Check out the new design

Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Ali Muhsin Albirwany * - Indice Traduzioni

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Traduzione dei significati Sura: Ash-Shu‘arâ’   Versetto:
قَالَ وَمَا عِلۡمِي بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Akasema: Nayajuaje waliyo kuwa wakiyafanya?.
Nuhu akasema: Kitu gani cha kunijuvya uchache wa hadhi yao na mali yao? Nikitakacho mimi kwao ni Imani yao bila ya kutafuta kuzijua kazi zao.
Esegesi in lingua araba:
إِنۡ حِسَابُهُمۡ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّيۖ لَوۡ تَشۡعُرُونَ
Hisabu yao haiko ila kwa Mola wao Mlezi, laiti mngeli tambua!.
Hapana wa kuwalipa kwa vitendo vyao na kazi zao ila Mola wangu Mlezi; kwani Yeye ndiye anaye yajua vyema ya undani wao. Kama nyinyi ni watu watambuzi mngeli tambua hayo.
Esegesi in lingua araba:
وَمَآ أَنَا۠ بِطَارِدِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini.
Wala mimi siye wa kuwafukuza watu wanao uamini wito wangu vyovyote itavyo kuwa hali yao ya ufakiri au utajiri, kwa sababu ati ya kukubalieni nyinyi kwa mtakalo ili ndio mpate kuniamini.
Esegesi in lingua araba:
إِنۡ أَنَا۠ إِلَّا نَذِيرٞ مُّبِينٞ
Mimi si cho chote ila ni Mwonyaji wa dhaahiri shaahiri.
Mimi si chochote ila ni Mtume niliye toka kwa Mwenyezi Mungu kuwaonya walio wajibikiwa kwa onyo lilio wazi, kwa ushahidi wa kutenganisha baina ya kweli na uwongo, bila ya farka yoyote baina ya mtukufu na mnyonge. Basi vipi itanifalia mimi kuwafukuza Waumini kwa sababu ya ufakiri wao?
Esegesi in lingua araba:
قَالُواْ لَئِن لَّمۡ تَنتَهِ يَٰنُوحُ لَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمَرۡجُومِينَ
Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe.
Wakasema: Ewe Nuhu! Ikiwa hutoacha huu wito wako basi jua yakini tutakupopoa mawe. Yaani wanakusudia kwa haya kumtishia kumuuwa.
Esegesi in lingua araba:
قَالَ رَبِّ إِنَّ قَوۡمِي كَذَّبُونِ
Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha.
Nuhu kuonyesha kushikilia watu wake kuukadhibisha wito wake, alisema: Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha! Kuthibitisha kuwa wanastahiki maapizo yake.
Esegesi in lingua araba:
فَٱفۡتَحۡ بَيۡنِي وَبَيۡنَهُمۡ فَتۡحٗا وَنَجِّنِي وَمَن مَّعِيَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Basi hukumu baina yangu na wao kwa hukumu yako, na uniokoe mimi na walio pamoja nami, Waumini.
Basi tuhukumie baina yangu na wao, kwa hukumu ya kuwaangamiza wanao pinga Upweke wako, na wakamkadhibisha Mtume wako! Na niokoe mimi na Waumini walio pamoja nami na adhabu ya uasi wao.
Esegesi in lingua araba:
فَأَنجَيۡنَٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ فِي ٱلۡفُلۡكِ ٱلۡمَشۡحُونِ
Kwa hivyo tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye katika marikebu iliyo sheheni.
Ndio hivyo tukamwokoa yeye pamoja na walio amini katika safina iliyo pakia pomoni wao hao pamoja na mahitaji yao, kwa kuitikia dua yake.
Esegesi in lingua araba:
ثُمَّ أَغۡرَقۡنَا بَعۡدُ ٱلۡبَاقِينَ
Kisha tukawazamisha baadaye walio bakia.
Baada ya kuokoka kwa Nuhu na walio amini, Mwenyezi Mungu aliwazamisha walio baki katika kaumu ya Nuhu walio kuwa hawakuamini.
Esegesi in lingua araba:
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
Hakika katika yaliyo simuliwa na Qur'ani juu ya khabari za Nuhu ni hoja ya kuthibitisha ukweli wa Mitume na uwezo wa Mwenyezi Mungu. Na katika watu walio somewa hadithi hizi si wengi walio amini.
Esegesi in lingua araba:
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Kina A'd waliwakanusha Mitume.
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu za kumuadhibu kila jabari mwenye inda, Mwenye kuwaneemesha wachamngu kwa kila namna ya fadhila.
Esegesi in lingua araba:
كَذَّبَتۡ عَادٌ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Kina A'd waliwakanusha Mitume.
