prev

Muhammad

next

1 : 47

ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ أَضَلَّ أَعۡمَٰلَهُمۡ

Wale waliokataa kwamba Allah Mtukufu Ndiye Peke Yake Mungu wa kweli Asiye na mshirika, na wakawazuia watu na Dini Yake, Allah Mtukufu Atazifuta amali zao na kuziporomosha, na Atawapa usumbufu kwa sababu ya amali zao hizo. info
التفاسير: |

2 : 47

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَءَامَنُواْ بِمَا نُزِّلَ عَلَىٰ مُحَمَّدٖ وَهُوَ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّهِمۡ كَفَّرَ عَنۡهُمۡ سَيِّـَٔاتِهِمۡ وَأَصۡلَحَ بَالَهُمۡ

Na wale waliomuamini Allah Mtukufu na wakafuata Sheria Zake na wakaamini Kitabu Alichomteremshia Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), nacho ndicho ukweli usiokuwa na shaka kutoka kwa Mola wao, Allah Mtukufu Atawasamehe maovu waliyoyafanya na hatawatesa kwa maovu hayo, na atawatengenezea mambo yao duniani na Akhera. info
التفاسير: |

3 : 47

ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱتَّبَعُواْ ٱلۡبَٰطِلَ وَأَنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّبَعُواْ ٱلۡحَقَّ مِن رَّبِّهِمۡۚ كَذَٰلِكَ يَضۡرِبُ ٱللَّهُ لِلنَّاسِ أَمۡثَٰلَهُمۡ

Kupoteza huko na kuongoza, sababu yake ni kwamba wale waliokufuru wamemfuata Shetani wakamtii, na kwamba wale walioamini walimfuata Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na yale aliyokuja nayo ya mwangaza na uongofu. Kama Alivyobainisha Allah Mtukufu vile Anavyoyafanya mapote mawili ya watu wa ukafiri na watu wa Imani kwa wanavyostahili, vilevile Allah Mtukufu, Aliyetakasika, Anawapigia watu mifano yao, ili kila watu wanaofanana (wa aina moja) wakutane na wale wanaonasibiana nao. info
التفاسير: |

4 : 47

فَإِذَا لَقِيتُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَضَرۡبَ ٱلرِّقَابِ حَتَّىٰٓ إِذَآ أَثۡخَنتُمُوهُمۡ فَشُدُّواْ ٱلۡوَثَاقَ فَإِمَّا مَنَّۢا بَعۡدُ وَإِمَّا فِدَآءً حَتَّىٰ تَضَعَ ٱلۡحَرۡبُ أَوۡزَارَهَاۚ ذَٰلِكَۖ وَلَوۡ يَشَآءُ ٱللَّهُ لَٱنتَصَرَ مِنۡهُمۡ وَلَٰكِن لِّيَبۡلُوَاْ بَعۡضَكُم بِبَعۡضٖۗ وَٱلَّذِينَ قُتِلُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَلَن يُضِلَّ أَعۡمَٰلَهُمۡ

Basi mkipambana, enyi Waumini, na wale waliokufuru katika viwanja vya vita, piganeni nao kidhati na mzipige shingo zao. Hata mtakapowadhoofisha kwa kuwaua kwa wingi na mkazivunja nguvu zao, wafungeni kisawasawa wale mnaowateka. Kisha basi ima muwasamehe kwa kuwafungua na kuwaacha bila kutoa fidia badala yake, au wajikomboe kwa kutoa fidia, au watiwe utumwani au wauawe. Na endeleeni kufanya hivyo mpaka vita vimalizike. Hiyo ndiyo hukumu iliyotajwa ya kuwatahini Waumini kwa makafiri na ushindi kuzunguka baina yao. Na lau Allah Mtukufu angetaka wangepata ushindi Waumini bila ya vita, lakini Allah Mtukufu Amejaalia mateso yao yawe mikononi mwenu, ndipo Akaweka sheria ya jihadi ili Awajaribu nyinyi kwa wao, na Ainusuru kupitia kwenu Dini Yake. Na wale Waumini waliouwawa katika njia ya Allah Mtukufu, hatayaporomosha Allah Mtukufu malipo mema ya matendo yao. info
التفاسير: |

5 : 47

سَيَهۡدِيهِمۡ وَيُصۡلِحُ بَالَهُمۡ

Atawaafikia siku za uhai wao duniani wawe watiifu Kwake na wafanye matendo ya kumridhisha awatengenezee hali zao, mambo yao na malipo mema yao duniani na Akhera. info
التفاسير: |

6 : 47

وَيُدۡخِلُهُمُ ٱلۡجَنَّةَ عَرَّفَهَا لَهُمۡ

Na Awatie kwenye pepo ambayo Aliwajulisha na Akawasifia, na Akawaafikia kusimama kuyafanya yale Aliyowaamrisha, na miongoni mwayo ni kufa shahidi katika njia Yake, kisha atawajulisha wao mashukio yao huko Peponi watakapoingia humo. info
التفاسير: |

7 : 47

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِن تَنصُرُواْ ٱللَّهَ يَنصُرۡكُمۡ وَيُثَبِّتۡ أَقۡدَامَكُمۡ

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kivitendo, mkiinusuru Dini ya Allah Mtukufu kwa kupigana jihadi katika njia Yake na kuhukumu kwa Kitabu Chake na kufuata amri Zake na kujiepusha na makatazo Yake, Allah Mtukufu Atawapa ushindi juu ya maadui zenu na Atazithibitisha nyayo zenu wakati wa kupigana. info
التفاسير: |

8 : 47

وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَتَعۡسٗا لَّهُمۡ وَأَضَلَّ أَعۡمَٰلَهُمۡ

Na wale waliokanusha, basi maangamivu ni yao, na Allah Mtukufu Atazifuta thawabu za matendo yao mema. info
التفاسير: |

9 : 47

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ كَرِهُواْ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأَحۡبَطَ أَعۡمَٰلَهُمۡ

Hayo ni kwa sababu wao walikichukia Kitabu cha Allah Mtukufu kilichoteremshwa kwa Mtume Wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), wakakikanusha, na Allah Mtukufu Akayabatilisha matendo yao kwa kuwa yalikuwa katika kumtii Shetani. info
التفاسير: |

10 : 47

۞ أَفَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۖ دَمَّرَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡۖ وَلِلۡكَٰفِرِينَ أَمۡثَٰلُهَا

Kwani hawakwenda makafiri hawa kwenye ardhi ya Allah Mtukufu wakayazingatia yale yaliyowapata ummah waliopita ya mateso? Allah Mtukufu Aliyavunjavunja majumba yao. Na makafiri hawa watakuwa na mwisho kama huo uliowafikia ummah hao. info
التفاسير: |

11 : 47

ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ مَوۡلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَأَنَّ ٱلۡكَٰفِرِينَ لَا مَوۡلَىٰ لَهُمۡ

Hilo tulilowafanyia watu wa mapote mawili: pote la Imani na pote la ukafiri, ni kwa kuwa Allah Mtukufu Ndiye Msimamizi wa Waumini na mwenye kuwanusuru, na kuwa makafiri hawana mwenye kuwasimamia wala kuwanusuru. info
التفاسير: |
prev

Muhammad

next
:
0:00 0:00