرۡسَىٰهَا
Na milima akaisimamisha imara.
अरबी तफ़सीरें:
مَتَٰعٗا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ
Kwa manufaa yenu na mifugo yenu.
अरबी तफ़सीरें:
فَإِذَا جَآءَتِ ٱلطَّآمَّةُ ٱلۡكُبۡرَىٰ
Basi itakapofika hiyo balaa kubwa,
अरबी तफ़सीरें:
يَوۡمَ يَتَذَكَّرُ ٱلۡإِنسَٰنُ مَا سَعَىٰ
Siku ambayo mtu atakumbuka aliyoyafanya,
अरबी तफ़सीरें:
وَبُرِّزَتِ ٱلۡجَحِيمُ لِمَن يَرَىٰ
Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona,
अरबी तफ़सीरें:
فَأَمَّا مَن طَغَىٰ
Basi ama yule aliyezidi ujeuri,
अरबी तफ़सीरें:
وَءَاثَرَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا
Na akakhiari maisha ya dunia,
अरबी तफ़सीरें:
فَإِنَّ ٱلۡجَحِيمَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ
Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake!
अरबी तफ़सीरें:
وَأَمَّا مَنۡ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِۦ وَنَهَى ٱلنَّفۡسَ عَنِ ٱلۡهَوَىٰ
Na ama yule anayeogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio,
अरबी तफ़सीरें:
فَإِنَّ ٱلۡجَنَّةَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ
Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makazi yake!
अरबी तफ़सीरें:
يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرۡسَىٰهَا
Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini?
अरबी तफ़सीरें:
فِيمَ أَنتَ مِن ذِكۡرَىٰهَآ
Una nini wewe hata uitaje?
अरबी तफ़सीरें:
إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَىٰهَآ
Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake.
अरबी तफ़सीरें:
إِنَّمَآ أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخۡشَىٰهَا
Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuihofu.
अरबी तफ़सीरें:
كَأَنَّهُمۡ يَوۡمَ يَرَوۡنَهَا لَمۡ يَلۡبَثُوٓاْ إِلَّا عَشِيَّةً أَوۡ ضُحَىٰهَا
Ni kama kwamba wao siku watakapoiona (hiyo Saa) hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake.
अरबी तफ़सीरें:
 
अर्थों का अनुवाद सूरा: अन्-नाज़िआ़त
सूरों की सूची पृष्ठ संख्या
 
क़ुरआन के अर्थों का अनुवाद - सवाहिली अनुवाद - अनुवाद अग्रदूत केंद्र - अनुवादों की सूची

इसका अनुवाद, अनुवाद अग्रदूत केंद्र द्वारा नियुक्त एक समूह ने अल-रब्वाह आह्वान संस्था और भाषाओं में इस्लामिक सामग्री की सेवा करने वाली संस्था के सहयोग से किया है।

बंद करें