Check out the new design

Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Ali Muhsin Al-Barwani * - Daftar isi terjemahan

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Terjemahan makna Surah: Al-Mursalāt   Ayah:
أَلَمۡ نَخۡلُقكُّم مِّن مَّآءٖ مَّهِينٖ
Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa?
Kwani hatukukuumbeni kutokana na maji yaliyo dhalili, nayo ni manii,
Tafsir berbahasa Arab:
فَجَعَلۡنَٰهُ فِي قَرَارٖ مَّكِينٍ
Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti?
Na tukayaweka maji haya katika pahala patulivu,
Tafsir berbahasa Arab:
إِلَىٰ قَدَرٖ مَّعۡلُومٖ
Mpaka muda maalumu?
Mpaka kutimilia kuumbwa kwake na kutengenezwa kwake kwa muda anao ujua Mwenyezi Mungu.
Tafsir berbahasa Arab:
فَقَدَرۡنَا فَنِعۡمَ ٱلۡقَٰدِرُونَ
Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria.
Nasi tukaweka vipimo katika kuumbwa kwake, na kutengenezwa kwake, na kutoka kwake. Basi wabora wa kupima na kukadiria ni Sisi.
Tafsir berbahasa Arab:
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
Ole wao hao wanao kadhibisha neema za kuumba na kukadiria.
Tafsir berbahasa Arab:
أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ كِفَاتًا
Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya
Kwani hatukuifanya ardhi kuwa imekusanya juu ya mgongo wake
Tafsir berbahasa Arab:
أَحۡيَآءٗ وَأَمۡوَٰتٗا
Walio hai na maiti?
Viumbe vilivyo hai visio hisabika, na vilio kufa visio kadirika,
Tafsir berbahasa Arab:
وَجَعَلۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ شَٰمِخَٰتٖ وَأَسۡقَيۡنَٰكُم مَّآءٗ فُرَاتٗا
Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu?
Na tukaweka milima iliyo thibiti imara mirefu, na tukakunywesheni maji matamu?
Tafsir berbahasa Arab:
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
Wataangamia siku hiyo hao wanao kadhibisha neema hizi!
Tafsir berbahasa Arab:
ٱنطَلِقُوٓاْ إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ
Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha!
Siku ya kupambanua wataambiwa makafiri: Nendeni huko Motoni mliko kuwa mkikukanusha.
Tafsir berbahasa Arab:
ٱنطَلِقُوٓاْ إِلَىٰ ظِلّٖ ذِي ثَلَٰثِ شُعَبٖ
Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu!
Nendeni kwenye joto la moshi wa Jahannamu ulio gawika kwa ukubwa wake mapande matatu.
Tafsir berbahasa Arab:
لَّا ظَلِيلٖ وَلَا يُغۡنِي مِنَ ٱللَّهَبِ
Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako.
Hapana cha kujikinga na joto la siku hiyo, wala kivuli hicho hakipunguzi joto la mwako hata kidogo.
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّهَا تَرۡمِي بِشَرَرٖ كَٱلۡقَصۡرِ
Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba!
Moto huo hutupa macheche yenye ukubwa kama majumba,
Tafsir berbahasa Arab:
كَأَنَّهُۥ جِمَٰلَتٞ صُفۡرٞ
Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano!
Au utaona hayo macheche kama ngamia weusi wenye kuingia rangi ya manjano.
Tafsir berbahasa Arab:
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
Wataangamia siku hiyo wanao kanusha kwamba hizi ndizo sifa za Moto.
Tafsir berbahasa Arab:
هَٰذَا يَوۡمُ لَا يَنطِقُونَ
Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu,
Haya uliyo simuliwa yatatokea katika siku ambayo hawatatamka kitu cha kuwanufaisha,
Tafsir berbahasa Arab:
وَلَا يُؤۡذَنُ لَهُمۡ فَيَعۡتَذِرُونَ
Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru.
Wala hawatakuwa na idhini ya kutamka, wala hawatatoa udhuru, kwani hawana udhuru.
Tafsir berbahasa Arab:
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
Wataangamia siku hiyo wanayo ikadhibisha siku hii.
Tafsir berbahasa Arab:
هَٰذَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِۖ جَمَعۡنَٰكُمۡ وَٱلۡأَوَّلِينَ
Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia.
Hii ndiyo siku ya kufafanua baina ya mwenye ukweli, na mwenye uwongo, kwa kuwa kila mmoja atalipwa kwa mujibu wa anavyo stahiki. Enyi mnao mkadhibisha Muhammad! Tumekujaalieni nyinyi na walio kutangulieni walio kadhibisha mfano wenu,
Tafsir berbahasa Arab:
فَإِن كَانَ لَكُمۡ كَيۡدٞ فَكِيدُونِ
kiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi!
Kama mnayo hila ya kujikinga na adhabu basi fanyeni hila hiyo. Basi njooni muepukane na adhabu yangu.
Tafsir berbahasa Arab:
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
Wataangamia siku hiyo wanayo ikadhibisha ahadi ya Mwenyezi Mungu.
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي ظِلَٰلٖ وَعُيُونٖ
Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem,
Hakika wachamngu wenye kujikinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu watakuwa katika kivuli kikubwa, na chemchem zinazo miminika,
Tafsir berbahasa Arab:
وَفَوَٰكِهَ مِمَّا يَشۡتَهُونَ
Na matunda wanayo yapenda,
Na matunda wanayo yaonea ladha, na wanayo yapenda,
Tafsir berbahasa Arab:
كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda.
Wataambiwa kwa kuamkiwa na kukirimiwa: Kuleni na mnywe chakula na vinywaji kwa starehe kwa sababu ya vitendo vyema mlivyo kuwa mkivitenda duniani.
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema.
Hakika Sisi huwalipa mfano wa malipo hayo matukufu watu wema.
Tafsir berbahasa Arab:
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
Wataangamia siku hiyo wanayo ikadhibisha Pepo.
Tafsir berbahasa Arab:
كُلُواْ وَتَمَتَّعُواْ قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجۡرِمُونَ
Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu!
Na makafiri wataambiwa: Kuleni na mjistareheshe kwa starehe isiyo baki muda mrefu, kwani hakika nyinyi ni wakosefu kwa kumshirikisha kwenu Mwenyezi Mungu.
Tafsir berbahasa Arab:
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
Wataangamia siku hiyo wanao ikadhibisha neema.
Tafsir berbahasa Arab:
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱرۡكَعُواْ لَا يَرۡكَعُونَ
Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami.
Na wakiambiwa: Swalini kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na mnyenyekeeni Yeye, hawanyenyekei wala hawaswali; bali hushikilia kiburi chao!
Tafsir berbahasa Arab:
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
Wataangamia siku wanao kadhibisha amri za Mwenyezi Mungu na makatazo yake.
Tafsir berbahasa Arab:
فَبِأَيِّ حَدِيثِۭ بَعۡدَهُۥ يُؤۡمِنُونَ
Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?
Basi maneno gani hawa watayaamini ikiwa hawaiamini Qur'ani, na hali hii ni muujiza ulio toka mbinguni?
Tafsir berbahasa Arab:
 
Terjemahan makna Surah: Al-Mursalāt
Daftar surah Nomor Halaman
 
Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Ali Muhsin Al-Barwani - Daftar isi terjemahan

Diterjemahkan oleh Ali Muhsin Al-Barwani.

Tutup