prev

Al-Munafiqun

next

1 : 63

إِذَا جَآءَكَ ٱلۡمُنَٰفِقُونَ قَالُواْ نَشۡهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ إِنَّكَ لَرَسُولُهُۥ وَٱللَّهُ يَشۡهَدُ إِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ لَكَٰذِبُونَ

Wanapohudhuria wanafiki kwenye kikao chako, (ewe Mtume), husema kwa ndimi zao, Tunakubali kuwa wewe ni Mtume wa Allah Mtukufu, na Allah Mtukufu Anajua kuwa wewe ni mtume wake, na Allah Mtukufu Anashuhudia kwamba wanafiki ni warongo katika ushahidi wao kwako walioudhihirisha na wakauapia kwa ndimi zao na huku wameuficha ukanushaji wao. info
التفاسير: |

2 : 63

ٱتَّخَذُوٓاْ أَيۡمَٰنَهُمۡ جُنَّةٗ فَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِۚ إِنَّهُمۡ سَآءَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Ukweli ni kwamba wanafiki wamevifanya viapo vyao wanavyoviapa ni kinga na ngao ya kuwakinga wasihukumiwe na kuadhibiwa, na wamejizuia wenyewe na kuwazuia watu na njia ya Allah Mtukufu iliyonyooka. Kwa kweli wao, ni maovu mno yale waliokuwa wakiyafanya. info
التفاسير: |

3 : 63

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ ءَامَنُواْ ثُمَّ كَفَرُواْ فَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَفۡقَهُونَ

Hilo ni kwa kuwa wao wameamini kijuujuu kisha kindanindani wamekufuru. Ndipo Allah Mtukufu Akapiga mhuri juu ya nyoyo zao kwa ukafiri wao, hivyo basi hawayaelewi yale yenye maslahi kwao. info
التفاسير: |

4 : 63

۞ وَإِذَا رَأَيۡتَهُمۡ تُعۡجِبُكَ أَجۡسَامُهُمۡۖ وَإِن يَقُولُواْ تَسۡمَعۡ لِقَوۡلِهِمۡۖ كَأَنَّهُمۡ خُشُبٞ مُّسَنَّدَةٞۖ يَحۡسَبُونَ كُلَّ صَيۡحَةٍ عَلَيۡهِمۡۚ هُمُ ٱلۡعَدُوُّ فَٱحۡذَرۡهُمۡۚ قَٰتَلَهُمُ ٱللَّهُۖ أَنَّىٰ يُؤۡفَكُونَ

Na unapowatazama wanafiki hawa, yanakufurahisha maumbile yao na mandhari yao, na wanapozungumza unayasikiliza mazungumzo yao kwa ufasaha wa ndimi zao, na hali wao kutokana na utupu wa nyoyo zao kuwa hazina Imani na akili zao kuwa hazina fahamu wala elimu yenye manufaa, ni kama vigogo vilivyotegemezwa kwenye ukuta, visivyokuwa na uhai, wanadhania kila sauti ya ukelele inawashukia wao na ina madhara kwao, kwa kujua kwao uhakika wa hali yao na uoga wao mwingi na hofu iliyojikita nyoyoni mwao. Wao ndio maadui wa kikwelikweli wenye uadui mwingi kwako na kwa Waumini. Basi jihadhari nao, Allah Mtukufu Amewadhalilisha wao na Amewatoa kwenye rehema zake. Basi ni vipi wanaiepuka haki na wanaelekea kwenye yale ambayo wamo ndani yake ya unafiki na upotevu? info
التفاسير: |
prev

Al-Munafiqun

next
:
0:00 0:00