Check out the new design

ಪವಿತ್ರ ಕುರ್‌ಆನ್ ಅರ್ಥಾನುವಾದ - ಸ್ವಾಹಿಲಿ ಅನುವಾದ - ರುವ್ವಾದ್ ಅನುವಾದ ಕೇಂದ್ರ * - ಅನುವಾದಗಳ ವಿಷಯಸೂಚಿ


ಅರ್ಥಗಳ ಅನುವಾದ ಅಧ್ಯಾಯ: ಅನ್ನಿಸಾಅ್   ಶ್ಲೋಕ:
لِّلرِّجَالِ نَصِيبٞ مِّمَّا تَرَكَ ٱلۡوَٰلِدَانِ وَٱلۡأَقۡرَبُونَ وَلِلنِّسَآءِ نَصِيبٞ مِّمَّا تَرَكَ ٱلۡوَٰلِدَانِ وَٱلۡأَقۡرَبُونَ مِمَّا قَلَّ مِنۡهُ أَوۡ كَثُرَۚ نَصِيبٗا مَّفۡرُوضٗا
Wanaume wana fungu katika yale wanayoyaacha wazazi na jamaa wa karibu. Na wanawake wanalo fungu katika yale waliyoyaacha wazazi na jamaa wa karibu. Kwa kile kilicho kidogo chake au kingi. Ni mafungu yaliyofaradhiwa.[1]
[1] Waarabu wakati wa Jahiliyya kwa sababu ya ukatili wao na ugumu wao walikuwa hawawarithishi wanyonge kama vile wanawake na watoto. Na walikuwa wakiwagawia urithi wanaume wenye nguvu tu. Kwa sababu walikuwa wakidai kuwa wao tu ndio wanaoweza vita, na kunyang’anya, na kupora.
ಅರಬ್ಬಿ ವ್ಯಾಖ್ಯಾನಗಳು:
وَإِذَا حَضَرَ ٱلۡقِسۡمَةَ أُوْلُواْ ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينُ فَٱرۡزُقُوهُم مِّنۡهُ وَقُولُواْ لَهُمۡ قَوۡلٗا مَّعۡرُوفٗا
Na wakihudhuria ugawi jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini, basi wapeni kwayo (yani mali ya urithi), na waambieni kauli njema.
ಅರಬ್ಬಿ ವ್ಯಾಖ್ಯಾನಗಳು:
وَلۡيَخۡشَ ٱلَّذِينَ لَوۡ تَرَكُواْ مِنۡ خَلۡفِهِمۡ ذُرِّيَّةٗ ضِعَٰفًا خَافُواْ عَلَيۡهِمۡ فَلۡيَتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلۡيَقُولُواْ قَوۡلٗا سَدِيدًا
Na wachelee wale ambao lau kuwa na wao wangeliacha nyuma yao dhuria wanyonge, wangeliwahofia. Basi nao wamche Mwenyezi Mungu, na waseme kauli iliyo sawa.
ಅರಬ್ಬಿ ವ್ಯಾಖ್ಯಾನಗಳು:
إِنَّ ٱلَّذِينَ يَأۡكُلُونَ أَمۡوَٰلَ ٱلۡيَتَٰمَىٰ ظُلۡمًا إِنَّمَا يَأۡكُلُونَ فِي بُطُونِهِمۡ نَارٗاۖ وَسَيَصۡلَوۡنَ سَعِيرٗا
Hakika, wale wanaokula mali za mayatima kwa dhuluma, hapana shaka yoyote wanakula matumboni mwao moto. Na wataingia Moto wenye Mwako mkali.
ಅರಬ್ಬಿ ವ್ಯಾಖ್ಯಾನಗಳು:
يُوصِيكُمُ ٱللَّهُ فِيٓ أَوۡلَٰدِكُمۡۖ لِلذَّكَرِ مِثۡلُ حَظِّ ٱلۡأُنثَيَيۡنِۚ فَإِن كُنَّ نِسَآءٗ فَوۡقَ ٱثۡنَتَيۡنِ فَلَهُنَّ ثُلُثَا مَا تَرَكَۖ وَإِن كَانَتۡ وَٰحِدَةٗ فَلَهَا ٱلنِّصۡفُۚ وَلِأَبَوَيۡهِ لِكُلِّ وَٰحِدٖ مِّنۡهُمَا ٱلسُّدُسُ مِمَّا تَرَكَ إِن كَانَ لَهُۥ وَلَدٞۚ فَإِن لَّمۡ يَكُن لَّهُۥ وَلَدٞ وَوَرِثَهُۥٓ أَبَوَاهُ فَلِأُمِّهِ ٱلثُّلُثُۚ فَإِن كَانَ لَهُۥٓ إِخۡوَةٞ فَلِأُمِّهِ ٱلسُّدُسُۚ مِنۢ بَعۡدِ وَصِيَّةٖ يُوصِي بِهَآ أَوۡ دَيۡنٍۗ ءَابَآؤُكُمۡ وَأَبۡنَآؤُكُمۡ لَا تَدۡرُونَ أَيُّهُمۡ أَقۡرَبُ لَكُمۡ نَفۡعٗاۚ فَرِيضَةٗ مِّنَ ٱللَّهِۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمٗا
Mwenyezi Mungu anawausia juu ya watoto wenu: Fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili. Na wakiwa ni wanawake zaidi ya wawili, basi wana theluthi mbili za alichokiacha maiti. Lakini akiwa mtoto mwanamke ni mmoja, basi fungu lake ni nusu. Na kwa wazazi wake wawili, kila mmoja wao apate sudusi moja katika kile alichokiacha, ikiwa ana mtoto. Na akiwa hana mtoto, na wazazi wake wawili wakawa wanamrithi, basi mama yake atapata theluthi moja. Na akiwa ana ndugu, basi mama yake atapata sudusi. Haya ni baada ya kutolewa alichousia au kulipa deni. Baba zenu na watoto wenu, nyinyi hamjui ni nani kati yao aliyekaribu zaidi kwenu kwa manufaa. Hiyo ni Sharia iliyotoka kwa Mwenyezi Mungu. Bila ya shaka, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima.[1]
[1] Kiliekwa kiwango cha mwanamke kuwa ni nusu ya kiwango anachokirithi mwanamume kwa sababu mwanamke hutoshelezwa na jamii, au mumewe. Naye mwanamume huwa amejukumishwa kumlea mwanamke katika maisha. (Uadilifu wa Mirathi ndani ya Usilamu cha Mnaswab Abdulrahman)
ಅರಬ್ಬಿ ವ್ಯಾಖ್ಯಾನಗಳು:
 
