വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - അബ്ദുല്ലാഹ് മുഹമ്മദ് & നാസ്വിർ ഖമീസ്.

പേജ് നമ്പർ:close

23 : 43

وَكَذَٰلِكَ مَآ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ فِي قَرۡيَةٖ مِّن نَّذِيرٍ إِلَّا قَالَ مُتۡرَفُوهَآ إِنَّا وَجَدۡنَآ ءَابَآءَنَا عَلَىٰٓ أُمَّةٖ وَإِنَّا عَلَىٰٓ ءَاثَٰرِهِم مُّقۡتَدُونَ

Hivyo ndivyo ilivyo, hatukutuma kabla yako, ewe Mtume, muonyaji yoyote kwenye kijiji chochote, mwenye kuwaonya na adhabu yetu kwa kutukanusha, na akawaonya na kuwatahadharisha na adhabu yetu, isipokuwa wale ambao ziliwatia kiburi neema miongoni mwa viongozi, na wakubwa huwa wakisema, ”Sisi tuliwakuta baba zetu kwenye mila na dini, na sisi ni wenye kufuata mwenendo wao na njia yao.” info
التفاسير: |

24 : 43

۞ قَٰلَ أَوَلَوۡ جِئۡتُكُم بِأَهۡدَىٰ مِمَّا وَجَدتُّمۡ عَلَيۡهِ ءَابَآءَكُمۡۖ قَالُوٓاْ إِنَّا بِمَآ أُرۡسِلۡتُم بِهِۦ كَٰفِرُونَ

Huyo Muonyaji, akiwa ni Mtume Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na wale Mitume waliomtangulia, huwa akisema kuwaambia waliompinga wakitumia udanganyifu huu uliotenguka, «Je, mtawafuata baba zenu, hata kama mimi nimewajia kutoka kwa Mola wenu na kitu chenye kuongoza zaidi kwenye njia ya haki, na chenye kuonyesha zaidi njia ya uongofu kuliko kile mlichowakuta baba zenu wakikifuata cha dini na mila?” Na wao huwa wakisema kwa ushindani, ”Sisi ni wenye kuyapinga na kuyakanusha hayo mliyotumwa nayo”» info
التفاسير: |

25 : 43

فَٱنتَقَمۡنَا مِنۡهُمۡۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُكَذِّبِينَ

Basi tukawalipizia hao (ummah) waliowakanusha Mitume wao kwa kuwateremshia mateso ya kuwadidimiza, kuwazamisha na mengineyo. Basi angalia, ulikuwa vipi mwisho wa mambo yao walipozikanusha hoja za Allah Mtukufu na mitume wake? Basi na wajihadhari watu wako wasiendelee kwenye ukanushaji wao ili yasiwapate wao yale yaliyowapata wale. info
التفاسير: |

26 : 43

وَإِذۡ قَالَ إِبۡرَٰهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوۡمِهِۦٓ إِنَّنِي بَرَآءٞ مِّمَّا تَعۡبُدُونَ

Kumbuka, ewe Mtume, pindi aliposema Ibrāhĩm alipomwambia baba yake na watu wake waliokuwa wakiabudu vitu ambavyo watu wako, ewe mtume, wanaviabudu, ”Hakika mimi najitakasa na vile mnavyoviabudu badala ya Allah Mtukufu. info
التفاسير: |

27 : 43

إِلَّا ٱلَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُۥ سَيَهۡدِينِ

Isipokuwa Yule Aliyeniumba, kwani Yeye Ataniafikia kufuata njia ya uongofu. info
التفاسير: |

28 : 43

وَجَعَلَهَا كَلِمَةَۢ بَاقِيَةٗ فِي عَقِبِهِۦ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ

Na Ibrāhĩm, amani imshukie, alilifanya neno la kumpwekesha Allah Mtukufu (Lā ilāha illā Allāh) ni lenye kusalia baada yake, kwa kutarajiwa warudi kumtii Mola wao na kumpwekesha. Na kutubia kutokana na ukanushaji wao na dhambi zao. info
التفاسير: |

29 : 43

بَلۡ مَتَّعۡتُ هَٰٓؤُلَآءِ وَءَابَآءَهُمۡ حَتَّىٰ جَآءَهُمُ ٱلۡحَقُّ وَرَسُولٞ مُّبِينٞ

Bali niliwastarehesha hawa washirikina wa watu wako, ewe mtume, na wazazi wao kabla yao kwa uhai, sikuwaharakishia adhabu kwa ukanushaji wao mpaka ikawajia Qur’ani na Mtume wa kuwabainishia wanachokihitajia katika mambo ya Dini yao. info
التفاسير: |

30 : 43

وَلَمَّا جَآءَهُمُ ٱلۡحَقُّ قَالُواْ هَٰذَا سِحۡرٞ وَإِنَّا بِهِۦ كَٰفِرُونَ

Na ilipowajia Qur’ani kutoka kwa Allah Mtukufu walisema, «Hii uliyotuletea ni uchawi wa kuturogea nao, na si wahyi unaotoka kwa Allah Mtukufu, na sisi tunaukanusha». info
التفاسير: |

31 : 43

وَقَالُواْ لَوۡلَا نُزِّلَ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانُ عَلَىٰ رَجُلٖ مِّنَ ٱلۡقَرۡيَتَيۡنِ عَظِيمٍ

Na hawa washirikina wa kikureishi walisema, Iwapo hii Qur’ani inatoka kwa Allah Mtukufu kikweli, basi si ateremshiwe mtu mkubwa (mwenye cheo) kutoka miji hii miwili: (Makkah au Ţāif.) info
التفاسير: |

32 : 43

أَهُمۡ يَقۡسِمُونَ رَحۡمَتَ رَبِّكَۚ نَحۡنُ قَسَمۡنَا بَيۡنَهُم مَّعِيشَتَهُمۡ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۚ وَرَفَعۡنَا بَعۡضَهُمۡ فَوۡقَ بَعۡضٖ دَرَجَٰتٖ لِّيَتَّخِذَ بَعۡضُهُم بَعۡضٗا سُخۡرِيّٗاۗ وَرَحۡمَتُ رَبِّكَ خَيۡرٞ مِّمَّا يَجۡمَعُونَ

Je, wao ndio wanaougawa huu utume wakauweka wanapotaka? Sisi tumewagawia wao maisha yao katika uhai wao wa kilimwengu ya riziki na vyakula, na tumewainua daraja baadhi yao juu ya wengine : huyu ni tajiri na huyu ni masikini, huyu ana nguvu na huyu ni mnyonge, ili baadhi yao wawe ni wenye kutumiwa na wengine katika maisha. Na rehema ya Mola wako, (ewe Mtume), ya kuwatia wao Peponi ni bora kuliko takataka za dunia zenye kutoweka. info
التفاسير: |

33 : 43

وَلَوۡلَآ أَن يَكُونَ ٱلنَّاسُ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ لَّجَعَلۡنَا لِمَن يَكۡفُرُ بِٱلرَّحۡمَٰنِ لِبُيُوتِهِمۡ سُقُفٗا مِّن فِضَّةٖ وَمَعَارِجَ عَلَيۡهَا يَظۡهَرُونَ

Na lau si kuwa watu wangejumuika pamoja kwenye ukafiri, tungefanya nyumba za wale wenye kumkanusha Mwingi wa Rehema ziwe na ghorofa za fedha na ngazi za kupandia. info
التفاسير: |
prev

Az-Zukhruf

next
:
0:00 0:00