クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - Abdullah Muhammad and Nasir Khamis * - 対訳の目次


対訳 節: (107) 章: 悔悟章
وَٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ مَسۡجِدٗا ضِرَارٗا وَكُفۡرٗا وَتَفۡرِيقَۢا بَيۡنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَإِرۡصَادٗا لِّمَنۡ حَارَبَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ مِن قَبۡلُۚ وَلَيَحۡلِفُنَّ إِنۡ أَرَدۡنَآ إِلَّا ٱلۡحُسۡنَىٰۖ وَٱللَّهُ يَشۡهَدُ إِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ
Na wanafiki waliojenga msikiti, kwa kuwadhuru Waumini, kumkanusha Mwenyezi Mungu na kuwagawanya Waumini, ili waswali humo baadhi yao na wauache msikiti wa Qubā’ ambao Waislamu wanaswali ndani yake, ili Waislamu watafautiane na wagawanyike kwa hilo, na kwa ajili ya kumngojea yule aliyempiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kabla ya hapo, naye ni Abū ‘Āmir al-Rāhib aliyeasi, ili pawe ni mahali pa kuwafanyia vitimbi Waislamu. Na wataapa tena wataapa, wanafiki hawa, kwamba wao hawakukusudia kwa kuujenga isipokuwa kuwafanyia wema na kuwahurumia Waislamu na kuwapa nafasi wanyonge wasioweza kwenda msikiti wa Qubā’ .Na Mwenyezi Mungu Anashuhudia kwamba wao ni warongo katika yale wanayoyaapia. Msikiti huo ulivunjwa na ukatiwa moto.
アラビア語 クルアーン注釈:
 
対訳 節: (107) 章: 悔悟章
章名の目次 ページ番号
 
クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - Abdullah Muhammad and Nasir Khamis - 対訳の目次

クルアーン・スワヒリ語対訳 - Dr. Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis

閉じる