Wala msifanye viapo vyenu ni njia ya kudanganyana baina yenu.Usije mguu ukateleza badala ya kuthibiti, na mkaonja maovu kwa sababu ya kule kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu, na mkapata adhabu kubwa. [94]
[94] Wala msishike njia ya khiana, mkafanya viapo ndio njia ya udanganyifu na khadaa. Kwa hivyo nyayo zenu zitateleza mlikosee lengo lilio sawa, na kwa hivyo ikapelekea mkaiwacha Njia ya Mwenyezi Mungu ya kutimiza ahadi, na mkawa ni mfano muovu wa khiana, na watu wakaja waona kuwa Waislamu ni watu wabaya, na wakautupilia mbali Uislamu wenyewe. Na uovu ukateremka duniani kwa sababu yenu kwa kuto kuaminini kwa vile mnavyo kwenda kinyume na njia ya haki, nanyi ikakuteremkieni adhabu kali yenye kutia machungu.
Wala msinunue ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa thamani ndogo. Hakika kilichoko kwa Mwenyezi Mungu ndicho bora kwenu, ikiwa mnajua. [95]
[95] Wala msibadilishe ahadi ya kweli kweli kwa kutaka pato la dunia, na hilo ni duni na lingali onekana kubwa. Maana yaliopo kwa Mwenyezi Mungu, malipo ya wanao hifadhi ahadi zao duniani, na malipo ya Akhera ya milele, ni bora kwenu kuliko yote yanayo kudanganyeni kwa kuvunja ahadi. Basi zingatieni na mfahamu, ikiwa nyinyi ni watu wa ilimu na utambuzi baina ya jema na lisio kuwa jema. Wala msitende ila lilio na maslaha kwenu duniani na Akhera.
Mlivyo navyo vitakwisha na vilivyoko kwa Mwenyezi Mungu ndivyo vitakavyo bakia. Na kwa yakini Sisi tutawapa walio subiri ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda. [96]
[96] Kwani neema mlizo nazo zina mwisho hata zingeli kaa muda mrefu. Na neema zilioko kwa Mwenyezi Mungu Akhera ni za milele wala hazishi. Na Sisi tutawalipa wenye kuvumilia mashaka ya taabu kwa ajili ya tuliyo waahidi, nayo ni kupata bora ya malipo marudufu kwa vitendo vyao, waneemeke kwayo daima milele Akhera.
Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini,tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda. [97]
[97] Hakika mwenye kutenda mema duniani, sawa sawa akiwa mwanamume au mwanamke, akajiingiza katika huo wema kwa nguvu za imani, kwa kila linalo wajibika kwa kuliamini, basi Sisi hatuna budi kumfanya aishi maisha mazuri yasiyo kuwa na machungu, yenye ndani yake ukinaifu na kuridhika na kuvumilia masaibu ya dunia, na shukrani kwa neema anazo zipata kwa Mwenyezi Mungu. Na Akhera hapana budi ya kuwa tutawalipa watu wa namna hii bora ya malipo kwa kuzidi marudufu kwa vitendo vyao vya duniani.
Na ukisoma Qur'ani mwombe Mwenyezi Mungu akulinde na Shetani maluuni. [98]
[98] Kinacho linda nafsi isighurike na pumbao ni Qur'ani. Ewe Muumini! Ukitaka kuishi maisha ya mbali na kuchezewa na Shetani, na upate wema wa kote kuwili, duniani na Akhera, basi Mimi nakuongoza kwenye jambo litakalo kusaidia kwa hayo. Jambo lenyewe ni kuisoma Qur'ani. Na unapo taka kusoma Qur'ani, anzia kwa kumuomba Mwenyezi Mungu kwa ikhlasi akuepushe na wasiwasi wa Shetani, aliye fukuzwa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu, na anaona uzuri kuwaghuri watu awaingize katika kumuasi Mwenyezi Mungu.
Hakika yeye hana madaraka juu ya walio amini na wakamtegemea Mola wao Mlezi. [99]
[99] Ukifanya haya kwa kumsafia niya Mwenyezi Mungu, basi atakulinda na Shetani, na atakuondolea wasiwasi. Kwani Shetani hana athari kwa walio jaa Imani ya Mwenyezi Mungu, na wakamtaka msaada na kumtegemea Yeye peke yake.
Hakika madaraka yake ni juu ya wanao mfanya rafiki yao, na wale wanao fanya ushirika naye. [100]
[100] Bali taathira yake Shetani na khatari yake ni juu ya wale ambao nyoyo zao hazina mfungamano wala mapenzi na Mwenyezi Mungu. Basi hao hawana la kuwalinda na athari za Shetani. Watamfuata huyo kama rafiki anavyo mfuata rafiki yake, mpaka watumbukie katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika kumuabudu pamoja na miungu mingine isiyo weza kuleta madhara wala manufaa.
Na tunapo badilisha Ishara pahala pa Ishara nyengine, na MwenyeziMungu anajua anayo teremsha, wao husema: Wewe ni mzushi. Bali wengi wao hawajui kitu. [101]
[101] Na tukikuletea muujiza badala ya muujiza ulio sawa na tulio waletea Manabii walio tangulia, na tukakuletea wewe hii Qur'ani kuwa ni muujiza wenyewe, wanakusingizia kuwa umeizua tu hii, na kwamba unamzulia Mwenyezi Mungu uwongo! Na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mjuzi kwa ujuzi usio pikuliwa kuijua miujiza anayo wateremshia Manabii wake. Lakini wengi wao watu hawa si watu wa ilimu wa kujua lilio kweli.
Sema: Ameiteremsha hii Roho takatifu kutokana na Mola wako Mlezi kwa haki, ili awathibitishe wale walio amini, na kuwa ni uwongofu, na ni bishara kwa Waislamu. [102]
[102] Ewe Nabii! Waambie kuwabainishia muujiza wako: Hakika hii Qur'ani kaniteremshia mimi Jibril, Roho safi, kutokana kwa Mola wangu Mlezi, kwa kufuatana na kukusanya Haki, ili kwayo azitie imara nyoyo za Waumini, na ili iwe ni Uwongofu kwa watu wote waongokewe, na iwape bishara njema ya neema Waislamu wote.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
លទ្ធផលស្វែងរក:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".