クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - Abdullah Muhammad and Nasir Khamis * - 対訳の目次


対訳 節: (146) 章: 高壁章
سَأَصۡرِفُ عَنۡ ءَايَٰتِيَ ٱلَّذِينَ يَتَكَبَّرُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّ وَإِن يَرَوۡاْ كُلَّ ءَايَةٖ لَّا يُؤۡمِنُواْ بِهَا وَإِن يَرَوۡاْ سَبِيلَ ٱلرُّشۡدِ لَا يَتَّخِذُوهُ سَبِيلٗا وَإِن يَرَوۡاْ سَبِيلَ ٱلۡغَيِّ يَتَّخِذُوهُ سَبِيلٗاۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَكَانُواْ عَنۡهَا غَٰفِلِينَ
Nitazipotoa nyoyo za wenye kufanya kiburi wakaacha kunitii na wenye kuwafanyia watu kiburi pasi na haki zisizielewe hoja na dalili zinazoonesha ukubwa wangu, sheria yangu na hukumu zangu, wawe hawamsikilizi Mtume yoyote kwa kiburi chao. Na wakiona, hawa wenye kuifanyia Imani kiburi, kila alama hawaiyamini, kwa sababu ya kupa mgongo kwao na kupingana kwao na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Wakiiyona njia ya uongofu hawaifanyi ni njia, na wakiiyona njia ya upotevu wanaifanya kuwa ni njia na ni dini. Hayo ni kwa sababu ya kukanusha kwao aya za Mwenyezi Mungu na kughafilika kwao kuziangalia na kuyatia akilini maana yake.
アラビア語 クルアーン注釈:
 
対訳 節: (146) 章: 高壁章
章名の目次 ページ番号
 
クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - Abdullah Muhammad and Nasir Khamis - 対訳の目次

クルアーン・スワヒリ語対訳 - Dr. Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis

閉じる