Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Abdullah Muhammad dan Nasir Khamis * - Daftar isi terjemahan


Terjemahan makna Surah: Surah Al-Muzzammil   Ayah:

Surat Al-Muzzammil

يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡمُزَّمِّلُ
Ewe ulijifinika nguo zako!
Tafsir berbahasa Arab:
قُمِ ٱلَّيۡلَ إِلَّا قَلِيلٗا
Inuka uswali kipindi cha usiku isipokuwa sehemu chache yake.
Tafsir berbahasa Arab:
نِّصۡفَهُۥٓ أَوِ ٱنقُصۡ مِنۡهُ قَلِيلًا
Inuka kwa muda wa nusu ya usiku au kupungua nusu kidogo mpaka ufikie theluthi.
Tafsir berbahasa Arab:
أَوۡ زِدۡ عَلَيۡهِ وَرَتِّلِ ٱلۡقُرۡءَانَ تَرۡتِيلًا
Au ongeza zaidi ya nusu mpaka ufikie theluthi mbili. Na usome Qur’ani kwa utaratibu na utulivu, uzifafanue herufi na vikomo.
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّا سَنُلۡقِي عَلَيۡكَ قَوۡلٗا ثَقِيلًا
Hakika sisi tutakuteremshia, ewe Nabii, Qur’ani tukufu inayokusanya maamrisho na makatazo na hukumu za kisheria.
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّ نَاشِئَةَ ٱلَّيۡلِ هِيَ أَشَدُّ وَطۡـٔٗا وَأَقۡوَمُ قِيلًا
Hakika ibada inayo inayofanya ndani ya usiku ina athari kubwa zaid moyoni, na maneno yanabainika zaidi, kwa kuwa moyo uko mtupu hauna mashughuli ya kilimwengu.
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّ لَكَ فِي ٱلنَّهَارِ سَبۡحٗا طَوِيلٗا
Hakika wewe katika kipindi cha mchana una wakati wa kuzunguka na kushughulika katika mambo yenye maslahi nawe na kufanya harakati nyingi kwa majukumu ya utume, basi wakati wa usiku ipe nafasi nafsi yako kumuabudu Mola wako.
Tafsir berbahasa Arab:
وَٱذۡكُرِ ٱسۡمَ رَبِّكَ وَتَبَتَّلۡ إِلَيۡهِ تَبۡتِيلٗا
Na ulitaje, ewe Nabii, jina la Mola wako, umuombe kwalo na utindikie Kwake kikamilifu katika ibada yako na ujitegemeze Kwake.
Tafsir berbahasa Arab:
رَّبُّ ٱلۡمَشۡرِقِ وَٱلۡمَغۡرِبِ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ فَٱتَّخِذۡهُ وَكِيلٗا
Yeye Ndiye Mmiliki wa Mashariki na Magharibi. Hakuna muabudiwa ka haki isipokuwa Yeye. Basi mtegemee Yeye na umuachie Yeye mambo yako.
Tafsir berbahasa Arab:
وَٱصۡبِرۡ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَٱهۡجُرۡهُمۡ هَجۡرٗا جَمِيلٗا
Na uvumilie kwa yale ambayo washirikina wanayasema kuhusu wewe na kuhusu Dini yako. Na uende kinyume na wao katika maneno yao ya ubatilifu pamoja na kuwapuuza na kuacha kuwalipiza.
Tafsir berbahasa Arab:
وَذَرۡنِي وَٱلۡمُكَذِّبِينَ أُوْلِي ٱلنَّعۡمَةِ وَمَهِّلۡهُمۡ قَلِيلًا
Na uniache mimi, ewe Mtume, na hawa wakanushaji wa aya zangu, wenye starehe na gogi la ulimwengu, na uwape muhula wa muda mchache kwa kucheleweshewa adhabu mpaka muda wa wao kuadhibiwa ufikie ukomo wake.
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّ لَدَيۡنَآ أَنكَالٗا وَجَحِيمٗا
Kwa hakika wao watapata kwetu sisi huko Akhera pingu nzito na Moto wenye kuwaka ambao watachomwa nao,
Tafsir berbahasa Arab:
وَطَعَامٗا ذَا غُصَّةٖ وَعَذَابًا أَلِيمٗا
na chakula cha kuchukiza chenye kusakama kooni kisicho na ladha, na adhabu inayoumiza.
Tafsir berbahasa Arab:
يَوۡمَ تَرۡجُفُ ٱلۡأَرۡضُ وَٱلۡجِبَالُ وَكَانَتِ ٱلۡجِبَالُ كَثِيبٗا مَّهِيلًا
Siku itakapotikisika na kusukikasukika ardhi na majabali mpaka majabali yawe mlima wa mchanga wenye kutiririka na kupeperuka, baada ya kuwa kwenye hali ya ugumu na ukavu.
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّآ أَرۡسَلۡنَآ إِلَيۡكُمۡ رَسُولٗا شَٰهِدًا عَلَيۡكُمۡ كَمَآ أَرۡسَلۡنَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ رَسُولٗا
Hakika sisi tumemtumiliza kwenu nyinyi, watu wa Makkah, Muhammad kuwa ni Mtume, mwenye kutoa ushahidi wa ukafiri na uasi unaotokana na nyinyi, kama vile tulivyomtumiliza Mūsā kuwa ni Mtume kwenda kwa Fir’awn aliyepita kiasi katika uasi.
Tafsir berbahasa Arab:
فَعَصَىٰ فِرۡعَوۡنُ ٱلرَّسُولَ فَأَخَذۡنَٰهُ أَخۡذٗا وَبِيلٗا
Basi Fir’awn akamkanusha Mūsā na asiukubali utume wake, na akakataa amri yake, tukamuangamiza maangamivu makali. Hapa pana onyo la kumuasi Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwa kuogopea isije ikamfika yule aliyeasi mfano wa kile kilichomfika Fir‘awn na watu wake.
