prev

Al-Ahqaf

next

1 : 46

حمٓ

“Ḥā, Mĩm” Maelezo kuhusu herufi zilizokatwa na kutengwa yametangulia mwanzo wa sura ya Al- Baqarah. info
التفاسير: |

2 : 46

تَنزِيلُ ٱلۡكِتَٰبِ مِنَ ٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَكِيمِ

Hii Qur’ani ni teremsho kutoka kwa Allah Mtukufu Mshindi Asiyeshindwa, Mwenye hekima katika uendeshaji mambo Wake na utengezaji Wake. info
التفاسير: |

3 : 46

مَا خَلَقۡنَا ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَآ إِلَّا بِٱلۡحَقِّ وَأَجَلٖ مُّسَمّٗىۚ وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ عَمَّآ أُنذِرُواْ مُعۡرِضُونَ

Hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina ya viwili hivyo isipokuwa kwa haki, si kwa mchezo na upuuzi, bali tumeziumba ili waja wapate kujua ukubwa wa Muumba wa hizo na wamuabudu Peke Yake na wajue kuwa Yeye ni Muweza wa kuwarudishia waja uhai baada ya kufa kwao, na ili wasimamishe haki na uadilifu baina yao, mpaka ufike wakati huo unaojulikana Kwake. Na wale waliokanusha kuwa Allah Mtukufu Ndiye Mungu wa Kweli, wanayapa mgongo yale ambayo Qur’ani inawaonya kwayo; wao hawawaidhiki wala hawafikirii. info
التفاسير: |

4 : 46

قُلۡ أَرَءَيۡتُم مَّا تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَرُونِي مَاذَا خَلَقُواْ مِنَ ٱلۡأَرۡضِ أَمۡ لَهُمۡ شِرۡكٞ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِۖ ٱئۡتُونِي بِكِتَٰبٖ مِّن قَبۡلِ هَٰذَآ أَوۡ أَثَٰرَةٖ مِّنۡ عِلۡمٍ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Sema, ewe Mtume, uwaambie hawa makafiri, “Hivi mnawaona waungu na masanamu mnaowaabudu badala ya Allah Mtukufu? Hebu nionesheni, ni sehemu gani waliyoiumba katika ardhi? Au kwani wao wana fungu katika uumbaji mbingu? Nileteeni kitabu kinachotoka kwa Allah Mtukufu kabla ya hii Qur’ani au mabaki yaliyosalia ya elimu, iwapo nyinyi ni wakweli katika madai yenu. info
التفاسير: |

5 : 46

وَمَنۡ أَضَلُّ مِمَّن يَدۡعُواْ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَن لَّا يَسۡتَجِيبُ لَهُۥٓ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَهُمۡ عَن دُعَآئِهِمۡ غَٰفِلُونَ

Hakuna aliyepotea zaidi wala aliye mjinga zaidi kuliko yule anayewaomba waungu wengine badala ya Allah Mtukufu, waungu wasioitikia maombi yake kabisa mpaka Siku ya Kiyama, kwa kuwa waungu hao ni wafu au mawe au miti na mfano wa hivyo, na hali hivyo havina habari ya maombi ya huyo mwenye kuviabudu, havina uwezo wa kumnufaisha au kumdhuru. info
التفاسير: |
prev

Al-Ahqaf

next
:
0:00 0:00