クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - Abdullah Muhammad and Nasir Khamis * - 対訳の目次


対訳 節: (158) 章: 高壁章
قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنِّي رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُمۡ جَمِيعًا ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۖ فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِ ٱلنَّبِيِّ ٱلۡأُمِّيِّ ٱلَّذِي يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَكَلِمَٰتِهِۦ وَٱتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ
Waambie, ewe Mtume, watu wote, «Mimi ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwenu nyote, si kwa baadhi yenu bila ya wengine, Ambaye ni wake ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake. Haifai kuelekezwa uungu na ibada isipokuwa Kwake, zilizotukuka sifa Zake, Mwenye uwezo wa kupatisha viumbe, kuwaondosha na kuwafufua. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na kubalini upweke Wake, na muaminini Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani imshukiye, Nabii asiyesoma wala kwandika, anayemuamini Mwenyezi Mungu na yale aliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wake na yale waliyoteremshiwa manabii kabla yake; Mfuateni Mtume huyu na jilazimisheni kuyafanya anayowaamrisha kwayo ya kumtii Mwenyezi Mungu kwa kutaraji muafikiwe kufuata njia iliyolingana sawa.»
アラビア語 クルアーン注釈:
 
対訳 節: (158) 章: 高壁章
章名の目次 ページ番号
 
クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - Abdullah Muhammad and Nasir Khamis - 対訳の目次

クルアーン・スワヒリ語対訳 - Dr. Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis

閉じる