បកប្រែអត្ថន័យគម្ពីរគួរអាន - បកប្រែជាភាសាស្វាហ៊ីលី - អាប់ទុលឡោះ មូហាំម៉ាត់ និង ណាសៀរ ខមីស

12 : 60

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ إِذَا جَآءَكَ ٱلۡمُؤۡمِنَٰتُ يُبَايِعۡنَكَ عَلَىٰٓ أَن لَّا يُشۡرِكۡنَ بِٱللَّهِ شَيۡـٔٗا وَلَا يَسۡرِقۡنَ وَلَا يَزۡنِينَ وَلَا يَقۡتُلۡنَ أَوۡلَٰدَهُنَّ وَلَا يَأۡتِينَ بِبُهۡتَٰنٖ يَفۡتَرِينَهُۥ بَيۡنَ أَيۡدِيهِنَّ وَأَرۡجُلِهِنَّ وَلَا يَعۡصِينَكَ فِي مَعۡرُوفٖ فَبَايِعۡهُنَّ وَٱسۡتَغۡفِرۡ لَهُنَّ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Ewe Nabii! Wakiwajia wanawake wenye kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na kuwaahidi kuwa hawatamshirikisha Allah Mtukufu katika kumuabudu, wala hawataiba chochote, wala hawatazini, wala hawataua watoto wao baada ya kuzaliwa au kabla yake, wala hawatawanasibishia waume zao watoto wasiotokana na wao, wala hawataenda kinyume na wewe katika jema unalowaamrisha kwalo, basi waahidi kwa hayo na uwaombee msamaha kutoka kwa Allah Mtukufu. Hakika Allah Mtukufu ni Mwenye kusamehe dhambi za waja Wake wenye kutubia, na ni Mwenye kuwarehemu. info
التفاسير: |
prev

Al-Mumtahanah

next
:
0:00 0:00