prev

As-Saffat

next

1 : 37

وَٱلصَّٰٓفَّٰتِ صَفّٗا

Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Anaapa kwa Malaika wanaojipanga, katika kuabudu kwao, mistari iliyofuatana na kushikana. info
التفاسير: |

2 : 37

فَٱلزَّٰجِرَٰتِ زَجۡرٗا

Na kwa Malaika wanaoyapeleka mawingu na kuyaongoza kwa amri ya Allah Mtukufu. info
التفاسير: |

3 : 37

فَٱلتَّٰلِيَٰتِ ذِكۡرًا

Na kwa Malaika wanaosoma utajo wa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na maneno Yake. info
التفاسير: |

4 : 37

إِنَّ إِلَٰهَكُمۡ لَوَٰحِدٞ

Kwamba muabudiwa wenu, enyi watu, ni Mmoja, Asiye na mshirika. Hivyo basi mtakasieni ibada na utiifu. Na Anaapa Allah Mtukufu kwa Anachotaka miongoni mwa viumbe Vyake. Ama kiumbe, hafai kuapa isipokuwa kwa Allah Mtukufu, kwani kuapa kwa asiyekuwa Allah Mtukufu ni ushirikina. info
التفاسير: |

5 : 37

رَّبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا وَرَبُّ ٱلۡمَشَٰرِقِ

Yeye Ndiye Muumba mbingu na ardhi na vilivyoko baina ya hivyo viwili, na Ndiye Mpelekeshaji jua katika sehemu zake za kuchomozea na zile za kuchwea. info
التفاسير: |

6 : 37

إِنَّا زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنۡيَا بِزِينَةٍ ٱلۡكَوَاكِبِ

Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota. info
التفاسير: |

7 : 37

وَحِفۡظٗا مِّن كُلِّ شَيۡطَٰنٖ مَّارِدٖ

Na tumeihifadhi hiyo mbingu, kwa nyota, na kila shetani mwenye kuasi, mjeuri, aliyefukuzwa (kwenye rehema za Allah Mtukufu). info
التفاسير: |

8 : 37

لَّا يَسَّمَّعُونَ إِلَى ٱلۡمَلَإِ ٱلۡأَعۡلَىٰ وَيُقۡذَفُونَ مِن كُلِّ جَانِبٖ

Hawawezi hao Mashetani kufika kwenye viumbe vya juu, navyo ni mbingu na Malaika waliyomo ndani yake, wakapata kuwasikiliza wanapoutamka wahyi ambao Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Anauleta, unaokusanya sheria Yake na makadirio Yake, na wanarushiwa vimondo kila upande. info
التفاسير: |

9 : 37

دُحُورٗاۖ وَلَهُمۡ عَذَابٞ وَاصِبٌ

Kwa kuwafukuza ili wasipate kusikiliza. Na huko kwenye Nyumba ya Akhera watakuwa na adhabu ya daima yenye kuumiza. info
التفاسير: |

10 : 37

إِلَّا مَنۡ خَطِفَ ٱلۡخَطۡفَةَ فَأَتۡبَعَهُۥ شِهَابٞ ثَاقِبٞ

Isipokuwa yule aliyenyakua, miongoni mwa Mashetani, mnyakuo wa haraka, nao ni lile neno analolisikia mbinguni kwa haraka, akamtupia aliyekuwa chini yake, na yule mwingine akamtupia aliyekuwa chini yake. Basi pengine huenda akafikiwa na kimondo chenye kutoa mwangaza kabla hajalitupa, na pengine huwa amelitupa kwa makadirio ya Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kabla ya kujiwa na kimondo kikamchoma, na yule mwingine akaenda nalo hadi kwa makuhani wakaongeza juu ya neno hilo maneno mia moja ya urongo. info
التفاسير: |

11 : 37

فَٱسۡتَفۡتِهِمۡ أَهُمۡ أَشَدُّ خَلۡقًا أَم مَّنۡ خَلَقۡنَآۚ إِنَّا خَلَقۡنَٰهُم مِّن طِينٖ لَّازِبِۭ

