Puslapio numeris:close

5 : 63

وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ تَعَالَوۡاْ يَسۡتَغۡفِرۡ لَكُمۡ رَسُولُ ٱللَّهِ لَوَّوۡاْ رُءُوسَهُمۡ وَرَأَيۡتَهُمۡ يَصُدُّونَ وَهُم مُّسۡتَكۡبِرُونَ

Na wanapoambiwa hawa wanafiki, Njooni huku hali ya kutubia mtake msamaha kwa hayo yaliyotokea kwenu ya maneno maovu na mazungumzo ya ufedhuli, ili Mtume awaombee kwa Allah Mtukufu msamaha wa dhambi zenu, huvigeuza vichwa vyao na wakavitikisa kwa njia ya shere na kiburi. Na utawaona, (ewe Mtume), wanakupa mgongo na huku wanalifanyia kiburi jambo la kufuata yale ambayo walitakiwa wayafuate. info
التفاسير: |

6 : 63

سَوَآءٌ عَلَيۡهِمۡ أَسۡتَغۡفَرۡتَ لَهُمۡ أَمۡ لَمۡ تَسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ لَن يَغۡفِرَ ٱللَّهُ لَهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡفَٰسِقِينَ

Hakuna tafauti kwa wanafiki hawa, uwaombee msamaha kutoka kwa Allah Mtukufu, (ewe Mtume), au usiwaombee, kwani Allah Mtukufu Hatazisamehe dhambi zao, kwa sababu ya kuendelea kwao na uasi na kujikita kwenye ukafiri. Hakika Allah Mtukufu Hawaelekezi kwenye Imani watu wanaomkanusha, waliotoka nje ya utiifu Kwake. info
التفاسير: |

7 : 63

هُمُ ٱلَّذِينَ يَقُولُونَ لَا تُنفِقُواْ عَلَىٰ مَنۡ عِندَ رَسُولِ ٱللَّهِ حَتَّىٰ يَنفَضُّواْۗ وَلِلَّهِ خَزَآئِنُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلَٰكِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ لَا يَفۡقَهُونَ

Wanafiki hawa ndio wanaosema kuwaambia watu wa Madina, «Msitoe kuwasaidia Maswahaba wa Mtume wa Allah Mtukufu waliohama mpaka wajiepushe naye.» Ni za Allah Mtukufu, Peke Yake, hazina za mbinguni na ardhini na vilivyomo humo miongoni mwa riziki, Humpa Anayemtaka na Humnyima Anayemtaka, lakini wanafiki hawaelewi kwamba riziki inatoka kwa Allah Mtukufu kwa ujinga wao wa kutomjua, kutakasika na kila upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake. info
التفاسير: |

8 : 63

يَقُولُونَ لَئِن رَّجَعۡنَآ إِلَى ٱلۡمَدِينَةِ لَيُخۡرِجَنَّ ٱلۡأَعَزُّ مِنۡهَا ٱلۡأَذَلَّۚ وَلِلَّهِ ٱلۡعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِۦ وَلِلۡمُؤۡمِنِينَ وَلَٰكِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ لَا يَعۡلَمُونَ

Wanasema hawa wanafiki, «Tutakaporudi Madina, kundi letu lenye nguvu zaidi litalitoa kundi la Waumini lililo Nyonge zaidi.» Kwa hakika, nguvu na ushindi ni vya Allah Mtukufu, Aliyetukuka, ni vya Mtume Wake, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na ni vya wenye kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake, si vya wale wasiokuwa wao, lakini wanafiki hawalijui hilo kwa ujinga wao uliokita mizizi. info
التفاسير: |

9 : 63

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تُلۡهِكُمۡ أَمۡوَٰلُكُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُكُمۡ عَن ذِكۡرِ ٱللَّهِۚ وَمَن يَفۡعَلۡ ذَٰلِكَ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo! zisiwashughulishe mali zenu wala watoto wenu na kumuabudu Allah Mtukufu na kumtii. Na yoyote atakayeshughulishwa na mali Yake na watoto Wake na hilo la kumuabudu Allah Mtukufu, basi hao ndio waliopunjwa hisa zao za kukurubishwa kwa Allah Mtukufu na kupata rehema zake. info
التفاسير: |

10 : 63

وَأَنفِقُواْ مِن مَّا رَزَقۡنَٰكُم مِّن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَ أَحَدَكُمُ ٱلۡمَوۡتُ فَيَقُولَ رَبِّ لَوۡلَآ أَخَّرۡتَنِيٓ إِلَىٰٓ أَجَلٖ قَرِيبٖ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن مِّنَ ٱلصَّٰلِحِينَ

Na toeni, (enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake), sehemu ya kile tulichowapa katika njia za kheri, mkilikimbilia hilo kabla ya kifo hakijamjia mmoja wenu na kuziona dalili zake na alama zake, na hapo aseme kwa kujuta, «Mola wangu! Si unipe muda na uahirishe kifo changu kipindi kifupi! Nipate kutoa sadaka sehemu ya mali yangu na niwe miongoni mwa watu wema wachamungu?» info
التفاسير: |

11 : 63

وَلَن يُؤَخِّرَ ٱللَّهُ نَفۡسًا إِذَا جَآءَ أَجَلُهَاۚ وَٱللَّهُ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ

Na wala Allah Mtukufu hataichelewesha nafsi yoyote utakapokuja wakati wa kifo chake na umri wake kukoma. Na Allah Mtukufu, kutakasika na kila sifa ya upungufu ni Kwake, ni mtambuzi wa yale mnayoyatenda: mema na mabaya, na Atawalipa kwa hayo. info
التفاسير: |
prev

Al-Munafiqun

next
:
0:00 0:00