ಅರ್ಥಗಳ ಅನುವಾದ ಅಧ್ಯಾಯ: ಅನ್ನಿಸಾಅ್
ಅಧ್ಯಾಯಗಳ ವಿಷಯಸೂಚಿ ಪುಟ ಸಂಖ್ಯೆ
 
ಪವಿತ್ರ ಕುರ್‌ಆನ್ ಅರ್ಥಾನುವಾದ - ಸ್ವಾಹಿಲಿ ಅನುವಾದ - ರುವ್ವಾದ್ ಅನುವಾದ ಕೇಂದ್ರ - ಅನುವಾದಗಳ ವಿಷಯಸೂಚಿ

ರಬ್ವಾಹ್ನಲ್ಲಿರುವ ದಾವಾ ಸಂಸ್ಥೆ ಮತ್ತು ಭಾಷೆಗಳಲ್ಲಿ ಇಸ್ಲಾಮಿಕ್ ವಿಷಯವನ್ನು ಸೇವಿಸುವ ಸಂಸ್ಥೆಯ ಸಹಕಾರದೊಂದಿಗೆ ರುವ್ವಾದ್ ಅನುವಾದ ಕೇಂದ್ರದ ತಂಡದಿಂದ ಅನುವಾದಿಸಲಾಗಿದೆ.

ಮುಚ್ಚಿ