Basi waulize, ewe Mtume, wenye kukanusha Kufufuliwa: Je kuumbwa kwao ni kugumu zaidi au ni hivi viumbe tulivyoviumba? Kwa hakika, tulimuumba baba yao Ãdam kwa udongo ulioshikana na kuambatana. info
التفاسير: |

12 : 37

بَلۡ عَجِبۡتَ وَيَسۡخَرُونَ

Bali ulistaajabu, ewe Mtume, kwa ukanushaji wao na kukataa kwao Kufufuliwa. Na la kustaajabiwa zaidi na lililo kubwa zaidi kuliko lile la kukataa kwao ni kwamba wao wanakucheza shere na kulidharau neno lako. info
التفاسير: |

13 : 37

وَإِذَا ذُكِّرُواْ لَا يَذۡكُرُونَ

Na wanapokumbushwa walichokisahau au walichoghafilika nacho, hawanufaiki kwa huo ukumbusho wala hawazingatii. info
التفاسير: |

14 : 37

وَإِذَا رَأَوۡاْ ءَايَةٗ يَسۡتَسۡخِرُونَ

Na wanapoiona miujiza yenye kutolea dalili unabii wako, wanakufanyia shere na wanastaajabu. info
التفاسير: |

15 : 37

وَقَالُوٓاْ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ مُّبِينٌ

Na wanasema, Halikuwa hili ulilotuletea isipokuwa ni uchawi uliojitokeza waziwazi. info
التفاسير: |

16 : 37

أَءِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ

Je, tunapokufa na tukawa mchanga na mifupa iliyochakaa, je sisi ni wenye kufufuliwa kutoka makaburini mwetu tukiwa hai? info
التفاسير: |

17 : 37

أَوَءَابَآؤُنَا ٱلۡأَوَّلُونَ

Au pia watafufuliwa baba zetu waliopita kabla yetu? info
التفاسير: |

18 : 37

قُلۡ نَعَمۡ وَأَنتُمۡ دَٰخِرُونَ

Waambie, ewe Mtume, «Ndio mtafufuliwa hali mkiwa wanyonge». info
التفاسير: |

19 : 37

فَإِنَّمَا هِيَ زَجۡرَةٞ وَٰحِدَةٞ فَإِذَا هُمۡ يَنظُرُونَ

Hakika ni kwamba huo utakuwa ni Mpulizo mmoja, wakitahamaki wao wamesimama kutoka makaburini mwao, wanatazama vitisho vya Kiyama. info
التفاسير: |

20 : 37

وَقَالُواْ يَٰوَيۡلَنَا هَٰذَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ

Na watasema, «Ewe maangamivu yetu! Hii ni siku ya kuhesabiwa na kulipwa!» info
التفاسير: |

21 : 37

هَٰذَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِ ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ

Hapo wataambiwa, «Hii ndiyo Siku ya Uamuzi wa haki baina ya viumbe, ambayo mlikuwa mkiikanusha duniani na mkiikataa». info
التفاسير: |

22 : 37

۞ ٱحۡشُرُواْ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ وَأَزۡوَٰجَهُمۡ وَمَا كَانُواْ يَعۡبُدُونَ

Na Malaika wataambiwa, «Wakusanyeni wale waliomkanusha Allah Mtukufu na wafananao na wao na waungu wao waliokuwa wakiwaabudu». info
التفاسير: |

23 : 37

مِن دُونِ ٱللَّهِ فَٱهۡدُوهُمۡ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلۡجَحِيمِ

Badala ya Allah Mtukufu, na muwasukume kwa nguvu hadi kwenye moto wa Jahanamu. info
التفاسير: |

24 : 37

وَقِفُوهُمۡۖ إِنَّهُم مَّسۡـُٔولُونَ

Na muwafunge kabla hawajafika kwenye moto wa Jahanamu, kwa kuwa wao ni wenye kuulizwa kuhusu matendo yao na maneno yao yaliyotokana na wao duniani, kwa namna ya kuwakemea na kuwakaripia. info
التفاسير: |
prev

As-Saffat

next
:
0:00 0:00