next

Al-Fil

prev

1 : 105

أَلَمۡ تَرَ كَيۡفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصۡحَٰبِ ٱلۡفِيلِ

Je hujui na hukusikia, (ewe Mtume), namna Alivyowafanya Mola wako watu wa ndovu: Abraha Mhebeshi na jeshi lake ambalo alikuja nalo ili kuivunja Al ka‘ba tukufu? info
التفاسير: |

2 : 105

أَلَمۡ يَجۡعَلۡ كَيۡدَهُمۡ فِي تَضۡلِيلٖ

Kwani hakuifanya mipango yao mibaya waliyoifanya ni yenye kuvunjika na kupita patupu? info
التفاسير: |

3 : 105

وَأَرۡسَلَ عَلَيۡهِمۡ طَيۡرًا أَبَابِيلَ

Na Aliwapelekea makundi ya ndege yaliyofuatana. info
التفاسير: |

4 : 105

تَرۡمِيهِم بِحِجَارَةٖ مِّن سِجِّيلٖ

Ndege hao walikua wakiwatupia vijiwe vya udongo mkavu na mgumu. info
التفاسير: |

5 : 105

فَجَعَلَهُمۡ كَعَصۡفٖ مَّأۡكُولِۭ

Vijiwe hivyo vikawapondaponda, wakawa ni kama majani makavu yaliyoliwa na wanyama na kisha kutupwa. info
التفاسير: |
next

Al-Fil

prev
:
0:00 0:00