Kilniojo Korano reikšmių vertimas - Suahilių k. vertimas - Ali Muchsen Al-Beruany * - Vertimų turinys

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Reikšmių vertimas Sūra: Sūra Al-Burūdž   Aja (Korano eilutė):

Surat Al-Buruj

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلۡبُرُوجِ
Naapa kwa mbingu yenye Buruji!
Naapa kwa mbingu yenye Buruj au Manaazil, njia au vituo ambavyo nyota hupitia katika nyendo zake, Buruuj au Manaazil ndio huu mkusanyiko wa nyota unao onekana kwa sura namna mbali mbali mbinguni. Hizo Buruuj zimegawika sehemu kumi na mbili ambazo ardhi inazipitia inapo lizunguka jua.
Tafsyrai arabų kalba:
وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡمَوۡعُودِ
Na kwa siku iliyo ahidiwa!
Na kwa Siku iliyo ahidiwa kuwa ndiyo Siku ya Hisabu na Malipo,
Tafsyrai arabų kalba:
وَشَاهِدٖ وَمَشۡهُودٖ
Na kwa shahidi na kinacho shuhudiwa!
Na kwa viumbe watao hudhuria Siku hiyo wakaona vitisho na ajabu zitakazo kuwepo,
Tafsyrai arabų kalba:
قُتِلَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأُخۡدُودِ
Wameangamizwa watu wa makhandaki.
Hakika Mwenyezi Mungu amewalaani watu walio chimba khandaki katika ardhi,
Tafsyrai arabų kalba:
ٱلنَّارِ ذَاتِ ٱلۡوَقُودِ
Yenye moto wenye kuni nyingi!
Wakawasha moto kuwatumbukiza ndani yake Waumini ili kuwatesa,
Tafsyrai arabų kalba:
إِذۡ هُمۡ عَلَيۡهَا قُعُودٞ
Walipo kuwa wamekaa hapo!
Na wao wamekaa ukingoni mwake wakishuhudia mateso yanayo wapata Waumini.
Tafsyrai arabų kalba:
وَهُمۡ عَلَىٰ مَا يَفۡعَلُونَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ شُهُودٞ
Na wao ni mashahidi wa yale waliyo kuwa wakiwafanyia Waumini.
Na wao wapo hapo wamehudhuria kwenye mateso wanayo watendea Waumini.
Tafsyrai arabų kalba:
وَمَا نَقَمُواْ مِنۡهُمۡ إِلَّآ أَن يُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ
Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa!
Na hapana walilo lichukia kwa hao Waumini ila ni kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu ambaye adhabu yake huogopwa, Msifiwa anaye tarajiwa thawabu zake.
Tafsyrai arabų kalba:
ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدٌ
Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni shaahidi wa kila kitu.
Ambaye, peke yake, ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni shahidi anashuhudia yote wayatendayo Waumini na makafiri na atawalipa kwayo.
Tafsyrai arabų kalba:
إِنَّ ٱلَّذِينَ فَتَنُواْ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ ثُمَّ لَمۡ يَتُوبُواْ فَلَهُمۡ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمۡ عَذَابُ ٱلۡحَرِيقِ
Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.
Hakika walio watia matatani Waumini wanaume na Waumini wanawake kwa maudhi na kuwaadhibu kwa moto, kisha wasitubu na kurejea nyuma watapata Akhera adhabu ya Jahannamu kwa ukafiri wao, na watapata adhabu ya kuunguzwa kwa kule kuwaunguza moto Waumini.
Tafsyrai arabų kalba:
إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمۡ جَنَّٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡكَبِيرُ
Hakika walio amini na wakatenda mema watapata Bustani zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
Hakika hao walio kusanya kwenye Imani ya Mwenyezi Mungu vitendo vyema watapata Mabustani yapitayo mito kati yake. Neema hiyo waliyo lipwa ni kufuzu kukubwa.
Tafsyrai arabų kalba:
إِنَّ بَطۡشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ
Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali.
Hakika mshiko wa Mola wako Mlezi kuwashika majabari umefika ukomo kwa ukali wake
Tafsyrai arabų kalba:
إِنَّهُۥ هُوَ يُبۡدِئُ وَيُعِيدُ
Yeye ndiye anaye anzisha na ndiye anaye rejeza tena,
Ni Yeye peke yake ndiye Mwenye kuanza kuumba, na kisha ni Yeye anaye rejeza tena,
Tafsyrai arabų kalba:
وَهُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلۡوَدُودُ
Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi,
Na Yeye ni Mwingi wa msamaha kwa mwenye kutubu na akarejea, na Mwingi wa mapenzi kwa mwenye kumpenda na akamt'ii.
Tafsyrai arabų kalba:
ذُو ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡمَجِيدُ
Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu,
Yeye ndiye Mwenye Kiti cha Enzi na Mwenye kukimiliki, na Mkuu kwa dhati yake na sifa zake.
Tafsyrai arabų kalba:
فَعَّالٞ لِّمَا يُرِيدُ
Atendaye ayatakayo.
Ni Mtendaji kwa alitakalo, na hendi kinyume na uweza wake yeyote anaye taka.
Tafsyrai arabų kalba:
هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلۡجُنُودِ
Je! Zimekuwasilia khabari za majeshi?
Je! Imekujia, ewe Muhammad, hadithi ya kile kikundi kilicho a'si katika mataifa yaliyo kwisha pita?
Tafsyrai arabų kalba:
فِرۡعَوۡنَ وَثَمُودَ
Ya Firauni na Thamudi?
Kaumu ya Firauni na Thamudi na yaliyo washukia katika malipo ya kushikilia kwao upotovu?
Tafsyrai arabų kalba:
بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فِي تَكۡذِيبٖ
Lakini walio kufuru wamo katika kukadhibisha.
Bali hao makafiri katika kaumu yako ni shadidi zaidi katika kukukadhibisha kuliko hawa walivyo wakadhibisha Mitume wao.
Tafsyrai arabų kalba:
وَٱللَّهُ مِن وَرَآئِهِم مُّحِيطُۢ
Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazunguka.
Na Mwenyezi Mungu anawaweza hao, na anawajua vilivyo.
Tafsyrai arabų kalba:
بَلۡ هُوَ قُرۡءَانٞ مَّجِيدٞ
Bali hii ni Qur'ani tukufu
Bali hii ulio waletea ni Qur'ani tukufu inadhihirisha hoja za ukweli wako.
Tafsyrai arabų kalba:
فِي لَوۡحٖ مَّحۡفُوظِۭ
Katika Ubao Ulio Hifadhiwa.
Imo katika Ubao Ulio Hifadhiwa, hapana uwezo unao weza kuipotoa au kuigeuza
Tafsyrai arabų kalba:
 
Reikšmių vertimas Sūra: Sūra Al-Burūdž
Sūrų turinys Puslapio numeris
 
Kilniojo Korano reikšmių vertimas - Suahilių k. vertimas - Ali Muchsen Al-Beruany - Vertimų turinys

Kilniojo Korano reikšmių vertimas į suahilių k., išvertė Ali Muchsin Al-Birvany.

Uždaryti