Kabila ya A'di ilimkanusha Mtume wao Hud a.s. Na kwa hivyo wakawa ndio wamewakadhibisha Mitume wote, kwa kuwa wito wao ni mmoja katika asli yake na lengo lake.
Esegesi in lingua araba:
إِذۡ قَالَ لَهُمۡ أَخُوهُمۡ هُودٌ أَلَا تَتَّقُونَ
Alipo waambia ndugu yao, Hud: Je! Hamchimngu?
Alipo waambia ndugu yao Hud: Hamumwogopi Mwenyezi Mungu, mkamsafia ibada?
Esegesi in lingua araba:
إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ
Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
Hakika mimi nimetumwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili nikuongoeni mfuate uwongozi, na ni mwenye kuulinda ujumbe wa Mwenyezi Mungu. Naufikisha ujumbe huo kama alivyo niamrisha Mola wangu Mlezi.
Esegesi in lingua araba:
فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini.
Basi ifuateni amri ya Mwenyezi Mungu. Na ikhofuni adhabu yake. Na t'iini ninayo kuamrisheni yanayo toka kwa Mwenyezi Mungu.
Esegesi in lingua araba:
وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Wala sikutakeni juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Wala kwa hii nasaha yangu na uwongozi wangu sitaki kwenu ujira. Sina malipo isipo kuwa kwa Muumba wa viumbe vyote.
Esegesi in lingua araba:
أَتَبۡنُونَ بِكُلِّ رِيعٍ ءَايَةٗ تَعۡبَثُونَ
Je! Mnajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho la kufanyia upuuzi?
Je! Mnasimamisha juu ya kila pahala palipo nyanyuka katika nchi jengo refu kwa ajili ya kujifakhirisha, na mnakutana humo kwa mambo ya upuuzi na fisadi? Mwenyezi Mungu Subhanahu anataka kwa haya kuwazindua watende yatakayo wanufaisha, na anawatahayarisha kwa kuacha kwao Imani na vitendo vyema.
Esegesi in lingua araba:
وَتَتَّخِذُونَ مَصَانِعَ لَعَلَّكُمۡ تَخۡلُدُونَ
Na mnajenga majengo ya fakhari kama kwamba mtaishi milele!
Na mnajenga majumba ya fakhari na imara, na mahodhi ya maji, kwa kutaraji kuishi milele katika dunia hii, kama kwamba hamtakufa.
Esegesi in lingua araba:
وَإِذَا بَطَشۡتُم بَطَشۡتُمۡ جَبَّارِينَ
Na mnapo tumia nguvu mnatumia nguvu kwa ujabari.
Na mnapo ingia kutesa, mnapita kiasi katika uasi na uvamizi wa jeuri, mnauwa, na mnapiga kwa chuki bila ya huruma.
Esegesi in lingua araba:
فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini.
Mwogopeni Mwenyezi Mungu katika kutumia nguvu, Na fuateni amri yangu katika ninayo kuitieni. Kwani hayo hakika ndiyo yatakayo kukufaeni na ndiyo yatakayo dumu zaidi.
Esegesi in lingua araba:
وَٱتَّقُواْ ٱلَّذِيٓ أَمَدَّكُم بِمَا تَعۡلَمُونَ
Na mcheni aliye kupeni haya mnayo yajua.
Na tahadharini na ghadhabu za Mwenyezi Mungu aliye kukunjulieni neema zake, kwa mnayo yajua yaliyo mbele yenu ya vipawa vyake vya namna mbali mbali.
Esegesi in lingua araba:
أَمَدَّكُم بِأَنۡعَٰمٖ وَبَنِينَ
Amekupeni wanyama wa kufuga na wana.
Kama alivyo kupeni mifugo kama ngamia, na ng'ombe, na kondoo, na mbuzi, na wana wenye nguvu, wakukulindieni mifugo yenu, na kukusaidieni katika shida za maisha.
Esegesi in lingua araba:
وَجَنَّٰتٖ وَعُيُونٍ
Na mabustani na chemchem.
Na mabustani yenye matunda, na chemchem zenye kutiririka maji mnayo yahitajia.
Esegesi in lingua araba:
إِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٖ
Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku Kubwa.
Mimi nina khofu asije Mwenyezi Mungu akakuteremshieni adhabu kali hapa duniani, na Akhera akakutieni katika Moto wa Jahannamu kwa sababu ya ujabari wenu na starehe alizo kustarehesheni Mwenyezi Mungu.
Esegesi in lingua araba:
قَالُواْ سَوَآءٌ عَلَيۡنَآ أَوَعَظۡتَ أَمۡ لَمۡ تَكُن مِّنَ ٱلۡوَٰعِظِينَ
Wakasema: Ni mamoja kwetu, ukitupa mawaidha au hukuwa miongoni mwa watoao mawaidha.
Wakasema kwa kumkejeli: Ni sawa kwetu, ukitupa waadhi na kutuonya au ukawa si katika wenye kutoa waadhi.
Esegesi in lingua araba:
 
Traduzione dei significati Sura: Ash-Shu‘arâ’
Indice delle Sure Numero di pagina
 
Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Ali Muhsin Albirwany - Indice Traduzioni

La sua traduzione di Ali Muhsin Albirwany.

Chiudi