Na tutawaonjesha adhabu khafifu kabla ya adhabu kubwa, huenda labda watarejea.
Na tunaapa: Hapana shaka tutawaonjesha duniani adhabu duni kabla hawajaifikia hiyo adhabu kubwa kabisa, nayo ni kudumu milele katika Moto. Huenda pengine watakao adhibiwa kwa hiyo adhabu duni watatubia, waache ukafiri wao.
Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye kumbushwa kwa Ishara za Mola wake Mlezi, kisha akazikataa? Hakika Sisi tutajilipiza kwa wakosefu.
Na hapana mtu yeyote aliye zidi udhaalimu kuidhulumu Haki na kuidhulumu nafsi yake, kuliko mtu anaye kumbushwa kwa Ishara za Mwenyezi Mungu na hoja zilizo wazi, kisha akaacha kuziamini juu ya kuwa ni wazi dhaahiri. Hakika Sisi tutajilipizia juu ya kila mkosefu!
Hakika Sisi tulikwisha mpa Musa Kitabu. Basi usiwe na shaka kuwa kakipokea. Na tukakifanya kuwa ni uwongofu kwa Wana wa Israili.
Na Sisi tulikwisha mpa Musa Taurati. Basi usiwe na shaka na kupokea kwa Musa Kitabu hicho. Na tumekijaalia Kitabu alicho teremshiwa Musa kiwe ni uwongofu kwa Wana wa Israili.
Na tukawafanya miongoni mwao waongozi wanao ongoa watu kwa amri yetu, walipo subiri na wakawa na yakini na Ishara zetu.
Na kutokana na Wana wa Israili tumejaalia wawepo Maimamu, waongozi, wa Dini, wasimame kuwaongoa watu, kwa kuitikia amri yetu kwa vile walivyo vumilia kuyatenda yaliomo katika Taurati, na wakawa wanazisadiki Ishara zetu ukomo wa kusadiki.
Je! Haijawabainikia kwamba kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao, nao wanapita katika maskani zao hizo? Hakika katika hayo zipo Ishara. Basi, je, hawasikii?
Je! Kwani Mwenyezi Mungu aliwaacha walio wakadhibisha Mitume wao, na hakuwabainishia kwamba Yeye aliwahilikisha wengi katika kaumu zilizo watangulia, na wao wanapita kwenye majumba yao, na wanatembea kwenye maskani zao? Hakika katika hayo pana mawaidha ya kuwaonyesha Haki. Wao wameingiwa na uziwi, hawasikii mawaidha haya.
Je! Hawaoni ya kwamba tunayapeleka maji kwenye ardhi kavu, kisha kwayo tunaitoa mimea wanayo kula wanyama wao na wao wenyewe? Je! Hawaoni?
Wameingia upofu, na wala hawaoni ya kwamba hakika Sisi tunapeleka mvua na mito kwenye ardhi za ukame ambazo hazimei mimea, na tukaziotesha mazao yake, wakala wanyama wao, na wao wenyewe wakala nafaka zake na matunda yake? Wamepofuka, na kwa hivyo hawazioni dalili za Mwenyezi Mungu za kuwafufua wafu.
Wanasema: Ushindi huu ni lini, kama mnasema kweli?
Na washirikina wanakwambia wewe na Waumini: Wakati gani Mwenyezi Mungu atakufungulieni mpate ushindi? Twambieni wakati wake ikiwa nyinyi ni wasema kweli.
Sema: Siku ya Ushindi, wale walio kufuru imani yao haitawafaa kitu, wala wao hawatapewa muhula.
Waambie: Siku ya hukumu na kufafanua ikikufikilieni, walio kufuru haitowafaa kitu imani yao, wala hawatapewa muhula hata chembe ya hiyo adhabu wanayo istahiki.
Na ikiwa kufanya maskhara kama hivi ndio mtindo wao, basi wapuuzilie mbali. Na wewe ngojea ukweli aliyo kuahidi Mola wako Mlezi juu yao, kwani wao wanakungojea ushindwe.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
සෙවීමේ ප්රතිඵල:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".