prev

Sad

next

1 : 38

صٓۚ وَٱلۡقُرۡءَانِ ذِي ٱلذِّكۡرِ

«Ṣād» Yametangulia maelezo kuhusu herufi zilizotengwa na kukatwa mwanzoni mwa sura ya Al-Baqarah. info
التفاسير: |

2 : 38

بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فِي عِزَّةٖ وَشِقَاقٖ

Anaapa Allah Mtukufu, Aliyetakasika, kwa Qur’ani inayokusanya ukumbushaji kwa watu kwa yale ambayo wao wameghafilika nayo. Lakini makafiri wanaifanyia kiburi haki na wanaenda kinyume nayo. info
التفاسير: |

3 : 38

كَمۡ أَهۡلَكۡنَا مِن قَبۡلِهِم مِّن قَرۡنٖ فَنَادَواْ وَّلَاتَ حِينَ مَنَاصٖ

Kuna ummah wengi tuliowaangamiza kabla ya hawa washirikina, wakaomba waokolewe na wakaita kutaka toba, na wakati si wakati wa kukubaliwa toba wala wakati wa kukimbia na kuokolewa na yaliyowapata. info
التفاسير: |

4 : 38

وَعَجِبُوٓاْ أَن جَآءَهُم مُّنذِرٞ مِّنۡهُمۡۖ وَقَالَ ٱلۡكَٰفِرُونَ هَٰذَا سَٰحِرٞ كَذَّابٌ

Na wameona ajabu washirikina hawa kuwa Allah Mtukufu Amewatumia binadamu miongoni mwao awalinganie kwa Allah Mtukufu na awaogopeshe adhabu Yake na wakasema, «Hakika yeye si Mtume bali yeye ni mrongo katika maneno yake, anawafanyia uchawi watu wake». info
التفاسير: |

5 : 38

أَجَعَلَ ٱلۡأٓلِهَةَ إِلَٰهٗا وَٰحِدًاۖ إِنَّ هَٰذَا لَشَيۡءٌ عُجَابٞ

Ni vipi atawafanya waungu wengi kuwa ni mungu mmoja? Hili alilolileta na akalingania kwalo ni jambo la ajabu. info
التفاسير: |

6 : 38

وَٱنطَلَقَ ٱلۡمَلَأُ مِنۡهُمۡ أَنِ ٱمۡشُواْ وَٱصۡبِرُواْ عَلَىٰٓ ءَالِهَتِكُمۡۖ إِنَّ هَٰذَا لَشَيۡءٞ يُرَادُ

Wakatoka viongozi wa watu na wakubwa wao wakiwahimiza watu wao kuendelea kwenye ushirikina na kuvumilia juu ya waungu wengi wakawaambia «Hili alilokuja nalo huyu Mtume ni jambo la kupangwa, lengo lake ni uongozi na ukubwa». info
التفاسير: |

7 : 38

مَا سَمِعۡنَا بِهَٰذَا فِي ٱلۡمِلَّةِ ٱلۡأٓخِرَةِ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا ٱخۡتِلَٰقٌ

Hatujasikia hili analolingania katika dini ya baba zetu wa kikureishi wala katika Unaswara; halikuwa hili isipokuwa ni urongo na uzushi. info
التفاسير: |

8 : 38

أَءُنزِلَ عَلَيۡهِ ٱلذِّكۡرُ مِنۢ بَيۡنِنَاۚ بَلۡ هُمۡ فِي شَكّٖ مِّن ذِكۡرِيۚ بَل لَّمَّا يَذُوقُواْ عَذَابِ

Je, amehusishwa Muhammad peke yake kwa kuteremshiwa Qur’ani bila ya sisi? Bali wao wako kwenye shaka ya kuwa mimi nimekuletea wahyi wewe, ewe Mtume, na kukupa utume. Bali wao walisema hilo kwa kuwa hawajaonja adhabu ya Allah Mtukufu, na lau wangeionja adhabu wasingethubutu kusema waliyosema. info
التفاسير: |

9 : 38

أَمۡ عِندَهُمۡ خَزَآئِنُ رَحۡمَةِ رَبِّكَ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡوَهَّابِ

Au kwani wao wanamiliki mahazina ya fadhila za Mola wako, Aliye Mshindi katika ufalme Wake, Aliye Mpaji wa Anachokitaka miongoni mwa riziki Yake na fadhila Zake kwa Anayemtaka miongoni mwa viumbe Vyake? info
التفاسير: |

10 : 38

أَمۡ لَهُم مُّلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَاۖ فَلۡيَرۡتَقُواْ فِي ٱلۡأَسۡبَٰبِ

Au kwani washirikina hawa wana mamlaka ya mbinguni na ardhini na vilivyoko baina ya viwili hivyo, hivyo basi wakatoa na kuzuia? Basi wajifanyie kamba zenye kuwafikisha mbinguni wapate kutoa uamuzi wanaoutaka wa kutoa na kuzuia. info
التفاسير: |

11 : 38

جُندٞ مَّا هُنَالِكَ مَهۡزُومٞ مِّنَ ٱلۡأَحۡزَابِ

Askari hawa wanaokanusha ni askari wenye kushindwa, kama walivyoshindwa wengineo miongoni mwa mapote ya watu waliokuwa kabla yao. info
التفاسير: |

12 : 38

كَذَّبَتۡ قَبۡلَهُمۡ قَوۡمُ نُوحٖ وَعَادٞ وَفِرۡعَوۡنُ ذُو ٱلۡأَوۡتَادِ

Walikanusha kabla yao watu wa Nûḥ, ‘Ãd, Fir‛awn mwenye nguvu kubwa. info
التفاسير: |

13 : 38

وَثَمُودُ وَقَوۡمُ لُوطٖ وَأَصۡحَٰبُ لۡـَٔيۡكَةِۚ أُوْلَٰٓئِكَ ٱلۡأَحۡزَابُ

Thamûd, watu wa Lûṭ, watu wa miti na mabustani, nao ni watu wa Shu‛ayb. Hao ndio ummah walioshirikiana wakawa pote moja juu ya ukafiri na ukanushaji na wakajikusanya juu yake. info
التفاسير: |

14 : 38

إِن كُلٌّ إِلَّا كَذَّبَ ٱلرُّسُلَ فَحَقَّ عِقَابِ

Hakuna watu wa pote lolote kati ya hawa isipokuwa walikanusha Mitume na kwa hivyo wakastahiki kupata adhabu ya Allah Mtukufu na yakawashukia wao mateso Yake. info
التفاسير: |

15 : 38

وَمَا يَنظُرُ هَٰٓؤُلَآءِ إِلَّا صَيۡحَةٗ وَٰحِدَةٗ مَّا لَهَا مِن فَوَاقٖ

Na hawangojei washirikina hawa, ili adhabu iwashukie wakisalia kwenye ushirikina wao, isipokuwa Mpulizo mmoja ambao hauna kurudi. info
التفاسير: |

16 : 38

وَقَالُواْ رَبَّنَا عَجِّل لَّنَا قِطَّنَا قَبۡلَ يَوۡمِ ٱلۡحِسَابِ

Na wamesema, «Mola wetu! Tuharakishie sehemu yetu ya adhabu duniani kabla ya Siku ya Kiyama.» Kusema huku kulikuwa ni uchezaji shere kutoka kwao. info
التفاسير: |
prev

Sad

next
:
0:00 0:00