prev

Al-Mu'minun

next

1 : 23

قَدۡ أَفۡلَحَ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ

Kwa hakika wamefaulu wenye kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake, wenye kuzitumia sheria Zake. info
التفاسير: |

2 : 23

ٱلَّذِينَ هُمۡ فِي صَلَاتِهِمۡ خَٰشِعُونَ

Wale ambao miongoni mwa sifa zao ni kwamba wao ni wanyenyekevu kwenye Swala zao, nyoyo zinajishughulisha na hiyo Swala tu na viungo vyao vimetulia kwayo. info
التفاسير: |

3 : 23

وَٱلَّذِينَ هُمۡ عَنِ ٱللَّغۡوِ مُعۡرِضُونَ

Na wale ambao wanaacha kila lisilo na wema ndani yake, la maneno na la vitendo. info
التفاسير: |

4 : 23

وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِلزَّكَوٰةِ فَٰعِلُونَ

Na wale ambao wanazitakasa nafsi zao na mali zao kwa kutoa Zaka za aina mbalimbali za mali zao. info
التفاسير: |

5 : 23

وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِفُرُوجِهِمۡ حَٰفِظُونَ

Na wale ambao wanazihifadhi tupu zao kwa kuziepusha na mambo aliyoyaharamisha Allah Mtukufu ya uzinifu, ulawiti na machafu mengine. info
التفاسير: |

6 : 23

إِلَّا عَلَىٰٓ أَزۡوَٰجِهِمۡ أَوۡ مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُهُمۡ فَإِنَّهُمۡ غَيۡرُ مَلُومِينَ

Isipokuwa kwa wake zao au wajakazi waliomilikiwa na mikono yao ya kulia. Hao, Waumini hawana lawama wala makosa kuwaingilia na kujistarehesha nao, kwa kuwa Allah Mtukufu Amewahalalishia. info
التفاسير: |

7 : 23

فَمَنِ ٱبۡتَغَىٰ وَرَآءَ ذَٰلِكَ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡعَادُونَ

Basi mwenye kutaka kujistarehesha na asiyekuwa mkewe au mjakazi wake, huyo ni miongoni mwa wenye kuikiuka halali na kuijia haramu na atakuwa amejiorodhesha nafsi yake kwenye mateso ya Allah Mtukufu na hasira Zake. info
التفاسير: |

8 : 23

وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِأَمَٰنَٰتِهِمۡ وَعَهۡدِهِمۡ رَٰعُونَ

Na wale ambao wanavitunza vitu vyote walivyoaminiwa navyo na wanatekeleza ahadi zao zote. info
التفاسير: |

9 : 23

وَٱلَّذِينَ هُمۡ عَلَىٰ صَلَوَٰتِهِمۡ يُحَافِظُونَ

Na wale ambao daima wanazitekeleza Swala zao kwa nyakati zake na kwa namna iliyowekwa na Sheria iliyokuja kutoka kwa Nabii, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie. info
التفاسير: |

10 : 23

أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡوَٰرِثُونَ

Hao ndio Waumini wenye kuirithi Pepo. info
التفاسير: |

11 : 23

ٱلَّذِينَ يَرِثُونَ ٱلۡفِرۡدَوۡسَ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Ambao watairithi Pepo ya juu kabisa na ya kati na kati, nayo ndiyo yenye mashukio bora zaidi kuliko zote, wao humo watakaa milele, neema zao hazitakatika wala hazitaondoka. info
التفاسير: |

12 : 23

وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ مِن سُلَٰلَةٖ مِّن طِينٖ

Na kwa hakika tulimuumba Ādam kutokana na udongo uliochukuliwa kutoka ardhi yote. info
التفاسير: |

13 : 23

ثُمَّ جَعَلۡنَٰهُ نُطۡفَةٗ فِي قَرَارٖ مَّكِينٖ

Kisha tukawaumba watoto wake wakiwa ni wenye kuzaana kutokana na tone la maji: nalo ni manii ya wanaume, yanatoka kwenye migongo yao na yanatulia ndani ya vizazi vya wanawake. info
التفاسير: |

14 : 23

ثُمَّ خَلَقۡنَا ٱلنُّطۡفَةَ عَلَقَةٗ فَخَلَقۡنَا ٱلۡعَلَقَةَ مُضۡغَةٗ فَخَلَقۡنَا ٱلۡمُضۡغَةَ عِظَٰمٗا فَكَسَوۡنَا ٱلۡعِظَٰمَ لَحۡمٗا ثُمَّ أَنشَأۡنَٰهُ خَلۡقًا ءَاخَرَۚ فَتَبَارَكَ ٱللَّهُ أَحۡسَنُ ٱلۡخَٰلِقِينَ

Kisha tukaliumba hilo tone kwa kuligeuza kulifanya pande la damu iliyo nyekundu, kisha tukaliumba pande la damu kwa kuligeuza kulifanya kinofu cha nyama kadiri ya kutafunika baada ya siku arubaini, na tukakiumba kinofu cha nyama kilicho laini kwa kukigeuza kukifanya mifupa, na tukaivisha nyama ile mifupa, kisha tukamfanya ni kiumbe kingine kwa kupuliza roho ndani yake. Ametukuka Allah Mtukufu Mwenye kheri nyingi Ambaye Ametengeneza umbo la kila kitu. info
التفاسير: |

15 : 23

ثُمَّ إِنَّكُم بَعۡدَ ذَٰلِكَ لَمَيِّتُونَ

Kisha nyinyi, enyi binadamu, baada ya vipindi vya maisha na umri kukoma, mtakufa. info
التفاسير: |

16 : 23

ثُمَّ إِنَّكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ تُبۡعَثُونَ

Kisha nyinyi, baada ya kufa na dunia kumalizika, mtafufuliwa mkiwa hai kutoka makaburini mwenu muhesabiwe na mlipwe. info
التفاسير: |

17 : 23

وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا فَوۡقَكُمۡ سَبۡعَ طَرَآئِقَ وَمَا كُنَّا عَنِ ٱلۡخَلۡقِ غَٰفِلِينَ

Kwa hakika tuliziumba juu yenu mbingu saba, moja juu ya nyingine, na hatukuwa tumeghafilika na viumbe, hatughafiliki na kiumbe wala hatumsahau. info
التفاسير: |
prev

Al-Mu'minun

next
:
0:00 0:00