Check out the new design

クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - ルゥワード翻訳事業センター * - 対訳の目次


対訳 章: 預言者たち章   節:
وَكَمۡ قَصَمۡنَا مِن قَرۡيَةٖ كَانَتۡ ظَالِمَةٗ وَأَنشَأۡنَا بَعۡدَهَا قَوۡمًا ءَاخَرِينَ
Na ni mingapi katika miji iliyokuwa ikidhulumu tumeiteketeza, na tukawasimamisha baada yao kaumu wengine.
アラビア語 クルアーン注釈:
فَلَمَّآ أَحَسُّواْ بَأۡسَنَآ إِذَا هُم مِّنۡهَا يَرۡكُضُونَ
Basi walipoihisi adhabu yetu, tazama, wakaanza kuikimbia.
アラビア語 クルアーン注釈:
لَا تَرۡكُضُواْ وَٱرۡجِعُوٓاْ إِلَىٰ مَآ أُتۡرِفۡتُمۡ فِيهِ وَمَسَٰكِنِكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تُسۡـَٔلُونَ
Msikimbie! Na rejeeni kwenye yale yale mliyostareheshwa kwayo, na maskani zenu, ili mpate kuulizwa!
アラビア語 クルアーン注釈:
قَالُواْ يَٰوَيۡلَنَآ إِنَّا كُنَّا ظَٰلِمِينَ
Wakasema: Ole wetu! Hakika sisi tulikuwa madhalimu.
アラビア語 クルアーン注釈:
فَمَا زَالَت تِّلۡكَ دَعۡوَىٰهُمۡ حَتَّىٰ جَعَلۡنَٰهُمۡ حَصِيدًا خَٰمِدِينَ
Basi hakikuacha hicho kuwa ndicho kilio chao mpaka tukawafanya kama waliofyekwa, wamezimika.
アラビア語 クルアーン注釈:
وَمَا خَلَقۡنَا ٱلسَّمَآءَ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا لَٰعِبِينَ
Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyo baina ya hivyo kwa mchezo.
アラビア語 クルアーン注釈:
لَوۡ أَرَدۡنَآ أَن نَّتَّخِذَ لَهۡوٗا لَّٱتَّخَذۡنَٰهُ مِن لَّدُنَّآ إِن كُنَّا فَٰعِلِينَ
Kama tungelitaka kufanya pumbao, tungejifanyia Sisi wenyewe, lau kwamba tungelikuwa ni wafanyao hivyo.
アラビア語 クルアーン注釈:
بَلۡ نَقۡذِفُ بِٱلۡحَقِّ عَلَى ٱلۡبَٰطِلِ فَيَدۡمَغُهُۥ فَإِذَا هُوَ زَاهِقٞۚ وَلَكُمُ ٱلۡوَيۡلُ مِمَّا تَصِفُونَ
Bali tunaitupa haki juu ya batili, ikaivunja na mara ikatoweka. Na ole wenu kwa mnayoyazua.
アラビア語 クルアーン注釈:
وَلَهُۥ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَمَنۡ عِندَهُۥ لَا يَسۡتَكۡبِرُونَ عَنۡ عِبَادَتِهِۦ وَلَا يَسۡتَحۡسِرُونَ
Na ni vyake Yeye tu vilivyomo mbinguni na katika ardhi. Na wale walioko kwake hawafanyi kiburi wakaacha kumuabudu, wala hawachoki.
アラビア語 クルアーン注釈:
يُسَبِّحُونَ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَ لَا يَفۡتُرُونَ
Wanamtakasa usiku na mchana, wala hawanyong'onyei.
アラビア語 クルアーン注釈:
أَمِ ٱتَّخَذُوٓاْ ءَالِهَةٗ مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ هُمۡ يُنشِرُونَ
Au wamejifanyia miungu katika ardhi inayofufua?
アラビア語 クルアーン注釈:
لَوۡ كَانَ فِيهِمَآ ءَالِهَةٌ إِلَّا ٱللَّهُ لَفَسَدَتَاۚ فَسُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ رَبِّ ٱلۡعَرۡشِ عَمَّا يَصِفُونَ
Lau wangelikuwamo humo miungu wengine isipokuwa Mwenyezi Mungu, basi bila ya shaka hizo mbingu na ardhi zingelihaliribika. Subahanallah (Ametakasika Mwenyezi Mungu), Bwana wa 'Arshi (Kiti cha Enzi) kutokana na hayo wanayoyazua.
アラビア語 クルアーン注釈:
لَا يُسۡـَٔلُ عَمَّا يَفۡعَلُ وَهُمۡ يُسۡـَٔلُونَ
Yeye haulizwi kwa ayatendayo, na wao ndio wanaoulizwa kwa wayatendayo.
アラビア語 クルアーン注釈:
أَمِ ٱتَّخَذُواْ مِن دُونِهِۦٓ ءَالِهَةٗۖ قُلۡ هَاتُواْ بُرۡهَٰنَكُمۡۖ هَٰذَا ذِكۡرُ مَن مَّعِيَ وَذِكۡرُ مَن قَبۡلِيۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ ٱلۡحَقَّۖ فَهُم مُّعۡرِضُونَ
Au wamejifanyia miungu mingine badala yake? Sema: Leteni ushahidi wenu! Haya ni ukumbusho wa hawa walio pamoja nami, na ukumbusho wa walio kabla yangu. Lakini wengi wao hawaijui haki, na kwa hivyo wanapeana mgongo.
アラビア語 クルアーン注釈:
 
対訳 章: 預言者たち章
章名の目次 ページ番号
 
クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - ルゥワード翻訳事業センター - 対訳の目次

ルゥワード翻訳事業センターとラブワ招待協会およびイスラームコンテンツサービス協会の共訳

閉じる