Check out the new design

ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី * - សន្ទស្សន៍នៃការបកប្រែ

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

ការបកប្រែអត្ថន័យ ជំពូក​: អាល់ហុិជរ៍   អាយ៉ាត់:
إِذۡ دَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَقَالُواْ سَلَٰمٗا قَالَ إِنَّا مِنكُمۡ وَجِلُونَ
Walipo ingia kwake na wakasema: Salama! Yeye akasema: Hakika sisi tunakuogopeni. [52]
[52] Ewe Muaminifu! Watajie pale walipo ingia kwake, naye akawaogopa. Wao wakamwambia: Amani kwako, na tulia! Yeye akasema: Sisi tunakuogopeni, kwani mmetujia kwa ghafla, sio wakati wa dasturi wa kufika wageni, na hatujui mna nini!
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قَالُواْ لَا تَوۡجَلۡ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَٰمٍ عَلِيمٖ
Wakasema: Usiogope. Sisi tunakubashiria kijana mwenye ujuzi. [53]
[53] Wakasema: Usiogope, na tuwa moyo! Kwani tunakubashiria mwana, ambaye Mwenyezi Mungu Mtukufu atampa siku zijazo za uhai wake ilimu kubwa. Inaonyesha hapa kuwa bishara hii si ya Ismail a.s. Kwani Ismail alikuwa kesha zaliwa, naye na mama yake Haajir walikuwa wapo Makka. Bishara hii ni ya Ibrahim na mkewe, basi kwa hivyo ni ya Is-haq mwana wa Ibrahim na Sara.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قَالَ أَبَشَّرۡتُمُونِي عَلَىٰٓ أَن مَّسَّنِيَ ٱلۡكِبَرُ فَبِمَ تُبَشِّرُونَ
Akasema: Mnanibashiria nami uzee umenishika! Basi kwa njia gani mnanibashiria? [54]
[54] Akasema: Vipi mnanibashiria mtoto na hali mimi nimekwisha patikana na udhaifu wa ukongwe. Kwa njia gani, basi, mnanibashiria jambo hili la ajabu?
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قَالُواْ بَشَّرۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ فَلَا تَكُن مِّنَ ٱلۡقَٰنِطِينَ
Wakasema: Tunakubashiria kwa haki; basi usiwe miongoni mwa wanaokata tamaa. [55]
[55] Wakasema: Sisi tunakubashiria jambo lilio thibiti, ambalo halina shaka kabisa. Basi usiwe katika wanao kata tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قَالَ وَمَن يَقۡنَطُ مِن رَّحۡمَةِ رَبِّهِۦٓ إِلَّا ٱلضَّآلُّونَ
Akasema: Na nani anaye kata tamaa na rehema ya Mola wake Mlezi ila wale walio potea? [56]
[56] Ibrahim akasema: Mimi sikati tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Kwani hawakati tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu ila walio potea wasio utambua utukufu wake na uwezo wake.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قَالَ فَمَا خَطۡبُكُمۡ أَيُّهَا ٱلۡمُرۡسَلُونَ
Akasema: Hebu nini amri yenu, enyi wajumbe? [57]
[57] Alivyo kuwa kaanza kuzoeana nao, alisema: Ikiwa mmenibashiria khabari hii nzuri, je mna jambo gani jenginelo mlilo nalo baada ya haya, enyi wajumbe mlio tumwa na Mwenyezi Mungu?
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قَالُوٓاْ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمٖ مُّجۡرِمِينَ
Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya wakosefu! [58]
[58] Wakasema hakika sisi tumetumwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa watu walio fanya ukhalifu katika Haki ya Mwenyezi Mungu na haki ya Nabii wao, na haki ya nafsi zao wenyewe. Ukhalifu ndio mtindo wao. Watu wenyewe ni kaumu ya Luut'i. Basi tutawateketeza.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
إِلَّآ ءَالَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمۡ أَجۡمَعِينَ
Isipo kuwa walio mfuata Luut'i. Bila ya shaka sisi tutawaokoa hao wote. [59]
[59] Wala hakusalimika na huo ukhalifu na adhabu yake ila ahli zake yeye Luut'i. Basi hao Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuamrisha tuwaokoe wote.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
إِلَّا ٱمۡرَأَتَهُۥ قَدَّرۡنَآ إِنَّهَا لَمِنَ ٱلۡغَٰبِرِينَ
Ila mkewe. Tunakadiria huyo atakuwa miongoni watao bakia nyuma. [60]
