Check out the new design

Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Pioneer Translation Center (Ruwwad at-Tarjama) * - Indice Traduzioni


Traduzione dei significati Sura: An-Nisâ’   Versetto:
أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ يَزۡعُمُونَ أَنَّهُمۡ ءَامَنُواْ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبۡلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوٓاْ إِلَى ٱلطَّٰغُوتِ وَقَدۡ أُمِرُوٓاْ أَن يَكۡفُرُواْ بِهِۦۖ وَيُرِيدُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَن يُضِلَّهُمۡ ضَلَٰلَۢا بَعِيدٗا
Je, hukuwaona wale wanaodai kwamba wameamini yale yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako? Wanataka kupeleka kesi yao kwa Twaghut, na ilhali kwa hakika waliamrishwa kwamba wazikufuru! Na anataka Shetani kwamba awapoteze kupotea kwa mbali.
Esegesi in lingua araba:
وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ تَعَالَوۡاْ إِلَىٰ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَإِلَى ٱلرَّسُولِ رَأَيۡتَ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودٗا
Na wanapoambiwa: Njooni kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu na kwa Mtume, utawaona wanafiki wanaepukana na wewe kuepuka kukubwa.
Esegesi in lingua araba:
فَكَيۡفَ إِذَآ أَصَٰبَتۡهُم مُّصِيبَةُۢ بِمَا قَدَّمَتۡ أَيۡدِيهِمۡ ثُمَّ جَآءُوكَ يَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ إِنۡ أَرَدۡنَآ إِلَّآ إِحۡسَٰنٗا وَتَوۡفِيقًا
Basi inakuwa vipi unapowasibu msiba kwa sababu ya yale iliyotanguliza mikono yao? Hapo, wanakujia wakiapa kwa Mwenyezi Mungu wakisema: Hatukutaka isipokuwa wema na mapatano.
Esegesi in lingua araba:
أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ يَعۡلَمُ ٱللَّهُ مَا فِي قُلُوبِهِمۡ فَأَعۡرِضۡ عَنۡهُمۡ وَعِظۡهُمۡ وَقُل لَّهُمۡ فِيٓ أَنفُسِهِمۡ قَوۡلَۢا بَلِيغٗا
Hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu anayajua yaliyo katika nyoyo zao. Basi wapuuze, na uwawaidhi, na uwaambie maneno ya kuathiri na kuingia katika nafsi zao.
Esegesi in lingua araba:
وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا لِيُطَاعَ بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ وَلَوۡ أَنَّهُمۡ إِذ ظَّلَمُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ جَآءُوكَ فَٱسۡتَغۡفَرُواْ ٱللَّهَ وَٱسۡتَغۡفَرَ لَهُمُ ٱلرَّسُولُ لَوَجَدُواْ ٱللَّهَ تَوَّابٗا رَّحِيمٗا
Na hatukumtuma Mtume yeyote isipokuwa atiiwe kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na lau pale walipozidhulumu nafsi zao, wangelikujia, wakamwomba Mwenyezi Mungu kuwafutia dhambi, na Mtume akawaombea kufutiwa dhambi, basi bila ya shaka wangelimkuta Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu.
Esegesi in lingua araba:
فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤۡمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيۡنَهُمۡ ثُمَّ لَا يَجِدُواْ فِيٓ أَنفُسِهِمۡ حَرَجٗا مِّمَّا قَضَيۡتَ وَيُسَلِّمُواْ تَسۡلِيمٗا
Hapana! Ninaapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye mwenye kuhukumu katika yale wanayohitalifiana, kisha wasipate uzito wowote katika nyoyo zao juu ya hukumu utakayotoa, na wajisalimishe kujusalimisha kukamilifu.
Esegesi in lingua araba:
 
Traduzione dei significati Sura: An-Nisâ’
Indice delle Sure Numero di pagina
 
Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Pioneer Translation Center (Ruwwad at-Tarjama) - Indice Traduzioni

Tradotta dal team del centro di traduzione "Pioneers" in collaborazione con "Association for call and awareness of communities" di al-Rabwah e "Association for Service of Islamic Content in Languages".

Chiudi