クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - Ali Muhsen Alberwany * - 対訳の目次

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

対訳 節: (92) 章: 家畜章
وَهَٰذَا كِتَٰبٌ أَنزَلۡنَٰهُ مُبَارَكٞ مُّصَدِّقُ ٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَلِتُنذِرَ أُمَّ ٱلۡقُرَىٰ وَمَنۡ حَوۡلَهَاۚ وَٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ يُؤۡمِنُونَ بِهِۦۖ وَهُمۡ عَلَىٰ صَلَاتِهِمۡ يُحَافِظُونَ
Na hiki ni Kitabu tulicho kiteremsha, kilicho barikiwa, chenye kuhakikisha yaliyo tangulia, na ili uuwonye Mama wa Miji na walio pembezoni mwake. Na wenye kuamini Akhera wanakiamini hichi, nao wanazihifadhi Sala zao.
Na hii Qur'ani tumeiteremsha - kama tulivyo iteremsha Taurati - ina kheri nyingi, na itabaki mpaka Siku ya Kiyama. Inasadikisha Vitabu vilivyo teremshwa mbele yake, inaeleza khabari ya kuteremkwa kwao, ili iwape bishara Waumini, na iwakhofishe makafiri wa Makka na pembezoni mwake pande zote za dunia juu ya ghababu ya Mwenyezi Mungu, ikiwa hawakuifuata. Na wale wanao isadiki Siku ya malipo, kule kutaraji kwao thawabu na kukhofu adhabu, kunawapelekea kuiamini hii Qur'ani. Na kwa hivyo wao wanahifadhi kutekeleza Swala kwa ukamilifu na utimilivu.
アラビア語 クルアーン注釈:
 
対訳 節: (92) 章: 家畜章
章名の目次 ページ番号
 
クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - Ali Muhsen Alberwany - 対訳の目次

クルアーン・スワヒリ語対訳 - Ali Muhsen Alberwany

閉じる