Tafsir berbahasa Arab:
فَكَيۡفَ تَتَّقُونَ إِن كَفَرۡتُمۡ يَوۡمٗا يَجۡعَلُ ٱلۡوِلۡدَٰنَ شِيبًا
Vipi mtajikinga nafsi zenu, mkikufuru, na adhabu ya Siku ya Kiyama ambayo huwafanya watoto wadogo watokwe na mvi kwa ukubwa wa janga lake na unguliko lake?
Tafsir berbahasa Arab:
ٱلسَّمَآءُ مُنفَطِرُۢ بِهِۦۚ كَانَ وَعۡدُهُۥ مَفۡعُولًا
Mbingu zitakuwa na pasuko Siku hiyo, kwa ukubwa wa janga lake, hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ya kuwa Siku hiyo itakuja ni yenye kutukia bila shaka.
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّ هَٰذِهِۦ تَذۡكِرَةٞۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلًا
Hakika aya hizi zenye kutisha ambazo ndani yake kuna vigongaji na vikemeaji ni mawaidha na mazingatio kwa watu. Basi mwenye kutaka kuwaidhika na kunufaika nazo, na achukue utiifu na uchamungu kuwa ni njia ya kumfikisha kwenye radhi za Mola wake Aliyemuumba na kumlea.
Tafsir berbahasa Arab:
۞ إِنَّ رَبَّكَ يَعۡلَمُ أَنَّكَ تَقُومُ أَدۡنَىٰ مِن ثُلُثَيِ ٱلَّيۡلِ وَنِصۡفَهُۥ وَثُلُثَهُۥ وَطَآئِفَةٞ مِّنَ ٱلَّذِينَ مَعَكَۚ وَٱللَّهُ يُقَدِّرُ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَۚ عَلِمَ أَن لَّن تُحۡصُوهُ فَتَابَ عَلَيۡكُمۡۖ فَٱقۡرَءُواْ مَا تَيَسَّرَ مِنَ ٱلۡقُرۡءَانِۚ عَلِمَ أَن سَيَكُونُ مِنكُم مَّرۡضَىٰ وَءَاخَرُونَ يَضۡرِبُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ يَبۡتَغُونَ مِن فَضۡلِ ٱللَّهِ وَءَاخَرُونَ يُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۖ فَٱقۡرَءُواْ مَا تَيَسَّرَ مِنۡهُۚ وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَقۡرِضُواْ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنٗاۚ وَمَا تُقَدِّمُواْ لِأَنفُسِكُم مِّنۡ خَيۡرٖ تَجِدُوهُ عِندَ ٱللَّهِ هُوَ خَيۡرٗا وَأَعۡظَمَ أَجۡرٗاۚ وَٱسۡتَغۡفِرُواْ ٱللَّهَۖ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمُۢ
Hakika Mola wako, ewe Mtume, Anajua kuwa wewe unasimama kwa swala ya Tahajudi kipindi cha usiku, wakati mwingine chini ya theluthi mbili za usiku, na wakati mwingine unasimama nusu yake, na wakati mwingine theluthi yake. Na wanasimama pamoja na wewe kundi la Maswahaba wako. Na Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Ndiye Anayekadiria usiku na mchana na Anajua vipimo vyake na kipindi kinachopita na kusalia cha mchana na usiku. Mwenyezi Mungu Anajua kwamba haiwezekani kwenu nyinyi kusimama usiku wote, hivyo basi akawafanyia mambo kuwa mepesi kwenu. Na msome kwenye Swala ya usiku kile kilichokuwa chepesi kwenu kukisoma katika Qur’ani. Mwenyezi Mungu anajua kuwa miongoni mwenu kuna wanaoelemewa na ugonjwa wasiweze kusimama usiku. Na kuna watu wengine wanatembea ardhini kwa biashara na kazi wakitafuata riziki ya Mwenyezi Mungu ya halali. Na kuna watu wengine wanapigana jihadi katika njia ya Mwenye kuliinua neno Lake na kutangaza dini Yake. Basi someni kutoka kwenye Qur’ani kile kilicho chepesi kwenu, na endeleeni kutekeleza faradhi za Swala, na toeni Zaka za lazima kwenu, na toeni sadaka za mali yenu katika njia za wema na hisani kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu. Na chochote kile mnachokifanya miongoni mwa njia za wema na kheri na matendo ya utiifu, mtapata malipo yake na thawabu zake kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama, hali ya kuwa ni bora zaidi kuliko kile mlichokitanguliza duniani na ni chenye thawabu kubwa zaidi. Na mtake msamaha wa Mwenyezi Mungu katika hali zenu zote. Hakika Mwenyezi Mumngu ni Msamehefu sana kwenu ni Mwenye huruma na nyinyi.
Tafsir berbahasa Arab:
 
Terjemahan makna Surah: Surah Al-Muzzammil
Daftar surah Nomor Halaman
 
Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Abdullah Muhammad dan Nasir Khamis - Daftar isi terjemahan

Terjemahan makna Al-Qur`ān Al-Karīm ke bahasa Sawahili oleh Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakar dan Syekh Nasir Khamis

Tutup