[60] Na hatoangamia katika ahli zake ila mkewe, kwani yeye hakumfuata mumewe, bali yu pamoja na hao wakosefu ambao wanao stahiki adhabu.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
فَلَمَّا جَآءَ ءَالَ لُوطٍ ٱلۡمُرۡسَلُونَ
Basi wale wajumbe walipo fika kwa Luut'i, [61]
[61] Wale Malaika walio tumwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kuteremsha yaliyo ahidiwa, walipo fika nchi ya Luut'i na watu wake,
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قَالَ إِنَّكُمۡ قَوۡمٞ مُّنكَرُونَ
Alisema (Luut'i): Hakika nyinyi ni watu msio juulikana. [62]
[62] Luut'i aliwaambia: Watu nyinyi sikujueni, na nafsi yangu inatishika nanyi. Naogopa msituletee balaa.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قَالُواْ بَلۡ جِئۡنَٰكَ بِمَا كَانُواْ فِيهِ يَمۡتَرُونَ
Wakasema: Bali sisi tumekuletea yale waliyo kuwa wakiyafanyia shaka. [63]
[63] Wakasema: Usituogope, kwani hatukukujia kwa unalo liogopa, bali tumekujia kwa jambo la kukufurahisha, nalo ni kuwateremshia adhabu hawa watu wako walio kukadhibisha na wakawa wanaitilia shaka hiyo adhabu au wanaikanya.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَأَتَيۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ وَإِنَّا لَصَٰدِقُونَ
Na tumefika kwako kwa Haki, na hakika sisi tunasema kweli. [64]
[64] Nasi tumekujia kwa amri iliyo thaabiti isiyo na shaka, nayo ni kuiteremsha adhabu. Na kutimiza ahadi ni katika sifa yetu, kwa amri ya Mwenyezi Mungu.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
فَأَسۡرِ بِأَهۡلِكَ بِقِطۡعٖ مِّنَ ٱلَّيۡلِ وَٱتَّبِعۡ أَدۡبَٰرَهُمۡ وَلَا يَلۡتَفِتۡ مِنكُمۡ أَحَدٞ وَٱمۡضُواْ حَيۡثُ تُؤۡمَرُونَ
Basi ondoka na ahli zako usiku ungalipo, nawe ufuate nyuma yao,wala yeyote kati yenu asigeuke nyuma. Na mwende mnapo amrishwa. [65]
[65] Ilivyo kuwa adhabu itawateremkia, basi wewe na ahli zako mlio andikiwa kuokoka, tokeni baada ya kwisha ingia usiku.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَقَضَيۡنَآ إِلَيۡهِ ذَٰلِكَ ٱلۡأَمۡرَ أَنَّ دَابِرَ هَٰٓؤُلَآءِ مَقۡطُوعٞ مُّصۡبِحِينَ
Na tukamfunulia hukumu hiyo, ya kwamba hata wa mwisho wao hao ikifika asubuhi atakuwa kesha katiliwa mbali. [66]
[66] Na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la alimfunulia Luut'i kwa kumwambia: Sisi tumewahukumia na kuwakadiria wakosefu kuteketea. Watang'olewa itapoingia asubuhi, wala hatobaki hata mmoja wao.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَجَآءَ أَهۡلُ ٱلۡمَدِينَةِ يَسۡتَبۡشِرُونَ
Na wakaja watu wa mji ule nao furahani. [67]
[67] Asubuhi kulipo pambazuka waliwaona Malaika kwa sura ya binaadamu wazuri. Wao wale wakawafurahia, wakaja ili wafanye nao vitendo vyao viovu, vya kuwaingilia wanaume.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قَالَ إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ ضَيۡفِي فَلَا تَفۡضَحُونِ
Akasema: (Luut'i) Hakika hawa wageni wangu, basi msinifedheheshe. [68]
[68] Luut'i akaogopa wasije wakatenda vitendo vyao viovu. Akasema: Hawa ni wageni wangu, basi msinifedheheshe kwa vitendo vyenu vibaya.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلَا تُخۡزُونِ
Na mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi. [69]
[69] Na mwogopeni Mwenyezi Mungu Mtukufu! Msifanye uchafu wenu, mkanipatisha hizaya na madhila mbele yao!
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قَالُوٓاْ أَوَلَمۡ نَنۡهَكَ عَنِ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Wakasema: Sisi hatukukukataza usimkaribishe yeyote? [70]
[70] Wale wakhalifu wakasema: Kwani si tulikukataza wewe usimkaribishe mtu yeyote, na hivi sasa tena unatuzuia tusifanye nao tunayo yatamani?
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
 
ការបកប្រែអត្ថន័យ ជំពូក​: អាល់ហុិជរ៍
សន្ទស្សន៍នៃជំពូក លេខ​ទំព័រ
 
ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី - សន្ទស្សន៍នៃការបកប្រែ

បកប្រែដោយលោកអាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

បិទ