Check out the new design

Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Pioneer Translation Center (Ruwwad at-Tarjama) * - Indice Traduzioni


Traduzione dei significati Sura: An-Nisâ’   Versetto:
ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۚ لَيَجۡمَعَنَّكُمۡ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ لَا رَيۡبَ فِيهِۗ وَمَنۡ أَصۡدَقُ مِنَ ٱللَّهِ حَدِيثٗا
Mwenyezi Mungu, hapana mungu isipokuwa Yeye. Kwa yakini, atawakusanya Siku ya Qiyama. Halina shaka hilo. Na ni nani mkweli zaidi katika mazungumzo kuliko Mwenyezi Mungu?
Esegesi in lingua araba:
۞ فَمَا لَكُمۡ فِي ٱلۡمُنَٰفِقِينَ فِئَتَيۡنِ وَٱللَّهُ أَرۡكَسَهُم بِمَا كَسَبُوٓاْۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَهۡدُواْ مَنۡ أَضَلَّ ٱللَّهُۖ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَلَن تَجِدَ لَهُۥ سَبِيلٗا
Basi mna nini mmekuwa makundi mawili kuhusiana na (habari ya) wanafiki, na ilhali Mwenyezi Mungu amewageuza kwa sababu ya yale waliyoyachuma? Je, mnataka kumwongoa yule ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza? Na mwenye kupotezwa na Mwenyezi Mungu, basi wewe hutapata njia yoyote kwa ajili yake.
Esegesi in lingua araba:
وَدُّواْ لَوۡ تَكۡفُرُونَ كَمَا كَفَرُواْ فَتَكُونُونَ سَوَآءٗۖ فَلَا تَتَّخِذُواْ مِنۡهُمۡ أَوۡلِيَآءَ حَتَّىٰ يُهَاجِرُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۚ فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَخُذُوهُمۡ وَٱقۡتُلُوهُمۡ حَيۡثُ وَجَدتُّمُوهُمۡۖ وَلَا تَتَّخِذُواْ مِنۡهُمۡ وَلِيّٗا وَلَا نَصِيرًا
Wanapenda lau kuwa mtakufuru kama walivyokufuru wao, ili muwe sawasawa. Basi, msifanye marafiki wandani miongoni mwao mpaka wahame katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka, basi wakamateni, na waueni popote mnapowapata. Wala msifanye miongoni mwao rafiki mwandani wala msaidizi.
Esegesi in lingua araba:
إِلَّا ٱلَّذِينَ يَصِلُونَ إِلَىٰ قَوۡمِۭ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَهُم مِّيثَٰقٌ أَوۡ جَآءُوكُمۡ حَصِرَتۡ صُدُورُهُمۡ أَن يُقَٰتِلُوكُمۡ أَوۡ يُقَٰتِلُواْ قَوۡمَهُمۡۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَسَلَّطَهُمۡ عَلَيۡكُمۡ فَلَقَٰتَلُوكُمۡۚ فَإِنِ ٱعۡتَزَلُوكُمۡ فَلَمۡ يُقَٰتِلُوكُمۡ وَأَلۡقَوۡاْ إِلَيۡكُمُ ٱلسَّلَمَ فَمَا جَعَلَ ٱللَّهُ لَكُمۡ عَلَيۡهِمۡ سَبِيلٗا
Isipokuwa wale waliofungamana na kaumu ambao kuna ahadi baina yenu na wao, au wanawajia hali ya kuwa vifua vyao vina dhiki juu ya kupigana nanyi, au kupigana na kaumu yao. Na lau angelipenda Mwenyezi Mungu, angeliwapa mamlaka juu yenu wangelipigana nanyi. Kwa hivyo, wakijitenga nanyi, na wasipigane nanyi, na wakawaletea amani, basi Mwenyezi Mungu hakuwapa nyinyi njia dhidi yao.
Esegesi in lingua araba:
سَتَجِدُونَ ءَاخَرِينَ يُرِيدُونَ أَن يَأۡمَنُوكُمۡ وَيَأۡمَنُواْ قَوۡمَهُمۡ كُلَّ مَا رُدُّوٓاْ إِلَى ٱلۡفِتۡنَةِ أُرۡكِسُواْ فِيهَاۚ فَإِن لَّمۡ يَعۡتَزِلُوكُمۡ وَيُلۡقُوٓاْ إِلَيۡكُمُ ٱلسَّلَمَ وَيَكُفُّوٓاْ أَيۡدِيَهُمۡ فَخُذُوهُمۡ وَٱقۡتُلُوهُمۡ حَيۡثُ ثَقِفۡتُمُوهُمۡۚ وَأُوْلَٰٓئِكُمۡ جَعَلۡنَا لَكُمۡ عَلَيۡهِمۡ سُلۡطَٰنٗا مُّبِينٗا
Mtawakuta wengine wanataka wapate salama kwenu na salama kwa watu wao. Kila wakirudishwa kwenye fitina, hudidimizwa humo. Na ikiwa hawajitengi nanyi, na wakawaletea salama, na wakaizuia mikono yao, basi wakamateni na waueni popote mnapowakuta. Na hao, tumewapa nyinyi hoja zilizo wazi juu yao.
Esegesi in lingua araba:
 
Traduzione dei significati Sura: An-Nisâ’
Indice delle Sure Numero di pagina
 
Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Pioneer Translation Center (Ruwwad at-Tarjama) - Indice Traduzioni

Tradotta dal team del centro di traduzione "Pioneers" in collaborazione con "Association for call and awareness of communities" di al-Rabwah e "Association for Service of Islamic Content in Languages".

Chiudi