クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - Abdullah Muhammad and Nasir Khamis * - 対訳の目次


対訳 節: (37) 章: 高壁章
فَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوۡ كَذَّبَ بِـَٔايَٰتِهِۦٓۚ أُوْلَٰٓئِكَ يَنَالُهُمۡ نَصِيبُهُم مِّنَ ٱلۡكِتَٰبِۖ حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُنَا يَتَوَفَّوۡنَهُمۡ قَالُوٓاْ أَيۡنَ مَا كُنتُمۡ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِۖ قَالُواْ ضَلُّواْ عَنَّا وَشَهِدُواْ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ أَنَّهُمۡ كَانُواْ كَٰفِرِينَ
Hakuna yoyote aliye na udhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, urongo au akazikanusha aya Zake zilizoteremshwa, hao itawafikia sehemu yao ya adhabu waliyoandikiwa katika Al-Lawh( Al-Mhfūd) (Ubao uliohifadhiwa) mpaka atakapowajia Malaika wa mauti pamoja na wasaidizi wake kuzichukua roho zao, watawaambia, «Wako wapi wale mliokuwa mnawaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, kati ya washirika, wategemewa na masanamu, waje wawaokoe na janga lililowafika?» Watasema, «Wametutoroka.» Wakati huo watakiri makosa kwamba wao duniani walikuwa ni wenye kuupinga na kuukanusha upweke wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka.
アラビア語 クルアーン注釈:
 
対訳 節: (37) 章: 高壁章
章名の目次 ページ番号
 
クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - Abdullah Muhammad and Nasir Khamis - 対訳の目次

クルアーン・スワヒリ語対訳 - Dr. Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis

閉じる