prev

Fatir

next

1 : 35

ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ فَاطِرِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ جَاعِلِ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ رُسُلًا أُوْلِيٓ أَجۡنِحَةٖ مَّثۡنَىٰ وَثُلَٰثَ وَرُبَٰعَۚ يَزِيدُ فِي ٱلۡخَلۡقِ مَا يَشَآءُۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Sifa njema zote asifiwe Allah Mtukufu kwa sifa Zake ambazo zote ni za ukamilifu, na kwa neema Zake za nje na za ndani, za Akhera na duniani. Muumba mbingu na ardhi na Muanzilishi wa hizo. Mwenye kuwafanya Malaika ni wajumbe kwa waja kwa Anayemtaka miongoni mwa waja Wake, na kwa amri Yake anayoitaka na makatazo Yake. Na miongoni mwa ukubwa wa uwezo wa Allah Mtukufu ni kuwafanya Malaika ni wenye mbawa, mbilimibili, tatutatu na nnenne, za kurukia: ili kukifikisha Alichoamrisha Allah Mtukufu. Katika uumbaji Wake Anaongeza Anachotaka. Hakika Allah Mtukufu kwa kila jambo ni Mjuzi, hakuna kitu kinachomshinda. info
التفاسير: |

2 : 35

مَّا يَفۡتَحِ ٱللَّهُ لِلنَّاسِ مِن رَّحۡمَةٖ فَلَا مُمۡسِكَ لَهَاۖ وَمَا يُمۡسِكۡ فَلَا مُرۡسِلَ لَهُۥ مِنۢ بَعۡدِهِۦۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Chochote kile Anachowafungulia watu Allah Mtukufu miongoni mwa riziki, mvua, afya, ujuzi na neema nyinginezo, hakuna yoyote wa kuzuia rehema hii, na chochote kile anachokizuia hakuna yoyote baada Yake, Kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, anayeweza kukiachilia. Na Yeye Ndie Mshindi Mwenye kukitendesha nguvu kila kitu, Mwingi wa hekima Ambaye Anaiachilia rehema na Anaizuia kulingana na hekima Yake. info
التفاسير: |

3 : 35

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡۚ هَلۡ مِنۡ خَٰلِقٍ غَيۡرُ ٱللَّهِ يَرۡزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِۚ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ فَأَنَّىٰ تُؤۡفَكُونَ

Enyi watu! Kumbukeni, kwa nyoyo zenu, ndimi zenu na viungo vyenu, neema ya Allah Mtukufu juu yenu. Hakuna muumba wenu isipokuwa Allah Mtukufu, Anayewaruzuku nyinyi kwa mvua kutoka mbinguni, na kwa maji, madini na vinginevyo kutoka ardhini. Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye, Peke Yake, Asiye na mshirika. Basi vipi nyinyi mtaepushwa na kumpwekesha? info
التفاسير: |
prev

Fatir

next
:
0:00 0:00